Wabongo wengi ni wajinga kiasi kwamba hata sikukuu yao hawajui namna ya kuisherekea

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,220
12,726
Nakumbuka miaka ya 90 mwishoni kuliandikwa habari kwenye magazeti kadhaa kuwa mlima Meru unaongezwa urefu. Kulikuwa na picha za Helkopta kuwa zitabeba mchanga kupeleka juu mlimani.

Picha nyingine ilimuonyesha mtu ameshika sururu eti ni mtaalamu wa kuongeza milima urefu. Iliandikwa kwa namna ya kuaminisha sana.

Na baadaye ukiamini na kuambiwa ni siku ya wajinga, unajiona mjinga hasa. Kwamba wanaongeza mlima urefu!! Kutoa habari ya sikukuu ya wajinga kunahitaji akili sana.

Sasa siku hizi hakuna ubunifu wowote wa siku ya wajinga. Mtu badala ya kutoa kitu "Absurd" anaishia kudanganya na kudai ni siku ya wajinga.

Mmoja anasema simba imetolewa superleague sababu ya kukosa vigezo. Mtu kuamini hilo si ujinga, ni jambo linalowezekana.

Mwisho aliyetoa ndiye anaonekana mjinga. Mwingine anaweza kukuambia mzazi wako kafariki!! Sasa huo kama siyo ujinga wenyewe ni nini.

Yaani nchi imejaa wajinga hadi wanashindwa kusherekea sikukuu yao wenyewe.
 
Nakumbuka miaka ya 90 mwishoni kuliandikwa habari kwenye magazeti kadhaa kuwa mlima Meru unaongezwa urefu. Kulikuwa na picha za Helkopta kuwa zitabeba mchanga kupeleka juu mlimani. Picha nyingine ilimuonyesha mtu ameshika sururu eti ni mtaalamu wa kuongeza milima urefu. Iliandikwa kwa namna ya kuaminisha sana. Na baadaye ukiamini na kuambiwa ni siku ya wajinga, unajiona mjinga hasa. Kwamba wanaongeza mlima urefu!! Kutoa habari ya sikukuu ya wajinga kunahitaji akili sana.

Sasa siku hizi hakuna ubunifu wowote wa siku ya wajinga. Mtu badala ya kutoa kitu "Absurd" anaishia kudanganya na kudai ni siku ya wajinga. Mmoja anasema simba imetolewa superleague sababu ya kukosa vigezo. Mtu kuamini hilo si ujinga, ni jambo linalowezekana. Mwisho aliyetoa ndiye anaonekana mjinga. Mwingine anaweza kukuambia mzazi wako kafariki!! Sasa huo kama siyo ujinga wenyewe ni nini.

Yaani nchi imejaa wajinga hadi wanashindwa kusherekea sikukuu yao wenyewe.

Tatizo kubwa litakuwa elimu:

1. Mtanzania, watanzania wote ni wajinga isipokuwa yeye.
2. Mtanzania, Mataifa wote ni wajinga isipokuwa yeye.
3. Mtanzania, anajua hata asivyovisomea Wala kuvijua.
4. Nk.

Kiufupi ni mjuaji mno wa kila kitu. Akisahau kabisa kuwa nyani haoni kundule.

Kazi kweli kweli.
 
Huyo ndiye mtanzania sasa kwenye ubora wake.

"Tujivunieni utanzania wetu ndugu zangu ndivyo tulivyo."
 
Back
Top Bottom