Si kweli kwamba miungu ya kizungu iliishinda miungu ya kiafrika

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Jumatano ni njema na angavu.

Kuna nadharia nyingi na simulizi za kweli kuhusu hoja za kwa nini miungu ya kiafrika haikutukomboa na utumwa wa Wazungu na Waarabu, ikiwa kweli ilikuwa na nguvu kama tunavyodai?

Nimekuwa kwenye tafakuri pana kuhusiana na hili, na hatimaye nimepata jibu kutoka kwenye tafiti zangu na za watu wengine, pia kutoka kwenye simulizi na historia mbali mbali za kweli na halisi.

Ni kweli KABISA miungu ya kiafrika, au Mungu wa Afrika, ana nguvu mara 1000+ zaidi ya miungu yoyote ya sayari hii. Hili halipingiki. Wazungu wanatambua hili, Waarabu wanatambua hili.

Ni Mungu mwenye nguvu sana. Sasa nitaeleza kwa nini watu wanasema alishindwa kutuokoa na utumwa kutoka kwa Waarabu na Wazungu?

USALITI

Kilichotupiga si Wakoloni, kilichotupiga ni wasaliti ambao ni Waafrika wenzetu tuliowaamini, walioamua kwa maslahi zao binafsi kuvujisha siri kwa maadui ambao ni Wazungu na Waarabu.

Kumbuka tulikuwa hatuna mavazi bado ya viwandani, hatukuwa na bunduki wala mizinga, ila wao walikuwa na vyote hivyo. Pamoja na hayo yote tuliwatwanga kama watoto wadogo.

Ushahidi wa hili unapatikana kwenye kisa cha Mtakatifu Mtwa Mkwawa, Chifu wa kabila la Wahehe. Aliwapiga Wajerumani ambao walikuwa na bunduki na mizinga, tena aliwapiga zaidi ya mara moja.

Naona unapata picha hapo namna Mungu wa Afrika alivyokuwa na nguvu sana. Wajerumani walihaha namna ya kumshinda mwamba huyu wa Afrika.

Njia waliyofanikiwa ni kutumia watu kutoka kwenye ngome ya Mkwawa, waliwalaghai na watu hao kuvujisha siri za ushindi wa Mkwawa. Hili si kosa la Mungu, na huwezi kusema Mungu wa Afrika alishindwa. Ni kosa na ni ujinga wa Waafrika wenyewe (wasaliti).

Waafrika waanakwamishwa na usaliti. Somo la uzalendo likianza kufundishwa mashuleni, na Waafrika wakianza kuwa wazalendo, mbona Wazungu kuwapindua ni kitu kidogo sana?

Kuna visa vingine vingi zaidi achana na hicho kisa cha Mtwa Mkwawa. Visa hivyo vyote vinahusu usaliti wa watu kutoka ndani na kuvujisha siri kwa maadui Wazungu na Waarabu.

The same applies kwa upande wa Machifu. Machifu walilaghaiwa na kuuza watu wao utumwani. Hoja kubwa ni usaliti wa Waafrika. Na usaliti huja kwa kukosa uzalendo. Ogopa sana Miungu ya Afrika.

Wachina walifanikiwa kwa sababu ya uzalendo, Wakorea hasa S Koreans nao walifanikiwa kwa sababu ya uzalendo. Hawa wote kuna miaka tulikuwa nao sawa hasa sisi Watanzania. Tulikuwa sawa kiuchumi.

Siku viongozi wa Afrika wakiwa wazalendo wa kweli, ndiyo siku mtu mweusi atakapobadilisha zama na dunia kwenda juu chini.

Mungu wa Afrika ana nguvu sana. Usaliti wa Waafrika wenzetu unatugharimu na sisi wengine.

Kama tuliwapiga tukiwa tunavaa magome, tukiwa na mikuki na mapanga huku wao wakiwa na bunduki na mizinga, vipi kuhusu sasa?

Propaganda za kizungu za kudharau Mungu wa Afrika zife tangu leo hii. Ushahidi upo wa kutosha kuwa Miungu ya Afrika ni hodari na ina nguvu sana.

Dini haijawahi na haitowahi kumsaidia mtu mweusi! Akili kichwani. Adui yako anakuleteaje dini ili ikusaidie? Anakuletea ili ikupumbaze. Akuibie.

Mwenye sikio na asikie!
RIP mashujaa wetu!
RIP Mtwa Mkwawa!
 
Sawa mkuu, tumekupata
 
Umepatia kabisa ni usaliti na kukosa uzalendo.

Na kila mmoja anaambiwa mwenzake ni msaliti ili naye amlipe huo usaliti kumbe ndio tunasalitiana hivyo. Ni kama ambavyo ccm atamsingizia chadema kafanya hivi na chadema naye akamsingizia ccm. Alimuradi tu taifa lisinene lugha moja. Mchawi ndo hiki.

Hii ndiyo mbinu ya kuwavuruga watu wasiwe wamoja kujiletea maendeleo. Ni kuwachanganya wasiseme kwa lugha moja tu.

Uimara na idhaifu wa jamii fulani umo katika namna wanaweza kushikamana au kutengana tu. Hakuna uchawi wala udini. Ni umoja na mshikamano tu. Akili mtu wangu
 
Sahihi. Akili tu! Bila kusalitiana kwa machifu, aisee Wakoloni wasingetutawala kabisa. Kilichotupiga ni usaliti wa ndani. Vinginevyo hawa weupe tungeendelea kuwachakaza sana.
 
Huenda upo sahihi, lakini kwa upande mwingine umewashutumu sana wenzetu kuwa walikuwa wasaliti, lakin hasha!! Watu walikuwa wanapigwa kuyakataa majina yao na kupewa majina mengine ya kiarabu,walikuwa wanalazimishwa kusali kanisani ili wafundishwe unyonge,upuuzi na unyenyekevu uliopitiliza ili msiwapige, na hili nimelishuhudia kwa wazazi wengi wa kiafrika, mtoto anachapwa kisa tu hataki kwenda msikitini, ni balaa zito kutoka kweny hili gereza walilotufungia, maana wamepiga kufuli kwa nje halafu wakasepa zao.
Wewe ukitaka kujua hili balaa angalia nyuzi nyingi za humu zinazozungumzia dini, ukionekana tu unaukataa uislam su ukristo wanakutishia kulaaniwa,na kuchomwa moto.
Yaani nafikir hili serikali inabidi iingilie uhuru wa dini ndimo tutakapokomboka katika gereza hili.
 
Miungu ya Afrika ina nguvu sana... usaliti umesababisha haya yote.
Samahan mkuu sijakuelewa, ni nguvu zipi hizo za miungu unazomanisha kama miungu yenyewe ilishindwa kutambua na kukabiliana na hila za kibinadamu.

Kama usaliti wa kibinadamu uliweza kushinda dhidi ya nguvu za kimiungu kuna haja gani ya kuipa hiyo miungu utukufu? Haingii akilini nguvu za miungu kushindwa na maarifa ya binadamu. Hiyo siyo miungu.
 
Mungu na miungu ukitaka kusema siku zote amewapa wanaadamu machaguo.

Ama kushirikiana ama kusalitiana.

Usimrudishie tena mpira yeye kutaka akusalitishe au akushirikianishe.

Sasa utashi huru amekuoa wa kazi gani.

Te a tambua kuwa ni sisi wanadamu tunaotenda kazi kwa nguvu tulizojaaaliwa na Mungu. In him we live move and have our being
 
Back
Top Bottom