Namna ya kunasa Vitoto vya kishua msimu huu wa Sikukuu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
NAMNA YA KUNASA VITOTO VYA KISHUA MSIMU HUU WA SIKUKUU

Anaandika, Robert Heriel

Kheri ya Christmas Wakuu!
Tuachane na mambo Serious kidogo, muda wa kupoza Injini ndio huu.
Wale wazee wenzangu wa pisikali zamoto tujadili kidogo hapa namna ya kuopoa vile vitoto vyakishua.

Tabia Mbaya! Tabia mbofu! Msinione ninatabia mbofu!
Kijana WA hovyo?! Kijana WA hovyo! Msinione kijana WA hovyo!
Hata hivyo sitajali, vyovyote mnionavyo. Hii ni sehemu ya Maisha yangu, mara moja! Kuishi mara moja!

"Pisikali! Nawapenda pisikali!
Njooni kwangu pisikali! Ooh! Sura zenu nzuri kama malaika, zang'aa na kumulika,
Sitaki Mimi mnitazame! Nahisi kuyoyoma moyoni, macho yenu mazuri yananidonoa donodono! Enyi pisikali!
Bilingebilinge bayoyo viuno vyenu mkikatika, nahisi kupata pumu; pumzi yangu yakatika.
Nyuma nyama kilo Mia, mumejazia mpaka nayanyongeza. Chopoeni mfukoni Pesa yangu mjilie Kwa Raha zenu. Chopoa! Chopoa! Chopoeni!"
Subiri Taikon, mbona kama umevurugwa; upo sawa kweli kichwani?
Nisameheni! Nilikunywa mvinyo mpya.

Taikon unajua utafukuzwa kazi na Meneja wako? Unaandika manini huku mtandaoni? Ndio maana hupandishwi cheo wala kuongezewa mshahara!

Potelea Pote! Niacheni! Bosi mkurugenzi kitambi Meneja, nipo Holiday hapa, niache! Sitaki kuwa Serious msimu wa holiday!

Msimu wa holiday ndio huu. Msimu wa mavuno ya Watoto wakishua. Si unajua holiday Watoto wakishua huachiwa kauhuru Fulani hivi.
Sio wote wataenda nchi za nje Kula bata, wengi tutakuwa nao humuhumu.
Mpango kazi upo, presentation tayari nimeiandaa, viwalo vipo, bajeti angalau ya kuratibu Mpango kazi nayo Ipo.

Namna ya kunasa Vitoto vya kishua msimu huu WA Sikukuu;

1. Andaa Mpango kazi.
Mpango kazi uwe na title isemayo; "MPANGO WA HOLIDAY WA ROYAL-DATE"
Kisha set Aina ya Pisikali unayemtaka, kama hivi
Rangi: Mrembo mweusi mtelezo
Umbo: Mrembo English Figure
Sura:. Nzuri kiasi
Kimo : Futi tano unusu
Sauti:. Laini Frequency 265Hz😉
Mitetemo: 4Magnitude (Sio mtoto Hana hata mitetemo bhana)🏃
Hiyo itakusaidia ukifika eneo la tukio usipagawe na warembo utakaowaona, kwamba kila demu unamtaka. Ukishakuwa umeshapanga Aina ya demu ukifika kazi yake ni kusoma windo lako tuu. Unakuwa kama Simba MLA nyama, yaani unakuwa na Target.

Mpango uonyeshe Location
Mahali: Mlimani City au fukwe za kigamboni.
Gharama zitakazotumika:. Laki tano.
Wasindikizaji/Escorts = Wawili

Mpango kazi uonyeshe muda wa kufika na muda wa kuondoka, yaani Fanya vitu kitaalamu.

2. Andaa viwalo.
Viwalo vinategemea zaidi Mpango kazi unasemaje.
Taikon nakushauri, usivae kishalobaro Sana. Vaa ki-classic, kijentomeni, aidha ni kadeti na Tsheti ya mikono mifupi kisha na saa. Au vaa jinsi isiyobana Sana na Flana na Kofia ya kishikaji, au Vaa Pensi iliyofika magotini isipande juu au kushuka Chini ya goti, vaa na Flana au Tshet, mkono WA kushoto Saa.
Chini pigilia raba flani hivi za kishikaji, au Sendo,
Kichwani nyoa vizuri kulingana na kichwa na uso wako. Kama unakipilipili na nywele nyekundu weka kokoto Kwa mbali Kwa kihisia gusia.
Nyoa ndevu vizuri au ziondoe zote,
Kama umenyoa kipara basi achia ndefu kiasi.

Kisha pulizia unyunyu wenye harufu nzuri.

3. Miondoko na mikao.
Tembea miondoko ya kijentomeni, kama vile umeitwa kwenye jukwaa la kimataifa kupewa tuzo. Usitembee kizembe zembe au kishamba. Usidunde dunde hovyo kama kijana mwenye tatizo la ubongo.
Nyosha mgongo ukiwa unatembea, weka shingo yako sawia kama kijana shupavu na mkakamavu lakini romantic.
Uso wako usiuzubaishe, usipoe Sana wala usiuchangamshe Sana.
Ukikaa kaa mikao ya kiume, usiupinde mgongo kama Mzee, weka Swaga za kitaaluma, kama MTU unayejiamini mwenye uhakika na Kesho.
Usishangae shangae ukiwa eneo la tukio. Jifanye uko bize lakini sio bize Sana.
Usiwe Serious kupitiliza, jitahidi kuwa mcheshi lakini ucheshi wa Akili wakiume. Sio uwe na masikhara ya kishamba shamba!

4. Weka Sauti yako vizuri.
Ongea Sauti yenye Mvuto ukiambatanisha na Facial expression na body language ili kuleta Sanaa katika mazungumzo yako.
Pandisha na shusha Sauti Kwa Swaga kuvuta hisia za atakayekusikiliza,
Jitahidi kuonyesha Sauti yako inajali hisia za anayekusililiza hasa huyo Mrembo.

5. Sanaa ya Utongozaji.
Ushafika eneo la tukio, umependeza, unatembea Kwa miondoko ya kuvutia, umeshachukua Siti yako na waliokusindikiza. Hakikisha waliokusindikiza wamekuweka Katikati, alafu wamevaa tofauti na wewe.
Kwenye kukaa wasindikizaji wakae opposite na wewe(mkabala) yaani mtazamane, Hii itafaa zaidi Mrembo unayemmendea awe Nyuma yao, au usawa WA pembeni kidogo iwe kushoto au kulia.

Jitahidi Mrembo uliyemuweka kwenye magnesaiti yako atambue kuwa umevutiwa naye. Kisha macho yako yawe kila saa yanashangaa uzuri wake. Yalinde macho yako yasipepesushwe kuangalia warembo wengine, Hii itamfanya Mrembo Targeted kuona haujatulia.
Kama ukiweza mkigongana macho jaribu kutabasamu kisha mpe ishara yenye kupendeza, kama vile kumkonyeza, au kumng'atia mdomo kidizaini au kumpa salute au ishara yoyote inayoendana na mazingira na jinsi huyo Mrembo anavyoonekana.

6. Tafuta upenyo wa kuchukua mawasiliano.
BAADA YA kusoma mazingira na kuwatambua waliomzunguka Mrembo Targeted, ukajua Nani ni Nani yaani Ndugu zake kama wapo, marafiki au msaidizi wa kazi, pamoja na Walinzi.
Kuna namna nyingi za kuchukua mawasiliano kutegemeana na mazingira yaliyopo, mazingira uliyoyaweka baina yako na yeye,
Unaweza MPA namba za simu Kwa ishara endapo anahofu na yupo Chini ya ulinzi mkali.
Unaweza kuchukua namba za simu Kwa Kutumia Watu wake wakaribu kama marafiki au Ndugu au mfanyakazi.
Unaweza kuchukua namba za simu Kwa kumpa ishara atoke pembeni mzungumze, ukifika usiwe na muda wa kupoteza,
Fika,
Salimia,
Msifie kadiri ya alivyo,
Eleza kuwa umeona mazingira hayaruhusu ninyi kuzungumza pale hivyo unahitaji mawasiliano yake, au mpe yako.
Jitahidi Sauti yako iwe kama nilivyokueleza hapo juu.

BAADA YA kuchukua mawasiliano, mpigie hapohapo. Kisha mueleze jinsi alivyomkarimu, msifie kwa lugha nzuri isionekane unafanya uchawa.
Kisha eleza jinsi ulivyofurahi na unavyotamani nafasi kama Ile ijirudie mara nyingi zaidi.
Kisha achaneni. Rudi mahali Pako.
Usikae muda mrefu tangu ulipochukua namba. Malizia kinywaji chako Kwa dakika 30 kisha ondokeni, huku ukimpa ishara ya Kwa kheri.

Then, mtafute BAADA YA siku mbili, omba Radhi Kwa kuchelewa kumtafuta. Eleza sababu yenye mantiki na ambayo itamfanya akuambie Pole na akuonee huruma. Be Smart.

Mambo AMBAYO Mwanamke yeyote anayatazamia kutoka kwako hata kama hauna Pesa au haujasoma;

1. Strong mindset/attitude.
Jitahidi Mrembo unayemtongoza akufahamu kuwa upo Strong kwenye Akili, fikra na mitazamo yako.
Ndio maana Wakati unamtongoza Mwanamke hata kama huyo Mwanamke ni mjinga hajasoma au ni masikini, wote watakuwa wanakupa challenge kupima mindset yako kuwahusu wao wenyewe, kuhusu Maisha, kuhusu wewe mwenyewe.
Mwanamke hata kama anataka kukubalia anauwezo wa kukujaribu ili kukupima unauelewa wa kiwango gani.

Je upo emotional kama wao?
Kwa mfano anauwezo wa kukunyali, au kukuambia wewe sio hadhi yake, hauna Pesa au anamtu wake ambaye ni HB na anapesa kukushinda. Sasa hapo atasoma saikolojia yako, emotional yako, na mara nyingi Wanawake wakikusemesha hivyo hukutazama machoni.

2. Utanashati
Wanawake Wanadhana tatu kuhusu mwanaume mtanashati
I. Romantic, Sex, Mvuto mwanaume mtanashati wanamuona kama anayeyajua mapenzi

ii. Kujiweza kiuchumi.
Wanaamini kuwa mwanaume mtanashati anapesa ndio maana anauwezo wa kujitunza.

iii. Anaakili na mwerevu.
Wanawake wanahusisha utanashati na Werevu na Akili.
Ukiwa mtanashati huwezi amini Wanawake wanakuona mwerevu, mwenye Akili, mjanja, mbunifu na ambaye unauwezo WA kutatua changamoto.
Sio ajabu Wanawake wote Duniani huamini mwanaume akivaa Suti au kuvaa Tai ni msomi. Na anafanya kazi nzuri.

Kazi zote zisizohusiana na kuwa mtanashati ni ngumu Sana kupendwa na Wanawake.

3. Ucheshi
Moja ya dalili ya kutokukubaliwa na Mwanamke unapomtongoza ni kushindwa kumfanya atabasamu au kucheka kabisa.
Wanaume wenye uwezo wa kuwafanya Wanawake watabasamu au kucheka kabisa wanapendwa zaidi za Wanawake.
Ucheshi Kwa Wanawake inamaanisha Akili, utundu, ujanja, upendo.
Mwanamke ni. Mwepesi Sana kuchekacheka lakini sio rahisi kucheka Kwa mwanaume ambaye sio mcheshi.

Ucheshi ni Sanaa
Ucheshi ni moja ya mbinu za kumshawishi Mwanamke akupende na akukubalie.
Wanawake hawapendi mwanaume anayechekacheka, ila wanpenda wanaume wanaowafanya wachekecheke.

Taikon nawashaurigi wanaume wenzangu waliooa. Wawe na tahadhari na Vijana wacheshi wanaowachekesha wake zao. Wenye masikhara na wake zao. Wengi wanafaulu kutingisha nyavu za Dada zetu.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Sasa Taikon kwa kipengele hicho sie wavuvi na mafundi mchundo tunakosa vigezo, ngoja tusubiri wamanga wao hawana mambo mengi.
 
Utamkuta mpwayungu village na 'Tiss Uchwara' nyboma wanavyojichanganya kwenye viwanja vya kishua kutafuta sifa za kijinga kwa kununua Jack Daniels na mishahara ya 250k take home. Na kupiga mizinga ya hatariiii.
 
Back
Top Bottom