Je, ni kweli Tanzania ni nchi ya wajinga?!

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,896
3,206
Tanzania kwa siku za hivi karibuni imedhihirisha kile ambacho Naibu waziri wa Afya Dk. Mollel aliwahi kusema; kwamba Tanzania wajinga ni wengi.

Kwa bahati mbaya sana hata viongozi wakubwa na wasaidizi wa Rais, nachelea kusema kwamba na wao wamejidhihirisha kwamba ni wajinga. Hii pamoja na mambo mengine, imekuja baada ya Mkataba wa Kimangungo-mangungo wa DP World.

Hivi kama kweli siyo ujinga na umbumbumbu, utaingia mkataba ambao hauna kikomo na wenye masharti ya kuondoa uhuru wa nchi na wananchi wake katika kutumia rasilimali walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu?!

Hivi kama kweli hatuongozwi na wajinga, mtatuleteaje mkataba ambao tayari Rais alishasaini yapata mwaka mzima huko nyuma, eti tuujadili (kupitia wawakilishi wetu wabunge ambao pia wamedhirisha ni wajinga wa kutupwa!?)? Kama siyo ujinga huu, nini basi??

Viongozi wengi wa Tanzania ni waoga!
Wengi wako kwa ajili ya maslahi ya matumbo yao wenyewe na familia zao.
Na huwezi kuutenganisha uoga na ujinga. Wengi wanajidhalilisha kwa kutetea mambo ya kijinga ili tu waendelee kuwepo kwenye nafasi zao au wapewe promotion!
Hivi kweli hadi lini tutaendelea kuongozwa na wajinga wa aina hii?!

Mwisho, japo siyo kwa umuhimu; mjinga huwa hapendi kukosolewa, maana utashangaa baada ya ujumbe huu kusomwa na wanajamvi (ambao pia wajinga ni wengi), utashangaa uzi unatoweka kwenye mazingira ya kutatanisha na kumfuatilia mwandishi badala ya kuhangaika na kuondokana na ujinga!

Hatuwezi kuendelea kushuhudia mambo ya kijinga yakifanywa na viongozi wajinga yakiendelea katika nchi yetu.

Yaani kina Nyerere walifanya juhudi za kututoa utumwani, halafu wajinga wachache wanataka kuturudisha huko tena kwa bei chee kabisa; HAIWEZEKANI.

Amandraaaaaaaa..................

Aluta continua.
 
Attachments

  • Screenshot_20230624-143440_Chrome.jpg
    Screenshot_20230624-143440_Chrome.jpg
    148.3 KB · Views: 10
Wajinga ni wale wanaochezeshwa Ngoma na "ma spin Doctors"wa mitandaoni kama wewe...

Kwanza ilianza ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani...Kamala Harris...
Watu walichezeshwa Ngoma humu Jf na mitandao yote kuwa Yule mama anakuja kusimamia watanzania wakubali mapenzi ya jinsia moja...
Hadi maandamano uchwara yakafanyika...bonge moja la kampeni Hadi Viongozi wa dini ambazo huko Ulaya ndo main supporter wa hizo ndoa hapa nchini wakajifanya wao ndo wako mbele kuongea kitu hata hao Wamarekani hakiko kwenye agenda zao walipokuja hapa......

Sasa limekuja la Bandari..."ma spin Doctors"kazi moja tu...
Haipiti dakika 20 threads tatu mpya zote Bandari na kutukana na kuponda serikali ....

Wajinga washasahau Ngoma waliyo chezeshwa wakati wa ziara ya Kamala Harris....wapo wanajazwa hofu na kuambiwa "waarabu wamepewa" bandari milele...🤣🤣🤣🤣🤣

Kweli hii nchi ina wajinga Wengi sana
 
Hata wewe kwa haya uliyoandika imejidhihirisha wazi ni mjinga. Badala ya kutetea nchi yako, kazi kupiga propaganda za kijinga za kuwatetea viongozi wajinga.
Huna akili kabisa
 
Tanzania kwa siku za hivi karibuni imedhihirisha kile ambacho Naibu waziri wa Afya Dk. Mollel aliwahi kusema; kwamba Tanzania wajinga ni wengi.

Kwa bahati mbaya sana hata viongozi wakubwa na wasaidizi wa Rais, nachelea kusema kwamba na wao wamejidhihirisha kwamba ni wajinga. Hii pamoja na mambo mengine, imekuja baada ya Mkataba wa Kimangungo-mangungo wa DP World.

Hivi kama kweli siyo ujinga na umbumbu, utaingia mkataba ambao hauna kikomo na wenye masharti ya kuondoa uhuru wa nchi na wananchi wake katika kutumia rasilimali walizojaaliwa na Mwenexi Mungu?!

Hivi kama kweli hatuongozwi na wajinga, mtatuleteaje mkataba ambao tayari Rais alishasaini yapata mwaka mzima huko nyuma, eti tuujadili (kupitia wawakilishi wetu wabunge ambao pia wamedhirisha ni wajinga wa kutupwa!?)? Kama siyo ujinga huu, nini basi??

Viongozi wengi wa Tanzania ni waoga!
Wengi wako kwa ajili ya maslahi ya matumbo yao wenyewe na familia zao.
Na huwezi kuutenganisha uoga na ujinga. Wengi wanajidhalilisha kwa kutetea mambo ya kijinga ili tu waendelee kuwepo kwenye nafasi zao au wapewe promotion!
Hivi kweli hadi lini tutaendelea kuongozwa na wajinga wa aina hii?!

Mwisho, japo siyo kwa umuhimu; mjinga huwa hapendi kukosolewa, maana utashangaa baada ya ujumbe huu kusomwa na wanajamvi (ambao pia wajinga ni wengi), utashangaa uzi unatoweka kwenye mazingira ya kutatanisha na kumfuatilia mwandishi badala ya kuhangaika na kuondokana na ujinga!

Hatuwezi kuendelea kushuhudia mambo ya kijinga yakifanywa na viongozi wajinga yakiendelea katika nchi yetu.

Yaani kina Nyerere walifanya juhudi za kututoa utumwani, halafu wajinga wachache wanataka kuturidisha huko tena kwa bei chee kabisa; HAIWEZEKANI.

Amandraaaaaaaa..................

Aluta continua.
Viongozi wengi hasa Bungeni na kwenye idara za serikali ndo wana hizo hulka!
Wakishafuzu wanakuja kupractice kwa wananchi...!

Jana nilianza kufuatilia kipindi cha KipimaJoto DP World... Mjadala ulihidhuriwa na wajinga... waoga! Watu maslahi!
Nikazima simu nikalala..
 
Wajinga ni wale wanaochezeshwa Ngoma na "ma spin Doctors"wa mitandaoni kama wewe...

Kwanza ilianza ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani...Kamala Harris...
Watu walichezeshwa Ngoma humu Jf na mitandao yote kuwa Yule mama anakuja kusimamia watanzania wakubali mapenzi ya jinsia moja...
Hadi maandamano uchwara yakafanyika...bonge moja la kampeni Hadi Viongozi wa dini ambazo huko Ulaya ndo main supporter wa hizo ndoa hapa nchini wakajifanya wao ndo wako mbele kuongea kitu hata hao Wamarekani hakiko kwenye agenda zao walipokuja hapa......

Sasa limekuja la Bandari..."ma spin Doctors"kazi moja tu...
Haipiti dakika 20 threads tatu mpya zote Bandari na kutukana na kuponda serikali ....

Wajinga washasahau Ngoma waliyo chezeshwa wakati wa ziara ya Kamala Harris....wapo wanajazwa hofu na kuambiwa "waarabu wamepewa" bandari milele...🤣🤣🤣🤣🤣

Kweli hii nchi ina wajinga Wengi sana
Huoni kama kelele tulizopiga, zilimwogopesha Kamala Harris asituletee ujinga wao?
Na hili la Bandari zetu za Tanganyika, lazima tulipigie kelele tu. Kwamba watatusikia au watatupuuza, haijalishi, ila muda ndo utakaoamua.
Haiwezekani kupokonywa uhuru ambao wazee wetu waliutafuta kwa gharama kubwa sana.
Wengine hadi walipoteza maisha katika kutafuta uhuru wa nchi hii, halafu wapuuzi wachache tu kwa sababu ya kuendekeza tamaa ya mali, watuuze kwa bei nafuu, NEVER.
 
Wengine hadi walipoteza maisha katika kutafuta uhuru wa nchi hii,
Hebu tupe hii list ya waliokufa

By the way, umeaandika pumba tupu
Japo ni kweli wabongo ni wajinga wengi tena sana, na sio viongozi, ni wananchi ndio wajinga wote
 
Inasikitisha sana kuongozwa na wajinga
 
Attachments

  • Screenshot_20230624-152658_Google.jpg
    Screenshot_20230624-152658_Google.jpg
    131.2 KB · Views: 8
Back
Top Bottom