Waandishi wa habari wa Tanzania, baadhi wasivyojua namna ya kusimamia maudhui ya taarifa za viongozi wa juu kama Raisi

kibangubangu

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
212
285
Wakati mwingine nadhani ni vizuri au busara kuto alika waandishi wa habari katika matukio ya ndani,au nyeti...Ambayo yatahitaji weredi wa nini kirushwe au nini kisirushwe....

Uvivu wa baadhi ya waandishi wa habari kuhariri,kulingana na muktadha kunasababisha baadhi ya watu kutoa taarifa ambazo si salama

Tazama video hizi mbili harafu utajua..tofauti...

VIDEO YA RAIS TANZANIA YA IKULU MEDIA

Official president video

VIDEO YA RAIS TANZANIA PRIVATE MEDIA

Wakati mwingine hawa waandishi wa habari binafsi ni busara wasiwepo kwenye matukio yenye matukio ya wazi ya kiintelejensia.
 
Hahaa ,upo sahh
Una miakili mingi sana...Hahhahaha mtu kama rais anahitaji muda kidogo kurusha maudhui yake....

Kama utafanya bila kuhariri maana yake unamuweka raisi wako katika matukio magumu kesho yake ni kama unaonesha matukio yanafanyikaje...ulinzii wake upoje...Anyway...She is a president...kila kitu lazima kiwe calculated!,😊
 
Naunga mkono hoja juu ya taarifa yako na angalizo lako.kikubwa inatakiwa hao waandishi wa habari waelimishwe namna ya uchukuaji wa matukio pamoja na maudhui ya kurusha.wapewe muongoza wa nini kirushwe na kipi kisirushwe. Nini kichukuliwe na kipi kinatakiwa kuachwa kwa vyombo vya serikali kuchukua matukio yake.

Kikubwa ni kupewa muongozi tu maana Hata wao ni binadamu tu wanaoweza kufanya makosa ya bila kukusudia kutokana tu na kukosa uelewa wa msuala ya kiusalama kama ilivyotokea hapo.
 
Tatizo mnamfuatilia rais kuliko mnavyofuatilia habari.

Naona video zote mbili zinafanya coverage ya rais, hakuna sehemu iliyofanya coverage ya wavuvi / wananchi wamepokeaje hotuba ya rais. Na hiyo ni sehemu iliyo muhimu kabisa.
 
Unauhakika boss?wakati na muda ni vitu muhimu sana ,kama ungekubari kutulia mbele ya simu yako angalau ingekuonesha yote hayo uliyo hoji au kuto yaona...Mmmh.,..Anyways. nimekusoma....
 
Unauhakika boss?wakati na muda ni vitu muhimu sana ,kama ungekubari kutulia mbele ya simu yako angalau ingekuonesha yote hayo uliyo hoji au kuto yaona...Mmmh.,..Anyways. nimekusoma....
Mkuu,

Katika video hizi mbili zilizoletwa hapa, hakuna sehemu ambayo wananchi wanahojiwa kutoa maoni yao kuhusu kazi zao, kuhusu hotuba ya rais.

Maana yake ni kwamba, katika sample ya videos za hili jambo zilizoletwa na mtoa mada, tunaona kuwa, kuanzia Ikulu mpaka waandishi wa habari wasio wa Ikulu wote wanamuangalia sana rais, lakini hawawaangalii wananchi wanasemaje.

Huu ni mfumo ulio "top down". Top heavy. Kila mtu anaangalia juu. Single point of failure. Tatizo kubwa sana.

Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Sinde Warioba alikuwa anapenda sana kusoma magazeti.Tulikuwa tunamuona Oysterbay kila siku asubuhi kwenye Mercedes Benz anasoma magazeti akiwa kwenye msafara wake.

Baadaye, nilikuja kusikia kutoka kwenye mahojiano yake, kumbe alikuwa ana msaidizi wake maalum wa kutazama maoni na malalamiko ya wananchi. Yule msaidizi wake alikuwa anasoma magazeti, ana highlight habari fulani, au barua za wasomaji fulani, anampatia Waziri Mkuu asome.

Mzee Warioba alisisitiza hili katika Baraza la Habari, ambalo yeye aliliongoza. Akisema kwamba, siku hizi habari zina focus sana kwa viongozi, hazi focus kwa wananchi.

Alitoa mfano kwamba, zamani dereva wake alipenda kusikiliza TBC au Radio One kwenye gari, siku hizi dereva wake akabadili channel, kupeleka Deutschewelle. Kwa sababu ya coverage yao.

Hili ni tatizo kubwa sana Tanzania. Rais akipiga chafya tu ni habari inakuwa covered mpaka leso aliyotumia kujifuta mtaijua, ila wananchi wana matatizo mengi sana hayapati press. Makonda pamoja na mapungufu yake mengi, ziara zake angalau zimeibua madudu mengi mpaka Mwanasheria Mkuu wa serikali anasema ameshtushwa na madudu mengi haya.

Ina maana Mwanasheria Mkuu wa serikali kalala siku zote?

Ina maana waandishi wa habari wamelala siku zote mpaka mambo yanaibuka kwenye ziara za Makonda?
 
Hii hapa ni makala kuhusu nasaha za Warioba.

WARIOBA AHIMIZA KUANDIKWA HABARI ZA WANANCHI

Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Baraza la Habari Tanzania, Joseph Warioba akizungumza katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza.

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kujikita zaidi kuandika habari za wananchi.

Akizindua Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, amesema sasa inaelekea wananchi wanafuatilia zaidi habari za vyombo vya nje kulinganisha na za vyombo vya hapa nchini.

Hii siyo sifa alisema Warioba katika uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Courtyard Jijini Dar es Salaam.

“Mimi napenda habari na madereva wangu wanajua …wakati wowote inapofikia kuwepo taarifa ya habari na nikiwa nipo kwenye gari, watafungulia ama TBC ama Radio One”, alisema.

Lakini sasa mambo yamebadilika . Badala ya kufungulia redio za hapa nchini watafungulia redio kama DW, VOA ama vituo vingine vya radio vya nje, alisema.

Alisema kuwa aliwahi kuambiwa na raffik yake kuwa StarTV ina kipindi cha Dira ya Dunia kinacoanza saa 3.00 usiku.

Hii maana yake ni nini? Warioba alisema inaelekea vyombo vya habari vya ndani haviwatoshelezi wananchi.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema kwa hali ya sasa vyombo vya habari vinaripoti zaidi kuhusu viongozi na msukumo umekuwa ni kutaka wananchi kuelimshwa.

Alitofautiana na mtazamo huo kwa kusema kuwa viongozi nao wanahitaji kujifunza kwa wananchi.

Aliendelea kuwa inaelekea vyombo vya habari vina woga na kwamba ule mtazamo asilia wa uandishi wa habari kuwa “mbwa anapomuuma mtu si habari bali pale mtu anapomuuma mtu ni habari” hauzingatawi katika uandishi wa habari. Alisema pia habari za utafiti na uchunguzi zinazochochea na kuamsha mawazo zimedorora.

Katika hotuba yake fupi na muhimu kwa mwelekeo wa vyombo vya habari nchini, alilisifia Baraza la Habari Tanzania kwa kuleta maendeleo makubwa kwa tasnia ya habari nchini.

Alikiri kuwa Baraza limefanya kazi kubwa na anachohimiza yeye ni maboresho zaidi.

Alisema kuwa awali kulikuwa na magazeti na vituo vichache vya vya redio na televisheni haikupwepo lakini sasa kuna vyombo vingi zaidi.

Pia alisema kuwa hakukuwa na kanuni za maadili wakati huo lakini sasa zipo zinazohusu vyombo aina mbalimbali vya habari.

Warioba aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Maadili ya MCT na hivi sasa ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, aliwakabidhi wajumbe wa Bodi mpya ya Baraza vitendea kazi ambavyo ni pamoja na Katiba ya Baraza.

Wanachama waliokuwepo katika uzinduzi wa Bodi ni pamoja na Rais mpya Jaji mstaafu Juxon Mlay na Makamu Rais Yusuf Khamis. Wengine ni Happiness Nkya, Edda Sanga, Bakari Machumu na Dk. Joyce Bazira

Wajumbe ambao hawakuwepo na kutoa udhuru ni pamoja na Tido Mhando mwenyekiti mpya wa Kamati ya Maadili, Teddy Mapunda na Anna Henga.

Hii ni Bodi ya tisa ya Baraza. Wajumbe wa Bodi hiyo walichaguliwa katika mkutano wa mwaka wa MCT uliofanyika Tanga, Septemba 28,2020.
 
Mkuu,

Katika video hizi mbili zilizoletwa hapa, hakuna sehemu ambayo wananchi wanahojiwa kutoa maoni yao kuhusu kazi zao, kuhusu hotuba ya rais.

Maana yake ni kwamba, katika sample ya videos za hili jambo zilizoletwa na mtoa mada, tunaona kuwa, kuanzia Ikulu mpaka waandishi wa habari wasio wa Ikulu wote wanamuangalia sana rais, lakini hawawaangalii wananchi wanasemaje.

Huu ni mfumo ulio "top down". Top heavy. Kila mtu anaangalia juu. Single point of failure. Tatizo kubwa sana.

Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Sinde Warioba alikuwa anapenda sana kusoma magazeti.Tulikuwa tunamuona Oysterbay kila siku asubuhi kwenye Mercedes Benz anasoma magazeti akiwa kwenye msafara wake.

Baadaye, nilikuja kusikia kutoka kwenye mahojiano yake, kumbe alikuwa ana msaidizi wake maalum wa kutazama maoni na malalamiko ya wananchi. Yule msaidizi wake alikuwa anasoma magazeti, ana highlight habari fulani, au barua za wasomaji fulani, anampatia Waziri Mkuu asome.

Mzee Warioba alisisitiza hili katika Baraza la Habari, ambalo yeye aliliongoza. Akisema kwamba, siku hizi habari zina focus sana kwa viongozi, hazi focus kwa wananchi.

Alitoa mfano kwamba, zamani dereva wake alipenda kusikiliza TBC au Radio One kwenye gari, siku hizi dereva wake akabadili channel, kupeleka Deutschewelle. Kwa sababu ya coverage yao.

Hili ni tatizo kubwa sana Tanzania. Rais akipiga chafya tu ni habari inakuwa covered mpaka leso aliyotumia kujifuta mtaijua, ila wananchi wana matatizo mengi sana hayapati press. Makonda pamoja na mapungufu yake mengi, ziara zake angalau zimeibua madudu mengi mpaka Mwanasheria Mkuu wa serikali anasema ameshtushwa na madudu mengi haya.

Ina maana Mwanasheria Mkuu wa serikali kalala siku zote?

Ina maana waandishi wa habari wamelala siku zote mpaka mambo yanaibuka kwenye ziara za Makonda?
Umakini wa watu wetu wa habari ni muhimu sana kwa kila hatua ya nchi...Ikiwemo Raisi...

Budi zipo juu ya nini kinaendelea huko ndani...lakini usalama wa Taaisi uwe wa kwanza...hakuna sababu ya kila hatua kuwa wazi...hasa za kiulinzi

Uwazi wa mambo ya ndani hata kama kwa bahati mbaya ni changamoto ya kiuslama wa Rais ukiwa wazi...ama uchi...

Sbababu hatua zinajulikana...na hatua ni muhimu kwenye ulinzi wake
 
Hili tukio si jepesi kwa leo ila lina gharama sana kesho sababu...kesho yetu ni raini sana kiutekelezaji wa uharifu😊

Camera ni jicho na jicho ni haramu kama tu litaona na kuonesha vitu ambavyo si rafiki kiusalama.
 
Pia habari hii ya Jaji Warioba iliandikwa na Mwanahalisi.

Wepesi wetu wa kuaminiana na undugu kitaifa ndiyo hatari ya kesho yetu ambayo ina maswali magumu na isiyo tingishika...

Matukio ya leo ya viongozi wa juu yanapasa kuilinda kesho ya nchi yetu na siyo kesho yao. ....

Matumizi ya camera au jicho la kidigitali ni muhimu sana kwa taasisi kubwa kama raisi....
 
Umakini wa watu wetu wa habari ni muhimu sana kwa kila hatua ya nchi...Ikiwemo Raisi...

Budi zipo juu ya nini kinaendelea huko ndani...lakini usalama wa Taaisi uwe wa kwanza...hakuna sababu ya kila hatua kuwa wazi...hasa za kiulinzi

Uwazi wa mambo ya ndani hata kama kwa bahati mbaya ni changamoto ya kiuslama wa Rais ukiwa wazi...ama uchi...

Sbababu hatua zinajulikana...na hatua ni muhimu kwenye ulinzi wake
Mimi mpaka sasa hivi, ukiondoa objection yangu kwamba media ina cover sana habari za rais kuliko za wananchi, sijawaelewa mnachoilalamikia media katika hii coverage ni kipi.

Sijawaelewa.

Na pengine tuna tofauti za kifalsafa.

Mnachoilalamikia media ni nini? Mnataka media ifanye self censorship?

Kama kuna itifaki za coverage zimevunjwa, hamuoni kuwa hilo ni kosa la watu wa Ofisi ya Rais kuto limit coverage inavyotakiwa? Media iko pale ku cover habari, mlitaka ifanye self censorship?

Unaelewa kwamba kama kuna weakness, hata usipo ionesha hiyo weakness itakuwapo tu?

Unaelewa kwamba, kama kuna weakness, inawezekana ikawa vizuri zaidi kuionesha hiyo weakness, ili irekebishwe, kuliko kuacha kuionesha na kufanya iendelee kuwepo?

Naona kama bado tunafanya kosa lile lile la kutaka kufanya Ofisi ya Rais haina makosa, na ikifanya makosa tuyafiche tusiyaoneshe, badala ya kujikita kwenye kuyajua makosa vizuri ili tuyabadilishe.

By the way, kama kuna makosa maadui wanataka kuyajua, maadui wakubwa waliojipanga hawatategemea video za mitandaoni kuyajua, watakuwa na sources za muhimu kabisa zinazoweza kuyajua vizuri.

Sasa, kwa nini mnajikita kuwasema wanahabari wanaotuonesha tu mambo yalivyo, badala ya kujikita kwenye kubadilisha mambo, kama kuna cha kubadilisha?
 
Wepesi wetu wa kuaminiana na undugu kitaifa ndiyo hatari ya kesho yetu ambayo ina maswali magumu na isiyo tingishika...

Matukio ya leo ya viongozi wa juu yanapasa kuilinda kesho ya nchi yetu na siyo kesho yao. ....

Matumizi ya camera au jicho la kidigitali ni muhimu sana kwa taasisi kubwa kama raisi....

If at all the event is worth covering, then muandishi wa habari akiacha ku cover habari mimi naona ndiyo kosa.

Unless rais kaanguka chini kabaki uchi, kwingine kote ni fair game.

Na kama si fair game, ni wajibu wa Ofisi ya Rais kutoa muongozo.

Kama Ofisi ya Rais imeshindwa kutoa muongozo, hapo kosa ni la Ofisi ya Rais, si la waandishi wa habari.
 
Nadhani jambo sahihi ni kukaa kimya na kusubiri wajati

If at all the event is worth covering, then muandishi wa habari akiacha ku cover habari mimi naona ndiyo kosa.

Unless rais kaanguka chini kabaki uchi, kwingine kote ni fair game.

Na kama si fair game, ni wajibu wa Ofisi ya Rais kutoa muongozo.

Kama Ofisi ya Rais imeshindwa kutoa muongozo, hapo kosa ni la Ofisi ya Rais, si la waandishi wa habari.
Kiutendaji wa kiuslama kiongozi au vyovyote....Je si busara baadahi ya picha hasa za maeneo nyeti kama haya yakimaandalizi ziruke kupitia ofisi ya Rais media na si vyombo binafsi?Nikiwa na maana taarifa za awali za picha za michakato ya kiitelejensia zisiruke kupitia vyombo binafsi????

Kama unajua haya mambo utaona ni namna gani hiyo video ya kampuni binafsi imaweka mambo ya uslama wa Rais wazi....

Yani nilikua nawaza tu...sababu kwa video binafsi nimkama inajaribu kunifundisha au kunielezea kitu...hicho kitu kama nitakujua itakua hatari kwa raiasi wangu??????
 
Hapana,

Unachotaka kufanya hapo kupeleka videos zipitiwe na Ikulu ni censorship kubwa sana ambayo dunia ya leo imeshaondoka huko.

Unaturudisha kwenye dunia ya kifalme au ya kikomunisti ambayo huwezi kusema chochote mpaka kipitishwe na mfalme au kiongozi mkuu na wapambe wake.

Ufalme wa Uingereza ulikuwa na mtindo huu wa kuweka kitu kinaitwa "embargo" kwenye habari za kuhusu familia ya kifalme. Utamaduni huu kwa kiasi kikubwa sana umeshindwa.

Dunia ya leo ya teknolojia na uwazi haitaki embargoes. Utazuia waandishi raia watapiga picha za cellphone na ku share online.

That is some Orwellian 1984 stuff.

Kitu ambacho kinaweza kufanyika katika dunia ya leo ya uwazi ni kuwepo kwa miongozo maalum ya kiusalama kutoka Ofisi ya Rais. Na miongozo hiyo pia inatakiwa isiminye uhuru wa wanahabari kutoa habari, maana yake inatakiwa kuwa na security justification za kimantiki.

Ndiyo maana nawauliza, kama kuna makosa yamefanyika hapa, hamuoni kwamba makosa ni ya watu wa Ofisi ya Rais hao wanaosemezana kama mambo yote yako bien, wakati waandishi wa habari wana cover kitu nyeti?

Hivi nyie hamjaweza kufikiri kwamba labda Ofisi ya Rais ndiyo inataka kuwaonesha watu kuwa Rais wa Tanzania si mtu wa mchezo mchezo anatembea na wanajeshi wa kutosha na kutisha wakimlinda?

Kuna mtu kaweka video ya msafara wa rais wa Marekani hapo juu.

Novemba 22 1963 Wamarekani walipata pigo kubwa la kuuawa rais John F. Kennedy. Rais Kennedy alikuwa anasafiri katika gari lililo wazi Dallas Texas, akapigwa risasi. Ilibidi wanausalama wa Marekani wakae chini wabadili itifaki zao za usalama.

Walichobadili ni itifaki za usalama, kama vile ku limit rais kupanda gari lililo wazi, kuongeza usalama katika gari la rais, etc.

Hawakusema kwamba tatizo ni wanahabari wamepiga picha sana msafara wa rais, tukataze wanahabari kupiga picha msafara wa rais.

In fact, wangependa zaidi kama kungekuwa nanwaandishi wa habari waliopiga picha na video tukio lile kwa karibu, iki wajifunze. Bahati mbaya kulikuwa na video moja tu ya Zapata iliyokuwa imepiga pichabkwa karibu.

Hapo utaona tunahitaji media coverage zaidi, hatuhitaji kuficha zaidi. Media coverage ndiyo itakayoanika mapungufu na kutufundisha cha kubadili.

Kuna wimbo mmoja wa Bongo Hip Hop, mstari mmoja wa Fid Q anaukiza, ukiangalia kioo na kuona kuwa sura unayoiona haikupendezi, utakichukia kioo kwa kukuonesha ulivyo mbaya au utakioenda kioo kwa kukuonesha ukweli wa mambo? I am paraphrasing his words, Fid Q said it better.

Sasa, hapa hamuoninkwamba wanahabari ni kioo tu cha jamii, na kama hatupendi sura mbaya tunayoiona kwenye kioo, hilo si kosa la kioo, inatubidi tubadilike sisi wenyewe?

Ukikataza wanahabari kupiga video msafara wa rais, unaweza kuishia kulificha tatizo badala ya kulitatua tatizo.

Kwa nini hatuelewi hilo?
 
Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema kwa hali ya sasa vyombo vya habari vinaripoti zaidi kuhusu viongozi na msukumo umekuwa ni kutaka wananchi kuelimshwa.

Ni kweli mfano habari hii ya wananchi wa Geita haieleweki wanazungumzia jambo gani mbali ya utitiri wa viongozi kuzungumza ktk clip hii. Inaonesha zile 5W + H1 za uandishi, mahojiano au upashanaji habari n.k hazizigatiwi labda kwa habari za udaku vitu vingi vya ndani ndiyo huanikwa

TOKA MAKTABA
Mlipuko wa moshi na matope Geita Tanzania 30 January 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=B2QgKLU4uUg
 
Back
Top Bottom