Maridhiano kati ya DC Simalenga na waandishi wa habari wa Simiyu yagonga mwamba

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
KLABU ya Waandishi wa habari mkoa wa Simiyu(SMPC)imeshindwa kufikia maridhiano na Mkuu wa wilaya ya Bariadi,Saimon Simalenga baada ya Dc huyo kukataa kukiri kosa la kuwadhalilisha Waandishi wa habari kwenye kikao cha DCC kwa kuwafukuza licha ya Waandishi hao kuwa na mwaliko wa kuhudhuria kikao hicho

Katika kikao Kilichofanyika Jana Machi 9,2024 katika Ukumbi wa hotel ya Mlashi mjini Bariadi chini ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Dkt Yahaya Nawanda na kuhudhuria na Rais wa Umoja wa KLABU za Waandishi wa habari Tanzania(UTPC)Deogratias Nsokolo,Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC,Kenneth Simbeye na Mwakilishi wa Msemaji wa Serikali,Zamaradi Kawawa.

Waandishi wa habari walimtaka Dc Simalenga kuomba radhi lakini alikataa na hivyo Waandishi wa habari nao kubaki na msimamo wao wa kutoshirikiana na Dc huyo kwa namba yoyote Ile.

Licha ya Rc Simiyu na Mwakilishi wa Msemaji wa Serikali kutumia lugha za vitisho kuwatisha Waandishi wa habari lakini hawakulegeza msimamo wao na kumsema waziwazi Dc huyo kutokana na matendo yake hata ya nyuma ikiwa ni pamoja na kuwatisha baadhi ya Waandishi wa habari kuwa atawashughulikia.

Waandishi hao walikuwa na Mkutano wao mkuu wa kawaida hivyo walifanya maandalizi ya Mkutano huo pamoja na chakula lakini cha kushangaza Dc huyo alikutana na baadhi ya Viongozi wa SMPC akiwemo MKT wa SMPC,Frank Kasamwa na kuwaeleza kuwa atagharamia chakula cha wajumbe 15 waliohudhuria Mkutano huo kwa gharama ya Sh 210,000/-ambazo alizituma kwa Mratibu wa SMPC,Paul Faustine bila kuwashirikisha Waandishi wa habari.

Waandishi wa habari walipopewa taarifa hiyo waliutaka Uongozi wao wa SMPC kuzirejesha mara moja fedha hizo kwa Dc Simalenga na kumuonya Mkt huyo kuacha masuala ya usaliti kwani tayari chakula cha Mkutano Mkuu wa SMPC kilikuwa kimelipiwa na michango ya Waandishi hao.

Mkutano huo ulimchagua Samira Yusuph kuwa Katibu wa SMPC kuziba nafasi ya Happy Severine aliyefariki Dunia mwishoni mwa mwaka 2023.
 
Huyo DC mpuuzi sana. Kinachoshangaza ni kuwa yeye mwenyewe alikuwa mwajiriwa wa Clouds kwa miaka mingi.
 
Laki mbili zikalipwa ili kulegeza mioyo ya waandishi hapa natata picha hii tasnia ya habari haina mpunga mrefu
 
Huyo DC mpuuzi sana. Kinachoshangaza ni kuwa yeye mwenyewe alikuwa mwajiriwa wa Clouds kwa miaka mingi.
Ndiyo wale waandishi wanaoitwa Makanjanja... Siku hizi media, hasa hizi za miaka hii, hazizingatii weledi wala taaluma ndiyo maana unakuta Masanja mkandamizaji, Kingwendu nk eti ni watangazaji...
 
Ndiyo wale waandishi wanaoitwa Makanjanja... Siku hizi media, hasa hizi za miaka hii, hazizingatii weledi wala taaluma ndiyo maana unakuta Masanja mkandamizaji, Kingwendu nk eti ni watangazaji...
Umeandika ushuzi
 
Kuna kila dalili waandishi wa habari kujipendekeza kwa DC, kuna haja gani ya kuhangaika na huyo DC
 
KumlazImisha mtu mzima kuomba radhi ni ujinga, hata ningekuwa Mimi siwezi kuomba radhi
 
Back
Top Bottom