Mwaka 2023 vimerekodiwa vitendo vingi zaidi vinavyozuia upatikanaji wa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuliko miaka 3 nyuma

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Baraza la Habari Tanzania (MCT) liliungana na Dunia katika kuadhimisha siku ya kukomesha na kuondosha kabisa vitendo vya ukatili dhidi ya waandishi wa habari (International Day to End Impunity for Crimes Against Journalists).

Kila mwaka siku hii imekuwa ikiadhimishwa kutokana na vitendo vinavyoenea katika nchi mbalimbali duniani. Katika kila sehemu bado waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kupoteza maisha wakati wa kutekeleza kazi zao.

Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu, MCT kupitia kanzidata yake limerekodi madhila 21 ya waandishi kufanyiwa vitendo ama vinavyozuia kupata taarifa au vinavyofanya aogope kutimiza majukumu yake kama mwandishi wa habari.

Madhila hayo ni pamoja na kunyimwa taarifa ya matukio (8), vitisho (5), kukamatwa (3), mashambulizi (2), na udhalilishaji (3).

Mwaka huu matukio ya kunyimwa taarifa yamekuwa mengi zaidi ukilinganisha na miaka mitatu iliyipita, ambapo kwa ujumla wake yalikuwa matukio 9 huku matukio mengi zaidi (4) kurekodiwa mkwaka 2021.

MCT imetoa wito kwa serikali kuweka mazingira rafiki ya utendaji kazi kwa waandishi wa habari, kuwachukulia hatua wote wanaokwamisha waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao pamoja na kusimamia suala la upatikanaji taarifa kwa haraka na kwa usahihi.

Imetoa wito pia kwa waandishi wa habari kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kufata maadili na miongozo ya uandishi wa habari, kuchukua tahadhari hasa ya mabadiliko ya teknolojia ili kuepukana na taarifa za uongo pamoja na kuendelea kuomba taarifa kwa kufata mujibu wa sheria.

MCT pia imeitaka jamii kuomba taarifa mbalimbali katika maeneo yao ili kupata haki zao na pale wanaponyimwa taarifa wasisite kuripoti katika taasisi husika.
 

Attachments

  • mct.pdf
    1.4 MB · Views: 1
  • mctt.pdf
    80.4 KB · Views: 2
Mbona vichache sana? Kila siku watu wa serikalini wakihojiwa utasikia "nipo nje ya ofisi siwezi kuliongelea hilo"
 
Back
Top Bottom