Waafrika ndivyo tulivyo?

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,422
2,000
Ndio tatizo hilo la kutoijua jamii yako, matokeo yake ni kutojitambua na kukosa mwelekeo- kama upo Dar tembelea barabara ya Ally Bin Said utaona Mbuyu wa Tambiko la Wabantu. Nchi hii haiwezi kujinusuru bila kuondoa kasumba za kikoloni - kasome mada ya Toba ya Mkapa kuhusu matokeo hasi ya Ubinafsishaji na Ugenisishaji!

Naomba tuwekee hiyo mada ya Toba ili tuisome. Nadhani sijakuelewa vizuri unaposema tukatambike, naomba nieleweshe kidogo. Lakini kama tabiko ni huko kutoa sadaka kwa mizimu - Unachinja myama, unaweka nyama sehemu fulani ati Babu/Bibi ale, na unapoondoka Mbwa/paka/kunguru au kitu kingine chochote kinapita na kula zile nyama unasema babu/Bibi amekula, mambo hayo yamepitwa na wakati.
Tutafute tatizo na shuluisho la matatizo na si vingineyo.
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,648
2,000
Ndio mkuu kutambika lazima, tena kwa kuwatoa kafara wale wote walioiingiza nchi katika mikataba feki na mafisadi kwa ujumla.
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,552
2,000
Mkuu,

hayo matambiko unayoyazungumzia ni sehemu ya laana tuliyo nayo sisi miafrika! kwani wanaoua maalbino wameiga kwa wazungu?

by the way ujamaa wenyewe tumedesa...
 
K4jolly

JF-Expert Member
May 21, 2009
366
0
Catoon imenichekesha, mmoja tu ndo sijamfahamu.

Wale mababu wa kutambika tiyari wameshakufa zamani. Waliopo sasa hivi hawana tena nguvu kwani wamekiuka mila.

Sasa hivi dini (kuokoka) ndo kunatawala. Karibu pale Ubungo Ufufuo na Uzima.
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,600
2,000
Naomba tuwekee hiyo mada ya Toba ili tuisome. Nadhani sijakuelewa vizuri unaposema tukatambike, naomba nieleweshe kidogo. Lakini kama tabiko ni huko kutoa sadaka kwa mizimu - Unachinja myama, unaweka nyama sehemu fulani ati Babu/Bibi ale, na unapoondoka Mbwa/paka/kunguru au kitu kingine chochote kinapita na kula zile nyama unasema babu/Bibi amekula, mambo hayo yamepitwa na wakati.
Tutafute tatizo na shuluisho la matatizo na si vingineyo.

Haya tunayoyafanya sasa hivi ya kuabudu uzungu ndio kwenda na wakati?
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,600
2,000
Catoon imenichekesha, mmoja tu ndo sijamfahamu.

Wale mababu wa kutambika tiyari wameshakufa zamani. Waliopo sasa hivi hawana tena nguvu kwani wamekiuka mila.

Sasa hivi dini (kuokoka) ndo kunatawala. Karibu pale Ubungo Ufufuo na Uzima.

Wokovu hivi sasa ni biashara, ni tofauti kabisa na ile Injili ya Masihi aliyekuwa hana makuu - ndio maana Marx alisema dini ni kileo cha Umma, ni umaskini na ulimbukeni wetu tu huu unaotufanya tukeshe tunacheza mayenu kanisani wakati tunajua kabisa mayenu yanachezwa kwenye kumbi za starehe!
 
Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,536
2,000
Likuvi, Linyangasa, Likatavi utupage Mvula, ....... utupage na mansundonsundo.....

Mlungu wa Kisa na kigongo, tulikulomba guku utudegelekage.

..... Ehhh nimesahau unga nyumbani.... kuna mtu anao aniazime ninyunyizie?

NB: Mie nimeshatambika kwa Kikimbu/Kivemba/Kinyamwezi.
 
Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,422
2,000
Haya tunayoyafanya sasa hivi ya kuabudu uzungu ndio kwenda na wakati?

Mbona huelekei? Ninacho sema ni kutafuta shuluisho la matatizo tuliyonayo hasa kuwa na viongozi wabovu wasiojali maslahi ya wananch bali matumbo yao.TAMBIKO haliwezi kuondoa matatizo hayo. KAma wewe unaabudu wazungu, unatatizo pia, na ndo maana badala ya kutafuta jinsi ya matatizo yanayoletwa na mikataba mibovu, wewe unashauri matambiko.
Wazungu kama wazungu wanamambo mengi wamefanya ambayo si vibaya kuyaiga, na yale ambayo hayanatija, tuyaache. Ninauhakika kabisa 90% ya maisha yako au mambo unaya fanya kunamchango mkubwa wa wazungu, mfano nguo ulizovaa,magari unayoutumia,simu,redio,tv n.k. yametokana na wazungu.
 
Unaonekana hujui maana ya tambiko. Unadhani watu walikuwa watambika kama misukule isiyofikiri. Huo ulikuwa ni muda maalum (solemn) wa kukutana, kujihoji na kujadili matatizo ya jamii na kuyatafutia ufumbuzi wa pamoja. Ndio maana nasema uzungu umewapumbaza hata hamjitambua wala kuijui jamii yenu. Alafu mnataka kuleta mabadiliko ya msichokijua. Endeleeni kuiga huo uzungu bila muktadha muone kama mtaendelea kama wazungu.
 
Eqlypz

JF-Expert Member
May 24, 2009
4,065
0
Hawa ndio viongozi wetu!!

A Ugandan government official says the bodies of those who die because of drinking a local illicit gin should be caned six times before burial as an example to the living.

Edwin Komakech spoke Saturday at a security meeting in the Amuru district about 217 miles (350 kilometers) north of Uganda's capital.
Some who make the local gin, called waragi, have begun distilling it with poisonous methanol. Last week, police said they would launch an investigation into the making of the illicit waragi.
Over 50 people have died in the last two months in Uganda from drinking the poisonous gin.

In Uganda, the bodies of those who commit suicide are also caned as a form of dishonor and to warn against such behavior for the living.
 
Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,600
2,000
Willey Lynch: "In my bag here, I have a foolproof method for controlling your Black slaves.I guarantee every one of you that if it is installed correctly, it will control the slaves for at least 300 years. My method is simple. Any member of your family or your overseer can use it. I have outlined a number of DIFFERENCES among the slaves, and I take these differences and make them bigger. I use FEAR, DISTRUST, and ENVY for control purposes.These methods have worked on my modest plantation in the West Indies and it will work throughout the South. Take this simple little list of differences, and and thinhink about them."

Read more in the attachment
 
Attachments

  • File size
    603 KB
    Views
    236

lukule2009

Senior Member
Sep 23, 2009
132
0
Unaonekana hujui maana ya tambiko. Unadhani watu walikuwa watambika kama misukule isiyofikiri. Huo ulikuwa ni muda maalum (solemn) wa kukutana, kujihoji na kujadili matatizo ya jamii na kuyatafutia ufumbuzi wa pamoja. Ndio maana nasema uzungu umewapumbaza hata hamjitambua wala kuijui jamii yenu. Alafu mnataka kuleta mabadiliko ya msichokijua. Endeleeni kuiga huo uzungu bila muktadha muone kama mtaendelea kama wazungu.

I support you... by the way hatat hao wazungu wenyewe wanatambika kwa wazee wao.. ukibisha soma history.

Kujidharau asili yako ni utumwa mkunbwa kabisa wa akili ...watu watakuheshimu wakijua unajijua wewe ni nani badala ya kuwashabikia wao .. .. hatat wao watakushangaa.. kudharau vyako kukweza vyao ...,(namjibu huyo aliyetangulia)
 
Iselamagazi

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,180
2,000
Huyu bwana Bundala alikuwa Mwenyekiti wa Engineers Registration Board wakati akiwa ana somea Ph.D. yake pale Mlimani; ni mtu makini na ana akili sana. Je sasa hivi ana madaraka gani katika serikali ya Tanzania?. Utashangaa kuwa watu wenye akili kama Bundala hawawezi kuwa na madaraka katika serikali ya TZ ila vilaza wenye Ph.D. na digrii nyingine za kununua ndio wanapewa madaraka makubwa.

Kaaazi kweli kweli!
Siku hizi watu wanaangalia mahusiano na urafiki wala si CV!
 
gairo

Member
Apr 21, 2014
40
95
Waafrika ni mataka wa wazungu,waamerika na sasa wachina ,wamekubali ku gumballs wa na kukubali kutotumia akili zao,uongozi Wote wa afrika hucheza ngoma wasioijua,bahati mbaya hata kwenye dini zetu wanatapeli
 
armi

Senior Member
Aug 11, 2014
140
0
"Meeeen we are black in colour and black in mind too"
"Ndo 2livyo"
.made in mby city.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom