Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
UTAJIRI WA NCHI NI AKILI ZA WATU, SIO RASILIMALI KAMA MADINI N.K.
Anaandika, Robert Heriel.
Huwaga namshangaa mtu anayesema nchi yetu ni Tajiri. Kwa kweli sio tuu anachekesha Bali pia anaonyesha jinsi alivyokuwa mjinga na asiyeweza kufikiri sawia.
Kama nikiulizwa hivi leo sababu gani inatufanya Waafrika ikiwemo nchi yetu kuwa Masikini, basi jibu litakuwa ni kuwa Sisi tunaakili ndogo Kama sio kuwa hatuna Kabisa.
Taifa ili kiwe Tajiri linahitaji watu wenye akili zaidi kuliko Rasilimali. Utajiri ni Akili na sio wingi wa Rasilimali.
Kuna msemo usemao, penye miti hapana wajenzi.
Akili ndio inaweza kufanya madini kuwa Rasilimali Kwa kuipa Value. Madini kama madini hayajui kama yenyewe ni yathamani, Ila wenye akili ndio wanajua thamani ya madini hayo kutokana na matumizi waliyoyabuni kwayo.
Kidunia Bara la Afrika ndilo bara lenye malighafi nyingi kuliko bara lolote lile. Lakini watu wake wameshindwa kuzigeuza malighafi hizo kuwa Rasilimali Kwa kuzipa thamani.
Ukisikia mtu anakuambia Yeye ni Tajiri Kwa sababu nchi yake inamadini, maziwa na Mito, Ardhi yenye Rutuba, wanyama wa kuvutia, na mambo mengine lakini watu wake ni Hali zao za maisha ni duni jua mtu huyo hajui kufikiri vizuri, na pengine akawa mwendawazimu.
Nchi haiwezi kuwa Tajiri Kama ndani yake inawatu wajinga wengi. Watu wasio na akili wakiwa wengi ndivyo nchi inavyozidi kuwa Masikini.
Mtu asiye na akili Hana tofauti na mnyama wa porini, ni Sawa na tumbili au ngedere anayeishi msituni ananyeshewa mvua na kuchomwa na Jua lakini anashindwa kujenga nyumba hata ya mbao Kwa sababu ya upeo mdogo wa Akili.
Wazungu walivyotuita Waafrika manyani kuna watu walifikiri walimaanisha maumbile yetu yanafanana na nyani😀😀 Kama nawe ulifikiri hivyo basi nawe upo kundi la watu wajinga.
Wazungu walituita manyani mbali na ubaguzi wao lakini walituona akili zetu hazijaachana Sana na tumbili na nduguye ngedere.
Nyani au ngedere ukimpelekea Dhahabu au Almasi wala hataiona inatofauti na jiwe jingine. Kutokana na upeo mdogo wa Akili.
Sisi Watanzania wengi wetu tunaakili ndogo mno na hiyo ndio sababu Sisi sio matajiri. Na tutaendelea kuwa Vivi hivi Kwa Karne kadhaa zijazo.
Watanzania wengi ni Kama wanyama Kwa mambo mengi, kama unavyomuona ng'ombe basi ndivyo wengi wetu tulivyo.
Sio ajabu ukakuta watu kwenye makazi Yao kuna mavi au maji machafu waliyoyasababisha yamewazunguka, yananuka na nzi wamejaa lakini wao hawaoni Shida. Wanalala, wanakula hapohapo, na wanakunya na kukojoa hapohapo.
Hapo ati wanasubiri kiongozi aje awaambie wawe wasafi tena wengine ifikie hatua ya kupelekwa serikali za mitaa kisa anaambiwa asizibue chemba za mavi yake na familia yake, come on!
Sio ajabu jitu linakunya chooni labda cha umma alafu hali-flash uchafu wake. Hivi mtu huyo anatofauti ipi na Mnyama?
Mtu anajua kabisa ili aishi anatakiwa awe na chakula cha kutosha kinachomtosha yeye na familia yake, badala awe na ghala la kuhifadhi chakula kinachomtosha yeye na watoto wake angalau Kwa miaka miwili kulingana na Hali ya hewa.
Yeye anakula Kama mnyama asijue kesho atakula nini. Halafu ikifika kesho anaanza kumlalamikia mtu mwingine labda ni serikali au viongozi. Jamani hivi tunaakili kweli?
Tena wakati mwingine tunazidiwa akili hata na Wanyama.
Hakuna mnyama ambaye atazaa watoto ambao hawezi Kuwatunza. Hakuna na hajawahi kutokea. Mfano Kuku anaouwezo wa kutaga mayai hata Mia moja.
Lakini atataga mayai kumi (10-12) kulingana na uwezo wake wakuyaatamia, sio atage mayai 20 alafu wakati wa kuatamia mengine ashindwe kuyaatamia yajitokeze nje.
Kisha Kwa mayai 10-12 anaouwezo wa kuwachunga na kuwakuza watoto hao.
Halikadhalika na mbwa, ng"'ombe, mbuzi, Simba n.k.
Lakini Sisi unakuta mtu anazaa watoto nje ya uwezo wake wa Kuwatunza, labda watoto 10 alafu ananilaumu serikali kuwa gharama za Shule au hospitali ziondolewe.
Au anaomba msaada Kabisa wa kusaidiwa kulelewa watoto.
Hivi tumelogwa au ni kitu gani?
Mtu unajua kabisa miti ndio huleta hewa Safi, huleta mvua na kivuli kizuri, na Kupunguza joto la nchi. Alafu unakuta watu wamekata miti mtaa mzima ili wajenge nyumba.
Unashangaa mtaa mzima miti ipo 20 Kwa eneo la kilometa moja. Alafu muda huohuo unasikia mwehu akipiga kelele jamani joto Kali, jamani jua linawaka! Mara kiyama kinakaribia.
Kiama ya mavi. Ujinga na wehu wako ndio unaita Kiyama?
Utajiri WA nchi ni akili za watu na sio Rasilimali Kama madini.
Chakufanya;
I. Tujifunze kuwa na Akili ili tuwe nchi yetu itajirike.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam