Waafrika ndivyo tulivyo?

Radio Butiama

Member
Aug 27, 2006
21
4
Bara la Afrika lina kila kitu kuanzia ardhi kubwa yenye rutuba, maziwa makubwa, mito, madini, mazao na mbuga za wanyama. Vilevile bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa na inasemekana binadamu wa kwanza aliishi Afrika.

Ingawaje Afrika inaongoza kwa kupewa misaada lakini ni bara linaloshika nafasi ya mwisho kwenye masuala mengi ya maendeleo? Je tatizo la waafrika ni nini? Ni vitu gani waafrika wanafaa kuvifanya ili kujikomboa? Je Waafrika Ndivyo Walivyo?

Dr. Malima Bundara mwandishi wa kitabu cha "Waafrika Ndivyo Walivyo?" anaelezea zaidi. Sikiliza.

Code:
http://butiama.podomatic.com/enclosure/2006-11-12T03_19_04-08_00.mp3
 
Bwana Deus Hongera sana, kwakweli redio yako inazidi kuvutia siku hadi siku. endelea kujitahidi na moyo huo, tutafika mbali na redio hii.
 
Bwana Deus Hongera sana Mzee!! Radio yako imekuwa sehemu muhimu ya kupata mafunzo, Leo hii nimejifunza misamiati mipya kutoka kwa Dr.Bundara, misamiati muhimu na ameitumia mahali panapostahilli, misamiati hiyo ni "subjectivity na objectivity".

Mahojiano yako na Dr Bundala yananipa moyo kuona kuwa tuna watanzania wasomi, wakereketwa na wachambuzi wa mambo wanaofuatilia kwa karibu mwendo wa nchi yetu! Tuwatumie hawa kwani ni rasilimali muhimu kwenye ujenzi wa Taifa hili Gonjwa (Tuna miaka 45 lakini bado tunatambaa).

Nitakutafuta kwa simu ili nipate copy ya hicho kitabu!
 
Huyu bwana Bundala alikuwa Mwenyekiti wa Engineers Registration Board wakati akiwa ana somea Ph.D. yake pale Mlimani, ni mtu makini na ana akili sana.

Je sasa hivi ana madaraka gani katika serikali ya Tanzania?. Utashangaa kuwa watu wenye akili kama Bundala hawawezi kuwa na madaraka katika serikali ya TZ ila vilaza wenye Ph.D na digrii nyingine za kununua ndio wanapewa madaraka makubwa.
 
Shukran kwa wote mliokuja kusikiliza mahojiano yangu na Dr. Bundara.Kweli Dr. Bundara ni mmoja wa watu walio makini sana na ni hazina kubwa san akwenye nchi yetu.Niliposoma tu kitabu chake nilisema lazma nimtafute na siku moja nije hata kuongea nae.

Mwawado,
Nitafute kama unahitaji hiko kitabu.Niandikie e mail kwenye butiama@podomatic.com au nitafute kwenye simu.
 
Hamna tatizo.Nitapata hivi vitabu toka Dar hapo November 20.Wasiliana na mie kwenye hiyo e mail na nitakutumia.
 
Naomba umuhoji na Mohamed Said ameandika kitabu kizuri sana cha harakati za uhuru. anafanya kazi bandari Tanga.
 
Radio Butiama,

Huyu msomi hakika utafikiri yupo kichwani mwangu. Isipokuwa kuna baadhi ya sehemu muhimu ambazo sikubaliani naye na pengine nitampa changamoto kama alivyokusudia.

Mimi sikufanya utafiti kama wake isipokuwa ni HALI HALISI ambayo haina uficho.

Mambo mengi sana nakubaliana naye nadhani nilishawahi kuyazungumzia kule Bsctimes na nikapigwa vita sana....na kaacha kipengele kikubwa sana ambacho najua kitazua HOJA nzito nzito!

Nitayaweka mawazo yangu hapa tukijaaliwa week ijayo maanake nipo katika msafara wa kwenda kumwona PM...
 
Jasusi,
Shukran kwa subra, nitajaribu kueleza mtazamo wangu kutoka ktk elimu yangu ya madrasa na pengine itaweza kuondoa ile question mark ya Mtaalam wetu ndugu Bundala.

UTUMWA:-
Sielewi kwa kiwango gani mheshimiwa ndugu Bundala kalifanyia swala hili utafiti lakini nimesoma mengi ambayo ni elimu ya kupandikizwa na hawa wazungu na waarabu ambao wanakataa kuwa responsible na mabaya yote waliyoyafanya kama wanavyokataa hao akina Bush, Augustino Pinochet kwa matokeo mabaya na hasa inapofikia ukiukaji wa haki za binadamu.

1.Waafrika hatukwenda utumwani kwa ridhaa yetu.

Sio kweli kabisa kuwa waafrika tulipelekwa utumwani kwa ridhaa yetu ati kwa sababu tu askari walikuwa wawili wakichukua maelfu ya wananchi.

Hapa nadhani hakutazama kuwa utawala ulikuwa wa nani? Leo hii askari wawili wanaweza funga mtaa mzima na tukawekewa sheria.. Bush na baraza lake anawapeleka askari vijana wao 150,000 kupigana Iraq na hakuna mtu anayesema ni ridhaa ya wananchi au wanajeshi.

Vita ya Vietnam haikutosha kuwa fundisho kubwa kuonyesha kuwa utawala ukitumiwa vibaya hutoa madhara ambayo si lazima wananchi wawe wameridhia na ni vizuri sana kukubali makosa yalifanyika katika process za healing. Kukataa kwao makosa ndiko kunakozidisha hizi lawama na hazitakwisha hadi hapo watakapo kiri kufanya makosa hayo.

Kuna historia nyingi sana za hawa hawa wazungu zinazoonyesha jinsi utawala wa akina Pharaoh na Warumi waliweza kutumia askari wachache sana kutawala na kuendesha biashara za utumwa bila ridhaa ya wananchi. Sijui hapa kuna tofauti gani kati ya mwafrika na mtu wa mataifa mengineyo.

Si kweli kuwa waafrika pekee yao ndio walichukuliwa utumwa isipokuwa mataifa mengi sana hasa yale yaliyotawaliwa kwa mabavu na askari haohao wachache unless tukubali kuwa hata kutawaliwa ilikuwa ridhaa ya wananchi.

2.Sii kweli kwamba maadam wananchi wanashiriki katika biashara fulani basi hakuna ukiukaji wa haki za kibinadamu

Leo hii huko Asia wanawatumia watoto wadogo kutengeneza vitu viwandani kwa mishahara midogo sana. Kumpiga mkeo ati kwa sababu bado yupo katika ndoa ni ridhaa yake kupigwa!... Kumtenga mtu mweusi kwa sababu ni yeye anayekwenda Ulaya na mengineyo mengi hayana kabisa upeo mzuri tunapotaka kulitumia neno RIDHAA hasa mahala panapotumika nguvu.

3. Wahindi, Wachina yaani wa Asia kwa ujumla walichukuliwa sana ktk ujenzi wa mabarabara na reli huko visiwa vya Carribean na Amerika ya kusini na hadi leo hii wamejaa huko tena basi nao wamepoteza lugha zao na culture kama Waamerika weusi..

Kutokana na sababu hizo hapo juu, sio kweli kuwa wahindi wekundu walikataa kuchukuliwa utumwa eti kwa madai kuwa walilala chini na kukataa kufanya kazi isipokuwa malengo ya utumwa wao hayakuwa katika kilimo. Waafrika tulichukuliwa utumwa kwa sababu ya kilimo na ndipo utakuta kuwa si waafrika wote walibebwa utumwani isipokuwa sisi wa BANTU.

Wabantu pekee ndio tulikuwa na ujuzi na kipaji ktk kilimo. Hata ukitazama ramani na njia za utumwa utakuta ni sehemu za wabantu zilizoathirika zaidi hali Wenzetu Nilotics (wavuvi) Hemitic na Nordic (wafugaji) walipeta hawana kabisa historia ya utumwa kama wetu sisi. Kwa hiyosera za kiuchumi zinazosisitiza Utambuaji wa vipaji haukuanza jana.

Tena basi watu kama Nilotics wengi walikuwa wakitumiwa kama manyapala yaani bodyguards askari kwa sababu ya ukubwa wa miili yao na utishaji wa sura zao (weusi wao). Hii inasemekana kuwa moja ya sababu zilizowafanya Wamakonde kuchanja chale ili waonekane pia wanatisha.. Kwa hiyo utumwa wa mwafrika ni utumwa katika kilimo na soko lilikuwepo kutokana na biashara ya kilimo kuwa uti wa mgongo katika maendeleo ya Marekani.

Huyo mhindi mwekundu alishindwa kulima, hakuwa na ujuzi wala kipaji hicho kwa hiyo alionekana kama mvivu asiyetaka kazi. Hiyoilichangia sana katika kutafutwa kwa watu wenye ujuzi, nguvu nakipaji cha ukulima wa mazao na Mbatu alipopatikana soko lake likapanda juu.

Waarabu, Wayahudi na Wazungu wakalivamia bara letu ktk utumwa..Kumbukeni tu ile rule ya demad na supply hutazama vipengele vingi sana ikiwa ni pamoja na quality.

Nadhani kwa leo hii imetohsa, nitaendelea na mjadala kesho... nakaribisha maoni zaidi toka kwenu pia.
 
He he!
Mmakonde alichanja chale ili aonekane anatisha sio!
teh teh!
 
Brutus,
Apparently it worked for him, au siyo? Tunasubiri Mkandara aendeleze tuition.
 
Naomba umuhoji na Mohamed Said ameandika kitabu kizuri sana cha harakati za uhuru. anafanya kazi bandari Tanga.

:rolleyes: Watafuteni free thinkers wote na muwahoji. Nchi yetu inahitaji kuzalisha watu wengi wa aina hiyo, watu wanaojua kuangalia mambo na kisha kutengeneza knowledge itakayoamsha waliolala. Jamii ni vigumu kuendelea kwa kutegemea sera na mikopo kutoka kwa mabepari. Maendeleo ya kweli sio kukusanya kodi nyingi, na kupokea mikopo na misaada ya kujenga barabara, hospitali na kupambana na njaa, bali ni evolution ya vichwa vya wanajamii. Hata siku moja mabepari hawatatupa misaada au mikopo ya kuboresha vichwa vyetu, bali hii ni kazi yetu wenyewe. Kwa vile wachawi wetu wako miongoni mwetu, na waganga halisi pia watapatikana miongoni mwetu. Hongera radiobutiama na jamboforums kwa kazi nzuri ya kupambana na wachawi wetu.:)
 
Hili linalofuata ni somo zito sana na sijui kama nitaliweza maanake sii mchezo mdogo lakini hata hivyo hapa natoa mawazo yangu toka elimu ya madrasa. Haya Bismillah!

Kama nilivyosema hapo juu ya kwamba nakubaliana sana na mheshimiwa Ndugu Bundara ktk utafiti wake ambao ameweza kugundua jinsi waafrika tulivyokuwa nyuma.

Bila shaka Hilo la FIKRA BINAFSI na FIKRA JUMUIYA nadhani ndilo linafunga hoja ya kitabu chake. - halina ubishi. Isipokuwa tu ameshindwa kuoanisha maswala haya mawili na hali halisi ktk nchi zinazo ONGOZWA na zile zinazo TAWALIWA..

Nashindwa kuungana naye anaposema kuwa Utumwa na Ukoloni haukuchangia kumfanya mwafrika kuwa - inferior kwa mzungu. Na kusema kweli nimeshangaa alipohoji kitabu cha Walter Rodney kwa kutumia misleading questions!
Kayaacha mambo haya muhimu sana ambayo yalichangia na bado hata leo hii yanadumishwa na hawa watawala ambao tunawaita viongozi. Fikra ni mbegu ambazo kuota kwake hutegemea Ardhi. Sasa basi tuitazame hiyo ardhi kwanza.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya KUONGOZA na KUTAWALA. Na sisi hutumia makosa makubwa tunapotafsiri neno kutawaliwa kama Kukoloniwa (colonized), chini ya uongozi wa walowezi. Ama watalitumia neno hili kwa ma dictator, falme n.k. lakini wote tutawaacha watawala wetu hawa ambao tunawaita viongozi wazawa wenye fikra binafsi. Kiongozi ni yule mwenye fikra jumuiya kwa hiyo tusiwaache nje viongozi kila tunajaribu kupima uwezo wetu kwa sababu bila kufanya hivyo huwezi kabisa kuona tofauti ya ukoloni na leo hii.

Kutawaliwa kulingana na hoja hii hauna rangi, uzawa, nasaba wala utashi wa mtu isipokuwa ni uongozi ulio base ktk fikra binafsi. Kiongozi mweusi mzawa anaweza kabisa kuwa mtawala sawa na mkoloni hata kama tumepata uhuru wa bendera. Dikteta au Mfalme anaweza kabisa kuwa kionmgozi ikiwa atatumia fikra jumuiya.

Na ukitazama kwa makini kila nchi iliyokuwa na UONGOZI wenye fikra jumuiya kwa muda mrefu ndizo zinazofanikiwa.

Gadaffi ni mfano mzuri na hata Nyerere anayesemwa sana kuwa alikuwa dikteta kwa maazimio yake…still alikuwa na fikra jumuiya isipokuwa sisi tulikuwa bado ktk fikra binafsi. Nakumbuka alipotangaza kuwa elimu ni LAZIMA kwa kila mtoto sio tena sunna wengi wetu tulianza kulalamika kuwa sasa tunalazimishwa hata shule jamani!..

Pia muhimu tuelewe kuwa hata hizo fikra binafsi na Fikra jumuiya kila moja yake ina mapana na marefu yake. Binafsi/Jumuiya zote mbili zinaweza kuwa na marefu ya mtu na familia yake, ukoo, nasaba,rangi, dini, gender n.k maadam tujue vitu hivi vinatengana wapi.

South Afrika ni mfano mzuri sana ingawa ndugu mheshimiwa kapindisha swala la ukoloni kutazama tu matokeo..na kaacha nje hizo fikra binafsi/jumuiya. Wakati wazungu wakitawala south walihakikisha kwamba mahitaji muhimu ktk maendeleo ya binadamu yanapewa jumuiya yao -fikra jumuiya. ELIMU, AFYA na USTAWI WA JAMII vilipatikana kwa wazungu tu -fikra binafsi.. Hata ukija tazama statistics zao utakuta zaidi ya asilimia 50 ya wazungu waliokwenda shule waliweza kupata kirahisi elimu ya juu. Kufikia mwaka 1960 nina hakika South Afrika ilikuwa na wasomi wengi kuliko hesabu ya wasomi wote bara zima la mtu mweusi. Wakati huohuo watu mweusi south walioweza kwenda juu kielimu hawakufika asilimia 1.

Kwa hiyo utaona kwamba hizo Fikra jumuiya za wazungu zilikuwa ktk zizi lao na ziliweza kufanikiwa tu kwa sababu ya KUTAWALA na sio umaskini wa mtu mweusi.

Haya baada ya huo Uhuru wa bendera hawa watawala ambao tunawaita viongozi ati kwa sababu tu tuliwachagua bado wanatunyima kile tulichopigania toka kwa wageni. ELIMU, AFYA na USTAWI wa JAMII bado ni wizara mbovu sana ktk nchi zote za kiafrika. Inferiority ya mtu mweusi imetokana na ukosefu wa vitu hivyo muhimu… Elimu, afya na ustawi wa jamii zao. Na hata leo hii mtu yeyote mwenye mapungufu hayo lazima awe inferior hata kama ni mzungu, Mchina yellow or Blue. Haihitaji rocket scientist..

Sasa basi tazama baada ya miaka 40 ya uhuru wa nchi za kiafrika bado utakuta ni asilimia chini ya 20 wanaopata nafasi ya kwenda secondary!..chini ya 10 vyuo kikuu, Afya na ustawi wa jamii hata hatuna statistics zake zaidi ya kuwasikiliza wazungu. Population inaongezeka mara 3 kila mwaka zaidi ya wenzetu na kubwa kuliko yote tuna watawala weusi. wanaofanya yaleyale ya mkoloni.. Sasa kama tunaamini elimu ndio msingi wa maendeleo hapa bado tuna question kitu gani!.

Ukikataa kuwa Ukoloni (kutawaliwa) haukutufanya tuwe nyuma ni sawa kabisa na kusema hukubali leo hi tunatawaliwa. Unless tunatumia neno uhuru kama freedom ama kuna tafsiri nyingine zaidi ya neno UHURU which means INDEPENDENCE.

Wakati wa Ukoloni tulitawaliwa na sasa hivi bara Afrika bado linatawaliwa tofauti yake ni rangi ya ngozi tu. Kawataja Nkurumah na Nyerere na kawapa sifa zao kwa sababu watu hawa hawakuwa Watawala bali viongozi wenye fikra jumuiya..Wengine waliobaki ndio hao watawala wenye kuvaa ngozi ya kondoo (viongozi) na fikra zao ni binafsi.

Ukija kwa waafrika kwa ujumla, nakubaliana sana na ndugu Bundara kuwa sisi tupo inferior ktk fikra zetu kwa sababu ya mapana ya hizo fikra.. Fikra Binafsi huwa zina malengo mafupi sana yaani short term, hali fikra jumuiya huwa zina malengo ya mbele - long term. Hivyo, sisi waafrika hiyo inferiority yetu imetokana na kutokuwa na malengo ya mbele ambayo chimbuko lake lime/lina tokana na kutawaliwa. Watu kama Nyerere na Nkurumah wameshindwa kueleweka wakati wa uhai wao kwa sababu walikuwa wakiongoza wananchi wenye Fikra binafsi with short term goals. Na ndio maana hadi leo hii tunashindwa kabisa kuelewa Nyerere alikuwa na malengo gani kwa sababu sisi wenyewe hadi leo hii bado tunafikiria short term goals chini ya kutawaliwa! Mtawala bora ni yule anayetupa short term goals.

Kutokana na hizo fikra binafsi ndio maana leo hii watu hawana imani na rais anayetoka jumuiya nyingine (i.e Muislaam/Mkristu) kwa sababu subconsciously hatutegemei kabisa kumpata KIONGOZI isipokuwa MTAWALA.

Nadhani jibu rahisi la hoja yake ambayo inauliza:- Mbona ukoloni umekwisha miaka kibao lakini hatujaendelea?.. Na kaitumia hoja hiyo hiyo hata kuhoji kitabu cha Walter Rodney hali huko mbele alipoanza kuongelea viongozi kasema vizuri kuhusu hawa viongozi wetu wa leo…yaani bado tunatawaliwa.

Viongozi wengi wa Afrika bado ni Watawala sio viongozi weyu na wamejaa Fikra binafsi. Hizi sababu muhimu sana kwa sababu uhuru tuliokuwa nao ni ule wa bendera lakini hadi leo wananchi wa kiafrika ndani ya nchi zao huru bado hawana uwezo wa kuwa huru – KUJITEGEMEA (independence). Mahitaji muhimu kama ELIMU na huduma za USTAWI WA JAMII ni almost zero…

Naomba maoni yenu na mtazamo wenu kwani lugha hii nzito sana na kama mjuavyo mimi sii mwandishi mzuri kabisa.
 
Mkandara,
Umeandika vizuri tu. Umeeleweka na kutoa darasa safi kabisa.Niliwahi kumwuliza Mwalimu Nyerere ni kwa nini kizazi chake kilitoa viongozi wazuri kama yeye, Nkrumah, Mandela( ingawa alikuwa jela lakini age wise ni kizazi kile kile) lakini viongozi waliofuata ni uchwara mtupu! Nikataja mifano ya akina Taylor wa Liberia, akina Moi, na hata Mkapa wetu. Mwalimu aliniangalia kwa muda na kwanza akakubali kuwa kweli viongozi wa enzi zake walikuwa makini. Lakini kitu alichosema ni kwamba they were driven with a purpose. A purpose to do away with colonialism, a purpose to return the dignity of the African and the purpose to empower the African and to an extent they succeeded. Lakini leo viongozi wetu wana purpose gani? Wanataka tu kuingia Ikulu. Wanashirikiana na wale waliotucolonise kunyonya maliasili zetu kwa mizengwe ya uwekezaji. Hakuna kiongozi yeyote leo Africa ambaye atathubutu kuuambia ulimwengu ulioendelea kuwa Afrika leo bado we sell cheap and buy dear. Tunakubali tu kila tunachoambiwa na taasisi za dola zinazotawala dunia hii. Hatuna sense of purpose.
 
Jasusi,

Nakubaliana kabisa na maneno ya Nyerere kupitia kwako.

Mimi nadhani tukitazama swala la umaskini wetu mshikaji circle yake ni kubwa sana. Na sio rahisi ikiwa kweli viongozi wetu hawana Purpose... Dira ya kitaifa. nafikiri tumepiga makelele sana humu kuhusu hili. na ajabu vyama vya upinzani navyo vinazidi kujiandikisha kila mwaka ktk kugombea kiti cha IKULU hali wakifahamu nchi yetu haina kabisa DIRA ya kitaifa...

Kitabu cha ndugu yetu Ndugu Bundara ni changamoto kubwa sana kwetu na wala kisije chukuliwa kama matusi kwani ni challenge kwetu sote na sio viongozi peke yao.

1. Tulitawaliwa:-
Hii ilitufanya sisi tuwe dependent! na moja ya mbinu kubwa ni kutunyima haki ktk elimu, Afya na ustawii wa jamii. Haya matatu ndiyo yanayotengeneza neno Maskini.. Ukisha kuwa maskini wa haya matatu basi lazima utakuwa inferior. Sasa mimi, nd. Bundara, wewe na wengine wote tufikirie njia za kujikwamua!..
Tukumbuke tu Utumwa ulipokuja ilikuwa rahisi sana kwao kama vile inavyokuwa rahisi kwao leo hii kueneza huu Utumwa wa biashara (globalization) ktk mfumo huu wa Ukoloni mambo leo. Na Viongozi wetu waache kuwa kama waume wale wanao-control wake na watoto zao..bali wajifunze upya kuwa waume wanawaongoza wake na familia zao.

Ndugu zangu,
Hakuna dawa ya kuondoa umaskini kama hatuta - reverse circle nzima na itakuwa vigumu sana kwetu kama tusipoanza na kupuuza yaliyopita kama vile Utumwa na Kutawaliwa. Wachina na wahindi wao walipita yote haya kama sisi lakini aghalab kuwasikia wakiyasema ama kukumbushia. Kwao yamebaki vitabuni, kunyoosha vidole haitasaidia kitu kwa hiyo wana deal na maisha ya leo. nadhani hatua ya kwanza kwetu waafrika ni KUYASAMEHE yaliyopita lakini TUSIYASAHAU kama walivyofanikiwa wachina na Wahindi.

2. Tegemezi:-
Hii mikopo ni moja ya mbinu zao kutufanya sisi tuwe dependent!..Hiyo mikutano ya G7 sijui 8 ni moja ya jumuiya zao zinazojenga kutawala - fikra binafsi. Na ajabu sote waafrika tulipiga vita sana Ukoloni Mambo leo na vitabu millioni viliandikwa lakini leo hii ndio kwanza tunaukumbatia. sasa hapa mshikaji ile circle inarudi... Kutawaliwa!...

3. Ulimbukeni:-
Mimi napinga sana matumizi ya elimu tunayopatiwa. Nimekwisha sema sana kuwa waafrika inabidi tutumie akili zetu vizuri wakati tunapo apply hizi elimu. Msomi mwenye Phd kufuga ng'mbe wa kizungu hali tunao Zebu na Ankole!.. msomi kupanda miti ya Ulaya Afrika hali Ulaya hawapandi miti yetu kwa sababu wanafahamu kuwa haiwezi kustawi na pengine itaharibu mazingira yao.. miti yetu haihitaji maji mengi na ardhi yao ina maji mengi. Nadhani mnakumbuka misitu yetu iliyopandwa miaka ya 80 miti yote ilikuja oza... yaani ni hasara tupu. Kuna misitu ya Kongo na Brazil ambayo ina miti mzuri sana kwa mazingira yetu lakini hatuoni kitu isipokuwa kile kinachofanana na cha mzungu - master bila kufahamu kwamba kinachotakiwa hapa ni mti sio mti gani!.. Kuku wetu siku hizi ndio hao wa sindano! Umeme unawashwa 24 hours.. hali hesabu ya kuku wa kienyeji ni kubwa sana...mswahili siku hizi hapandi tena Kisanvu na matembele isipokuwa Spinach!..Haya maswala ya kujianika beach mchana jua la saa nane....eti tupate suntan!. dada zetu nao hawakosi vipodozi vya kubadilisha rangi ya ngozi, makeup zinatumiwa na wazungu ili wapate kuwa na rangi kidogo (brown) kwa sababu sura zao ni nyeupee (pale). na mengine mengi tu hayana hata hesabu ni athari za ile circle...yaani subconsciously tunataka tuwe kama master wetu.

4. Fikra binafsi:-
Hii mshikaji ni ngoma!... sidhani kama ina dawa zaidi ya kuamini kuwa ni matokeo (results) za ile circle nzima. Tulipotawaliwa wakoloni walihakikisha wana sera zinazovunja kabisa fikra jumuiya na walifanikiwa sana. Leo hii hatuna imani kabisa na walivyokuwa wajanja wakatuletea dini ili tusije shtuka!..maana madhambi (sin) yote yanatokana na fikra binafsi. Binafsi naamini dini zimeletwa kwetu kama DAWA - therapy yaani sisi ni sinners na njia ya kuondokana na madhambi ni kumwogopa Mungu na kufuatana yale yaliyoandikwa badala ya Dini kuwa UKUMBUSHO wa mema ambayo hujenga hizo fikra jumuiya.

Safari ndefu sana ila nawaomba wanabodi waulizeni sana hawa viongozi wetu hiyo siku ya jamhuri kuhusu hili neno Independence!... hivi kweli - are we independent?..
 
Jasusi,
1. Tulitawaliwa:- Hii ilitufanya sisi tuwe dependent![...]

Hebu tujadili kidogo hapa. Afrika, Asia, Amerika, hata Ulaya wenyewe kwa wenyewe walitawalana. Na kuna nchi za kiafrika inasemekana wakoloni walishindwa kuwatawala wakalala mbele (Ethiopia, Somalia),lakini na zenyewe hali ndio inatisha zaidi:) Au by kutawaliwa, kwa tanganyika km. tunaongelea hata kabla ya 1884? Enzi za wafanyabiashara wa kigeni?

Vilevile, kama ni kutawaliwa kwa Utumwa, waafrika tunalia kila siku na utumwa lakini sio peke yetu tuliofanywa watumwa. Hata race nyingine pia zilichukuana utumwa.

So, Why Africans should be dependent just because of being colonized? Mchango wangu hapa ni kuwa kama kutawaliwa/utumwa kumetuathiri, basi ni kwa sababu ya rangi: watawala na slavemaster wetu hawakuwa weusi kama sisi. Nakumbuka hata kwa wamisionary waliotumwa na papa wakaeneze injili na kubatiza kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu:
- Walioenda Amerika, badala ya kufanya kazi iliyowapeleka, yaani kubatiza, wao wakaanza kwanza na kazi ya kueneza upendo, wakatengeneza watoto na hao wenyeji wa amerika, ndo tunaiona latin amerika ya leo
- Waliokuja Afrika, walifanya tu ile kazi waliyotumwa na papa, yaani kubatiza, wao walisahau upendo; hawakutengeneza watoto na vigoli wakiafrika
:D

Kama colour ilifanya watawala wasieneze 'upendo', basi huenda ni hii colour pia ndio inayotufanya tuwe too much dependent, bila kusahau pia matatizo ya mtu mweusi yanafanana popote alipo, kutoka USA, Brazil, hadi Kimanzichana:rolleyes:
 
Back
Top Bottom