EP cosmetics
JF-Expert Member
- Oct 18, 2015
- 2,469
- 3,840
KAZI YA WANAUME – KUTAFUTA: Sehemu ya I
Wanasayansi wanasema na ndivyo ilivyokusudiwa na Mungu. Mwanaume Adamu aliwekwa bustanini Edeni ailime na kuitunza (Mwa 2:15). Hata yeye na mkewe Hawa walipochafua uhusiano wao na Mungu aliadhibiwa katika mstari huo huo wa kazi akiambiwa atakula kwa jasho lake hata siku atakaporudia ardhi ambamo kwamo alitwaliwa.
Imeandikwa ifuatavyo: “(Mungu) akamwambia Adamu, ‘Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale, ardhi imelaaniwa (maana yake imekorofishwa katika uhusiano wake na wewe mwanadamu) kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi’” (Mwa 3:17-19).
Mwanamke hakuadhibiwa katika mistari ya utafutaji isipokuwa katika mistari ya ofisi yake ya kuuzaa na kuutunza uhai. Ndipo mintarafu mwanamke tunasoma, “(Mungu) akamwambia mwanamke, ‘Hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala’”(Mwa 3:16).
Maelfu ya Tofauti kati ya Wanaume na Wanawake
Kwa namna hii mwanaume ameumbiwa afanye kazi ngumu. Hapa Wamakonde wameshatangulia mbali kimawazo. Wao hujumlisha majukumu na nafasi ya utafutaji ya mwanaume kwa kukubali kwamba ni lazima mwanaume ataabike kwa kazi ngumu kusudi familia yake na jamii yake ikidhi mahitaji yake ya lazima wakisema, “Nnume alage” yaani “mwanaume lazima apate taabu kwa ajili ya kukidhi maisha yake binafsi, maisha ya familia yake na ya jamii yake kwa ujumla.
Kumbe tofauti na mwanamke aliyeumbwa, awe kwa namna ya pekee, mama na afisa wa uhai, mwanaume ameumbwa awe mtafutaji kusudi uhai upate kulishwa na kudumishwa kwa chakula, malazi na mavazi. Hapa ndipo tofauti za sifa na majukumu kati ya wanaume na wanamke zinapoanzia.
Sayansi inatuambia kati ya wanaume na wanawake kuna tofauti zipatazo 6,500. Tofauti hizi zinagawanyika katika mafungu matatu: tofauti za kisifa, tofauti za kitabia na tofauti za kimaumbile.
Je, nielezee zote? Hapana. Nakataa. Sitaki. Mimi si mtumwa wako. Hivi, kwa kukidhi hoja yangu ninayoijenga katika makala hii acha nizidokeze tofauti za kisifa tu.
Ni hivi, kwa vile Mungu anawapenda waja wake wote, wanaume na wanawake, amewapa sifa tofauti kusudi kila jinsia imudu majukumu yake. Sifa za wanaume ni kumi: 1) kutafuta mahitaji, 2) kupambana na kushindana, 3) nguvu nyingi, 4) kutumia akili, 5) kuamua haraka, 6) kubuni zana na mipango, 7) kujikwamua kwenye shida, 8) kujiamini na kutoogopa, 9) kuvutika na wanawake na 10) kuleta furaha.
Kifupi, hizi ndizo sifa 10 za mwanaume naye anasimama kama mwindaji (hunter). Ushahidi wa kwamba mwanaume ameandikiwa moyoni mwake na ameumbwa na Mungu kwa upande wa uwindaji, ni kwamba tangu utotoni yeye huanza kucheza na vitu vya kutafutia mahitaji: manati, ndoana, visu, bunduki na kadhalika.
Kwa upande wao, sifa za wanawake ni kumi na tano: 1) kuupenda, kuuzaa na kuutunza uhai, 2) upole na amani, 3) uvumilivu wa malezi, 4) kuona shida mapema na kusaidia, 5) kufariji na kutuliza, 6) kutamani kupendwa, 7) kusikiliza, 8) kusimulia, 9) kuamini kwa nguvu, 10) kupenda kwa nguvu, 11) kulinganisha mambo katika uzuri, 12) bidii ya kazi nyingi ndogondogo na kusimamia mambo, 13) kuwategemea wengine, 14) kuwateka wengine na 15) kuwastaajabia wengine.
Hizi ndizo sifa 15 za mwanamke naye anasimama kama mtunza kiota (nest keeper). Ushahidi wa kwamba mwanamke ameandikiwa moyoni mwake na ameumbwa na Mungu kwa upande wa utunzaji kiota, ni kwamba tangu utotoni yeye huanza kucheza na vitu vya kulelea uhai: midoli (wanasesere), maji, vyungu, vikombe na kadhalika.
Mungu Hajawahi Kumwonea Mtu
Kwa nini Mungu amewapanga wanadamu kwa namna hii? Jibu ni rahisi: Mungu si mwonevu. Hata siku moja yeye hataki kuwaonea waja wake. Hakika Mungu hajawahi kumtwisha mtu yeyote mzigo wowote pasipo kumwandalia mabega. Ndiyo maana yeye hajawahi kumuumba ndege na kumwamuru aruke angani pasipo kumpa mabawa wala hajawahi kumuumba samaki aogelee majini pasipo kumpa mapezi.
Mwanaume ni Kiongozi wa Maendeleo
Tukubali, tusikubali ipo hivyo na itabaki hivyo. Mungu si mpumbavu kuwatofautisha wanaume na wanawake katika vipengele 6,500. Nisikilize wewe! Kwa sifa yake ya utafutaji mwanaume hatagemewi kupoa, la sivyo atakuwa Marioo. Hali kadhalika kwa sifa yake ya kupambana na kushindana. Kwa sifa yake ya nguvu nyingi, kwa vile alivyo na oksijeni nyingi mwilini mwake, mwanaume hategemewi kulegea legea. Unyoronyoro si uanaume. Badala yake mwanaume anatagemewa afanye kazi ngumu, kama vile za kujenga nyumba kubwa na imara, kulima mashamba makubwa, kuchimba visima virefu, kupasua mbao, kujenga barabara nzuri, kutengeneza samani imara kusudi mwanadamu akae na alale pazuri na kadhalika.
Kwa sifa yake ya kubuni zana na kupanga mipango, mwanaume anategemewa atengeneze zana za kurahisishia kazi na kupanga mipango ya miaka mingi ya usoni. Hapa ndipo wanaume wenzetu wa Ulaya na Asia walipobuni risasi, bunduki na mabomu wakati sisi tukibaki na mikuki, pinde na mishale. Hapa ndipo wenzetu walipobuni baiskeli, pikipiki, treni na ndege, sisi tukibaki kutembea kwa miguu na kujibembeleza kwa hadithi za kuruka kwa nyungo, pembe, mbweha na fisi.
Kwa sifa yake ya kuamua haraka na kujikwamua kwenye matatizo, mwanaume anategemewa kuwa mtatuaji wa shida au matatizo ya jamii kusudi jamii isilimatie kwenye matatizo. Hapa ndipo wanaume wenzetu walipoamua kutufanyiza kazi, kutengeneza matrekta na mitambo na kujikita katika biashara kubwa kubwa, sisi tukibaki na hadithi za kuiba mazao kwa ushirikina na hadithi za chumaulete. Kwa sifa yake ya kujiamini na kutoogopa, mwanaume anategemewa kuondoa woga katika jamii. Hapa ndipo wanaume wenzetu walipoamua kuyavamia mabara ya Afrika, Amerika na Australia pasipo kutuogopa wanaume wenzao. Huko Amerika Wahindi wekundu “wakahanithiwa” kama sisi na huko Australia Aborijini “wakahanithiwa” pia.
Aghalabu, kwa sifa yake ya kuleta furaha, mwanaume anategemewa kuwa chombo cha kukabiliana na huzuni. Hadi hapa, kwa kujumlisha, shida, matatizo, woga na huzuni ni vitu vibaya sana kwa vile huharibu siha, kuzeesha watu mapema na hatimaye kuleta vifo pasipo adabu. Soma YbS 30:21-25. Kama unanibisha mimi basi waulize wanasaikolojia na madaktari wa wanadamu.
Wanaume Wengine Wanajitambua Isipokuwa Waafrika
Wanaume wengine, isipokuwa wa Waafrika, wanajitambua sana ndiyo maana tangu mwanzo hadi leo wamekuwa watafutaji wa mahitaji yao binafsi na ya jamii zao. Wao ni wachakarikaji. Wao ni wawindaji kweli kweli. Wanawinda popote. Ndiyo maana wanawinda hata barani mwetu. Wakiwa wanajitambua hivyo, waligundua tangu mapema kwamba wanaume wa Afrika walikuwa hawajitambui. Waligundua sisi hatuko mbali sana na wanawake. Ndipo wanaume wa mabara mengine wamekuwa “wakituhanithi” wanaume wenzao hapa Afrika. Kumbe sasa uelewe kwa nini historia ya dunia ilikwenda na inakwenda nitakavyokusimulia. Ngoja nikutaliishe katika mambo matano: kuvumbuliwa mabara, biashara ya utumwa, kugawanywa kwa bara la Afrika, ukoloni mkongwe na ukoloni mambo leo.
1. Kuvumbuliwa Mabara
Katika karne ya 15, wanaume wa Ulaya walikwenda safari za mbali na za hatari kutafuta mahitaji kwa ajili ya wake na watoto wao. Walitoka kwenda kuwinda. Hapa wakumbuke akina Christopher Columbus (Mwitaliano wa Genoa 1451 - 1506) na Vasco da Gama (Mreno 1469-1524) waliosafiri mbali na bara lao la Ulaya. Columbus alikwenda bara la Amerika kwa kutumia marekebu yake Santa Maria. Vasco da Gama alikwenda India kutafuta viungo akilizunguka bara letu la Afrika. Wakati hao wakiwinda hivyo, sisi wanaume wa Afrika tulikuwa tunapiga usingizi wa pono. Sana sana, sisi tulikuwa tunawinda kereng’ende, sungura, swala, nyati na ndovu tu. Nakuambia, inayoitwa kazi ya uvumbuzi wa nchi mpya ilikuwa kazi za wanaume (wawindaji) wenzetu, wanaume wa Afrika tukiwa tumelala tu.
Wanawake Wazungu waliambiwa na waume zao watulie majumbani wawalee watoto. Basi, wanaume wakajitosa katika “kulaga” kama Wamakonde wanavyosema. Si haba wakayapata mabara ya Afrika, Amerika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini kama mashamba ya bibi. Haya ni mabara waliyoyang’ang’ania kama kupe kwenye shingo za kondoo.
2. Biashara ya Utumwa
Kwa kuwa sisi wanaume wa Afrika tulikuwa hatujitambui kuwa tuna nguvu, wakaja Waarabu na Wazungu kutukamata utumwa, wapate kuzitumia nguvu zetu “kwa che.” Walitufuma wanaume wenzao, na wake zetu na watoto wetu tukiwa na misuli mikubwa lakini pasipo kujitambua. Tukakamtwa na kuuzwa kwenye minada kama wauzwavyo mbuzi, kondoo na ng’ombe. Tukanunulika kwa bei za kutupa kabisa.
Tusisahau, biashara ya kutuuza Waafrika ilidumu karibu miaka 400 (tangu 1526 -1867). Waarabu walitukamata na kutuuza Waafrika tusiopungua milioni 18. Je, humkumbuki mwanaume mmoja aliyeitwa Hamad ibn Muhammad ibn Jum’ah ibn Rajab ibn Muhammad ibn Said al Murjabi (maarufu Tippu Tib) aliyekuwa anawakamata watumwa Kongo na Wanyamwezi wa Tabora na kuwaswaga hadi kuwauza huko Bagamoyo? Mkumbuke basi walau machozi yakikulengalenga. Eti wanaume wenzetu walishindwa kupambana naye.
Baadaye Wazungu (hususan Wareno, Wahispania, Wadachi na Waingereza) wakatukamata na kutuuza huko Amerika ya Kusini na Kaskazini Waafrika tusiopungua milioni 12.5. Inasikitisha sana, katika kutusafirisha tulikufa Waafrika tusiopungua milioni 1.8. Mizigo ya watumwa wapya ilikuwa inafikishwa kwanza huko Rio de Janeiro (Brazili). Hapo ndipo Wazungu walipokuwa wanakuja kutununua kwa jumla au kwa reja reja. Biashara ya utumwa ilikuwa biashara yenye kulipa na kutajirisha sana. Laiti ningelikuwapo enzi hizo na mimi ningeliwauza Waafrika wenzangu kuwakomesha ulofa wao. Hapa niwieni radhi.
Hebu niendelee kusema. Sisi tulikuwa bidhaa kama mbuzi, kondoo, ng’ombe, farasi na punda tu. Ukitaka kujua kwamba, huko Marekani, Wazungu walikuwa wanataka nguvu zetu tu, mkunbuke mtumwa mmoja aliyeitwa Pata Seca. Mtumwa huyu aliyekuwa baunsa mwenye nguvu na umbo kubwa la miraba minne na kimo cha mita 2.14 alikuwa akitunzwa na kulishwa kwa kazi moja tu ya kuwabebesha mimba watumwa wanawake waliokuwa wanaletwa kwake na mabwana zao “kupandishwa” kama vile watu wanavyokwenda kuwapandisha ng’ombe wao majike kwa dume fulani la mbegu.
Pata Seca alikuwa dume la mbegu mwanadamu. Historia inasema, kwa kazi hiyo ya “kuwapanda” watumwa wanawake aliweza kuzaa watoto wanaokadiriwa kutopungua 200. Ndiyo kisa ukiwatazama Wamarekani weusi na watu wengine weusi huko Amerika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini wanafanana fanana kwa sababu babu yao ni mmoja, huyo Pata Seca.
3. Kugawanywa kwa Bara la Afrika
Baada ya utumwa, wanaume Wazungu waligawana bara letu kwa rula katika mkutano wao wa miezi mitatu kule mjini Berlin, Ujerumanni. Hapo mwanzoni bara la Afrika lilikuwa limevamiwa na Wazungu pasipo utaratibu. Wanaume Wazungu wakaketi kitako kuweka utaratibu wa kisheria. Ndipo wanaume Wazungu walikusanyika hapo 15.11. 1884 kuanza mkutano wa kuratibu nidhamu ya kulichukua bara letu. Baada ya kughairisha kidogo hapo katikati, wanaume Wazungu walimaliza mkutano wao 25.2.1885.
Kifupi, mkutano huu uliamua kisheria kwamba Afrika inaweza kuchukuliwa na kukaliwa na Wazungu wowote wanaoweza kufanya hivyo. Wakati wote huo sisi wanaume wa Afrika hatukuwa na habari. Yaani, tulikuwa kama ng’ombe wanaopangiwa kutolewa kama mahari wasivyokuwa na habari ya mpango huo wa wanadamu. Mkutano huu uliitishwa na Kansela wa Ujerumani, Otto von Bismarck, kwa maagizo ya Mfalme Leopold II wa Ubelgiji.
Tukijikumbusha, wanaume Wazungu, akina David Livingstone (1813-1873), Henry Morton Stanley (1841-1904) John Hanning Speke (1827-1864), Richard Francis Burton (1821-1890) walishafika kutuchungulia kama Waafrika tulikuwa tumelala. Wanaume hawa walivinjari kila kona ya Afrika kututazama kwa karibu. Ripoti zao ziliwaambia Wazungu kwamba wanaume wa Afrika tulikuwa tumelala wakati huo huo tukiwa tumekalia rasilmali nyingi sana. Sikiliza sasa. Eti walipopita huko na huko waliokota milima, maziwa na mito yetu.
Ndiyo waliokota. Ndiyo maana waliweza kutoa vitu hivyo kama zawadi kwa viongozi wao. Kwa mfano wakipookota Ziwa Nyanza, walilitoa kama zawadi kwa Malkia Victoria (1819 – 1901). Ndiyo kisa Ziwa Nyanza linaitwa Ziwa Viktoria hadi leo. Wanaume wa Kisukuma, Kiluo, Kikuria, Kizanaki, Kiruli, Kihaya, Kihangaza, Kinyambo, Kisubi, Kikerewe, Kijita, Kikara, Kizinza wala hawakuwa na habari kwamba ziwa lao limeokotwa na Wazungu.
Mzee wenu Pd. Titus Amigu
(Itaendelea)