Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom, nimeweka vocha kabla sijajiunga wala kutumia mkakata shilingi 2 nikashindwa kujiunga, sijakaa sawa zikakatwa tena toka 498 mpka 438,,naogopa hata kuweka salio kwani ni mchezo unaojirudia mara kwa mara, majibu tafadhali
 
Nilikuwa naomba mnirekebishie laini yangu iwe spesho namba yaani namba za mwisho ziwe zinafanana na za lain zangu zingine
 
Nilikuwa naomba mnirekebishie laini yangu iwe spesho namba yaani namba za mwisho ziwe zinafanana na za lain zangu zingine
 
Mimi Nikiwa kama mteja wenu wa muda mrefu naombeni msaada wenu usiku wa rarehe 19 mwenzi wa Tatu mwaka huu niliibiwa com yangu sina ya tecno j7 niliripoti polisi na rb ninayo nilikuwa naombeni msaada wenu je ili niweze kuipata com yangu nifuate taratibu zipi na gharama ni kiasi gani? Number za imei number ninazo
 
Laini ya mtu ikisajiriwa Mara moja, baada ya miaka2 au 3 mnamtumia SMS ya kukamilisha usajiri, eti mwanzo ilikuwa ni usajiri wa awali na asipofanya hivyo mtamfungia, hii haini ingii akilini, kwani MTU akinunua lain Mara ya kwanza na kuisajiri kwann huwa hamkamilishi usajiri.

Huu ni usumbufu, sababu hamjui MTU yupo wapi na anashughuli gan kwa kipindi icho au kabanana na nn! Kwann msikamilishe usajiri siku hiyo hiyo ya kwanza. Ni usumbufu aisee!!!
 
Jana m-pesa imezingua sana tumeshindwa kudownload pesa aisee, wamenisababishia hasara kubwa.
 
Wadau
........kampuni yetu ilikuwa na mkataba na Vodacom ambao ulishaisha muda mrefu....sasa hatuna tena mkataba nao lakini wanatulazimisha kutubana na vigezo vya mkataba ambao haupo ....hivyo hatupo free na line/namba zetu binafsi...kwa mfano nashindwa kuswap line yangu sababu ya ukiritimba/uhuni huo ... nahitaji kuwasiliana hasa kwa email na mabosi wa Vodacom na TCRA ili nipate ufumbuzi. ....naomba mwenye mawasiliano hayo anisaidie kwani mawasiliano ya kawaida (barua,simu kadhaa)na watendaji wengine wa Vodacom hayajazaa matunda bado wanatusumbua
 
Back
Top Bottom