Yaliyojiri Mahakamani katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, Januari 13, 2022. Kesi imeahirishwa hadi Januari 14 2022

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,111
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 13/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Kufahamu ilipoishia, soma hapa:Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe leo Januari 11, 2022. SP Jumanne Malangahe amaliza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Januari 13, 2022

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.


UPDATES:

Jaji ameingia, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naomba Kuwatambulisha

Pius Hilla Abdallah
Chavula Jenitreza
Kitali Nassoro
Katuga Esther
Martin Tulimanywa
Majige Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala, nipo pamoja na wakili:

Jeremiah Mtobesya
John Mallya Dickson
Matata Seleman
Matauka Faraji
Mangula Gaston
Garubindi Maria
Mushi Khadija Aaron

Jaji anaita washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika kuwa wapo Mahakamani

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja na sote tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji: atakuwa ni Shahidi Wa Ngapi huyo?

Wakili wa Serikali: Robert Kidando atakuwa Shahidi Wa 09 Mheshimiwa Jaji Shahidi anaingia ni Mdada amevaa Miwani Mweupe na Mrefu Kidogo Kavaa Koti la blue

Jaji: Majina yako

Shahidi: Gladisi Fimbari

Jaji: Miaka

Shahidi: 36

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Jaji: Kazi yako

Shahidi: Mwanasheria kampuni ya Airtel_Tanzania

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakaotoa utakuwa ni Kweli, kweli tupu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ataongonzwa na Jenitreza Kitali

Wakili wa Serikali: unafanya Kazi wapi

Shahidi: Nafanya kazi Airtel Tanzania

Wakili wa Serikali: Unafanya Kazi kama nani

Shahidi: Nafanya kazi Airtel PLC

Wakili wa Serikali: Kama Nani

Shahidi: Awali niliajiriwa Kama Afisa wa Sheria. Baadae 2021 Mwezi March nilibadilishwa Cheo na Kuwa Meneja Kitengo cha Sheria

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama kampuni ya AIRTEL PLC inajihusisha na nini

Shahidi: Inajihusisha Na Kupiga na Kupigiwa Simu, Huduma ya Miamala ya Fedha kupitia Airtel Money

Wakili wa Serikali: Sasa hiyo Kampuni ya AIRTEL PLC Inatoa hizo huduma kwa Watu gani

Shahidi: Ili Upate Huduma Kutoka Airtel TEL lazima uwe na Simu Handset na lazima uwe na Simcard ya AIRTEL\

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi tueleze huyo Mteja anapataje hiyo simcard ya AIRTEL?

Shahidi: Ili uweze Kuwa Mteja lazima ufike katika Ofisi za Airtel au Kwa Mawakala wa Airtel utanunua Sim Card lakini Baada ya Hapo lazima ufanyi we Usajili wa ile Line

Wakili wa Serikali: Sasa Mteja amemunua Sim Card ya AIRTEL Lazima afanye Usajili, Je Usajili unafanyikaje

Shahidi: Lazima Mteja awepo katika Usajili, atajitambulisha Majina yake yote, lazima awe na Kitambulisho Chake cha Taifa yani NIDA card, anaye Msajili atachukia hiyo namba na Kuingiza Katika Mifumo yetu, Kisha Atatakiwa aweke Dole Gumba na Kisha Msajili wetu atafanya Uhakiki (Verification) Kupitia Mifumo ya NIDA ambayo imeunganishwa na Mifumo yetu ya NIDA Baada ya Verification na Uhakiki atapata Namba ya NIDA Kuhusiana na Mifumo yetu, baada ya Kupata Uhakiki Kutoka NIDA, Taarifa Zote zitaifadhiwa Katika Mifumo yetu na Baada ya Hapo Usajili utakuwa Umekamilika..

Wakili wa Serikali: Ifafanulie Mahakama Vizuri, umesema Afisa Usajili Wa Airtel atafanya Uhakiki Kutoka NIDA, JE Afisa Wenu Usajili anapataje Taarifa Kutoka NIDA na Kuingiza Katika Mifumo yetu, Kisha Atatakiwa aweke Dole Gumba na Kisha Msajili wetu atafanya Uhakiki (Verification) Kupitia Mifumo ya NIDA ambayo imeunganishwa na Mifumo yetu ya NIDA Baada ya Verification na Uhakiki atapata Namba ya NIDA Kuhusiana na Mifumo yetu, baada ya Kupata Uhakiki Kutoka NIDA, Taarifa Zote zitaifadhiwa Katika Mifumo yetu na Baada ya Hapo Usajili utakuwa Umekamilika..

Wakili wa Sehemu: Ifafanulie Mahakama Vizuri, umesema Afisa Usajili Wa Airtel atafanya Uhakiki Kutoka NIDA, JE Afisa Wenu Usajili anapataje Taarifa Kutoka NIDA

Shahidi: Ok, Ni kwamba Mifumo Yetu imeunganishwa...........

Wakili PETER KIBATALA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Huyu shahidi ameingia akasema yeye ni Mwanasheria Hakuna Mahala yoyote ameongozwa Kusema Kama Ana utaalam wa Usajili..... Kwa Maoni yetu hiyo ni "HEAR SAY"

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ni mapema kwa Wakili kuibua Hiyo Hoja kama ni Hearsay au Lah

Jaji: Kwa nini Unasema ni Hearsay

Kibatala: kwa Sababu Yeye hajasema anafanya Jukumu la Usajili, Bali kasema Kuwa yeye ni Mwanasheria, Hakuna Mahala kasema ni Jukumu lake Kusajili

Jaji: Kwani Hearsay ni nini

Kibatala: Ni Jambo lolote ambalo halitoki Kwa Shahidi Bali kwa Third Party, Ndiyo Maana anasema Juu ya Afisa Msajili ambaye siyo yeye

Jaji: Mimi nafikiri ni Mapema Sana Kusema Ni Hearsay kwa sababu bado anaendelea Kutoa Ushahidi Wake

Wakili JEREMIAH MTOBESYA: Napata taabu Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Shahidi Msingi Wake unajengwa na Matukio, Hakuna Mahala kasema Kama alishawahi Kupata Training au Lah, anachotoa Ni opinion tu....

Jaji: Sasa Si mtamuuliza Maswali Baadae Katika Kumuuliza Maswali, Kwa sababu Hatuwezi Kusema Tuukatae Ushahidi Wa Namna hii, Ni Hatari Kama Kila Shahidi akija Tuukatae Ushahidi Kwa sababu Hana Knowledge Ya Kutosha

JEREMIAH MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji ni Hatari Sana Mbele Ya Sheria, Tufuate Sheria Inasemaje

Jaji: ninyi Mtapata Nafasi ya Kumfanyia Cross Examination, Tusubiri wakati huo

Wakili wa Serikali: Tuendelee Gladisi....

Shahidi: Majukumu yangu ni Kutoa Ushauri Juu ya Mambo Mbalimbali ya Kisheria, Lakini pia Kuandaa Tathimini Za Kisheria, Kuandaa Nyaraka Za Kisheria, Kufuatilia Kesi zinazohusu Kampuni ambazo zipo Mahakamani, Pia natoa Taarifa ninapoombwa, Juu ya Taarifa, za Kiuchunguzi Kwa Taasisi za Kiuchunguzi au Baada ya Kupokea Amri ya Mahakama Na hiyo Ndiyo Taarifa yangu Kwenye Maeneo hayo

Wakili wa Serikali: Sasa ieleze Mahakama Juu ya Mfumo wa MOBIQUIT Jinsi unavyofanya kazi katika Utunzaji Wa Kumbukumbu za Miamala

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Una Elimu gani ambayo inakuwezesha Kutekeleza Majukumu uliyo taja

Shahidi: Nina Shahada ya Sheria, Niliyopata Mwaka 2006 Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Nina Certificate ya Basic Skills za Computer ambayo nimepata Kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UCC

NA pia nilipojiunga Airtel Mwaka 2004 nilipata Mafunzo ya Ziada ya Mifumo ninayotumia katika Majukumu yangu Nilipata Mafunzo ya Mfumo wa MOBIQUIT Kwa ajili ya Kuhifadhi Taarifa za Miamala Ya Fedha inayofanywa na Mteja Mafunzo hayo niliyapata Kwa muda Wa Wiki Mbili Airtel

Nilijifunzwa Mafunzo kuhusiana na Bussiness Intelligence, Mfumo ambao unatunza Mawasiliano ya Mteja Nilipofika Mwaka 2018/2019 nilipata Mafunzo ya Mfumo Unaitwa AGILE huu ni Mfumo wa Kutunza Taarifa za Usajili Wa Mteja wa Ki BIOMETRIC

Katika Mifumo hiyo tunafundishwa Mambo Mbalimbali Ikiwamo Jinsi Taarifa inavyo chukuliwa na Kuhifadhi wa katika Mifumo hiyo Usalama wa Mifumo Endapo Kuna tolea tatizo la Kimtandao au tatizo la Kiteknolojia ni nini tunatakiwa kufanya na Utuzanji Wa zile Taarifa

Na hiyo Ndiyo Taarifa yangu Kwenye Maeneo hayo

Wakili wa Serikali: Sasa ieleze Mahakama Juu ya Mfumo wa MOBIQUIT Jinsi unavyofanya kazi katika Utunzaji Wa Kumbukumbu za Miamala

Shahidi: Kama Nilivyotaja Mfumo wa MOBIQUIT, Mfumo huu unatunza Taarifa za Miamala pale ambapo Mteja anatuma au Kupokea Pesa Automatic, Mfumo unachukua Zile Taarifa Na Kwenda Kuzihifadhi Kwenye Sever na Baada ya hapo, Ilikuweza Kuzifikia hizi Taarifa unatumia Mfumo

Wakili wa Serikali: VIpi kuhusiana na Mfumo wa BUSSINESS INTELLIGENCE unafanyaje kazi

Shahidi: Pale ambapo Mteja anafanya Mawasiliano, Akiwa Karibu na Mnara, Automatically Mawasiliano Yake Yanachukuliwa Kupitia Mifumo na Kwenda Kutunza Kwenye Sever, Baada ya hapo Unapotoa Kuzifikia Hizi Taarifa Ndipo unatumia Mfumo wa BUSSINESS INTELLIGENCE

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama ni Mawasiliano ya Namna gani Mfumo huu ndiyo unafanya kazi

Shahidi: Anapopiga simu, anapotuma Ujumbe Mfupi, anapopokea Simu na anapotaka Huduma za Internet, inakuwa Captured kwenye Mfumo wetu

Wakili wa Serikali: Shahidi Umetaja Mfumo Mwingine Wa AGILE Ifahamishe Sasa Mahakama ni Kitu gani

Shahidi: Anapopiga simu, anapotuma Ujumbe Mfupi, anapopokea Simu na anapotaka Huduma za Internet, inakuwa Captured kwenye Mfumo wetu

Wakili wa Serikali: Shahidi Umetaja Mfumo Mwingine Wa AGILE Ifahamishe Sasa Mahakama ni Kitu gani

Shahidi: Kama Nilivyoeleza Kuwa Mfumo wa AGILE unafanya kazi Mteja anapotaka Kwenda Kusajili Line yake, anapotaja Namba ya Utambulisho Wa NIDA Msajili anaingia namba za NIDA kwenye Mfumo, na Baada ya Taarifa hizi Mteja Kuweka Kidole Gumba zinakwenda Kuhakikiwa NIDA na Majibu Yatakurudi Kisha Taarifa Hizo zinaenda Kuhifadhi wa katika Mfumo wetu wa AGILE

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama, Ka wewe ni Mtumiaji wa hii Mifumo ni Kwa Muda gani Umetuma Hii Mifumo

Shahidi: Kwa Upande wa MOBIQUIT na BUSSINESS Intelligence Niliweza Kutumia Mifumo hii tangu Nipo Jiumga na Airtel Mwaka 2004 na Kwa Upande wa AGILE ni tangu Mwaka 2019 Mpaka Sasa

Wakili wa Serikali: Sasa Wakati wa Ushahidi Umeeleza Mahakama Majukumu yako, Na Moja ya Majukumu yako ni Kutoa Taarifa Chunguzi kwa Vyombo Vya Uchunguzi, Ifahamishe Mahakama Taarifa unazo toa ni Kwa vipi na zipi

Shahidi: Kwanza Nikianza, Tunatoa Kwa Jeshi la Polisi, Tume ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PCCB, Tume ya Kupambana na Madawa ya Kulevya, Mamlaka ya Mawasiliano na Financial Intelligence, na pale Mteja anapohitaji Kupewa Taarifa zake anaruhusiwa Kupewa

Wakili wa Serikali: taarifa ya namna gani?

Shahidi: Kila Taasisi Zinaomba Taarifa za Mawasiliano Kwa Ujumla nikimaanisha Kupiga na Kupokea Simu, Miamala ya Fedha na Pia Usajili wa line

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Utaratibu Wa Maombi huwa Unafanyikaje

Shahidi: Taratibu Kubwa ni Chombo Chunguzi Kuleta Barua ya Maombi ya Taarifa, Na Maombi haya Yana Wasilishwa Airtel Kupitia Upande wetu wa Mapokezi Ya kisha pokelewa yanaratibiwa Katika Register Yetu na Kupelekwa kwenye Kitengo Cha Sheria Kufanyiwa kazi na Baada ya Hapo Mkuu wa Kitengo Cha Sheria anatoa Ruhusa Kwa Muhusika Juu ya Kufanyia Kazi Maombi hayo

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Barua ya Maombi Imeshafika na Mkuu wa Idara ameshasaini, Sasa Huyu aliye na Barua anafanya nini kazi

Shahidi: Lazima afanye Kazi Barua Kwa Kujiridhisha Kwanza, Juu ya anuani ya Taasisi Kama Barua hiyo Imeelekezwa kwa Airtel? , Je Barua hiyo Ina Nembo ya Taaaisi husika? , Taarifa hizo ni za Kiuchunguzi? Na Kama siyo Za Kiuchunguzi haiwezi Kufanyia Kazi, lakini Pia iwe na Sahihi na Muhuri Wa Taaaisi Husika

Wakili wa Serikali: Umesema Afisa Anahakiki Vitu Vyote ikiwemo Taarifa ya Kiuchunguzi, Nini Unaangalia Kujua Kama Kiuchunguzi au siyo

Shahidi: Barua zote za Kiuchunguzi zinataja Kosa. Kuna ambazo zinataja Jalada namba Ili Kuonyesha Kwamba Kuna Kesi inaendelea

Wakili wa Serikali: Ni watu gani hasa sasa wanao fanyia kazi Maombi

Shahidi: Ni watu wa Kitengo Cha Sheria

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Kitengo cha Sheria ni watu Wangapi Wanashughulikia hizo kazi

Shahidi: Ni watu Wawili ambapo ni Mimi na Mwenzangu

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Assignment Imefika Mezani Kwako na Maombi yote Umepangwa yamefuata Utaratibu

Shahidi: Ofisini Kwangu Kumeanganishwa na Mifumo Niliyotaja Kupitia Computer Yangu yangu MOBIQUIT, BUSSINESS INTELLIGENCE NA AGILE. Na Kila Mfumo ni Credentials zangu za Kuniruhusu Kuingia Kwa Kila Ninapo ingia

Wakili wa Serikali: USER name Unapata wapi?

Shahidi: Kitengo Cha IT ambapo ni Mimi Mwenyewe na Kitengo Cha IT Hakuna Mwingine anayefahamu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuingiza hizo Credentials Kitu gani kinafuata

Shahidi: Mfumo wenyewe Unakuletea Sasa sehemu Ya Kuingiza Namba ya Simu ya Mteja lakini pia Muda ambao Unataka zile Taarifa Na automatically Mfumo wenyewe Unachakata zile Taarifa na Kuleta Katika Computer Yako

Wakili wa Serikali: Taarifa zinachakatwa na Zinakuja Kwenye Page yako (Computer Yako) Je Zinakuwa zimehifadhiwa wapi

Shahidi: Zinakuwa zimehifadhiwa Katika saver, zinahifadhiwa na Mfumo

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Taarifa Ku Display katika Page yako nini Kinafuata

Shahidi: Baada ya Hapo Ni Uhakika Wa Taarifa ukitoka Katika Mfumo na Taarifa Husika Kama Ni Namba husika, Je ni sahihi na Kama Vile Unavyotaka, Kisha Nina Print Taarifa

Wakili wa Serikali: Sasa Ukiisha Print Kitu gani kinafuata

Shahidi: Nilisha Print Inafanya tena Uhakiki

Wakili wa Serikali: Uhakiki wa Namna gani

Shahidi: Kwa Kulinganisha na Barua ya Maombi, Nagomga Muhuri na Kusaini pamoja na Kuweka Tarehe, Kisha naandaa Cover Later Kwa ajili ya Kuambatanisha Taarifa hizo

Shahidi: Ni naweka Vizuri na Kuiwasilisha Kwenye Mamlaka husika Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Umesema Hapa Mahakamani Kwamba Wewe huwa Unapewa Credentials na Watu wengine Kuwezesha Kuingia Katika Mifumo, Je ni watu Gani Wengine Katika Taasisi yenu

Shahidi: Kuna Watu wa aina Mbili, Watu wa Call Centers, Watu Wa Customer Care hawa Ndiyo wenye Uwezo wa Kuona, Kama Nilivyosema Kwa Ajili ya Kuhudumia Wateja Kwa ajili ya Kuona Miamala Kama Imekosewa au lah. Na Watu wengine ni Watu wa Ku Extract Zile Taarifa, Huyu ni Mtu pekee Kutoka Kitengo Cha Sheria

Wakili wa Serikali: Sasa huyu Mtu aliyepewa Uwezo Wa Kuingia na Kuona zile Taarifa, Ni Kitu gani Kingine anaweza Kufanya katika Taarifa

Shahidi: Huyu aliyepewa Access ya Kuona hana Uwezo wa Kufanya lolote zaidi ya Kuona, Kwani Taarifa hizo Zinakuwa katika Mfumo wa READ ONLY (kuweza Kusoma tuh)

Wakili wa Serikali: Hawa watu wenye Uwezo wa Kuona tuh ni watu wa Idara zipo.?

Shahidi: Ni watu wa Customer service pamoja na Call Center, na Wale ambao Wapo Kwenye Kitengo Cha IT

Shahidi: Kundi la 2 Ni Kitengo Cha Sheria, Sisi tumepewa Uwezo Wa Kuona na Ku print lakini pia hatuna Uwezo Wa Kufanya chochote Katika ile Taarifa, na sisi Pia inakuja kwa mfumo wa READ ONLY

Wakili wa Serikali: Sasa shahidi umeeleza Mahakama Juu ya Mifumo, Je umadhubuti wa Hiyo Mifumo Ikoje

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Taarifa zetu ni Automatic generator Designated, Hakuna Mtu Anayeweza Kuzalisha Taarifa za hiyo Mifumo, Mifumo hiyo pia inalindwa kwa kuwekwa software za Usalama (Firewalls) kwa Kulinda Usalama wa Mifumo na Taarifa Endapo Imetokea Muingilio wa aina yoyote

Mifumo hiyo pia inafanyiwa SYSTEM AUDIT Mara kwa mara Kuangalia Uimara wake, Lakini si Kila Mtu ana access ya hii Mifumo, Ni baadhi ya Watu ambao Wamepewa Credentials ambazo Zinawaruhusu Kuingia katika Mifumo.

Lakini Mifumo hii Imeunganishwa na AIRTEL Kwa Maana Hauwezi kuwa Mahala Popote Kuingia katika Mifumo hii, Lakini pia Uwezi Kutumia Kifaa Chochote Kuingia Katika Mifumo yetu

Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Sababu ya Kutoingia Ukiwa popote

Shahidi: Katika Mifumo yetu Mtu hawezi Kuingia pasipo Kuwa na Kifaa Ambacho Kinatambulika na Airtel Kuweza Kuingia Katika Mifumo yetu

Wakili wa Serikali: Unaposema Kifaaa/Vifaa ni Vya Namna gani

Shahidi: Namaanisha Computer yaani Desktop au Laptop

Wakili wa Serikali: Ulikuwa Unaelezea Umadhubuti wa Hiyo Mifumo, Je ni Kitu gani Kingine

Shahidi: Kwenye Mifumo Hii lazima Uwe na Hivyo Vifaa ambavyo vimeunganishwa na Airtel na siyo Kila Mtu anaweza Kuingia katika mifumo

Wakili wa Serikali: hiyo Mifumo inausalama gani Kuhakikisha nyie watumiaji na Mliyotumia ni Salama

Shahidi: Kwanza Kuna software ambazo ni Firewall ambazo zitatambua endapo Kuna Mtu anajaribu Kutaka Kuingia, Na Lakini pia Endapo Patakuwa na Tatizo la kimtandao zile Taarifa haziathiriwi Kwa Namna yoyote

Wakili wa Serikali: Unaposema Kifaaa/Vifaa ni Vya Namna gani

Shahidi: Namaanisha Computer yaani Desktop au Laptop

Wakili wa Serikali: Ulikuwa Unaelezea Umadhubuti wa Hiyo Mifumo, Je ni Kitu gani Kingine

Shahidi: Kwenye Mifumo Hii lazima Uwe na Hivyo Vifaa ambavyo vimeunganishwa na Airtel na siyo Kila Mtu anaweza Kuingia katika mifumo

Wakili wa Serikali: hiyo Mifumo inausalama gani Kuhakikisha nyie watumiaji na Mliyotumia ni Salama

Shahidi: Kwanza Kuna software ambazo ni Firewall ambazo zitatambua a endapo Kuna Mtu anajaribu Kutaka Kuingia, Na Lakini pia Endapo Patakuwa na Tatizo la kimtandao zile Taarifa haziathiriwi Kwa Namna yoyote

Wakili wa Serikali: Na Je Utendaji Kazi wa Huu Mfumo Ukoje

Shahidi: Mfumo wetu ni Madhubuti na hauna hitilafu yoyote, na Inapotokea pale unapoingiza Credentials, kuwa Kuna tatizo na huwezi Kuzifikia Taarifa za Mteja

Wakili wa Serikali: Nini Kinatoa Endapo network inakuwa Chini kwa Taarifa mnazotunza

Shahidi: Network Inapokuwa Down Haiathiri Vile Vilivyomo Ndani, Pale ambapo imerekebishika unaweza Kupata Taarifa

Wakili wa Serikali: Na Kurudisha Nyuma, Ulisema wakati wa Usajili Mteja anaweka Dole Gumba katika Kifaa Je Hilo Kifaa Kinaitwaje

Shahidi: Msajili anakuwa na Vifaa Viwili, Handset na Kifaa cha Dole Gumba ambapo Airtel tunatumia Kifaa Kinaitwa FALOPO

Wakili wa Serikali: Kuna Suala la Intergrity ya Mfumo (uadilifu wa Huo Mfumo) ukoje

Shahidi: Mfumo Wetu sisi ni Automatic generated, Hakuna Taarifa ya Ziada ya Kuongeza, Mifumo yetu Inafanya kazi Vizuri, Tuna Vifaa (software) ili Kusaidia Usalama wa Hiyo Mifumo

Wakili wa Serikali: Intergrity ya Vifaa Mnavyotumia Ofisini Ukoje

Shahidi: Tunatumia Desktop au Laptop, Ambapo Vifaa Hivi vimeunganishwa na Mifumo ya AIRTEL Na uwezi Kufanya lolote, Vifaa hivi vimeunganishwa na Mifumo ambayo inatoa ALERT pale ambapo unafanya Kinyume

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa hiyo Mifumo NI Mifumo ipi

Shahidi: Mifumo ya Kuweza Kupata Taarifa za Mihamala ni MOBIQUIT kama Nilivyo eleza Ni Mfumo wa Kuchukua Taarifa na Kuhifadhi Miamala

Shahidi: Mfumo Mwingine ni AGILE ambapo Mteja anapofika Dukani na Kufanya Usajili, Basi Uhakiki wa Taarifa Hizo, Zile Taarifa zinaenda Kuhifadhi wa Kwenye Mfumo wa AGILE, Na Kupitia Mfumo huo unaweza Kuzipitia Taarifa hizo

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa hiyo Mifumo NI Mifumo ipi

Shahidi: Mifumo ya Kuweza Kupata Taarifa za Mihamala ni MOBIQUIT kama Nilivyo eleza Ni Mfumo wa Kuchukua Taarifa na Kuhifadhi Miamala

Shahidi: Mfumo Mwingine ni AGILE ambapo Mteja anapofika Dukani na Kufanya Usajili, Basi Uhakiki wa Taarifa Hizo, Zile Taarifa zinaenda Kuhifadhi wa Kwenye Mfumo wa AGILE, Na Kupitia Mfumo huo unaweza Kuzipitia Taarifa hizo

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Ieleze Mahakama Mnamo Tarehe 02 July 2021 ulikuwa wapi

Shahidi: Mnamo tarehe 02 July 2021 nikiwa Ofisi za Airtel Morocco Nikiwa nafanya Majukumu yangu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Morocco ipo Maeneo gani

Shahidi: Ofisi za Airtel Zipo Morocco hapa hapa Dar es Salaam ambapo Ndipo Kitengo Cha Sheria Kilipo

Wakili wa Serikali: Sasa Wakati Upo Ofisini Kwako Kilitokea Kitu gani

Shahidi: Wakati naendelea na Majukumu yangu ya Sheria, Mkuu wetu wa Idara alini assign Kushughulikia Maombi ya Taarifa

Wakili wa Serikali: Maombi hayo yalitaka nini

Shahidi: Kushughulika na Maombi ya Miamala Ya Fedha ya Namba 0782237913, 0787555200, 0784789944 pamoja na Taarifa za Miamala Iliomba Pia na Taarifa za Usajili

Wakili wa Serikali: Maombi hayo yalitaka nini

Shahidi: Kushughulika na Maombi ya Miamala Ya Fedha ya Namba 0782237913, 0787555200, 0784789944 pamoja na Taarifa za Miamala Iliomba Pia na Taarifa za Usajili

Wakili wa Serikali: baada ya Kupokea Maombi hayo Ulifanya Kitu gani

Shahidi: Nilihakiki Barua kama Imetoka Kwenye Taasisi Husika, ya Uchunguzi Wa Kisayansi, Barua ilikuwa inaongelea Taarifa ya Kiuchunguzi na niliangalia Taarifa Gani inayoombwa, Nilihakiki kama Imegongwa Muhuri Wa Taaaisi Husika

Shahidi: Baada ya Kujiridhisha nili ingia Kwenye Kifaa Changu cha Kazi ambacho ni Computer, Kisha Nikaingia Kwenye Mfumo wa AGILE, Na Mfumo huo Ulifanya kazi Vizuri nikaingiza namba Moja ya Simu ambayo imeombewa Taarifa, na Kisha ikanitolea Taarifa Husika Baada ya Kuchakata

Wakili wa Serikali: Taarifa Inayohusiana na Nini?

Shahidi: Taarifa ambayo Nimeomba Kuhusiana na Zile namba tatu nilizo zitaja awali

Wakili wa Serikali: Kwenye Barua Iliombwa Taarifa za Miamala Ya Fedha na Usajili, Hapa Unaomgelea Kuingia Kwenye Mfumo wa AGILE Je Ulipata Taarifa Ipi

Shahidi: Nilipata Taarifa za Usajili Wa Namba

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusu namba zingine

Shahidi: Hiyo ilikuwa Kwa namba 0784789944 ni kafanya kwa namba ya Pili 0782237913 na Ni kafanya Vilevile Kwa namba ya tatu 0787555200 ambapo Zote nilipata Usajili wa Namba hizo Nika Print

Wakili wa Serikali: Kitu gani Ulifanya Baada ya Kupata hizi Nyaraka

Shahidi: Niliingia Tena Katika Mfumo Wa MOBIQUIT ambapo ni lazima Uinhize Namba na Muda, Tofauti na Ule Mfumo wa AGILE

Wakili wa Serikali: Sasa Kwa Namba hiyo Uliyotaja Unasema iingiza namba na Muda, endelea

Shahidi: Nilipo ingia Namba na Muda, Window Yangu ya Computer Ikaniletea Zile Taarifa,.

Wakili wa Serikali: Baada ya Taarifa hizo Kuja Nini Ulifanya

Shahidi: Nilihakiki tena, Ile namba ambayo imeombewa Taarifa, na baada ya Kujiridhisha nili print na Nikaendelea Kwa Namba Nyingine

Wakili wa Serikali: Nini Kilifanyika Baada ya Zoezi hilo

Shahidi: Baada ya Ku print Kwanza Niligonga Muhuri Wa Airtel Katika Nyaraka zote, Kisha Nikaweka Sahihi Pamoja na Tarehe Lakini Pia Niliandaa Barua (Cover Later) ambayo niliambatanishia Taarifa

Wakili wa Serikali: SASA ieleze Mahakama Hali ya Hiyo Mifumo Uliyotumia Siku hiyo Kama ilikuwa Inafanya kazi Vizuri

Shahidi: Mifumo Hiyo ilikuwa Inafanya Kazi Vizuri, Hapakuwa na Tatizo la Kimtandao na Hakukuwa na Changamoto yoyote Wakati na Print hizo Taarifa

Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusiana na Kile Kifaa Kazi ambacho Ulikuwa unakitumia

Shahidi: Kifaa Kilikuwa katika Hali Nzuri na Hakikuwa na Tatizo lolote wala Changamoto Yoyote na Endapo Kingekuwa na Tatizo lolote Basi Pale ambapo Unaingiza Credentials zingakukatalia na Kukutaarifu Kuna tatizo, lakini Katika Kifaa Changu Hapakuwa na Tatizo hilo Siku hiyo

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuandaa hizo Taarifa na Kuweka Cover Later nini Kilifuata

Shahidi: Baada ya Hapo Ni Wasilisha Taarifa hizo Ofisi ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Nini Kilifanyika Baada ya Zoezi hilo

Shahidi: Baada ya Ku print Kwanza Niligonga Muhuri Wa Airtel Katika Nyaraka zote, Kisha Nikaweka Sahihi Pamoja na Tarehe Lakini Pia Niliandaa Barua (Cover Later) ambayo niliambatanishia Taarifa

Wakili wa Serikali: SASA ieleze Mahakama Hali ya Hiyo Mifumo Uliyotumia Siku hiyo Kama ilikuwa Inafanya kazi Vizuri

Shahidi: Mifumo Hiyo ilikuwa Inafanya Kazi Vizuri, Hapakuwa na Tatizo la Kimtandao na Hakukuwa na Changamoto yoyote Wakati na Print hizo Taarifa

Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusiana na Kile Kifaa Kazi ambacho Ulikuwa unakitumia

Shahidi: Kifaa Kilikuwa katika Hali Nzuri na Hakikuwa na Tatizo lolote wala Changamoto Yoyote na Endapo Kingekuwa na Tatizo lolote Basi Pale ambapo Unaingiza Credentials zingakukatalia na Kukutaarifu Kuna tatizo, lakini Katika Kifaa Changu Hapakuwa na Tatizo hilo Siku hiyo

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuandaa hizo Taarifa na Kuweka Cover Later nini Kilifuata

Shahidi: Baada ya Hapo Ni Wasilisha Taarifa hizo Ofisi ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: SASA ieleze Mahakama Hali ya Hiyo Mifumo Uliyotumia Siku hiyo Kama ilikuwa Inafanya kazi Vizuri

Shahidi: Mifumo Hiyo ilikuwa Inafanya Kazi Vizuri, Hapakuwa na Tatizo la Kimtandao na Hakukuwa na Changamoto yoyote Wakati na Print hizo Taarifa

Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusiana na Kile Kifaa Kazi ambacho Ulikuwa unakitumia

Shahidi: Kifaa Kilikuwa katika Hali Nzuri na Hakikuwa na Tatizo lolote wala Changamoto Yoyote na Endapo Kingekuwa na Tatizo lolote Basi Pale ambapo Unaingiza Credentials zingakukatalia na Kukutaarifu Kuna tatizo, lakini Katika Kifaa Changu Hapakuwa na Tatizo hilo Siku hiyo

Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuandaa hizo Taarifa na Kuweka Cover Later nini Kilifuata

Shahidi: Baada ya Hapo Ni Wasilisha Taarifa hizo Ofisi ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Hizo Nyaraka Ukiziona Hapa Mahakamani Unaweza Kuzikumbuka

Shahidi: ndiyo

Wakili Wa Serikali: Eleza Utajuaje

Shahidi: Niliandaa na Cover later Niliyo andaa Ilikuwa na Logo ya Airtel, Zile Taarifa, Katika Cover Later hiyo Kuna Jina Langu, Sahihi Yangu na Muhuri Wa Airtel

Katika Cover Later hiyo niliambatanishia Barua ya Maombi Kutoka Ofisi Ya Uchunguzi ya Tarehe ya 01 July 2021 ambayo Inaonyesha Jalada namba ilikuwa ni CD/IR/2097/ 2020 lakini pia Ina namba 3 ambazo ziliombewa Taarifa ambazo 0787555200, 0782237913, 0784779944

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Zile Taarifa Za Usajili Wa Namba za Simu. Kitu gani Kitakufanya Ukiziona Uzikumbuke

Shahidi: Taarifa hizo Zina namba ya Simu, Majina yangu na Signature Yangu na nimegonga Muhuri Kwa Barua zote pamoja na Tarehe

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Zile Taarifa Za Usajili Wa Namba za Simu. Kitu gani Kitakufanya Ukiziona Uzikumbuke

Shahidi: Taarifa hizo Zina namba ya Simu, Majina yangu na Signature Yangu na nimegonga Muhuri Kwa Barua zote pamoja na Tarehe

Wakili wa Serikali: Taarifa ya Kwanza Ambayo utaweza Kuitambua ni ya namba Ipi

Shahidi: Taarifa ya Kwanza ni 0787 555200 Ya Pili ni 0782 237913 Namba ya Mwisho ni 0784789944

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusu Taarifa za Miamala

Shahidi: Kuna Taarifa Ya Miamala Ina Jina Langu, Sahihi Yangu, Muhuri Wa Kampuni na Tarehe

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Wetu Nyaraka hizo

Wakili wa Serikali: Angalia hiyo Nyaraka na Uniambie ni Kitu gani

Shahidi: Nyaraka Mkononi Mwangu ni Cover letter ambapo Inaonyesha Anuani

Wakili wa Serikali: Angalia Nyaraka Hizo Unazitambua au huzitambui

Shahidi: Cover letter Hii naweza Kuitambua Kwa Sababu Zifuatazo Kwa Sababu ina anuani ya Kampuni ya AIRTEL, Ina namba Ambazo zimeombewa Taarifa, Ina Jina Langu, na Muhuri Wa Airtel

Shahidi: Nyaraka Inayofuata ni Barua KUTOKA Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi, na Nimeitambua Sababu, ina Namba ya Jalada Niliyo taja, Ina Muhuri Wa Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi.

Shahidi: Lakini pia akuna Taarifa za Usajili Ambazo Zina namba Iliyo ombewa Taarifa, Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe

Wakili wa Serikali: Unasema Kuna namba ambayo Umetaja Mwanzoni, Ni ipi

Shahidi: Ni 0784789944, Kuna Taarifa Ya Usajili Pia wa Namba 0782237913

Wakili wa Serikali: Umeitambuaje

Shahidi: Kutokana na hiyo Namba lakini Pia Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe

Shahidi: Lakini pia akuna Taarifa za Usajili Ambazo Zina namba Iliyo ombewa Taarifa, Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe

Wakili wa Serikali: Unasema Kuna namba ambayo Umetaja Mwanzoni, Ni ipi

Shahidi: Ni 0784789944, Kuna Taarifa Ya Usajili Pia wa Namba 0782237913

Wakili wa Serikali: Umeitambuaje

Shahidi: Kutokana na hiyo Namba lakini Pia Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe

Shahidi: Cover letter Hii naweza Kuitambua Kwa Sababu Zifuatazo Kwa Sababu ina anuani ya Kampuni ya AIRTEL, Ina namba Ambazo zimeombewa Taarifa, Ina Jina Langu, na Muhuri Wa Airtel

Shahidi: Nyaraka Inayofuata ni Barua KUTOKA Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi, na Nimeitambua Sababu, ina Namba ya Jalada Niliyo taja, Ina Muhuri Wa Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi.

Shahidi: Lakini pia akuna Taarifa za Usajili Ambazo Zina namba Iliyo ombewa Taarifa, Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe

Wakili wa Serikali: Unasema Kuna namba ambayo Umetaja Mwanzoni, Ni ipi

Shahidi: Ni 0784789944, Kuna Taarifa Ya Usajili Pia wa Namba 0782237913 Wakili wa Serikali: Umeitambuaje Shahidi: Kutokana na hiyo Namba lakini Pia Ina Muhuri Wa Kampuni, Sahihi ambayo ni Ya Kwangu na Tarehe

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Unaiomba Nini Mahakama Kuhusiana na Nyaraka Zote Hizo hapa Mahakamani

Shahidi: Naiomba Ipokee Kama Vielelezo NYARAKA ZINA PELEKWA UPANDE WA UTETEZI Jopo la Mawakili Wa Utetezi Wanazizunguka na Kuanza Kuzichambua

Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kwa Niaba ya Mshtakiwa Wa Kwanza Hatuna Pingamizi Kwa Kuzingatia Haki ya Kufanya Cross Examination

Wakili John Mallya: Kwa Upande wangu sina OBJECTION

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande Wangu sina Pingamizi

Wakili Peter Kibatala: Kwa Niaba ya Mshtakiwa Wa Nne hatuna Pingamizi NYARAKA ZINATOKA UPANDE WA UTETEZI ZINAENDA JUU KWA MHESHIMIWA JAJI KUPITIA WASAIDIZI WAKE Jaji anazitizama Mahakama Bado ipo Kimyaaaa

Jaji: tuliishia Kielelezo Namba 14, Si Ndiyo..? Wnaitika NDIYOO!

Bado Mahakama ipo kimya, nyaraka zote kutoka airtel Tanzania kama Ushahidi katika kesi hii ya Jamhuri Vs. FREEMAN Mbowe na wenzake watatu, zipo pale Juu kwa Jaji anazipitia na kuandika masuala yake...

Jaji: Kwa Maana Riport za Transactions ni Namba Mbili Siyo tatu, Si Ndiyo..?

Kibatala: kwa Maana Print Out au Barua Kutoka Airtel.?

Wakili Peter Kibatala: Na sisi tumeona Mbili Jaji Kwa Hiyo Kwenye Registration ni Namba 3 ila Kwenye Transactions ni Namba 2

Jaji: Basi Mahakama Inapokea Vielelezo Kama Ifuiatavyo Barua ya Kwenda Ofisi ya Uchunguzi no Kielelezo namba 15 Barua ya Kuomba Taarifa ni Kielelezo 16 Taarifa Usajili ya 0784789944 ni Kielelezo namba 17 Taarifa ya Usajili ya namba 0782237913 ni Kielelezo namba 18

Taarifa ya Usajili ya namba 0797555200 ni Kielelezo namba 19 Taarifa ya Miamala ya Namba 0787555200 ni Kielelezo namba 20 Taarifa ya Miamala ya Namba 0784789944 ni Kielelezo namba 21 Mawakili wa pande zote 2 wanakubaliana na Uamuzi Jaji na Kusimama. Na Kuinama

Jaji: Sasa taarifa zote zinatakiwa kusomwa na Shahidi kama ulivyo utaratibu

Shahidi ameanza kusoma barua ya Airtel Kwenda Ofisi Ya Uchunguzi Wa Kisayansi Shahidi anasoma sasa barua kutoka Ofisi ya uchunguzi wa kisayansi maombi ya taarifa

Shahidi: anasoma Taarifa ya Usajili wa namba ya Usajili wa Namba 0784789944 Shahidi sasa anasoma taarifa ya usajili wa Namba 0782237913

Shahidi anasoma taarifa ya Usajili wa Namba 0787555200 namba ya Luten Denis Urio

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Kielelezo kinachofuata cha Mihamala ya Namba 0787 555200, Tusomee Miamala ya Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Muamala wa Kwanza wa Tarehe 20 July 2020 Namba ya muamala, namba Iliyotuma ni 0784789944, Receiver ni 0787555200 kiasi Kilichotumwa ni TSh 500,000

Wakili wa Serikali: Naomba Utusomee Muamala Wa 22 July 2020

Shahidi: Kuna Miamala mitatu

Wakili wa Serikali: Naomba Utusomee Muamala Wa Pili wa 22 July 2020

Shahidi: Transactions, Muamala Umetoka 0780900244 ametumiwa TSh 199,000 akawa na Jumla ya Tsh 300,000. Kwenda 0787555200

Shahidi: Transactions ID CI200722.1528.A80515. Muamala wa 22 July 2020 kutoka Namba 0780900244 kwenda namba 0787555200 Jumla ya Pesa Iliyotuma ni 199,000 Muhusika alikuwa na Salio 121,296, Jumla akawa na Kiasi cha TSh 320,296 baada ya Cash na Muamala Ilikuwa successfully

Wakili wa Serikali: Twende kwenye kielelezo Namba 21 cha Mahakama, Tusomee muamala wa mwisho

Shahidi: Muamala namba PP 200731.0041. B77783 mjamala wa Tarehe 31 July 2020 Kutoka Namba 0784779944 kwenda Kwenye namba 0782 237913 kiasi Kilikuwa Tsh 80,000 Salio lilikuwa ni Tsh 104,284 baada ya kutuma alibaki na TSh 23,684 na Transaction ilikuwa successfully

Wakili wa Serikali: Kitu gani tena Ulichokifanya Baada ya Kutuma hizo Taarifa

Shahidi: niliendelea na Kazi zangu zingine Mpaka Nilipoitwa Kituo cha Kati Central Kwa ajili ya Kutoa Maelezo ya Nyaraka ambazo niliziwasilisha

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani namrudisha Kwenye muamala Wa Kielelezo Namba 20, aiambie Mahakama Nini Kilitokea Shahidi: Kwa Tarehe 20 July Muamala Mwingine Uliofanyika Ulikuwa ni CO 0200720.1803.C00390 Tarehe ni 20 July 2020 Namba 0787555200 ilituma Fedha kwenda 0785191954

kiasi Kilikuwa Tsh TSh 300,000 na Mhusika alikuwa na Salio la Tsh 549,646 baada ya kutuma akabakiwa TSh 243,646 Wakili wa Serikali:

Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu ni hayo tu

Kibatala: Mheshimiwa Jaji tulikuwa tunaongea na wenzetu Tu' break kwa 45 minutes

Jaji: Kwa hiyo tunarudi saa nane na nusu?

Kibatala: Ndiyo saa nane na nusu

Jaji: Kwamba tunahairisha kwa muda wa dakika 45, mpaka saa nane na nusu ambapo tutaendelea na upande wa utetezi

Jaji amerejea Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji Quorum ipo Kama Awali na tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kuendelea Jaji anaandika Kidogo Wakati Mahakama Ipo Kimyaaa Anamruhusu Mtobesya Kusimama na Kuendelea

Mtobesya: Lakini nitakuwa Sahihi Nikisema Hukusema ni Mfumo upi wa Firewall lakini Hukusema Mfumo upi wa FireWall sababu ipo tofauti tofauti

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Nilisikia Pia Unasema Kuwa Mnafanyia Audit hii Mifumo

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Na Audit Mnayofanya siyo ya Ubora wa Mifumo ya Ulinzi

Shahidi: Ni Mifumo yote Iliyo Chini ya Airtel Kuangalia Ubora wake na Uimara wake Endapo itaingiliwa inaweza Kutoa alert

Mtobesya: Nilisikia Pia Unasema Kuwa Mnafanyia Audit hii Mifumo

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Na Audit Mnayofanya siyo ya Ubora wa Mifumo ya Ulinzi

Mtobesya anatembea kumfuata Shahidi Kizimbani alipo na Makabrasha yake Mkononi

Mtobesya: Shahidi nimekusikia Kwenye Ushahidi Wako Ukieleza Mahakama Kuwa Mfumo Uliyotoa Taarifa, Mifumo yake ya Ulinzi ni FIREWALL

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Lakini nitakuwa Sahihi Nikisema Hukusema ni Mfumo upi wa Firewall lakini Hukusema Mfumo upi wa FireWall sababu ipo tofauti tofauti

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Nilisikia Pia Unasema Kuwa Mnafanyia Audit hii Mifumo

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Na Audit Mnayofanya siyo ya Ubora wa Mifumo ya Ulinzi

Shahidi: Ni Mifumo yote Iliyo Chini ya Airtel Kuangalia Ubora wake na Uimara wake Endapo itaingiliwa inaweza Kutoa alert

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Nikisema kuwa Audit inafanyiwa na Credited Companies za audit

Shahidi: Inategemea

Mtobesya: Kwa hiyo Kwenu wanafanya wakina nani

Shahidi: Watu wetu wa IT

Mtobesya: Kwani Hapa Mahakamani Ulielezea Ushawahi Kufanya Kazi za IT

Shahidi: Hapana Sikusema

Mtobesya: Kwani Ulielezea Mahakama Kama Taarifa Za audit Mnazipata Kutoka Kwa Watu wenu wa IT

Shahidi: Hapana Sikueleza

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Naomba Kielelezo Namba 15 na 16

Mtobesya: Hiyo ni Barua Uliyosema Ulifanyia kazi,

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji akimaliza Msomee Kifungu Kilicho Ku Move wewe Kutoa Taarifa, Kifungu namba Ngapi na Sheria ipi

Shahidi: Imeandaliwa Chini ya Kifungu cha 34 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya Mwaka 2015

Mtobesya: katika Shughuli zako Ulishawahi Kukutana na Sheria ya Makosa ya Mtandao

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Wakati Unatoa Taarifa zako Ulipata nafasi ya Kupitia hicho Kifungu.?

Shahidi: Ndiyo nilipitia

Mtobesya: Wakati Unasoma hiyo Sheria, Ulipata Kusoma hicho Kifungu cha 36

Shahidi: Siku Kukiangalia

Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Nikisema Kuwa Kifungu cha 34 aliye Ombwa Taarifa anaweza Kukataa na Yule anayeomba akaenda Mahakamani Kuomba Order

Shahidi: Ni Kweli

Mtobesya: Huwa Mnalindaje Siri (Taarifa) za Wateja wenu

Shahidi: Mteja Kwetu ni Paramount, Mtu ambaye tunamthamini na Tuna hakikisha Taarifa zake hazitolewi Kiholela

Mtobesya: Kwa Mfano Mimi nikija Kuomba Taarifa Ya Mtu ambaye ni Mteja wa Airtel Mtanipa

Shahidi: Hatuwezi Kukupa, Kwa sababu Taarifa hizi tunatoa Kwa Miongozo

Mtobesya: Kama Mlikuwa na Nafasi ya Kukataa Kutoa Taarifa za Wateja wenu, Ili anayetaka aende Mahakamani akapewe Court Order, mkawapa tu Mnalindaje Taarifa Za Wateja Wenu?

Shahidi: Kwa Mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao Kifungu Cha 34 kwa Ujumla, nikikupeleka kwenye Hiki Kifungu Kina sema 34(1)....... For the Purpose of investigation a Police Officer........ ANASOMA

Mtobesya: Kisome Pia Kifungu cha 36

Shahidi: Kifungu cha 36 kina Sema........ ANASOMA

Mtobesya: Kwa hiyo 36 unasemaje pale ambapo Mtu anakuwa amenyimwa Taarifa

Shahidi: Atatakiwa Kuja na Court Order

Mtobesya: Kwanini sasa Kama kama Mlikuwa na Nafasi ya Kuzuia Kutoa Taarifa, Mkachagua Kutoa Taarifa

Shahidi: Mheshimiwa Mimi Naamini Kuwa Naenda Majukumu yangu kwa Kufuata Sheria Mbalimbali siyo Moja tu

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Barua Yako Waliomba Taarifa Kwa Sheria gani

Shahidi: Kwa Sheria Ya Makosa ya Mtandao

Mtobesya: Soma na Barua ya Taarifa Mlizotoa

Shahidi: Nimepokea Barua Yako Tar 1 July 2021 yenye Kumbukumbu FB/CYBER /2021/71 Airtel Imeambatanisha Taarifa Za Miamala Tarehe 1 June 2020 Mpaka 31 July 2020 Pamoja na Usajili wa Namba 0784779944 na 0797555200

Mtobesya: Kwa hiyo hii Ndiyo Barua iliyotoka Kwenu?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Mheshimiwa Naomba Sasa Twende Kwenye Kielelezo Namba 17. Wakati Unatoa Maelezo Yako Nilikusikia Unazungumzia suala la Msajili, Je Huyo Msajili anaweza kuonekana Kwenye Taarifa ya Usajili?

Shahidi: Hapana hawezi

Mtobesya: Kwa hiyo Mtu anawezaje Kujua Kuwa Taarifa hiyo ilisajiliwa na fulani

Shahidi: Ili Kufahamu aliyesajili, Unaweza Kuomba

Mtobesya: Sasa Kwenye Taarifa Hizi ambazo unasema ni za Msajili tunafahamu vipi

Shahidi: Kwenye Taarifa hizo Hakuna Msajili

Mtobesya: Kwenye Ushahidi Wako Ulisema Kuwa Hapa Hakuna Msajili lakini aliomba atapatikana

Shahidi: Sikusema hivyo

Mtobesya: Kwa hiyo Ulileta Taarifa tatu za Usajili na zote tatu hazionyeshi Msajili wa hizo namba

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Nilikusikia Unazungumzia Kwa Umaridadi sana Kuhusu Usajili, Je Ulimueleza Mheshimiwa Jaji Kwamba Ushawahi Kuwa Msajili

Shahidi: Hapana Sijamwambia

Mtobesya: Nitakuuliza swali kama una Utaalamu nalo Utasema Ndiyo Kama HUFAHAMU Utasema hufahamu, Je Unafahamu Juu ya Watu wanaitwa Hackers Katika Mitandao?

Shahidi: Ndiyo Nafahamu

Mtobesya: Je Unafahamu Kuwa hao Hackers Wanaweza Kuingia Katika Mifumo Wa Kaingia Kwenye Mifumo na wakabadili Taarifa

Shahidi: Kwa Uelewa Wako

Mtobesya: Wewe Unafahamu nini

Shahidi: Ni watu ambao wanaweza Kuingilia Mifumo na Kubadili Data

Mtobesya: Ikiwemo Taarifa

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Wakati Unaongozwa kuhusu Intergrity ya Mifumo yenu Hapa Ulisema Kuwa Kuna watu wanaoingilia Mifumo

Shahidi: Hapana Sikusema

Mtobesya: Nilisikia Unasema Ulienda Central Police Dar es Salaam Kutoa Maelezo Yako, Je Unaweza Kukumbuka au Nikuombee kwa Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Nafikiri itakuwa Vizuri zaidi Nikipewa

Mtobesya: Ikague Kama Ndiyo hiyo, Kama Ndiyo Yenyewe Soma Kwa Sauti

Shahidi ....... ANASOMA

Mtobesya: Mweleze Mheshimiwa Jaji Kwenye Maelezo Yako Kama Ulisema Una utaalamu wa Kuingia Kwenye Mifumo na Kutoa Taarifa

Shahidi: Hapana Sikusema

Mtobesya: Asubuhi Nilisikia Kuwa Unasema Ulipata Training ya Kuingia Katika Mifumo

Shahidi: Hapana Sikueleza

Mtobesya: Nilisikia Pia Asubuhi Ulisema Kuwa Wakati Una Print Mifumo ilikuwa Intact

Shahidi: Nilielezea Ku Print Tu

Mtobesya: Haukuelezea Ubora wake

Shahidi: Sikuelezea

Mtobesya: Kwamba Mlikuwa na Mikataba na Makampuni Mengine ya Miamala ya Fedha, Ipo Humo

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Je Ungependa Maelezo Yako yaingie Katika Kumbukumbu za Mahakama

Shahidi: Nikipata Miongozo

Mtobesya: Nakuuliza wewe, Si Umesema Ndiyo Maelezo Yako

Shahidi: Nahitaji Nafasi Kidogo Ya Kutafakari

Shahidi: Nilisha Wasilisha Vielelezo Vya awali, Naomba hii Isiingie

Mtobesya: Kwa hiyo hutaki

Shahidi: Sijasema kuwa sitaki, ila Nishatoa Vielelezo Vya awali Shahidi: Nisha Jibu swali Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba niwe Guided Kuwa amekubali au amekataa

Jaji: Kwani wewe Umesikiaje

Mahakama: kicheko

Jaji: Nafikiri tumpe Muda wa Kushauriana na Mawakili wake

Mtobesya: Lakini hairuhusiwi Hiyo, Nimemuuliza shahidi Kizimbani sitegemei afundishwe Majibu

Jaji: Nyie Upande wa Serikali mnasemaje

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nafikiri kasha Jibu swali

Jaji: Bado haja Jibu swali

Wakili wa Serikali: Basi Wakili aendelee na Cross Examination

Jaji: Kuimove Mahakama au Cross examination,.?

Wakili wa Serikali: Vyovyote Vile Mheshimiwa Jaji

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Sisi tunaomba Kui' move Mahakama Kuwa tunaomba Maelezo Yake aliyoyatia Polisi Yaingie Katika Taarifa Za Mahakama Kwa Kutumia Kifungu cha 154 na Pamoja na 164 (1)C ya Sheria ya Ushahidi

Mheshimiwa Jaji 154 ndiyo Nimeanza nayo Kutengeneza nayo Misingi Inasema....... WAKILI ANASOMA Na 164(1) C inasema Kuwa......... WAKILI ANASOMA

Sasa nilianza hivyo Kwa sababu Wenzetu walishaleta Kesi Katika Mahakama Hii Iliyokuwa Inaeleza Mahakama Hii, Kwamba Kabla Ya Kuchanganya Shahidi na Kujichanganya apewe Maelezo Yake aweze Kusoma Ndiyo Iweze Kuingia Katika Mahakama hii

Material to The Extent Kwamba Wakati Mahakama Inafanya Maamuzi yake, Kwa Mujibu Wa Kesi ya MENDEZ Ione kuwa Taarifa Zilizoachwa na Zile Zilizo Chukuliwa Ione kwamba Nini athari Yake Shahidi, Ichukue Ushahidi Wake au iache

Kwa Bahati Mbaya Sijabeba Kesi ya Alberto Mendez, lakini Ipo Katika Website ya Mahakama Kwa Kui gezea nasisitiza Kuwa Substance Yote ya Ushahidi Ni Muhimu Shahidi apewe aweze Kujiandaa tena Ipo Katika Commital Bundle

Tena Shahidi anafanya hivyo akiwa katika Witness Box Ukisoma Kifungu Cha 246 cha CPA, Kina sema Mshitakiwa Apewe The Whole Substance, there is a reason to that Kwa Kusema hayo Mheshimiwa Jaji naomba Statement Iweze Kuingiza ili niweze Kuitumia Kumcontradict

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji samahani kidogo tuna Discussion...

Wakii wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tumesikia Maombi ya Wakili Msomi Mtobesya aliyoyaleta Kifungu Cha 154 na 164 (1) C ya Sheria ya Ushahidi... Mheshimiwa Jaji Wakati tukiwa tunakubali na Position Ya Kisheria, Tunakubali Msimamo wa Kisheria Kama alivyo rejea, Lakini Mazingira aliyoyatanguliza

Wakili wa Serikali: (premises) aliyojenga Hoja wakati Anamuhoji Shahidi, Hai' support Alichokiomba Hapa Mahakamani.. Kile alichodai Kwamba ni Contradiction haijafika Kuwa Kiwango Cha Kuwa Contradiction Mheshimiwa Jaji Tafsiri Ya What amount to Contradiction kupitia Internet Kupitia translation

Cambridge Dictionary inatafsiri What amount is Contradiction Na inasema The Fact of something being the Opposite of something else or very different from something else, so that One of them Must Be wrong

Na hiyo inaweza Kuwa accessed kupitia Loading... Mheshimiwa Jaji Shahidi Ameulizwa Maswali Manne Kuhusiana na Majibu yake yakitanguliwa na Neno "SIKUSEMA" sasa Swali la Msingi la Kujiuliza Hapa Kama Hakusema Je Hiyo ni Contradiction?

Na Je Inakinzana na Nini Kama Kwenye Statement Hakipo? Jibu ni Kwamba Hakuna Inachokinzana nacho

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji cross examination ni Eneo ambalo ni Muhimu katika Kukamilisha Mahojiano na Shahidi.. Na Ina Masharti Yake Kisheria.. Kama Wakili Msomi Mwenzetu angejielekeza Kinachotakiwa Kisheria asingeshindwa Kuona Kuwa Premises alizozijenga ameshindwa Kufikia Yeye Mwenyewe

Kwa hicho alichokiita ni Contradiction Hivyo Mheshimiwa Jaji Tunaona Ombi hilo Kwa Tafsiri Ya 154 na 164 (1) C kwa Purpose Ya a Kuonyesha Kuwa Kuna inconsistency, Basi inconsistency hiyo ameshindwa Kuonyesha na Ombi hilo Halina Mashiko Kisheria

Sambamba na hiyo Hoja yetu, Tunasema Kuwa ameshindwa Kufikia Kiwango hicho cha Kuonyesha Inconsistency, Ndiyo Maana anaomba Sasa Yeye Statement Hiyo Shahidi aitoe, Sisi tunaona Yeye emefeli Kwasababu Maneno hayo Hayajatoka Kwa Shahidi

Mheshimiwa Jaji Wakati akiwa anawasilisha hiyo Hoja alikuwa Vilevile analalamika Swala la Non disclosure, Mheshimiwa Jaji sisi tunaona Hoja hii imekuwa Misplaced

Wakati wa Cross examination, Tena kutokana na Failure yake Yeye Mwenyewe, Hoja hiyo imeletwa katika Wakati ambao Siyo Sahihi na haiwezi Kuwa entertained Nasisitiza tena Kuwa Huu ni Wakati Wa Cross Examination, Wakili Msomi angejielekeza Katika Kuuliza Maswali

Hivyo Mheshimiwa Jaji Tunaomba Ombi hilo likataliwe na Wakili aelekezwe Kuendelea na Cross Examination Kwa Mujibu wa Sheria Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Addition Kidogo kwa alichosema Mr Kidando Mheshimiwa Jaji Inapokuwa suala la Allegations kuwa Kielelezo Kimeji' Contradict, Ni suala la Evidence

Mheshimiwa Jaji kinachoombwa ni Document na Tumesha submit Mara Kadhaa Rules za Kwenye kesi za SHARIF MOHAMMED Na Kesi ya GEZILAHABO Wakili

MTOBESYA: OBJECTION Mheshimiwa Jaji sisi hatukufika huko

Jaji: Sijaelewa Vizuri

Mtobesya: Wakili Msomi, Pius Hilla anaanza hapa kusema Mambo ya competence ya Shahidi

Jaji: lakini Mna nafasi na Nyinyi ya Kusimama

Mtobesya: Sawa

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa anaye Omba ni Wakili Mtobesya, Whether anayeomba ni Nani, Rules ni zilezile Mheshimiwa Jaji

Mheshimiwa Jaji Kielelezo Kinataka Kuingia Mahakamani Bila Kufuata procedure

Mheshimiwa Jaji ni ufahamu wetu Kwamba itakuwa Ni Kinyume cha Sheria Wakili Ku' tender Kielelezo Katika Mazingira Kama hayo Vifungu alivyosema Mheshimiwa havitumiki hivyo Mheshimiwa Jaji Wakili Abdallah Chavula anaomba Kidogo tuh aeleze Jambo

KIIBATALA: Mheshimiwa Jaji tumeomba Dakika Moja kabla ya Wakili Abdallah Chavula

Wakili Jeremiah Mtobesya: Nimeshauriwa na Wenzangu sababu ya Muda Niondoe Hoja yangu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wao Wajibu tuh, Tumeshajibu zaidi ya asilimia 90 kwa nini waondoke Hoja yao, Wao wajibu tu

Wakili Mtobesya: Mheshimiwa Jaji sitojibu kwa namna yoyote ilee, watake au wasitake wao kama wanataka waendelee ila mimi sitojibu

WS Abdallah Chavula: mheshimiwa Jaji basi tumekubali waondoe hiyo hoja

Jaji: Basi statement yao warudishie

Mtobesya: Mheshimiwa naejea Kwenye Kielelezo namba 20 na 21

Mtobesya: Kisha Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Kwenye Hiyo Taarifa ya Miamala Kuna Namba za Wateja wengine Mbali na Wale Mlizoombwa wateja zao

Shahidi: Ndiyo zipo Taarifa za Wateja Wengine

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Jaji katika Kielelezo namba 20, Je Kuna Namba Ngapi za Wateja Wengine tofauti na Wateja waliopo Au Transactions za P20 ni za Namba zipi?

Shahidi: Ni namba 0787555200

Mtobesya: Ni namba ya Nani

Shahidi: Ni namba ya Denis Urio

Mtobesya: Rudi Kwenye Kielelezo namba 20, Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuna namba Ngapi za Wateja wa Airtel zaidi ya hiyo

Shahidi: ANAENDELEA KUHESABU

Shahidi: Kwa Transactions Ya Kwanza Kuna namba za Wateja 19

Mtobesya: Sasa Mwambie Mhe Jaji Kuwa hizo Namba zilikuwa Zinafanya Transactions Za Namba hiyo inayoishia na 200?

Shahidi: sawasawa

Mtobesya: Kwa Namna hiyo unaweza Kusema Ulilinda Taarifa za hao watu?

Shahidi: Hizo Taarifa ziliombewa na Ofisi ya Uchunguzi Wa Kisayansi, Taarifa hizi Unapotoa unakosa access ya Kufuta au Edit Taarifa

Mtobesya: Unakwepa swali, Je hao watu wengine Walilindiwa Taarifa zao?

Shahidi: Ndiyo, Kwa sababu tulipeleka Kwenye Taasisi ambazo zinahusika na Uchunguzi

Mtobesya: Nilisikia Unasema Kuwa Mnayo mikataba na Makampuni ya Mawasiliano Juu ya Biashara ya Miamala, Je Ulitoa Mikataba Hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Kwa Taarifa hiyo ilivyo unaweza Kutambua namba za Wateja ambao Siyo wa Airtel Kwamba ni Namba ya Mtu fulani

Shahidi: Kwa Taarifa hiyo jinsi Ilivyo huwezi kuitambua

Mtobesya: Kwa Taarifa Uliyotupatia hapa Mahakamani Ya Miamala, Je Unaweza Kutuambia Kuwa Mtu fulani alituma Pesa kwa Ajili gani Shahidi: Hapana Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia hapo

Mallya: Unafahamu Makosa wanayoshitakiwa hawa Watuhumiwa Wanne?

Shahidi: Hapana

Mallya: Basi mimi nakufahamisha Kuwa Mshtakiwa wa nne, Bw. Freeman Mbowe Anashitakiwa kwa kuwatumia hawa Pesa ya Kufanyia Ugaidi...

Mallya: Kwenye hiyo Barua Uliombwa Transactions Za Watu Wangapi?

Shahidi: Haija' specify

Mallya: Tunakubaliana kuwa Umeombwa Miamala ya Namba Ngapi

Shahidi: Tatu

Mallya: we Umepeleka Mingapi

Shahidi: Miwili

Mallya: Kwa nini?

Shahidi: Oversight, (Kupitiwa tu)

Mallya: Mimi siamini kuwa Ulipitiwa..

Mallya: Hebu Nisomee Muamala Wa Mwisho Kwenye Kielelezo namba 20 una Involve TSh 80,000?

Shahidi: Ndiyo Elfu 80,000

Mallya: namba hiyo Uliombwa Kutoa Miamala yake?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Nikisema unaleta makusudi muamala wa Khalfani Bwire ambao umeombwa, Ila Kwa sababu Khalfani Bwire alikuwa anafanya Ugaidi Na Kingai Ukaona usilete Mahakamani???

Shahidi: MHESHIMIWA JAJI BADO NASIMAMIA JIBU LANGU KUWA NILIPITIWA

Mallya: Kwenye Miaamala ya Khalfani Bwire unasema Kuna Kupitiwa, Je sisi tutajua Kuna Kupitiwa Mara Ngapi?

Shahidi: Hatuwezi Kujua

Mallya:Sasa Kwenye Miamala ya Khalfani Bwire, Ina onyesha alikuwa anatumiwa Fedha na Waziri wa Ulinzi Kipindi Kile Ambaye ni Hussein Mwinyi ambaye sasa ni Rais wa Zanzibar, Ila Wewe Ukaona Ufiche tusione Miamala hiyo..

Jaji: Bwana Mallya, Unatoa wapi Maelezo hayo?

Mallya: Kwa Mteja wetu Mheshimiwa Jaji

Jaji: Ilikuwa Chini ya Kiapo?

Mallya: Hapana, lakini Wateja Wetu wanatupatia Taarifa za Kesi yao Kila Siku

Jaji: Nafikiri Si Vyema Kutaja Watu wasiokuwepo Mahakamani, Au Mna mpango wa Kumuita Rais Hussein Mwinyi Mahakamani?

Mallya: Ndiyo Mheshimiwa Jaji tutamuita Tukihitaji Baada ya Kupata Miamala Ya Bwire

Jaji: Basi naomba watu ambao Hawapo Mahakamani na hajawajitokeza Kwenye Proceedings tusiwataje sababu wanaweza wasipate nafasi ya Kuja Mahakamani Kujitetea

Mallya: Sawa Mheshimiwa Jaji

Mallya: Shahidi Makosa yako ya Kutokuleta Miamala ya Bwire, Je nani atakuja Kurekebisha Kosa hilo?

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Je Taarifa zenu za Usajili (Format) Zina fanana?

Shahidi: Ndiyo Muundo au Format Unafanana

Mallya: Hapa umesajili mtu Mmoja anaitwa Mbowe, Katika Kielelezo namba 18 Je Unaweza Kuona sehemu ya Juu Imeandikwa Kanda, Je Kanda gani?

Shahidi: Morogoro

Mallya: Ukitizama pia Taarifa za Denis Urio, Sehemu ya Kanda Kwa Denis Urio, Ipo au Haipo

Shahidi: Ipo Kwa Denis Urio

Mallya: Sasa angalia Kielelezo namba 17 cha Freeman Mbowe Kama Kuna sehemu ya Kanda au Mnapendelea Wanajeshi?? Ukiona Mwambie Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Haionekani

Mallya: Haionekani au haijaandikwa?

Shahidi: Haijaandikwa

Mallya: Ni sahihi Sasa Kwa Kuwa mtu anaitwa Freeman Mbowe, hakuna Sehemu imeandikwa Kanda ni sahihi hizo Taarifa zipo Tofauti?

Shahidi: Ndiyo Neno Kanda halija onekana

Mallya: ulitoa hiyo Clarification wakati wa Chief Examination?

Shahidi: Si Kuulizwa

Mallya: nakushauri Jibu Ulitoa au hukutoa

Shahidi: Nimeshajibu

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu swali Langu sasa

Jaji: Umeelewa Swali?

Shahidi: Si Kutoa Mheshimiwa Jaji

Mallya: Kwenye Kielelezo namba 20 Miamala WA Tarehe 20 July 2020, Ulisema P to P Maana Yake ni Nini

Shahidi: Airtel Kwemda Airtel

Mallya: na hiyo Cash in..?

Shahidi: Namba ya Mhusika Ambayo Imepokea

Mallya: Ikipokea Kutoka kwa Wakala itaandikaje?

Shahidi: zote Zina onekana kama Cash in, Kama. Mteja Kwa Mteja ni P to P

Mallya: Sasa Mimi Interest yangu ni Tarehe 20 July 2020, cash in ni Wakala?

Shahidi: Kuna ufafanuzi

Mallya: Ufafanuzi Utampatia Dada Yangu Kitali, Mimi nataka Majibu

Shahidi: zote Zina onekana kama Cash in, Kama. Mteja Kwa Mteja ni P to P Mallya: Sasa Mimi Interest yangu ni Tarehe 20 July 2020, cash in ni Wakala?

Shahidi: Kuna ufafanuzi

Mallya: Ufafanuzi Utampatia Dada Yangu Kitali, Mimi nataka Majibu

Mallya: katika hawa Washtakiwa wanne Kuna Hata Mmoja Kasajiliwa Kama Wakala?

Shahidi: Miye sifahamu..

Mallya: Mheshimiwa Jaji Nina Maswali Bado Kwa Shahidi Wetu, Na Muda Umetutupa Mkono, Ningeleta Ombi Kwako tuhairishe Hadi Kesho tuendelee na Mahakama

Wakili wa Serikali Robert Kidando: ni kweli Mheshimiwa Jaji Muda Umetutupa tu. Naomba tuhairishe Mpaka Kesho

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tulikuwa tunaomba Kama wenzetu Watakuwa na Shahidi, Wanaweza Kuja naye hata Kama Tukianza naye Kesho si Mbaya..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji inategemea Sasa na availability na Shahidi ambaye tulikuwa tumemuandaa kwa sababu alikuwa anauguliwa na Mama Yake Mzazi....

Jaji:
basi Shauri hili lina hairishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi Shahidi kesho ataendelea kuwa mahakamani na upande wa mashtaka mjitahidi kuleta shahidi mwingine kesho Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho Asubuhi JAJI anatoka
 
Hiyo menyu *102# ina namba za benki za Nyendo? Ama ndio wanaita utapeli huu? Shukurani ni muhimu hata kuliko pesa. Usiwe materialistic hivyo. Wengine tuna moyo wa kushukuru kwa kadiri ya uwezo wetu.
mnashukuru kila siku bila chochote mwaka mzima.Inachosha arifu

Bonyeza *102# utapata details za bank.
 
Wangemwita yule mama aliyesema kuwa Mbowe ni gaidi, alitoroka, wenzake walikwishahukumiwa.

Hapa ndipo nilipomwona huyu mama ni mwongo, mfitini na mnafiki mkubwa aliyebeba roho ya shetani. Utawezaje kutoa kauli ka hiyo huku ukijua kabisa kuwa ni uwongo. Kwa hili, huyu nitaendelea kumwona ni takataka katika Ulimwengu wa waliostaarabika.

Heshima ya mtu hupatikana kwa matendo na maneno yake, na wala siyo kwa cheo chake.
 
Wangemwita yule mama aliyesema kuwa Mbowe ni gaidi, alitoroka, wenzake walikwishahukumiwa.

Hapa ndipo nilipomwona huyu mama ni mwongo, mfitini na mnafiki mkubwa aliyebeba roho ya shetani. Utawezaje kutoa kauli ka hiyo huku ukijua kabisa kuwa ni uwongo. Kwa hili, huyu nitaendelea kumwona ni takataka katika Ulimwengu wa waliostaarabika.

Heshima ya mtu hupatikana kwa matendo na maneno yake, na wala siyo kwa cheo chake.
Kale ka mama ni takataka,siku chache kabla ya mwenyekiti kukamatwa alipata msiba wa kaka yake na kenyewe kakamtumia salamu za pole.
 
Back
Top Bottom