Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Team ya kampeni ya Lissu inaongozwa na

1. TCRA
2. Polisi
3. Ofisi ya Mashtaka
4. Ndugai
5. Magufuli
6. Sirro

Hawa ndo watu na taasisi wanaoongeza kura na mashabiki kwa Tundu Lissu.

Kwa matendo yao dhidi ya Lissu , Lissu anaweza hata asipige kampeni ila akashinda vibaya sana uchaguzi wa mwaka huu!!
 
TCRA wakiongea na vyombo vya habari vya Tanzania wamesema ni marufuku vyombo vya ndani kujiunga ma vyombo vya habari vya nje kama BBC, DW au VOA bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Pia vyombo ambacho kitakuwa kinarusha matangazo hayo na chombo hicho cha nje kikatoa maudhui ambayo wao TCRA wataona yanakiuka sheria za nchi basi chombo hicho cha ndani kitawajibishwa.

Dotto Bulendu akipata muda aje atugafanulie maana ndio alikuwa anahojiwa na DW mchana huu
Yaan umaskini wa akili ni umaskini.mnaya sana
 
Naishangaa sana corona kumuacha mtu kama huyu mpaka mida hii maana anatutungia sheria ambazo zitafanya wajukuu wetu kutushangaa tuliwezawezaje kukubali kutawaliwa
Safi Sana TCRA, mnalitendea mema taifa letu👏👏👏! Mungu azidi kutulinda Tz!
 
TCRA wakiongea na vyombo vya habari vya Tanzania wamesema ni marufuku vyombo vya ndani kujiunga ma vyombo vya habari vya nje kama BBC, DW au VOA bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Pia vyombo ambacho kitakuwa kinarusha matangazo hayo na chombo hicho cha nje kikatoa maudhui ambayo wao TCRA wataona yanakiuka sheria za nchi basi chombo hicho cha ndani kitawajibishwa.

Dotto Bulendu akipata muda aje atugafanulie maana ndio alikuwa anahojiwa na DW mchana huu
Baadaye tutaambiwa ili kuongea au kuhojiwa na chombo cha habari cha nje unatakiwa pia uombe kibali.
 

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo amevitaka Vituo vya Utangazaji (Radio, Televisheni, Blogs na Online Tv) kuzingatia Kanuni mpya za Maudhui Mtandaoni 2020 na Kanuni Mpya za Redio na Televisheni 2020.

Mihayo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya TCRA na Vituo vya Utangazaji (Radio,Televisheni,Blogs na Online Tv) Kanda ya Ziwa ambacho pia kimehudhuriwa na Maandishi wa Habari wa vituo hivyo, kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 10,2020 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Kikao hicho kilichoandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na COSOTA kililenga kukusanya maoni ya wadau yatakayotumika kwenye marekebisho ya Kanuni za hakimiliki,uwasilishaji mada za namna ya kuripoti wakati wa Uchaguzi mkuu na marekebisho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za 2020.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Mihayo alisema Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya Habari na Utangazaji imetoa maboresho ya Kanuni za maudhui mtandaoni zijulikanazo kama “THE ELECTRONIC AND POSTAL COMMUNICATIONS (ONLINE CONTENT) REGULATIONS,2020” ambapo Kanuni hizo zimelenga kuboresha huduma za maudhui mtandao na usimamizi wake kutokana na uzoefu uliopatikana kwa kipindi cha miaka miwili toka Kanuni za zamani zilipoanza kutumika mwaka 2018.

Mkuu huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa,alisema Kati ya maboresho muhimu yaliyofanyika kwenye Kanuni za mwaka 2018, na kuingizwa kwenye Kanuni mpya za maudhui mtandao mwaka 2020 ni pamoja na Mgawanyo wa makundi ya leseni mtandao.

Alitaja makundi hayo kuwa ni Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya Habari na Matukio (News and Current Affairs), Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya waburudishaji kama vile filamu, muziki, vichekesho, cartoon, drama n.k (entertainment), Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya utoaji elimu tu (education programmes) na Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya maudhui ya dini (religious content).

“Kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana kwa miaka miwili, Kundi la watoa huduma za maudhui ya elimu na dini limepunguziwa gharama za leseni na malipo ya kila mwaka kwa asilimia 50%. Kutoka fedha ya Kitanzania Million moja (1,000,000/=) mpaka laki tano (500,000/=) Punguzo hilo limelenga kuwafanya watanzania wengi washiriki kutoa huduma za maudhui mtandao bila kuvunja Sheria”,alisema Mhandisi Mihayo.

Alibainisha kuwa Kanuni mpya za maudhui mtandao 2020 imeweka vifungu vya maelekzo ya kuwalinda watoto na maudhui yasiyofaa na kuzuia maudhui yasiyofaa mtandaoni huku akiwasisitiza watoa huduma mtandaoni kuepuka kutangaza vitu ambavyo hawana uhakika navyo.

Aidha kwa upande wa adhabu kwa wenye leseni za kutoa huduma mtandao alisema adhabu kwa wenye leseni za kutoa huduma za maudhui mtandao zimefafanuliwa na kuongeza adhabu zingine ambazo ni sasa mtoa huduma mtandaoni atapewa Onyo kali,Kuomba msamaha kutumia vyombo vya habari na Kuamriwa kuondoa maudhui yasiyofaa.

Katika hatua nyingine Mihayo alivitaka Vituo vya Utangazaji vinavyojiunga na vyombo vya habari vya nje kuomba kibali TCRA ili kupatiwa kibali cha kujiunga na vyombo vya nje ili kuendelea kupokea matangazo.

View attachment 1532913
Mhandisi Mwandamizi TCRA Kanda ya Ziwa,William Mnyippembe akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za uchaguzi katika kikao kati ya TCRA na Vituo vya Utangazaji (Radio,Televisheni,Blogs na Online Tv) Kanda ya Ziwa.

CHANZO: Malunde
Sheria kandamizi hizi pascal Mayala upo naamini kuna malice cyo bure
 
Watasikika bila kutaka wasikike.Ni swala la frequence, washirika kuna hadi online radio. Dunia inakimbia kwa kasi ni swala la wewe na mahitaji yako tu.
kwani Radio Free Africa inasikika UK na Ujerumani??
 
Back
Top Bottom