Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Maudhui.PNG

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo amevitaka Vituo vya Utangazaji (Radio, Televisheni, Blogs na Online Tv) kuzingatia Kanuni mpya za Maudhui Mtandaoni 2020 na Kanuni Mpya za Redio na Televisheni 2020.

Mihayo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya TCRA na Vituo vya Utangazaji (Radio,Televisheni,Blogs na Online Tv) Kanda ya Ziwa ambacho pia kimehudhuriwa na Maandishi wa Habari wa vituo hivyo, kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 10,2020 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Kikao hicho kilichoandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na COSOTA kililenga kukusanya maoni ya wadau yatakayotumika kwenye marekebisho ya Kanuni za hakimiliki,uwasilishaji mada za namna ya kuripoti wakati wa Uchaguzi mkuu na marekebisho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za 2020.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhandisi Mihayo alisema Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya Habari na Utangazaji imetoa maboresho ya Kanuni za maudhui mtandaoni zijulikanazo kama “THE ELECTRONIC AND POSTAL COMMUNICATIONS (ONLINE CONTENT) REGULATIONS,2020” ambapo Kanuni hizo zimelenga kuboresha huduma za maudhui mtandao na usimamizi wake kutokana na uzoefu uliopatikana kwa kipindi cha miaka miwili toka Kanuni za zamani zilipoanza kutumika mwaka 2018.

Mkuu huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa,alisema Kati ya maboresho muhimu yaliyofanyika kwenye Kanuni za mwaka 2018, na kuingizwa kwenye Kanuni mpya za maudhui mtandao mwaka 2020 ni pamoja na Mgawanyo wa makundi ya leseni mtandao.

Alitaja makundi hayo kuwa ni Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya Habari na Matukio (News and Current Affairs), Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya waburudishaji kama vile filamu, muziki, vichekesho, cartoon, drama n.k (entertainment), Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya utoaji elimu tu (education programmes) na Leseni za maudhui mtandao kwa ajili ya maudhui ya dini (religious content).

“Kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana kwa miaka miwili, Kundi la watoa huduma za maudhui ya elimu na dini limepunguziwa gharama za leseni na malipo ya kila mwaka kwa asilimia 50%. Kutoka fedha ya Kitanzania Million moja (1,000,000/=) mpaka laki tano (500,000/=) Punguzo hilo limelenga kuwafanya watanzania wengi washiriki kutoa huduma za maudhui mtandao bila kuvunja Sheria”,alisema Mhandisi Mihayo.

Alibainisha kuwa Kanuni mpya za maudhui mtandao 2020 imeweka vifungu vya maelekzo ya kuwalinda watoto na maudhui yasiyofaa na kuzuia maudhui yasiyofaa mtandaoni huku akiwasisitiza watoa huduma mtandaoni kuepuka kutangaza vitu ambavyo hawana uhakika navyo.

Aidha kwa upande wa adhabu kwa wenye leseni za kutoa huduma mtandao alisema adhabu kwa wenye leseni za kutoa huduma za maudhui mtandao zimefafanuliwa na kuongeza adhabu zingine ambazo ni sasa mtoa huduma mtandaoni atapewa Onyo kali,Kuomba msamaha kutumia vyombo vya habari na Kuamriwa kuondoa maudhui yasiyofaa.

Katika hatua nyingine Mihayo alivitaka Vituo vya Utangazaji vinavyojiunga na vyombo vya habari vya nje kuomba kibali TCRA ili kupatiwa kibali cha kujiunga na vyombo vya nje ili kuendelea kupokea matangazo.

TCRA2.JPG

Mhandisi Mwandamizi TCRA Kanda ya Ziwa,William Mnyippembe akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za uchaguzi katika kikao kati ya TCRA na Vituo vya Utangazaji (Radio,Televisheni,Blogs na Online Tv) Kanda ya Ziwa.

CHANZO: Malunde
 
TCRA wakiongea na vyombo vya habari vya Tanzania wamesema ni marufuku vyombo vya ndani kujiunga ma vyombo vya habari vya nje kama BBC, DW au VOA bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Pia vyombo ambacho kitakuwa kinarusha matangazo hayo na chombo hicho cha nje kikatoa maudhui ambayo wao TCRA wataona yanakiuka sheria za nchi basi chombo hicho cha ndani kitawajibishwa.

Dotto Bulendu akipata muda aje atugafanulie maana ndio alikuwa anahojiwa na DW mchana huu
 
Mwananchi walifungiwa kupost kwenye page yao ya instagram.Mpaka leo mwananchi hawapost chochote kwenye page yao ya instagram.
Na maisha yanaendelea .. ndugu Mello kafunguliwa kesi juu ya kesi za kutosha ila ni ukweli usiopingika kwamba si waliobambika kesi tu bali hata mahakimu wa kesi zake wapo huku kusoma misimamo ya waananchi na jinsi vitendo vya uonevu vinavyozidi kuweka ufa.
 
Back
Top Bottom