GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,694
- 6,396
Kama ambavyo wapigania uhuru wa awali waliiwezesha Tanganyika kupata uhuru kwa njia ya amani, hata sasa njia za kidiplomasia zinaweza kusaidia Tanganyika kurejeshewa uhuru wake.
Katika mapambano ya awali, viongozi wa dini walishiriki japo si kwa uwazi sana.
Historia inaonesha kuwa viongozi wa dini kutoka dini ya Kiislamu na Catholic walishiriki pakubwa katika kuwahamasisha watu wao umuhimu wa kujitawala. Madhalani, mapadri wa Catholic walizitumia Biblia kuwafundisha waumini wao ubaya wa kutawaliwa na faida za kujitawala.
Kuna masimulizi kuwa Mmisionari wa Kikatoliki alikuwa akikutana kwa siri na viongozi wa dini ya Kiislamu na madhehebu mengine ya Kikristo na kushauriana jinsi ya kuwaandaa watu wao kwa ajili ya kudai uhuru.
Kwa jinsi ambavyo Tanganyika imeendelea kufichwa kwenye koti la Tanzania, ni dhahiri kuwa kutahitajika Elimu kwa Watanganyika ili waone umuhimu na faida ya kudai kurejeshewa nchi yao. Naamini viongozi wa dini wanajua athari za jina la nchi moja kumezwa na jina la nchi nyingine.
Nitoe wito kwa viongozi wetu wa dini kufuata nyayo za Desmond Tutu aliyesimama kidete pamoja na wananchi wa Afrika Kusini kupaza sauti hadi ubaguzi wa rangi ukafutiliwa mbali.
Askofu Zakaria Kakobe alishajaribu, lakini hapaswi kuishia hapo. Aendelee kuelimisha hadi somo lieleweke.
Tafadhalini sana viongozi wa dini. Waelimishemi kwa upendo waumini wenu cha kufanya ili nchi yao ya Tanganyika iweze kurejeshwa.