GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,694
- 6,396
Hivi nani mmiliki wa Tanzania? Watanganyika hawaitaki, kadhalika na Wazanzibar.
Ikiwa wote hao hawaridhishwi na wala kunufaishwa na uwepo wa Tanzania, ni nani hasa mnufaika wake?
Ni kama vile Tanzania ni chombo kilichoundwa kwa lengo la kuinyonya Tanganyika na Watanganyika. Kwa nini nisiamini hivyo ikiwa waliopaswa kuona ufahari wa uwepo wake hawataki hata kuisikia?
Tanganyika ilianza kujitegemea mwaka 1961. Lakini hata kabla haijakaa sawa, mnamo mwaka 1964, ilitwishwa zigo la kuilea nchi nyingine iitwayo Zanzibar kwa mgongo wa Muungano.
Haikuishia hapo, ilifanyiwa na ukatili wa hali ya juu mno. Mwaka huo huo ilinyang'anywa jina lake ililolifahamau tokea utotoni mpaka siku iliporuhusiwa kujisimamia. Badala ya jina lake, iliamriwa itumie jina la kushea na jirani yake aitwaye Zanzibar ambaye ni sawa na mtoto wake.
Tokea kipindi hicho, Tanganyika haikuwahi kuwa sawa. Imekuwa ikitumikishwa kwa namna mbalimbali iliyo rasmi na isiyo rasmi.
Wakati wa vita vya ukombozi barani Afrika, ndiyo iliyokuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi husika. Rasilimali zake na raia wake walishiriki mno katika hizo harakati.
Japo ilijulikana kuwa watu na vitu vilitoka Tanzania, lakini ukweli ni kuwa ni Tanganyika ndiyo iliyoubeba huo mzigo. Wazanzibar walikuwa wachache hivyo isingekuwa busara kuwapunguza kwa kuwapeleka raia wake vitani, na wala hawakuwa na fedha za kuchangia kwani sehemu kubwa ya fedha waliyokuwa nayo walikuwa wakipatiwa na baba yao mlezi, Tanganyika.
Imekuwa hivyo kwa miaka yote na ingali hivyo hata sasa.
Fikiri hali ya sasa. Zanzibar ingali ikiifaidi sana Tanganyika kwa mgongo wa Muungano.
Kama si Tanganyika kulazimishwa kuibeba Zanzibar, ingewezekana kwa Wazanzibar kushika nafasi kubwa ya uongozi Tanganyika?
Kama si Tanganyika kulazimishwa kuibeba Zanzibar, idadi kubwa ya Wazanzibar wangeweza kupata ajira Tanganyika kama ilivyo sasa?
Kama si Tanganyika kupewa jukumu la kuilea Zanziba, Tanganyika ingekubali raia wake waishi Zanzibar kama wageni wakati Wazanzibar wakijinafasi Tanganyika kama watoto walio kwa baba yao?
Ni dhahiri kwamba Tanganyika haijawahi kuufaidi uhuru wake tokea ikabidhiwe na Mzungu hadi sasa. Haina hata wimbo wake wa Taifa, wakati nchi zingine zote za Afrika, Zanzibar ikiwemo, zikiwa na nyimbo zao kwa manufaa yao. Wimbo wa sasa unaotumika kama wa Taifa nchini Tanganyika, huanza kwa maombi ya kuiombea Afrika kisha Tanzania. Kwa maana hiyo, tokea huo wimbo uanze kutumika,inawezekana Tanganyika haijawahi kujiombea.
Ni lini watawala wataacha kuitumikisha Tanganyika kwa manufaa ya nchi zingine kwa kutumia mwamvuli uitwao Tanzania?
Lini Tanganyika itarejea kwenye uhuru wake halisi ilioupata tarehe 09/12/1961?