Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Mwanakijiji!
Hii imetulia kaka. hii itachangia kuondoa fikra za wale wanaodhani wewe ni (Anti-government).

Makala hii imestrike "a delicate balance" moja ya hali ya juu, kimantiki na kimtazamo, kwani hakuna kiongozi wa dini yeyote au muumini anayeweza kudai kuwa dini yake imekuwa offended, hapa kaka nakupa tano! kwa sababu kuwaweka onboard viongozi wa dini hizi mbili kwa kutumia sentensi ile ile na mifano ile ile inahitaji umakini wa hali ya juu.otherwise waumini wanaweza kufikiri unajaribu kuattack dini fulani, na matokeo yake wakashindwa kupata ujumbe uliokusudiwa.

Halafu makala imetulia sana katika matumizi ya lugha, nimeona mle tashbiha, sitiari,mbalagha, mifano halisi na tamathali nyingi za semi. kiufupi nimependa fasihi andishi iliyotumika katika makala hii.
 
Big up kaka, hebu itoe pia kwenye Mwanahalisi wapate ujumbe watu wengi, nilisema hapa hawa hawajui majukumu yao.
 
Ee mola utuepushie sisi na watu kama huyu mwandishi. Hivi kaka mwanakjj ingawa sikubaliani na wewe mara nyingi na mara chache ninazokubaliana ninakuwa niko impressed, lakini katika hili nadhani umechemsha big time!

Hivi wewe ni nani hata uwaandikie "wachungaji" na kuwatolea maneno makali namna hiyo. Hawa watu wanamtumikia Mungu hawaitumikii serikali, sasa kama una tatizo na mambo yao ya kidini hilo liende kwenye dini, ila kama una tatizo na wanasiasa endelea kuwapigia kelele hao hao.

Sidhani kama itakuwa jambo jema kuwaona kina Pengo, Kakobe (my favorite preacher) na kina Simba wanasimama mitaani na mabango. Nakusihi sana waacha wahubiri waendelee kuhubiri mambo ya dini, na kama una tatizo na wanasiasa endelea na wanasiasa wako!

Ushindwe kabisa na uregee, ila mengine nakusupport ingawa nakushauri ufanye kila kitu kwa kiasi maana wanaokuchekelea hapa leo hii, ndio hao watakuzomea huko mbeleni!!

Asante sana.
 
naona watu siku hizi wamekuwa superior kuliko hata wanavyodhani wao, rais ana respect anayotakiwa, lakini watu bila kufahamu ( hata kama wanafahamu basi ni wabishi wa kuheshimu urais ) huongea kama vile wao wapo above the law, which really is sad ! kama mtu unajiona wewe ni superior vizuri kwako, lakini kuongea maneno makali ukidhani ndio utafikisha ujumbe, sio sahihi. Pengine ndio maana watu hupuuzia vioja vingi kwa maana ujumbe unatolewa kwa njia isiyo sahihi ! kama utaendelea hivyo sidhani kama una tofauti na lowassa, kutoa amri (wakati unaomba) ukijua kabisa viongozi (najua hii mada inaongelea viongozi) wa serikalini walishapanga yao"ILANI" ya kutekeleza na unapoomba kitu kama hakipo kwenye ilani, then omba kwa njia sahihi, otherwise kama watapuuzia nadhani ni safi tu !

No matter how hard you learn, you'll never understand everything !
 
Ee mola utuepushie sisi na watu kama huyu mwandishi. Hivi kaka mwanakjj ingawa sikubaliani na wewe mara nyingi na mara chache ninazokubaliana ninakuwa niko impressed, lakini katika hili nadhani umechemsha big time!

Hivi wewe ni nani hata uwaandikie "wachungaji" na kuwatolea maneno makali namna hiyo. Hawa watu wanamtumikia Mungu hawaitumikii serikali, sasa kama una tatizo na mambo yao ya kidini hilo liende kwenye dini, ila kama una tatizo na wanasiasa endelea kuwapigia kelele hao hao.

Sidhani kama itakuwa jambo jema kuwaona kina Pengo, Kakobe (my favorite preacher) na kina Simba wanasimama mitaani na mabango. Nakusihi sana waacha wahubiri waendelee kuhubiri mambo ya dini, na kama una tatizo na wanasiasa endelea na wanasiasa wako!

Ushindwe kabisa na uregee, ila mengine nakusupport ingawa nakushauri ufanye kila kitu kwa kiasi maana wanaokuchekelea hapa leo hii, ndio hao watakuzomea huko mbeleni!!

Asante sana.

HII NI KUCHANGANYA MADAWA BABAKE, KUBERI NA ZE LAGER ! NDIO MAANA KUNA KITU (MAREKANI) KINAITWA SEPARATION OF CHURCH AND STATE ! sina haja ya kuandika mengi najua wengi mngechukia !
 
Ninapokaa chini kuwaandikia waraka huu wapendwa watumishi wa Mungu, ninajihisi kutostahili na kutofaa kusema nitakayosema. Mikono yangu yanitetema na vidole vyangu kama vina ganzi kwa hofu lakini moyo wangu unadunda kwa shauku. Kwenu nyote msimamao katika nyumba zetu za ibada na kuwaongoza watu wetu katika safari ya kiroho, ninyi ambao mnajua mmeitwa kumtumikia Mungu Mwenyezi katika makundi ya imani zenu mbalimbali, ninyi ambao watu huwaita “wahudumu wa Bwana” na Watendaji kazi katika shamba la Mungu, kwenu nyote Saalam!

Ninapozungumzia “wachungaji” simaanishi wale tu wa Wachungaji wa Kilutheri au makanisa ya Kiprotestanti au wale ambao wanaongoza parokia na sharika mbalimbali; na sina maana ya wale tu ambao ni viongozi wa dini ya Kikristu. “Wachungaji” ninaowazungumzia hapa ni wale ambao kwa maana ya msingi kabisa ya neno hilo, wanajukumu la kuchunga na kutoa mafunzo ya kiroho kwa waamini wao. Hapa najumlisha viongozi wote wa kidini wa dini zote na madhehebu yote, wale ambao jukumu lao la kwanza ni katika kuwaongoza watu katika mafundisho na maadili ya kidini. Wale wenye kukiri Imani ya Mitume na wale wenye kukiri Shahda, wale wenye kusimama makanisani na wale wenye kusimama misikitini. Nina maana ya wale wote ambao kimsingi wanachunga maisha ya kiroho ya watu kwa kutoa maongozo, maelekezo na mausia ya kiroho ili waamini wao waweze siku moja kufika mbinguni. Hawa ndiyo wachungaji ambao ninakusudia waraka huu.

Kwenu nyote Mashehe, Mapadre, Maimamu, Wachungaji n.k bila ya shaka mnafahamu wajibu wenu mkubwa katika maisha ya kiroho ya waamini wenu na bila ya shaka mmekuwa mkijitahidi kila kukicha kuwapatia waamini wenu mafundisho na maelekezo ambayo mna uhakika yatawasaidia kiroho. Hata hivyo ni kwa masikitiko makubwa niseme wazi kuwa kwa kiasi kikubwa mmewaangusha Watanzania. Sauti yenu haisikiki kama inavypaswa katika kuongoza “kondoo” wenu, na matokeo yake badala ya nyinyi kuwa katika kundi la wanaoongoza, sasa hivi mnajikuta mnafuata.

Ninayasema haya hasa baada ya kusoma Tamko la Baraza Maaskofu Katoliki lililotolewa hivi karibuni. Niliposoma tamko hilo nilijikuta natikisa kichwa kwa mashaka kwani walichotaka kukisema hawakukisema na wasichotakiwa kukisema walijaribu kukisema, na matokeo yake walitumia herufi na maneno mengi waliyoyapanga vizuri kwa lugha “endelevu” lakini bila kusema kitu! Ni ubutu huu ambao ninawaandikia ili muunoe na viongozi wengine wa madhehebu mengine ya dini watakapotoa tena matamko wafikirie vizuri.

Viongozi wetu wa dini mmekuwa butu! Mnameremeta kama kisu kwenye ala, na mnang'aa kama sime iliyoinuliwa. Mnapendeza kwa kanzu na majoho yenu na kwa hakika mnavutia mnapozungumza kwa maneno yaliyopangwa. Hata hivyo hamna tena makali ya kukata kwani mmekuwa butu kwa muda mrefu na sasa mmbakia kama ishara ya “kile kilichowahi kuwepo”.

Mlikuwa wapi wakati watanzania 900 walipokufa kwenye ajali ya MV. Bukoba? Mlikuwa wapi wakati wa ajali ya MV. Kilombero, ajali ya treni Dodoma, na ajali ya basi kule Singida? Leo hii Rais Joseph Kabila amemtimua Waziri wake wa Usafiri baada ya ajali nyingine ya ndege iliyoua watu zaidi ya thelathini. Hivi hapa Tanzania ni hadi watu wangapi wafe kwenye ajali zisizo za lazima ndipo wachungaji wetu mtaungana na wanaharakati kutaka viongozi goi goi wawajibishwe? Zilipotokea vurugu Mwembechai na baadaye mauaji ya kisiasa kule Pemba, mbona hatukuwaona mkiikemea serikali, vyama vya kisiasa na wananchi kwa ujumla na mkaliacha jambo hilo kwa watu wachache? Wakati serikali inanunua ndege ya bilioni 50, rada ya bilioni 50, magari mawili ya milioni mia mbili, na kuingia mkataba wa Richmond, wachungaji wetu mlikuwa wapi? Hata hili suala la sasa linaloendelea la Buzwagi na Karamagi, mbona mmechelewa kuamka na mnafumbua macho kama mliolazimishwa au kukatishwa usingizi?

Ninyi mnaojitambua kuwa ni watumishi wa Mungu, mbona mmekuwa kimya na mnagwaya mbele ya watawala wetu? Mbona hivi karibuni kiongozi mmoja wa ngazi za juu alitamka mbele ya viongozi wa dini kuwa taasisi za dini zinapojenga mahospitali n.k zinashiriki katika utekelezaji wa ilani ya CCM, mbona hamkukosoa, au zile hisia kuwa kanisa ni sehemu ya CCM zina ukweli? Kuna wakati lazima muwe mashahidi wa ukweli!

Wako wapi kina Sheikh Khalifa Bin Khamisi watetezi wa “mali” za waislamu? Je na wao wamekuwa kama CCM kuwa mali za Watanzania wote zikipotea kama zilivyopotea Benki Kuu haziwaumi, ila zile za Waislamu na za CCM ndizo huwauma? Iko wapi ile Shura ya Maimamu ambao kila baada ya muda wanatishia maandamano ili kuishinikiza serikali kufanya hili au lile? Mbona hadi leo hawajatishia maandamano kutaka kujua ukweli wa Benki Kuu, Buzwagi, Richmond, n.k ? Au ndio huo uongozi wa kidini mambo leo ambao wapendwa watumishi wa Mungu mnauendeleza? BAKWATA wako wapi wakati nchi yetu iko katika wakati mgumu?

Wako wapi wale wahubiri wa Injili, wahubirio miujiza? Yuko wapi Mchungaji Kakobe ambaye yuko tayari kukemea “mapepo” wakati watu wanatoana upepo? Ni lini ataacha kwa dakika chache kuhubiri miujiza na badala yake aje kuwajuza watu, kuhusu udhambi wa maisha ya kujikuza, na ya kutweza wengine? Haitoshi kuimba mapambio, haitoshi kusikiliza kasida, na haitoshi kushika vitabu vya dini mikononi, huku nchi na wananchi wanakosa mwelekeo katika maisha yao ya kawaida. Sala nyingine za miujiza zinaweza kuwa si za lazima endapo watu watakua na matumaini wanapoenda mahospitalini, wanapata huduma nzuri serikalini n.k

Wapendwa wachungaji wetu, ninahofu kuwa inawezekana hamkemei na kupiga vita uovu wazi wazi na pasipo utata kwa sababu ninyi nanyi mnanufaika kwa namna moja au nyingine na uongozi mbovu na tabia za kifisadi. Je yawezekana ni kwa sababu baadhi yenu wamelala kitanda kimoja na ufisadi, wakijifunika mablanketi ya unafiki, huku wanajipepea upepo wa uzandiki? Inawezekana ni kwa sababu baadhi ya miradi yenu (binafsi na vinginevyo) isingewezekana isipokuwa kwa baraka za “walio katika viti vya enzi vivunjikavyo”?

Ni wazi mara nyingi mna hofu ya kutotaka kuichukiza serikali. Tunatambua kuwa mkipiga kelele sana viongozi watawanyoshea vidole na kuwaonya, na watawaambia “fanyeni kazi zenu za dini, msiingilie serikali” Tunajua hilo linaweza kuwafanya mgwaye, kwani wanaweza wakaanzisha uchunguzi dhidi yenu au kujaribu kuwaumbua kutokana na madhaifu yenu mbalimbali kama ilivyomkuta Askofu Ncube wa Zimbabwe. Je ni hilo ndilo mnaloogopa, kiasi cha kwamba mikataba mibovu inasainiwa na hakuna mwenye ujasiri wa kuitisha Waziri Karamagi ajiuzulu au awajibishwe?

Tunafahamu pia kuwa wakati mwingine hamna ujanja isipokuwa kula sahani moja na watawala wetu alimradi mkiwaalika kwenye harambee zenu watokee, vinginevyo mnahofu kuwa michango yenu na makusanyiko yenu hayatafanikiwa. Lakini kama kilichotokea Burma hivi karibuni ni fundisho, basi kuna wakati ambapo viongozi wa dini ni lazima wafanye uchaguzi aidha kufumba macho na kuendelea kufurahia hisani ya watawala, au kuwa majasiri na kuongoza mapambano ya kifikra ili kuamsha dhamira za wananchi wetu ili tuweze kujenga taifa lile la kimaadil mnalolihubiri kila siku.

Ni kiongozi gani kati yenu ambaye atakuwa tayari kusimama juani, kuandamana, na kushika mabango na sisi wanakijiji kuihoji na kuikemea serikali? Ni nani kati yenu ambaye atakuwa tayari hata kwenda kifungoni katika harakati za kutetea haki za raia na wananchi? Itakuwa ni siku ya uamsho mkubwa tukimuona Kardinali Pengo mtaani, Mufti Simba mtaani, kina Kakobe, Mwakasege, Mwaipopo na wengine mtaani wakiongoza kelele za kutaka serikali iwajibike. Katika Tanzania ambayo viongozi wa dini na serikali hawawezi kufanya kazi pamoja isipokuwa hadi wakubaliane, na ambao hawawezi kupingana bila kuvunjiana mahusiano, ni vigumu kwa viongozi wetu wa dini kwenda kinyume na serikali na hicho ndicho kiini cha ubutu wenu.

Niwakumbushe kuhusu kiongozi mwingine wa dini ambaye alionesha kilele cha “Uchungaji Bora” siyo tu kwa kwenda jela na kufungwa, bali kutoa uhai wake mbele ya risasi muuaji. Dr. Martin Luther King Jr, alipokuwa amefungwa kwenye jela ya Birmingham kule Alabama Marekani, baadhi ya viongozi wa dini walimshangaa kwanini amekuwa anapiga kelele sana, na walimshauri apunguze makali yake kwani yeye ni kiongozi wa dini. Akiwa kifungoni, Dr. King aliandika barua yake maarufu ijulikanayo kama “Barua toka Jela ya Birmingham” (Letter from Birmingham Jail) ambayo ndani yake alieleza ni kwanini yeye kama kiongozi wa kidini hakuweza kukaa kimya. Na hata alipouwa kule Memphis, alikuwa tayari moyoni amejua kuwa ameshafika “kilele cha mlima”!

Alisema jambo moja ambalo natumani litawasha moto ya uzalendo na kusababisha mlipuko wa utumishi wa umma ndani yenu. Alisema “ukandamizaji mahali popote, ni tishio la haki mahali pote.” Haiwezekani viongozi wa dini wakakaa katika kisiwa cha mahekalu yao, huku watu wanataabika, wananyimwa haki au kwa namna moja au nyingine kufanywa duni. Ndio maana ninawauliza, mlikuwa wapi wakati vijana zaidi ya ishirini wa Kitanzania wamekwama Ukraine na kupigwa na ubaridi nje ya ubalozi wa Uingereza kisa serikali imejifanya mbabe? Mbona hamjauliza hatima yao ikoje? Na kwa nini hamkuibana serikali kutoa majibu ya kina badala ya majibu ya kibabe iliyoyatoa?

Leo hii mnaposimama na kutuhubiria maadili, hivi mnaweza kweli kusimama mbele ya Mungu mnayemtumkia na kusema ninyi ni mawakili wazuri wa maadili mnayotuambia tuyafuate? Wapendwa viongozi wa dini, wakati uko mbioni na sasa umefika ambapo mnatakiwa mfanye uchaguzi, tena uchaguzi wa haraka na wa makusudi. Nina mapendekezo machache kwenu kufikia uchaguzi huo.

Kwanza kabisa mtakapotoa matamko mengine huko mbeleni na hasa yale yaliyokusudiwa kutuma ujumbe kwa watawala wetu, acheni kuzunguka mbuyu, semeni mnachotaka kusema badala ya kutumia maneno mengi kutosema kitu! Kuweni kama Yohana Mbatizaji (Nabii Yahya A.S) na watangazieni watawala wetu kwamba wakati wa toba umefika na ya kuwa shoka limekwishainuliwa juu ya shina! Pili, vunjeni hii ndoa haramu ambayo mlijifungisha na watawala wetu na muwe huru kweli kweli. Leo hii mnashindwa kukemea maovu moja kwa moja kwa sababu mnaowakemea ni watu ambao wanawanufaisha!

Ndio maana leo mmekuwa bubu kukemea tabia ya Rais kufanya biashara Ikulu, na mmekuwa bubu mabilioni ya fedha kupotea Benki Kuu, na kwenye taasisi mbalimbali na halmashauri mbalimbali nchini. Mnashindwa kunyosha kidole kwani mkinyosha kimoja mnaogopa vitatu vinawaelekea nyinyi wenyewe na gumba linashuhudia mbinguni! Mnatetemeka mbele ya saluti na mnagwaya mbele ya vimulimuli!

Na mwisho, muwe tayari kusimama upande wa haki si kwa matamko yasiyokwisha na mausia yasiyokoma bali kwa hatua dhahiri na za makusudi. Muwe tayari kufanya kile ambacho Yesu wa Nazareti (Nabii Issa Bin Maryam A.S) alikisema kuhusu Mchungaji Mwema kuwa “Mchungaji Mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake”. Kuna siku (Mungu aiepushie mbali) ambapo Taifa letu litapitia ile “Saa ya Mjaribu” na mtatakiwa wakati huo kuchagua uhai wenu au hatima ya kondoo, natumaini mtafuata mifano ya wale walioenda mbele yenu, mifano ya kina Oscar Romero, Martin Luther King, Malcom X, na watawa wa Kibudha kule Burma ambao wiki chache zilizopita baadhi yao wamekwenda kwenye vifo vyao wakitetea haki za wananchi wenzao. Siku ambapo Taifa lenu litawaita kutoa sadaka kubwa mtakuwa tayari au mtaandika barua nyingine ya kichungaji au kuitisha vyombo vya habari?

Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu mnayemtumikia mpate ujasiri wa kusimama kama manabii na kunyosha mikono ya haki mbele zake, na kuwaongoza watu wetu siyo tu katika “malisho ya majani mabishi” ya mbinguni, bali katika kupata mana itokayo mbinguni hapa hapa duniani kwanza. Ni matumaini yangu hatamjaribu kujenga ufalme au paradiso mpya mbinguni bali mtaanza kushiriki katika kujenga paradiso ya Bongo hapa hapa duniani! Msipofanya hivyo, kama kile kinachowakuta CCM leo na nyinyi mjiandae kitawakuta, nacho ni kuwa mkianza kutuyeyusha na kutupiga soga za kizamani, Watanzania watawahesabu kuwa na ninyi hamna mpango (you'll become irrelevant) . Natumaini, hilo halitatokea. Myakumbuke maneno ya Nabii Yeremia kuwa “Ole wenu Wachungaji, wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu” Yer. 23.1

Ni mimi msafiri mwenzenu katika safari ya Kiroho,

mwanakijiji -at-jamboforums.com

naomba nikupe ushauri wa bure ambao ni nje ya mada (politics)

vizuri kwa uliyoandika lakini vile vile acha nisema kwamba, kama kweli utaamua kumuweka Mungu kama hivyo ulivyoandika hapo juu basi nakushauri usichanganye Mungu na uongo aidha katika siasa kama kutumia strategy kubomoa watu fulani, na instead tumia hekima, ustaarabu ulio nao kushauri viongozi ili kuhakikishis maslahi mazuri taifa letu, lakini unapochanganya mambo ya M/Mungu na mambo ya kidunia mzee, yatakaupata mengi (hata kama sio sasa hivi) !Huo ndio ushauri wangu tu kwako kwa leo, sisemi kama unasingizia watu lakini just a lil advice !
 
Kwani wewe Kada na Bi senti ni nani kuamulia watu cha kusema.

Yeye katoa maoni yake na kama hukubaliano that is up to you.
Come on hii sio Russia bwana........

Mkjj can say whatever the heck anapenda na kuna watu watapenda anachopenda na watakifuata na wale msiopenda mtakiacha.

grrrrrrrrrrrr
 
hivi nani yule aliyeandika "LIKUKUUMIA UJUE LIMEKUHUSU"? kama yeye kaandika whatever the heck he wants, then why not me baby ? good enough, umesema kama hukubaliani nayo, its up to you gyal !so wat a gwan mi byebye !
 
Mwanakijiji hii makala ni nzuri sana na ni kama vile ulinisoma maana siku zote nimekuwa najiuliza hawa viongozi wa Dini wako wapi, mbona wako kimya wakati mambo mengi yanatokea na kuendelea kuiathiri nchi yetu. Viongozi wa dini ni viungo muhimu sana katika mapambano mbalimbali ya kuleta haki kwa wananchi wote, ni muhimu pia katika kuleta na kuongeza uadilifu katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiserikali.

Naheshimu mawazo ya wanaopinga hii makala lakini nadhani wengi wao wanashindwa kuelewa umuhimu wa viongozi hawa katika jamii zetu au tuseme labda wameamua kuwa magoigoi wa kuelewa umuhimu wa hawa wachungaji kwenye vita dhidi ya rushwa, uhamasishaji wa uongozi bora na usimamizi wa haki kwa wote. Dini ni sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku, kwa hiyo viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika jamii zetu. Makala ya Mwanakijiji itumike kama changamoto kwa viongozi wote wa dini ambao midomo yao imezibwa kwa gundi kali ya CCM na Serikali.
 
Nimekusikia kada, next time.. nitazungumza kwa upole zaidi..!
Hakuna cha kuzungumza kwa upole wala nini Mwanakijiji kwa sababu kwa miaka 40 Watanzania wamekuwa wakizungumza kwa upole na unyenyekevu lakini matokeo yake wamefanywa kama majuha na hawa viongozi.
 
mkjj,
that was incredibly what's up!!. Nimependa references....inaonyesha jinsi gani ulivyojiandaa, dhamira ya kuwa mwandishi mzuri mwenye kujua historia na dini. Hongera nyingi kwako.
Nina swali, Je umejiandaa vyema iwapo kutakuwa na counter attacks toka kwa hao "wachungaji."??...
 
Mkijiji, nimeisoma makala yako kwa makini Kazi nzuri sana Mungu akuzidishie. Makala imekaa vyema kuwaamsha wachunga kondoo wa bwana waache kujibweteka wakidhani hayawahusu!

Huwezi kumhubiria mtu neno la Mungu ama awe na upendo wakati Mtu kalala njaa ama hata hana mahali pa kuishi eti we unampelekea neno la Mungu!

Muumini ni lazima awe katika hali nzuri na mawazo yaliyo tulia ndipo anaweza kutafakali ukuu wa Mungu, Vinginevyo watakuwa wanatwanga maji kwenye kinu!

Kwa maana hiyo hali hii ya kuhujumu maisha ya waumini wao inayo fanywa na mafisadi inawahusu moja kwa moja!

Bravo, ujumbe umefika na naamini watatafakari kwa hekima itokayo juu ili wafanye sehemu yao! Asante kwa uamusho!
 
"wachungaji" kwa upande wao wanamajukumu mengine kidini, jukumu moja ni kwamba wanasheria zinazowalazimish kuwaheshimu viongozi wa nchi na sheria za nchi wanayoishi.

aidha, wachungaji wengi wanachukuliwa kama "marais" wadogo wa wale wanaowaongoza, neno atakalolisema mwanakijiji tu, halitakuwa na uzito kwangu au kwako kama lile litakalosema na mchungaji wako, ikimaanisha kwamba wachungaji hawa inabidi wawe makini zaidi kwa kile wanachokisema, wasiseme kitu kisichokuwa na ushahidi wa asilimia 100, wasiseme kitu kwa ushabiki tu.

kutokana na sababu hizo basi, wachungaji hawawezi kuwa sawa na raia wengine wakati wa kutoa maoni yao juu ya jambo fulani, hasa kwenye sehemu zao wanazo"chungia"
 
Kwanza kula tano Mwanakjj. hapo umeshika kweli kweli.

We kada rahisi aheshimiwi kwa kuwa amepewa jina la rahisi,lazima kwanza yeye aheshimu nafasi aliyopewa vinginevyo haya unayoyaona na kuyasoma ni matokeo ya yeye kutoheshimu nafasi aliyopewa.
Huwezi kuwa unakunywa KANGARA hadi unalala mitaroni theni utegemee kuwa watu watakuheshimu tu eti kwa kuwa we ni rais.Hatuwezi kumheshimu rais kwa kuwa watanzania wahakumtuma kwenda kukumbatia majambazi. Yeye kaamua kukumbatia majambazi na wahujumu uchumi,hivyo akubaliane na matokeo yake.
Heshima hailazimishwi ila ni matokeo ya matendo ya mtu.
 
WAKATI WA FRENCH REVOLUTION; WATAWA NA WACHUNGAJI WA MUNGU WALIKUWA WA KWANZA CHAPWA FIMBO NA KUBURUZWA NA WANANCHI, NA WENGINE KUUWAWA, NAMI NAWAAMBIA ITAKUWA VILEVILE HATA ENZI HIZI

Pia walikuwepo alkina kada, walioona mambo kichanya tu.......

zamani katika kanisa la kikatoliki, wachungaji walitokea kuwa watakatifu kwa kumfia yes. hii ilikua baada ya kukataa amri za wafalme wao ambazo haziendani na matendo ya yesu. wengine walikuwa watakatifu kwa kuwatetea wanyonge huku wakiwapinga watawala wao na kuwakemea kwa maovu waliokuwa wanayafanya.

hao hao wachungaji wanajiita wafuasi wa yesu aliyehai. wanafanya kazi za yesu, je hizi ni kazi gani?

kada mpinzani sijui ni dini gani, ila hizi ni kazi ambazo yesu alizifanya;

1. Alikemea watawala wa dunia wanafiki, ambao wakati ule walikuwa wafarisayo, an kuwaambia kuwa kamwe wasingeuona ufalme wa mbinguni.
je, hawa wanafanya hivyo? au wanafumba midomo yao kama bubu, na kukenulia vizawadi na sadaka kubwa wanazozitoa madhabahuni? kumbuka yesu na yule bibi kizee aliyetoa dinali mbili na wale matajiri waliotoa ela kubwa, yesu alisemaje?


2. yesu aliwatuma hawa wafuasi wake kwa kusema kuwa, wao ni kondoo kati ya mbwa mwitu, na kuwa wasiogope, sasa hawa wachungaji wetu wanaogopa hawa mbwa mwitu na kujichanganya nao, hapa mbwa mwitu ni wala rushwa na wezi wakubwa. tunatarajia kazi ya zitto ifanywe nao.

je kazi hii inafanyika? la hasha, wanachojua ni kuvaa nguo nyeupe ili zisichafuke.

3. hawa wachungaji wamejikusanyia digrii za kigiriki na kusahau digrii za kimungu, wamekuwa wajanja kuliko hata mungu wao. wamekuwa waoga kuliko hata akina Mwanakijiji katikati ya mbwa mwitu. Yesu anasema sio kila aniitaye bwana bwana ataona ufalme wa Mungu, bali wale ambao matendo yao yanafana na yangu.

4. yesu hata sikumoja hakujificha kwenye hekalu, na kuongelea madhabahuni tu. alitembea hadhalani, kakemea hadhalani na kuonyesha njia iliyosahii hadhalani. ona hawa wa sasa hivi wanajificha huko waliko na kuipigia kampeni chama cha mapinduzi, na kutoa makala za kumsifia Zitto wakiwa wamejificha. Kada mpinzani unajua kwa nini wakati wa french revulution, watawa na watakatifu wa mungu "wachungaji" ndio walikuwa wa kwanza kufuatwa na kutiwa bakora huko huko madhabahuni, na Mungu wao akawafumbia macho?

sababu ni kwamba hawakufanya walilopaswa kulifanya na ndiyo maana immunity za Mungu zilikuwa mbali nao.

5.Kada Mpinzani, yesu anasema, siku ile ya hukumu, nitawahukumu kwa kuwatenganisha kama kondoo na mbuzi. nitawaambia kondoo rudini hapa na moto tayari kwa kuwaangamiza. sababu nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu hmkunipa maji, nilikuwa mgonjwa hamkuja kunitazama...... nao watasema bwana mkubwa lini tulikuona hivyo na hatukukutendea, nami nitamjibu vile vile ambavyo hamkunitendea wale ndugu zangu waliokuwa na shida ndiyo hivyo hamkunitendea mimi.

Je hawa wachungaji watawaonaje wenye njaa kama hawajishughulishi na jamii. kama hawawatetei wale wanaonyanyaswa migodini, wanaolazimishwa waende njaa kwa kutoa rushwa, au kufia njiani sababu ya ukosefu wa hospitali, au ela ya walala hoi kupelekwa mifukoni mwa wajanja huku watanzania wakilala njaa?

Kuna uwezekano hawa watu pia wakazomewa kama ilivyo sasa kwa sisiem. zomea zomea hii ilitamba hata kipindi cha french revolution, matokeo yake yakawa hivi.

TUWAPATE WAPI HAKINA YOHANA MBATIZAJI MBELE YA HERODI. au hao whawakuzaliwa na mwanamke kama akina pengo na kakobe waoga.NI UONGO MTUPU KUNIAMBIA ETI SIASA NA DINI VINATENGANISHWA, WAKATI DINI NI MAADILI NA SIASA NI MAADILI. LABDA NIELEZEE ZAIDI ILI NIELEWE ZAIDI KAMA YESU NDIYE ALIYEWEKA MPAKA. Maana yesu kusema ya mungu mpeni mungu na kaisari mpeni kaisari, na pia yesu kuonekana akitoa zaka ni dhahiri tosha kuwa yesu alijishughulisha na yote mawili.
 
JF kiboko bwana. Watu wanachambua mambo kama hawana akili nzuri vile. Nawapa tano wanaJF wote. Wale wabishi pia nawashukuru kwa kuwa wanasababisha wazee wazichambue hoja kwa ufasihi mkubwa.
Mwanakijiji na Mushobozi mmeguisa kundi muhimu sana ambalo lilitakiwa siku nyingi lipate habari hizi. Hakuna kumuogopa mtu hapa. Wachague kama wamejitolea kumtumikia SHETANI au MUNGU, tujue moja sio kukalia kula sadaka za waumini tu.
 
Mwanakijiji,
Hii makala yako ungeomba ichapishwe na magazeti ya Kiongozi na An-Nuur.
 
Back
Top Bottom