Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa dini nao ni watu ambao hawaeleweki hata kidogo, kwani inapofika mahali tunaletewa mvua za Lowassa za kichawi kutoka kwa wanaoabudu ngombe na wao wanakka kimya hapa naanza kupoteza imani kidogokidogo.
 
Sheikh Ponda awaponda mawaziri wa Kikwete

na Moses Mabula, Tabora
Tanzania Daima


ALIYEWAHI kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, jana aliingia matatani baada ya kukwaruzana na wananchi katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Batilda Burian.

Matata hayo yalijitokeza wakati Ditopile alipoomba kipaza sauti, ili kumsaidia Dk. Burian kujibu shutuma kali zilizotolewa na kiongozi mmoja wa kidini, dhidi ya mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Sheikh Ponda Alli Ponda, wa madhehebu ya Shia, alitoa shutuma hizo muda mfupi baada ya waziri huyo kumaliza kuwahutubia wananchi na kuwataka waulize maswali au kueleza kero zao.

Sheikh huyo alimtuhumu Dk. Burian kuwa miongoni mwa mawaziri wanaokwamisha maendeleo ya Serikali ya Awamu ya Nne.

Dk. Burian alikuwa katika mkutano wa hadhara, ambapo baada ya kuhutumbia kuhusu ubora wa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2007/08, alitoa fursa kwa wananchi kuuliza maswali na kueleza kero zinazowakabili.

Huku akishangiliwa na wananchi, Sheikh Ponda alimtaka Rais Jakaya Kikwete, kutowalaumu viongozi wa upinzani kwa kitendo chao cha kuzunguka nchi nzima kuwajengea chuki kwa wananchi, kwa kuwa mawaziri wake ni mafisadi na wala rushwa.

Ponda alisema uamuzi wa wapinzani unaonyesha namna walivyo na uchungu na rasilimali za nchi yao na kwamba wao ndio wakombozi wa wanyonge walio wengi.

“Ninyi mawaziri ndio mnamsaliti Rais Kikwete, lazima niseme ukweli, nasema hivyo kwa sababu nchi yetu ina amani… sioni ubaya wa rais, bali ninyi mawaziri ndio wabaya, kamwambieni rais wetu asiwalaumu wapinzani, awalaumu mawaziri wake.

“Sisi kamwe hatuwezi kupuuzia kauli za kina (Freeman) Mbowe na Kabwe) Zitto kama ulivyotuambia, wale ni mashujaa wetu… ni wakombozi wa wananchi maskini kama sisi,” alisema Ponda.

Aidha, kiongozi huyo wa kidini alisema kuwa Rais Kikwete, alipokuwa akiomba ridhaa ya wananchi wakati wa kampeni mkoani hapa, alitoa ahadi mbalimbali, ikiwemo maisha bora kwa kila Mtanzania, kupitia upya mikataba ya madini, kupambana na rushwa na kujenga barabara kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mikoa ya Tabora, Kigoma, Rukwa na Mbeya, lakini ameshindwa kutekeleza ahadi hizo hadi sasa.

Aidha, alihoji ulazima wa serikali kutumia fedha nyingi za umma kuwasambaza mawaziri na manaibu wao mikoani kufanya kazi inayostahili kufanywa na wabunge wa maeneo husika.

Kutokana na kauli hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, aliinuka na kuomba kipaza sauti ili kumsaidia Dk. Buriani kujibu shutuma hizo, hali ambayo naye ilimtia matatani baada ya kutakiwa na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kwenda kulala.

Wananchi hao walimweleza Ditopile kuwa kwa sasa hana lake ndani ya serikali, hivyo ni bora ajikite zaidi kwenye biashara yake ya asali na asijiingize kwenye masuala mazito ya serikali.

Baada ya kauli hizo, Ditopile alihamaki na kuwajibu wananchi hao kwamba wakawaambie wake zao walale na si yeye, huku akionyesha kuchukizwa.

Awali, katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya sanamu ya Mwalimu Nyerere mjini hapa, waziri Burian, aliwaeleza wananchi hao kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania kama yalivyoahidiwa, hayawezi kuja kwa kushushwa na mnyororo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtaka Mbunge wa Karatu (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, na viongozi wengine wa upinzani kuacha kuipaka matope serikali, kwa kuwa mwisho wake watajipaka wenyewe.

Nchimbi, alitoa kauli hiyo jana mjini Monduli wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri, madiwani na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa ndani akiwafafanulia kuhusu uzuri wa bajeti ya mwaka huu na mikakati ya kusimamia utekelezaji wake.

Alisema wapinzani wataendelea kupiga kelele huku serikali ikipata mafanikio kwa kasi na ifikapo mwaka 2010 wataona aibu kwa kukosa hoja za kuombea kura.

“Nawaambia mzushi yeyote katika nchi hii hivi sasa anaitwa Slaa na nimesoma katika gazeti moja la kila siku anadai eti anakwenda Marekani kueleza ufisadi wa serikali, ili nchi inyimwe misaada wakati hajui hata njia ya kuelekea katika Bunge la Congres,” alisema naibu waziri huyo kijana.

Alisema wapinzani wamekuwa wakilalamika kuhusu ziara za rais nje ya nchi ambazo zinatoa mafanikio kwa nchi wakitaka abaki ikulu kulinda njiwa, ili nchi isipate maendeleo na wapinzani wapate hoja za kuzungumza wakati wa uchaguzi.

“Wapinzani hivi sasa wanaingiwa kiwewe kuona kasi ya maendeleo ya elimu na ujenzi wa barabara, hivyo wanaanza kuwapaka matope viongozi bila sababu yoyote lakini mwisho wa wao umefika na mzushi Slaa atabainika,” alisema.

Alisema, wao kama mawaziri wataendelea kuzunguka nchi nzima kuongelea masuala ya bajeti na mbinu za maendeleo bila woga kwani tayari wanayo ridhaa ya wananchi kutekeleza waliyotumwa.
 

Viongozi wa dini za Kiislam pamoja na Kikristo TANZANIA wanatia aibu kwa kukaa kimya bila kukemea jinsi serikali ilivyo wasahau wananchi NA maskendo yanayohusiana na RUSHWA yalivyokithiri

na lawama hizi naziwakilisha moja kwa oja kwa viongozi wa KANISA ambao kwa kiasi kikubwa wanauwezo mkubwa wa kuinfluence mambo serikalini lakini so far kimya

Nasema hiv kwa sababu tunajua jinsi gani walivyokuwa na sauti na wanavyozikosoa serikali zilizopo serikalini na mfano mzuri angalia Bush na Republicans wanavyo wasikiliza hao ma evangelical Christians,hapa UK kila kukicha huyo SENTAMU wa Anglikana na MURPHY wa wakatoliki hawaiaichii safasi serikali ya BLAIR

Issue za Rushwa na Utawala bora nadhani zilitakiwa ziwe zinapewa ajenda kubwa na hawa jamaa wa kidini lakini sasa najiuliza vipi na wao wamenunuliwa?

Kwa upande wa waislam nadhani kazi ni kubwa kidogo kwa sababu hawana Kiongozi mmoja kama KADHI wa kuikemea serikali na majority ya waislam hawaitambui BAKWATA na hata hiyo Shekhe mkuuu hana nafasi sana kwani wanaona kama kawekwa na serikali na hata gari analotembelea kaewa na serikali sasa lilobaki ni kwa ma SHEKHE na MAIMAMU kuwa active katika kukosoa Serikali na kero zinazowaumiza wanainchi lakini so far naona KIMYAAA hauna na Basaleh wala Gorogosi aliyezungumzia issue ya RICHMOND

Tazama kule Kenya akina Cardinal OTUNGA walivokuwa active

Hivi Krisimasi hotuba zilkuwa nini huko makanisani?Maana najua wengi walienda makanisani lakini wanajua fika Hawana pesa za kulisha familia zao wala hawajui watakula nini wakati watawala wanaendelea kuinshi maisha kamavile wako peponi sasa hata kama serikali ikidai hakuna RUSHWA nani ataamini? the GAP between the haves and Have nots inazidi kupanuka, Kazi hakuna,Zinaa ndio kama dini,Ulevi imekuwa kawaida...sasa jamiii ya namna gani hiyo? No wonder kila kona kuna matangazo ya kuwashawishi watu wanywe ...after all pombe zetu slogan ni URITHI WETU!

Hivi kwa nini viongozi wetu wa kidini hawawi kama wenzao walioko huko LATIN AMERICA au SOUTH EAST ASIA?

Je is it far kusema kuwa nao hawa ni wala rushwa kama wanasiasa?
 
Ukisoma vizuri hiyo thread inaonekana kama ya zamani, maana inagusia serikali ya Blair (ambayo sasa haipo) pia mambo ya Krismasi ambayo hatujayafika. Hebu mtoa hoja tueleweshe una lenga wapi, maana kwa wiki sasa tumewasikia viongozi wa Dini wakishinikiza serikali kuhusu rushwa.
 
Ukisoma vizuri hiyo thread inaonekana kama ya zamani, maana inagusia serikali ya Blair (ambayo sasa haipo) pia mambo ya Krismasi ambayo hatujayafika. Hebu mtoa hoja tueleweshe una lenga wapi, maana kwa wiki sasa tumewasikia viongozi wa Dini wakishinikiza serikali kuhusu rushwa.

They are not doing enough
 
Msitumie makanisa kufichamaovu - Kardinali Pengo

2007-10-07 11:10:20
Na Sosthenes Isengwa
SOURCE: Nipashe


Waumini wa kanisa Katoliki wameaswa kuwa na maadili mema na kutotumia makanisa kama sehemu ya kufichia maovu yao katika jamii.

Hayo yalisemwa jana na Askofu mkuu wa dhehebu hilo, Mwadhama Policape Kardinali Pengo wakati alipozindua ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.

Alisema kumekuwa na waumini ambao wamekuwa wakitumia makanisa kama mahala pa kufichia maovu wanayoyatenda katika jamii na kuwataka waache kufanya hivyo na badala yake wawe na maadili mema.
Aidha baada ya kuzindua kanisa hilo aliwaonya viongozi wa kanisa na waumini kutoingiza maswala ya siasa kanisani na kwamba jambo hilo haliwezi kuingiliana na imani ya dini yao kwani ni nyanja mbili tofauti.

``Msije mkaleta siasa humu kanisani maana siasa huweza kuwagawa waumini kimakundi na kuwafanya watofautiane kitu ambacho si kizuri hata kidogo, hivyo mahala hapa panapaswa kuwa mahala pa kufanya ibada na si vinginevyo``,alisema.

Kadhalika aliwataka viongozi wa kanisa hilo kujenga umoja kwa waumini na kuwafanya wasiwe na mifarakano ili waweze kuwa raia wema hata wanapokuwa mitaani.

Kuzinduliwa kwa kanisa hilo kumefanya parokia za dhehebu hilo kufikia 54 katika jimbo kuu zima la Dar es salaam na ujenzi wake umegharimu kiasi cha pesa sh.milioni 80 mpaka kukamilika.

Kanisa hilo limejengwa ili kuwawezesha waumini Wakatoliki wanaoishi Mbezi Luis kuabudu kwa urahisi zaidi kutokana na kanisa walilokuwa wakisali awali kuwa mbali na makazi yao.
 
The traditional role of the church in Tanzania has changed dramatically. Zamani kanisa lilikuwa ni sehemu ya kuendeleza ukristo, kufundisha maadili mema ya kidini, kutoa misaada kwa wanaohitaji na kutangaza Amani. Pamoja na kuwa sasa hivi hayo bado yanaendelea ukingalia siku hizi kuna wachungaji wa ajabu kama kina Munishi, kuna mapdre ambao wanawafanyia mambo ya ajabu watoto wa kiume( wasichana imekuwa ni kawaida kabisa) na hata waumini wengine wamekuwa wanatumia kanisa kama sehemu ya refuge baada ya kufanya machafu yao na kuona kuwa jamii inaanza kuwatenga taratibu. Ingawa mimi sio mtu wa kujudge, lakini ukiangalia utagundua kuwa the church is increasing becoming a hide out of evil doers. You can ask yourself why would ........... go to Church? what is the purpose for them going there, is it to ask God to help them to steal more and lie more to us? or to ask God to forgive them for what they will do on monday? NI kuyeyushana tu kanisani siku hizi.
 
Viongozi wa dini ‘wamtwanga’ rais waraka mkali!

Mwandishi Wetu
Tanzania Daima


MHE. rais, kama tulivyodokeza hapo awali, waraka huu umetokana na mawazo yaliyotolewa na waumini wetu wa dini wa madhehebu mbalimbali tunaowaongoza. Tumeutayarisha tukiamini fika kuwa maelezo haya ni kielelezo cha mawazo ya jamii kwa ujumla. Baada ya kuyatafakari na kuyachambua, tunayawasilisha kwako kwa ufupi kama ifuatavyo.

Mamlaka ya Rais:

Tumezingatia ukweli kuwa uliingia madarakani baada ya ushindi wa kihistoria wa zaidi ya asilimia 80 ya kura za urais. Pia kutokana na umaarufu wako, chama chako kiliweza kunyakua viti vingi bungeni. Maana yake ni kwamba warembo walikupenda, walikuamini na kukupa mandate ya pekee ili uwaongoze, uwakomboe na kuwaletea maisha bora. Tumerejea pia katika hotuba yako ya kufungua Bunge iliyowatia wananchi hamasa, imani na matumaini kwamba unayo dhamira thabiti ya kuwaletea maendeleo.

Lakini miaka miwili baada ya uchaguzi, hali haijabadilika na warembo wapowapo tu kama watoto yatima. Hawajui wakimbilie wapi na wamebaki wakilalama tu, na katika kufanya hivyo, baadhi yao wamepigwa virungu, wamenyanyaswa na hata nyakati nyingine kutishiwa kwa silaha mithili ya Soweto ya miaka ya 1960! Tunaona aibu kulisema hili, lakini hivyo ndivyo ukweli ulivyo.

Mhe. Rais, baada ya tafakuri ya kina juu ya hali ya kisiasa, tunadiriki kusema kuwa bado hujaweza kushika barabara hatamu za uongozi na kuelewa uzito wa mamlaka yako ya kuliongoza taifa. Sisi tunaamini kuwa Rais wetu lazima atekeleze majukumu yake kwa mujibu wa mamlaka na madaraka aliyopewa chini ya katiba kwa umakini usiotetereka, atoe maamuzi yenye haki na uhakika na pia awe na mwelekeo thabiti. Tunatarajia Rais aelewe mandate aliyopewa na wananchi na kwamba atachagua viongozi waadilifu watakaomsaidia kutekeleza wajibu wake huo.

Na hayo ndiyo matumaini yetu sisi na warembo wote juu yako. Ukiwajibika ipasavyo Mwenye ezi Mungu atakusaidia maana mamlaka yote ya haki hutokana na baraka zake Mwenyeezi.

Hivyo basi, tunakuomba na kukuombea mamlaka yako uyatekeleze kwa haki ili uweze kulinusuru taifa hili kutokana na hayo mambo mengine tutakayobainisha hapo baadaye. Tunatambua wewe kama Kalete ni binadamu mume, mzazi, mwenyekiti wa chama tawala pamoja na mambo mengine, lakini daima ukumbuke kuwa wewe ni Rais wa Urembo, kinara na kikomo cha madaraka ya nchi hii. Tunaamini utatuelewa ili ulete mabadiliko halisi katika uongozi na kwamba utakuwa chemchemu ya uongozi bora kama ulivyoahidi Bungeni. Waswahili wamenena: “Ahadi ni deni”.

Tunakuomba pia uwe kiongozi mwenye subira na usiogope kupokea malalamiko, manung’uniko wala lawama. Umuombe Mwenye ezi Mungu akupe uwezo na busara ya kuchambua mazuri na mabaya, na kutenganisha kati ya ukweli na uongo. Wahenga wamesema: “Ukubwa ni jaa”, kwa hiyo kifua chako lazima kiwe kipana na huku ukijua kuwa urais ni dhima kubwa na nzito na haipaswi kupuuza majukumu yake.

Kwa hiyo, Mhe Rais, zidisha umakini ili wananchi wakuone hivyo na watulie, zidisha umakini wasaidizi wako waogope kuendeleza upuzi katika kazi zao na mwisho ongeza umakini ili marafiki zako na wapambe wao waweze kutenganisha baina ya mambo binafsi na kazi za umma.

Mustakabali wa taifa:

Ulipozindua Bunge miaka miwili iliyopita, ulitaja kuwa na tunakunukuu: “Mwisho nakusudia kuitisha mkutano wa kitaifa kujadili umoja wa kitaifa. Mimi nitatoa ajenda ya serikali yangu; nyinyi mtachagua wadau wote wa kushiriki katika mjadala huo … Nitawaombeni mchague wawakilishi wenye visheni, busara, utaifa, na uzalendo”. Haya ni mawazo ya busara na endelevu na tunaamini utekelezaji wake utaharakisha umoja wa kitaifa.

Wakati huo huo tunatarajia serikali yako ionyeshe kuwa ina mipango na mikakati thabiti kwa manufaa ya Warembo na kuweka vipaumbele mahsusi katika kipindi hiki cha miaka mitano, yaaani 2006/2010, bila kung’ang’ania wimbo wa manifesto ya chama chako. Hiyo ilikuwa kama “interview” ya kuombea kazi ya kutuongoza. Baada ya kushinda uchaguzi mkuu mnawajibika kuonyesha umahiri wenu katika utendaji kazi badala ya maneno ya majukwaani. Tulifurahi ulivyoanza ziara za mikoani na kuelewa matatizo yao, lakini hatuoni kama wasaidizi wako wamejifunza lolote kutokana na mfano wako. Tunahitaji “Mipango ya Maendeleo ya Taifa ya miaka mitano” itakayoainisha vipaumbele na mikakati ya maendeleo ya kitaifa. Nchi haiwezi kuendelea kwa mkakati wa kunukuu ilani ya uchaguzi tu. Ilani sio mpango madhubuti wa kuendeleza nchi. Ilani ni bla bla za chama chochote kwa ajili ya uchaguzi tu.

Katika hili, Mhe. Rais, mustakabali wa taifa utategemea mipango thabiti na miradi endelevu. Tuachane na mipango ya kukurupuka ambayo ni legelege na ya kiujumla isiyokuwa na ‘impact’ katika dunia ya sasa. Mathalan, uamuzi wa kujenga Chuo Kikuu Dodoma haukuendana na matayarisho ya kutosha. Pamoja na umuhimu wa elimu, uamuzi wa kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma wakati kuna uhaba mkubwa wa walimu hapa nchini pamoja na nyenzo za kufundishia imeonyesha udhaifu mkubwa. Matokeo yake sasa ni kuwa vyuo vikuu vingine - vya serkali na binafsi - vinahaha kutafuta walimu kutokana na walimu wao kukimbilia Dodoma. Ni kama vile serikali ‘inapoach’ wafanyakazi wake yenyewe. Pili, nini mantiki ya kuanzisha vyuo vingi vya masomo ya Arts (sanaa) wakati “uti wa mgongo wa uchumi wetu ni kilimo? Ziada ya teknohama kwa nini Chuo cha Dodoma kisiwe pia cha Ufundi na Kilimo?

Mhe. Rais, tunachosema hapa ni kuwa mipango ya kitaifa ikiwa maridhawa na miradi itakuwa endelevu. Tuondokane na miradi inayokufa baada ya msimu mmoja wa mvua. Aidha itisha mkutano wa wadau wote kwa ajili ya kupata maridhiano ya kitaifa kama ulivyoahidi pale mwanzoni na tena bila ya kujali itikadi za kisiasa za washiriki ilimradi wote ni Warembo.

Tuwahimize Warembo wajione kitu kimoja na watangulize uzalendo wao kabla ya makabila yao. Wakati tunaafiki kuwa njia mojawapo ya kuimarisha uzalendo ni michezo hususan kandanda, ni vyema tukasanifu njia zilizo bora zaidi na ambazo zitazalisha hisia za ukereketwa kwa nchi yao miongoni mwa wananchi wetu. Uzoefu umetuonyesha kuwa ushabiki wa kandanda hautabiriki na hauna uhusiano madhubuti na uzalendo. Hatua hizi nyingine zitufikishe mahali wananchi watakapojijengea hulka ya kuwa na uchungu na maslahi ya taifa. Watajiona wao kuwa ni sehemu ya taifa na si watawaliwa tu. Hatua hii itaturahisishia vita yetu dhidi ya ufisadi kwa maana kila mmoja wetu atakuwa askari muangalifu na mkakamavu wakati wote.

Mmomonyoko wa maadili:

Taarifa za ukaguzi wa mahesabu ya serikali, Takukuru, Tume ya Uongozi, na matokeo ya kesi mahakamani, pamoja na uchunguzi wa magazeti ni vielelezo tosha vya kukithiri kwa wizi, ubadhilifu na rushwa katika sekta ya umma. Vitendo hivi vimejikita kwenye ufisadi. Tutatoa mifano michache ya jumla.

Tumeelezwa mfano wa jinsi watumishi wa umma wanaotunukiwa ujumbe wa bodi za mashirika ya umma na kulipwa “marupurupu” (allowance) manono hadi sh. 500,000 kwa ajili ya kikao kimoja cha saa chache wakati daktari, mwalimu au hakimu muadilifu hapati kiasi hicho kama mshahara wa mwezi mmoja. Hivi kweli hii ni haki? Isitoshe wajumbe hao hulipwa “annual fees” za takriban sh 1,000,000 kwa mwaka, kama bakshishi wakati pensheni ya watumishi waandamizi waadilifu wastaafu haizidi sh.40,000 kwa mwezi. Huu ni mzaha wa hatari!

Mfano wa pili ni jinsi kila kukicha watumishi wa umma wanavyopanga semina na makongamano kama miradi ya kutafuna fedha. Kwanza semina hizo ni miradi ya kulamba fedha za umma au wafadhili. Lakini baya zaidi semina hizo zinapangwa kwa namna inayotoa fursa ya wajumbe kufanya mambo mengine ya kipuuzi kinyume na viapo vyao vya ndoa kwa kutumia muda na fedha za umma. Je, huu si ufisadi?

Mfano mwingine wa mmomonyoko wa maadili ni kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wadogo wa kike wanaobebeshwa mimba. Kwa vile hawajalalamikia wala kulaumu wanafunzi wenzao, ni wazi kuwa ni watu wazima tu wanaoharibu maisha ya binti zetu. Mambo kama hayo pamoja na wizi, uporaji, ubadhirifu, rushwa, ufuska n.k. ni uozo katika jamii ambao neno lake fasaha ni ufisadi. Ingawaje jamii kwa jumla lazima tubebe lawama, lakini vyombo husika vya serikali haviwezi kukwepa jukumu. Lazima serikali iache kutoa leseni holela za biashara za starehe, nyingi zikiwemo zile zinazopepelea ufuska..

Mhe. Rais, tunakuomba ukemee kwa nguvu zote nyimbo zenye matusi makavu zitokazo nchi za magharibi na ambazo hurushwa na vyombo vya habari vyote vikiwamo vile vya umma. Matusi ni matusi hata kama yatasemwa kwa lugha nyingine mbali na Kiswahili.

Aidha, nyimbo na kazi nyingine za sanaa zilizoasisiwa humu humu nchini nazo hazikubaki nyuma. Nazo zina matusi tele na udhibiti wa aina fulani unahitajika. Sinema na michezo mingine hali kadhalika. Hapo zamani kulikuwa na Bodi ya Udhibiti (Censor Board) iliyokuwa ikipitia sanaa na filamu zote kabla ya kuzitangaza ili kudhibiti yale yanayoenda kinyume na maadili yetu. Tunataka udhibiti huu urudishwe.

Mhe. Rais, vijana wetu siku hizi wanatembea uchi kabisa nasi tunaona ni sawa. Kweli, sisi wazazi wote tunao wajibu wa kurekebisha hilo kutoka ngazi ya nyumbani lakini serkali inaowajibu wa kuweka mipaka ya maadili na kuisimamia. Biashara ya ngono nayo pia imeshamiri na ukiuliza unaambiwa ni kwa sababu ya utandawazi. Tuweke mazingira ya kupunguza tabia hii chafu kwa kuwapa ajira hawa wasichana wetu na pili kubana penyu zote zinazosababisha biashara hii kufanyika hadharani kweupe kana kwamba ni biashara halali!

Mhe. Rais, tuwausie wananchi kuwa vitendo vya kujichubua ngozi ili wawe weupe ni kinyume na maadili yetu kama vile kuvaa nywele refu za singa za bandia. Ni vyema tukaanza pale tulipo, kwako wewe uanze kukemea jambo hili kwenye Baraza lako la Mawaziri, ili iwe mfano kwa raia wengine. Mbona hatuoni mtu hata mmoja akivaa wigi zenye nywele za Kiafrika? Tujaribu kuwaondolea wananchi wetu udhaifu wa nafsi yaani “inferiority complex”. Uchubuaji ngozi na mawigi ni dalili za unyonge kwa watu wetu!

Sisi tumeazimia kushirikiana na serikali kukemea maovu haya, na tunaamini serikali yako itakubali kujenga uhusiano na ushirikiano wa karibu na wa dhati na taasisi za kidini ili kujenga malezi bora na kurejesha heshima ya taifa.

Inaendelea.

jmrusufi@yahoo.com
Simu: 0763 356352
 
Huhitaji kwenda mbali kujua kama hii haitoki kwa viongozi wa kidini ( kwa maana viongozi wakuu ) Lugha iliyotumika ni ya kimitaani haifanani na lugha za viongozi wa kidini.

Inawezekana ikiwa ni viongozi wa kidini kwa maana ya self appointed leaders!
 
Hata mini sijaona uhusiano wa barua hiyo na viongozi wa dini. Labda kama kuna "muumini" aliyejiita mwanadini na kusanyiko la vingozi wa dini. Lakini as far as i know, such kind of a letter would have been edited, to suit the purpose. In otherwords, barua hiyo si ya viongozi wa dini!
 
Barua kama hii inatakiwa iende kwenye habari nyepesi nyepesi, sio hapa. Viongozi wa dini hawawezi kuandika barua kama hii, yenye mchanganyiko wa lugha.
 
Mbali na lugha iliyotumika kwenye barua hii,ila imesema hali halisi na mwelekeo wa taifa kwa sasa.Mie sijali aliyeiandika ni nani,bora ujumbe ufike,message sent.
 
maneno hayooooooo,mmmmmmmmmmm jamani mweeeeeeeeeeeee,hawa kweli viongozi wa dini?au viongzi wa dinner?Hiko ni kikuundi cha wajanja sio viongiz wa dini atall!!!
 
kuna dini nyingi sana inawezekana ni viongozi wa kikundi cha Mungiki!!
 
Message kutoka kwa viongozi wa Dini kwenda kwa Rais ina ujumbe mzuri na inaongea ukweli, ila tu lugha iliyotumika inanipa wasiwasi kwamba haijatoka kwa viongozi wa Dini!
 
Nakumbuka nilipokuwa Boarding Skull Mwalimu wa Nidhamu alinipiga marufuku baada ya kujikuta nimeanzisha ka dini kangu kalikokuwa na waumini "vimwana" watupu..sala zetu zilikuwa zikisikiwa!!
 
Ninapokaa chini kuwaandikia waraka huu wapendwa watumishi wa Mungu, ninajihisi kutostahili na kutofaa kusema nitakayosema. Mikono yangu yanitetema na vidole vyangu kama vina ganzi kwa hofu lakini moyo wangu unadunda kwa shauku. Kwenu nyote msimamao katika nyumba zetu za ibada na kuwaongoza watu wetu katika safari ya kiroho, ninyi ambao mnajua mmeitwa kumtumikia Mungu Mwenyezi katika makundi ya imani zenu mbalimbali, ninyi ambao watu huwaita “wahudumu wa Bwana” na Watendaji kazi katika shamba la Mungu, kwenu nyote Saalam!

Ninapozungumzia “wachungaji” simaanishi wale tu wa Wachungaji wa Kilutheri au makanisa ya Kiprotestanti au wale ambao wanaongoza parokia na sharika mbalimbali; na sina maana ya wale tu ambao ni viongozi wa dini ya Kikristu. “Wachungaji” ninaowazungumzia hapa ni wale ambao kwa maana ya msingi kabisa ya neno hilo, wanajukumu la kuchunga na kutoa mafunzo ya kiroho kwa waamini wao. Hapa najumlisha viongozi wote wa kidini wa dini zote na madhehebu yote, wale ambao jukumu lao la kwanza ni katika kuwaongoza watu katika mafundisho na maadili ya kidini. Wale wenye kukiri Imani ya Mitume na wale wenye kukiri Shahda, wale wenye kusimama makanisani na wale wenye kusimama misikitini. Nina maana ya wale wote ambao kimsingi wanachunga maisha ya kiroho ya watu kwa kutoa maongozo, maelekezo na mausia ya kiroho ili waamini wao waweze siku moja kufika mbinguni. Hawa ndiyo wachungaji ambao ninakusudia waraka huu.

Kwenu nyote Mashehe, Mapadre, Maimamu, Wachungaji n.k bila ya shaka mnafahamu wajibu wenu mkubwa katika maisha ya kiroho ya waamini wenu na bila ya shaka mmekuwa mkijitahidi kila kukicha kuwapatia waamini wenu mafundisho na maelekezo ambayo mna uhakika yatawasaidia kiroho. Hata hivyo ni kwa masikitiko makubwa niseme wazi kuwa kwa kiasi kikubwa mmewaangusha Watanzania. Sauti yenu haisikiki kama inavypaswa katika kuongoza “kondoo” wenu, na matokeo yake badala ya nyinyi kuwa katika kundi la wanaoongoza, sasa hivi mnajikuta mnafuata.

Ninayasema haya hasa baada ya kusoma Tamko la Baraza Maaskofu Katoliki lililotolewa hivi karibuni. Niliposoma tamko hilo nilijikuta natikisa kichwa kwa mashaka kwani walichotaka kukisema hawakukisema na wasichotakiwa kukisema walijaribu kukisema, na matokeo yake walitumia herufi na maneno mengi waliyoyapanga vizuri kwa lugha “endelevu” lakini bila kusema kitu! Ni ubutu huu ambao ninawaandikia ili muunoe na viongozi wengine wa madhehebu mengine ya dini watakapotoa tena matamko wafikirie vizuri.

Viongozi wetu wa dini mmekuwa butu! Mnameremeta kama kisu kwenye ala, na mnang'aa kama sime iliyoinuliwa. Mnapendeza kwa kanzu na majoho yenu na kwa hakika mnavutia mnapozungumza kwa maneno yaliyopangwa. Hata hivyo hamna tena makali ya kukata kwani mmekuwa butu kwa muda mrefu na sasa mmbakia kama ishara ya “kile kilichowahi kuwepo”.

Mlikuwa wapi wakati watanzania 900 walipokufa kwenye ajali ya MV. Bukoba? Mlikuwa wapi wakati wa ajali ya MV. Kilombero, ajali ya treni Dodoma, na ajali ya basi kule Singida? Leo hii Rais Joseph Kabila amemtimua Waziri wake wa Usafiri baada ya ajali nyingine ya ndege iliyoua watu zaidi ya thelathini. Hivi hapa Tanzania ni hadi watu wangapi wafe kwenye ajali zisizo za lazima ndipo wachungaji wetu mtaungana na wanaharakati kutaka viongozi goi goi wawajibishwe? Zilipotokea vurugu Mwembechai na baadaye mauaji ya kisiasa kule Pemba, mbona hatukuwaona mkiikemea serikali, vyama vya kisiasa na wananchi kwa ujumla na mkaliacha jambo hilo kwa watu wachache? Wakati serikali inanunua ndege ya bilioni 50, rada ya bilioni 50, magari mawili ya milioni mia mbili, na kuingia mkataba wa Richmond, wachungaji wetu mlikuwa wapi? Hata hili suala la sasa linaloendelea la Buzwagi na Karamagi, mbona mmechelewa kuamka na mnafumbua macho kama mliolazimishwa au kukatishwa usingizi?

Ninyi mnaojitambua kuwa ni watumishi wa Mungu, mbona mmekuwa kimya na mnagwaya mbele ya watawala wetu? Mbona hivi karibuni kiongozi mmoja wa ngazi za juu alitamka mbele ya viongozi wa dini kuwa taasisi za dini zinapojenga mahospitali n.k zinashiriki katika utekelezaji wa ilani ya CCM, mbona hamkukosoa, au zile hisia kuwa kanisa ni sehemu ya CCM zina ukweli? Kuna wakati lazima muwe mashahidi wa ukweli!

Wako wapi kina Sheikh Khalifa Bin Khamisi watetezi wa “mali” za waislamu? Je na wao wamekuwa kama CCM kuwa mali za Watanzania wote zikipotea kama zilivyopotea Benki Kuu haziwaumi, ila zile za Waislamu na za CCM ndizo huwauma? Iko wapi ile Shura ya Maimamu ambao kila baada ya muda wanatishia maandamano ili kuishinikiza serikali kufanya hili au lile? Mbona hadi leo hawajatishia maandamano kutaka kujua ukweli wa Benki Kuu, Buzwagi, Richmond, n.k ? Au ndio huo uongozi wa kidini mambo leo ambao wapendwa watumishi wa Mungu mnauendeleza? BAKWATA wako wapi wakati nchi yetu iko katika wakati mgumu?

Wako wapi wale wahubiri wa Injili, wahubirio miujiza? Yuko wapi Mchungaji Kakobe ambaye yuko tayari kukemea “mapepo” wakati watu wanatoana upepo? Ni lini ataacha kwa dakika chache kuhubiri miujiza na badala yake aje kuwajuza watu, kuhusu udhambi wa maisha ya kujikuza, na ya kutweza wengine? Haitoshi kuimba mapambio, haitoshi kusikiliza kasida, na haitoshi kushika vitabu vya dini mikononi, huku nchi na wananchi wanakosa mwelekeo katika maisha yao ya kawaida. Sala nyingine za miujiza zinaweza kuwa si za lazima endapo watu watakua na matumaini wanapoenda mahospitalini, wanapata huduma nzuri serikalini n.k

Wapendwa wachungaji wetu, ninahofu kuwa inawezekana hamkemei na kupiga vita uovu wazi wazi na pasipo utata kwa sababu ninyi nanyi mnanufaika kwa namna moja au nyingine na uongozi mbovu na tabia za kifisadi. Je yawezekana ni kwa sababu baadhi yenu wamelala kitanda kimoja na ufisadi, wakijifunika mablanketi ya unafiki, huku wanajipepea upepo wa uzandiki? Inawezekana ni kwa sababu baadhi ya miradi yenu (binafsi na vinginevyo) isingewezekana isipokuwa kwa baraka za “walio katika viti vya enzi vivunjikavyo”?

Ni wazi mara nyingi mna hofu ya kutotaka kuichukiza serikali. Tunatambua kuwa mkipiga kelele sana viongozi watawanyoshea vidole na kuwaonya, na watawaambia “fanyeni kazi zenu za dini, msiingilie serikali” Tunajua hilo linaweza kuwafanya mgwaye, kwani wanaweza wakaanzisha uchunguzi dhidi yenu au kujaribu kuwaumbua kutokana na madhaifu yenu mbalimbali kama ilivyomkuta Askofu Ncube wa Zimbabwe. Je ni hilo ndilo mnaloogopa, kiasi cha kwamba mikataba mibovu inasainiwa na hakuna mwenye ujasiri wa kuitisha Waziri Karamagi ajiuzulu au awajibishwe?

Tunafahamu pia kuwa wakati mwingine hamna ujanja isipokuwa kula sahani moja na watawala wetu alimradi mkiwaalika kwenye harambee zenu watokee, vinginevyo mnahofu kuwa michango yenu na makusanyiko yenu hayatafanikiwa. Lakini kama kilichotokea Burma hivi karibuni ni fundisho, basi kuna wakati ambapo viongozi wa dini ni lazima wafanye uchaguzi aidha kufumba macho na kuendelea kufurahia hisani ya watawala, au kuwa majasiri na kuongoza mapambano ya kifikra ili kuamsha dhamira za wananchi wetu ili tuweze kujenga taifa lile la kimaadil mnalolihubiri kila siku.

Ni kiongozi gani kati yenu ambaye atakuwa tayari kusimama juani, kuandamana, na kushika mabango na sisi wanakijiji kuihoji na kuikemea serikali? Ni nani kati yenu ambaye atakuwa tayari hata kwenda kifungoni katika harakati za kutetea haki za raia na wananchi? Itakuwa ni siku ya uamsho mkubwa tukimuona Kardinali Pengo mtaani, Mufti Simba mtaani, kina Kakobe, Mwakasege, Mwaipopo na wengine mtaani wakiongoza kelele za kutaka serikali iwajibike. Katika Tanzania ambayo viongozi wa dini na serikali hawawezi kufanya kazi pamoja isipokuwa hadi wakubaliane, na ambao hawawezi kupingana bila kuvunjiana mahusiano, ni vigumu kwa viongozi wetu wa dini kwenda kinyume na serikali na hicho ndicho kiini cha ubutu wenu.

Niwakumbushe kuhusu kiongozi mwingine wa dini ambaye alionesha kilele cha “Uchungaji Bora” siyo tu kwa kwenda jela na kufungwa, bali kutoa uhai wake mbele ya risasi muuaji. Dr. Martin Luther King Jr, alipokuwa amefungwa kwenye jela ya Birmingham kule Alabama Marekani, baadhi ya viongozi wa dini walimshangaa kwanini amekuwa anapiga kelele sana, na walimshauri apunguze makali yake kwani yeye ni kiongozi wa dini. Akiwa kifungoni, Dr. King aliandika barua yake maarufu ijulikanayo kama “Barua toka Jela ya Birmingham” (Letter from Birmingham Jail) ambayo ndani yake alieleza ni kwanini yeye kama kiongozi wa kidini hakuweza kukaa kimya. Na hata alipouwa kule Memphis, alikuwa tayari moyoni amejua kuwa ameshafika “kilele cha mlima”!

Alisema jambo moja ambalo natumani litawasha moto ya uzalendo na kusababisha mlipuko wa utumishi wa umma ndani yenu. Alisema “ukandamizaji mahali popote, ni tishio la haki mahali pote.” Haiwezekani viongozi wa dini wakakaa katika kisiwa cha mahekalu yao, huku watu wanataabika, wananyimwa haki au kwa namna moja au nyingine kufanywa duni. Ndio maana ninawauliza, mlikuwa wapi wakati vijana zaidi ya ishirini wa Kitanzania wamekwama Ukraine na kupigwa na ubaridi nje ya ubalozi wa Uingereza kisa serikali imejifanya mbabe? Mbona hamjauliza hatima yao ikoje? Na kwa nini hamkuibana serikali kutoa majibu ya kina badala ya majibu ya kibabe iliyoyatoa?

Leo hii mnaposimama na kutuhubiria maadili, hivi mnaweza kweli kusimama mbele ya Mungu mnayemtumkia na kusema ninyi ni mawakili wazuri wa maadili mnayotuambia tuyafuate? Wapendwa viongozi wa dini, wakati uko mbioni na sasa umefika ambapo mnatakiwa mfanye uchaguzi, tena uchaguzi wa haraka na wa makusudi. Nina mapendekezo machache kwenu kufikia uchaguzi huo.

Kwanza kabisa mtakapotoa matamko mengine huko mbeleni na hasa yale yaliyokusudiwa kutuma ujumbe kwa watawala wetu, acheni kuzunguka mbuyu, semeni mnachotaka kusema badala ya kutumia maneno mengi kutosema kitu! Kuweni kama Yohana Mbatizaji (Nabii Yahya A.S) na watangazieni watawala wetu kwamba wakati wa toba umefika na ya kuwa shoka limekwishainuliwa juu ya shina! Pili, vunjeni hii ndoa haramu ambayo mlijifungisha na watawala wetu na muwe huru kweli kweli. Leo hii mnashindwa kukemea maovu moja kwa moja kwa sababu mnaowakemea ni watu ambao wanawanufaisha!

Ndio maana leo mmekuwa bubu kukemea tabia ya Rais kufanya biashara Ikulu, na mmekuwa bubu mabilioni ya fedha kupotea Benki Kuu, na kwenye taasisi mbalimbali na halmashauri mbalimbali nchini. Mnashindwa kunyosha kidole kwani mkinyosha kimoja mnaogopa vitatu vinawaelekea nyinyi wenyewe na gumba linashuhudia mbinguni! Mnatetemeka mbele ya saluti na mnagwaya mbele ya vimulimuli!

Na mwisho, muwe tayari kusimama upande wa haki si kwa matamko yasiyokwisha na mausia yasiyokoma bali kwa hatua dhahiri na za makusudi. Muwe tayari kufanya kile ambacho Yesu wa Nazareti (Nabii Issa Bin Maryam A.S) alikisema kuhusu Mchungaji Mwema kuwa “Mchungaji Mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake”. Kuna siku (Mungu aiepushie mbali) ambapo Taifa letu litapitia ile “Saa ya Mjaribu” na mtatakiwa wakati huo kuchagua uhai wenu au hatima ya kondoo, natumaini mtafuata mifano ya wale walioenda mbele yenu, mifano ya kina Oscar Romero, Martin Luther King, Malcom X, na watawa wa Kibudha kule Burma ambao wiki chache zilizopita baadhi yao wamekwenda kwenye vifo vyao wakitetea haki za wananchi wenzao. Siku ambapo Taifa lenu litawaita kutoa sadaka kubwa mtakuwa tayari au mtaandika barua nyingine ya kichungaji au kuitisha vyombo vya habari?

Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu mnayemtumikia mpate ujasiri wa kusimama kama manabii na kunyosha mikono ya haki mbele zake, na kuwaongoza watu wetu siyo tu katika “malisho ya majani mabishi” ya mbinguni, bali katika kupata mana itokayo mbinguni hapa hapa duniani kwanza. Ni matumaini yangu hatamjaribu kujenga ufalme au paradiso mpya mbinguni bali mtaanza kushiriki katika kujenga paradiso ya Bongo hapa hapa duniani! Msipofanya hivyo, kama kile kinachowakuta CCM leo na nyinyi mjiandae kitawakuta, nacho ni kuwa mkianza kutuyeyusha na kutupiga soga za kizamani, Watanzania watawahesabu kuwa na ninyi hamna mpango (you'll become irrelevant) . Natumaini, hilo halitatokea. Myakumbuke maneno ya Nabii Yeremia kuwa “Ole wenu Wachungaji, wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu” Yer. 23.1

Ni mimi msafiri mwenzenu katika safari ya Kiroho,

mwanakijiji -at-jamboforums.com
 
Shukrani sana mzee,..... unaonyesha uzalendo wa hali ya juu!! Big up sana...

Hii ungeitoa kwenye magazeti ya bongo pia. Huku jambo hawafiki wengi, ni mtazamo wangu tu.
 
Back
Top Bottom