Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian, Emmaus Mwamakula, amemjibu Paul Makonda, akidai kuwa kauli zake za kulitaka Kanisa kuacha “kunyooshea kidole” Serikali zinaonesha kutolijua vizuri Kanisa na historia yake.
Akizungumzia kauli ya Makonda kwamba Kanisa linalonyooshea Serikali kidole si Kanisa analolijua, Mwamakula amehoji ni Kanisa gani analolijua kiasi cha kuwaelekeza maaskofu wajibu wao.
“Walio karibu na Makonda wamueleze kuwa sisi maaskofu tunaujua wajibu wetu na hatuhitaji kufundishwa na yeye!”.
Amesisitiza kuwa Kanisa litaendelea kutoa maoni kuhusu Serikali na masuala ya nchi, akisema kuwa viongozi wa Serikali wana vyombo vya dola huku viongozi wa Kanisa wakiwa na Biblia.
“Tutaendelea kuisema Serikali ya CCM pamoja na Serikali zitakazofuata baadaye!” amesema.