Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

maaskofi wana mbwembwe bwana!

mafisadi waliopelekwa mahakamani karibuni wote wakatoliki...bora wangeanza na waumini wao mafisadi kabla ya kumparamia JK

Mbona walikuwa kimya wakati wa MKAPA ambaye ni mkatoliki mwenzao? ufisadi huuu wa leo haukuanza leo kwani ni endelevu ya ufiadi wa Ben & Co sasa bora hawa maaskofu wakatupumzisha

My brother, hawa maaskofu sio wakatoliki ni Anglikana na vitu viwili tofauti! Soma tena habari. Lakini hata hivyo ufisadi na mambo mengine ya ovyo hayana dini na kwa taarifa yako katika watuhumiwa wa ufisadi walio mahakamani wakatoliki ninaowajua mimi ni mmoja naye ni Kweka wa BoT. Fanya uchungizi kidogo utaona hilo. Kuleta uduni kwenye mambo ya kitaifa ni ufinyu wa mawazo. Mwizi ni mwizi hata kama ni mkatoliki, mpagani au baniani. Mwenye ushaidi dhidi ya Mkapa autoe na hakuna mkatoliki atakaye mtetea. Kama aliiba aliwaibia watanzania wote regarless of religion. It is that simple.
 
we discussed this the day b4 y'day-mbona huwa unarudia thread? au husomagi kwanza za wenzio???
 
Mara nyingi katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na harakati za dini/madhehebu mbali mbali ya kidini kutoa matamko yao kuhusu uchaguzi mkuu ujao. Kwa mfano pale Serikali ilipoelezea nia yake ya kuyaondolea mashirika ya Kidini msamaha wa Kodi, tulisikia vitisho vikiibuka kuwa viongozi wa dini watawashawishi waumini wao kutoichagua CCM kwenye uchaguzi ujao. Mara tukasikia kuwa Serikali imefuta mpango wake dhidi ya mashirika hayo.

Pia kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, yameibuka malalamiko kutoka kwa waislamu kuwa Serikali haijali waislamu na ndiyo maana inasua sua kuhusu uanzishwaji wa mahakama yao, kubwa zaidi wanarejea Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005. Hapa napo tumesikia vitisho vya kutokipigia kura CCM kwenye uchaguzi ujao kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu. Kwa upande wa wakristo, pia kunawaka moto kueleza kutoridhishwa kwao na hatua yeyote itakayochukuliwa na Serikali kuanzisha hiyo Mahakama. Kwa kifupi chama Tawala kwa sasa kipo katika wakati mgumu, kiegemee upande upi.

Sasa maswali yangu ni hivi:
1. Ina maana hawa viongozi wetu wa dini inapofika kipindi cha uchaguzi huwashawishi waumini wao kukipigia kura CCM kwa matarajio kuwa watakuwa wanafaidika na uwepo wa CCM madarakani?

2. Kwa nini Kila uamuzi unaofikiwa na Serikali kama hauendani na matakwa yao kitu wanachokimbilia kufanya ni kutoa vitisho kuwa hawatokipigia kura CCM na hapo tunaona CCM ikihaha?

3. Kwa mtindo huu kuna uwezekano kweli wa kuing'oa madarakani CCM ilhali huwa wanapata Support kubwa kutoka kwa viongozi wetu wa Kiroho? (

4. Je kama wametoa kauli kuwa watawashawishi waumini wao kutoipigia kura CCM na tukaona jinsi Serikali ilivyostuka kwa hizo kauli, watanishawishi vipi kuwa hiyo siyo tabia yao yaani kuwashawishi waumini kuipigia kura CCM?

Just thinking aloud....

Nitafurahi mkinisaidia kunifumbua macho waungwana...

Mbarikiwe sana
 
Viongozi wa Dini wanafaidika kwa njia moja ama nyingine kupitia serikali ya CCM.

Waswahili wanasema "Zimwi likujualo halikuli likakwisha."
 
Haya mambo ya udini yanaanzishwa ili kuondoa focus toka kwenye ufisadi unaofanywa na serikali ya Kikwete kwenda kwenye migawanyo ya kidini.
 
Kuzitenganisha dini na siasa ni kujidanganya.
 
Hapa napo tumesikia vitisho vya kutokipigia kura CCM kwenye uchaguzi ujao kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu.
1. Ina maana hawa viongozi wetu wa dini inapofika kipindi cha uchaguzi huwashawishi waumini wao kukipigia kura CCM kwa matarajio kuwa watakuwa wanafaidika na uwepo wa CCM madarakani?
Inaelekea ndo hivyo !!
Mbarikiwe sana
Na iwe hivyo, ubarikiwe nawe pia.
 
Kuzitenganisha dini na siasa ni kujidanganya.

Sasa kama ndiyo hivyo basi hakuna umuhimu wa Serikali ya CCM kudai kuwa haina dini ilhali inaonekana wazi kuwa Uislam na Ukristo ndiyo wapiga kampeni wakubwa wa CCM na unaonaje kama huko mbeleni ikiamua kuegemea zaidi kwenye dini moja? tutamlaumu nani? Usalama utakuwepo tena kweli?

Tutafakari kwa kina.

Ubarikiwe sana.
 
Mie naona mambo ya dini na siasa yapo tangu enzi za babu zetu. Sema viongozi wetu hawa wa dini walikuwa hajahamasika katika kuiongoza jamii kutembea katika haki. Hivyo inapotokea viongozi wetu kutuhabarisha wajibu wetu kama wana jamii basi kinakuwa kizazaa. Na hii ndiyo hali halisi viongozi wetu kutuongoza katika mema. Sema darasa limeangukia pabaya kwenye uchaguzi??!!
 
Mie naona mambo ya dini na siasa yapo tangu enzi za babu zetu. Sema viongozi wetu hawa wa dini walikuwa hajahamasika katika kuiongoza jamii kutembea katika haki. Hivyo inapotokea viongozi wetu kutuhabarisha wajibu wetu kama wana jamii basi kinakuwa kizazaa. Na hii ndiyo hali halisi viongozi wetu kutuongoza katika mema. Sema darasa limeangukia pabaya kwenye uchaguzi??!!

Hapo sasa!
 
Mokiwa: Kesi za ufisadi ni usanii

​
• Ataka hatima ya mashitaka yao ijulikane kabla 2010

na Mwandishi Wetu

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Mhashamu Dk. Valentino Mokiwa, ameitaka serikali kuziendesha kesi za ufisadi kwa kasi, vinginevyo zitaonekana kama ni usanii kwa wananchi.

Pia ameitaka serikali kuifanyia maboresho ama marekebisho sheria ya makosa ya jinai inayotumika hivi sasa katika kukabiliana na matukio ya ufisadi ili iweze kufanya kazi zake kwa haraka katika kipindi hiki ambapo taifa linakabiliana na vita dhidi ya ufisadi.

Akizungumza hivi karibuni mjini Tabora wakati akitoa mahubiri katika ibada maalumu ya kuweka wakfu Kanisa jipya la Mtakatifu Stephano, Askofu Mokia alisema wananchi wameanza kupoteza imani na serikali juu ya kesi hizo, kwani hatua ya kuwafungulia mashitaka baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi haitoshi bila kuwapo kwa kasi ya uendeshaji wake na hatima yake kujulikana mapema.

Huku akishangiliwa na umati wa waumini wa kanisa hilo mkoani Tabora, akiwamo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, Askofu Mokiwa alisisitiza kuwa ugoigoi katika kuharakisha kesi za watuhumiwa wa makosa ya ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, unakwaza wananchi japo kuwa serikali inajitetea kwa kusema sheria ni msumeno.

“Ingekuwa vyema kwa serikali kuwa na utaratibu kama unaotumika katika hospitali za umma kama Muhimbili na zile za binafsi wa huduma za haraka, yaani (first track) katika kushughulikia kesi za mafisadi, kwa vile wameangamiza nchi na kusababisha madhara makubwa kwa jamii,” alisema Askofu Mokiwa.

“Kufikishana tu mahakamani si njia ya kuwafanya wananchi kujenga imani na serikali, lakini hatima ya kesi na uchunguzi wake unaweza kurudisha imani za wananchi hao kwa serikali yao na hili tunataka kuiuliza serikali, kulikoni na ufisadi? Mnataka kila Mtanzania ajiuliuze swali hili?” alisema Askofu Mokiwa.

Kuhusu kufutwa kwa misahama ya kodi kwa taasisi za kidini na baadaye kurejeshwa upya, Askofu Mokiwa alisema anasikitishwa na baadhi ya viongozi wa serikali kushangilia hatua ya serikali ya kufuta misamaha ya kodi kwa asasi za kidini kwa vile kuna baadhi ya viongozi wa makundi hayo wamekuwa wakiitumia vibaya misamaha hiyo.

“Ni kweli inawezekana kuwa wapo baadhi yetu na hili nalisema ili kila kiongozi wa kidini, kwa vile sisi si malaika, kujichunguza na kubaini kama anafanya hivyo atubu, kwani hiyo ni dhambi mbele ya Mungu wetu, lakini pia mbona kesi za ufisadi zinaonekana kama ni usanii kwa wananchi?” alihoji Askofu Mokiwa.

“Ninawaomba mtoe kwanza boriti katika macho yenu ndipo mpate vibali vya kuona boriti katika macho ya wenzenu, viongozi wa umma na dini ni kitu kimoja na inawezekana askofu kama mimi na wengine wakaingia katika mkumbo wa ufisadi, ninadhani jinsi ya kushughulikia kesi zao itofautiane na ile ya watu wa chini, kwa nia ya kuonyesha msimamo wa dola,” alisema Askofu Mokiwa kwa kujiamini na kuongeza kuwa ni vyema kesi hizo zikamalizika kabla ya mwaka 2010.

Huku akimkazia macho Spika wa Bunge, Sitta, Askofu Mokiwa alisema wananchi wana imani kubwa na Bunge, lakini pia kuna dalili kwamba chombo hicho cha maamuzi, kinazidiwa nguvu na mamlaka nyingine zilizopo nchini na kuhoji, suala la kashfa ya Richmond linawezaje kumalizwa kwa baadhi ya viongozi kujiuzulu tu.

Waliojiuzulu kutokana na kuguswa kwa kashfa hiyo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa (Monduli).

Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi; na aliyekuwa akishikilia wadhifa huo kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha.

“Ina maana kujiuzulu tu kwa nafasi za viongozi wetu katika sakata zito la Richmond inatosha? Na hii ina maana gani? Je, ni kwa ajili ya kuhakikisha watu wa aina hiyo wanaendelea kupewa heshima ama ndiyo sifa ya kuwapo kwa utawala bora?” alihoji Askofu Mokiwa huku mamia ya waumini na viongozi wa kanisa hilo wakimshangilia.

Ingawa Askofu Mokiwa hakutaja majina ya watu waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ni aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gray Mgonja.

Mwingine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona. Yumo pia Amatus Liyumba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wafanyabiashara maarufu, ambao wanakabiliwa na kesi hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Pia askofu huyo alielezea umuhimu wa kulinda amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu mwakani, kwa kuwataka wananchi kutowachagua viongozi wanaotaka kuingia madarakani hata kama damu itamwagika.

Aliposimama kutoa salamu zake kutokana na mwaliko aliopewa na kanisa hilo, Spika Sitta hakusita kuonyesha jinsi anavyokerwa na suala la ufisadi na kwamba, ndiyo maana yuko mstari wa mbele kukabiliana nalo.

“Ndugu zangu, kwanza nawashukuru kwa kunipa heshima hii kubwa, najisikia mwenye raha ninapokuwa miongoni mwenu, lakini nawaomba niungane na Baba Askofu, kukemea tabia ya ufisadi katika jamii, kwani si nzuri,” alisema Spika Sitta.

Spika aliongeza kwamba ufisadi umechangia kuharibu miundombinu katika jamii, ambapo hali hiyo imesababisha kukosekana kwa maji salama ya kunywa na kuwafanya wananchi wengi kunywa maji machafu, hali inayochangia vifo vya kina mama na watoto wadogo.

“Kwa uhakika ninachukia ufisadi, na hata nikiwa bungeni ninalalamikia suala hili kwa nguvu zangu zote, lakini nimekuwa nikishikilia msimamo wa Kibiblia, ambapo kuna mahala kitabu hiki kitakatifu kinasema kwamba, “Mtetezi wangu yu hai na ananipigania katika mazito yote ninayoyapitia,” alisema.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mama Margaret Sitta, aliyemwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alisema serikali iko tayari kushirikiana na taasisi za dini katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Source: Tanzania Daima
 
Ni vema wafanye hivyo ili kutorudia ya 2005 ya kusema mgombea ni chaguo la Mungu na hadi leo ni kichekesho.

Viongozi wa kanisa walisema JK chaguo la Mungu, hivi Mungu anakoseaga?
Wakuu mmesoma 1st post lakini? Ni maaskofu wote walosema 'JK ni chaguo la Mungu'? Au ndio samaki mmoja akioza wameoza wote?

BTW: Tumeifanyia editing hii topic ili kuweza kuweka records vizuri hasa kwa kuweka references kwenye 1st topic. Hii ni mada ya tangu 2006
 
Duuh, naona topic imefanyiwa highl evel referencing na editing...watu watakaopotea njia tena hao watakuwa wamedhamiria!
 
2010 itatoa jibu,mchakato si umeanza tuone kama wananchi watadanganyika tena.
 
Viongozi wa dini za Kiislam pamoja na Kikristo TANZANIA wanatia aibu kwa kukaa kimya bila kukemea jinsi serikali ilivyo wasahau wananchi NA maskendo yanayohusiana na RUSHWA yalivyokithiri

Na lawama hizi naziwakilisha moja kwa oja kwa viongozi wa KANISA ambao kwa kiasi kikubwa wanauwezo mkubwa wa kuinfluence mambo serikalini lakini so far kimya

Nasema hiv kwa sababu tunajua jinsi gani walivyokuwa na sauti na wanavyozikosoa serikali zilizopo serikalini na mfano mzuri angalia Bush na Republicans wanavyo wasikiliza hao ma evalengical christians,hapa UK kila kukicha huyo SENTAMU wa Anglikana na MURPHY wa wakatoliki hawaiaichii safasi serikali ya BLAIR

Issue za Rushwa na Utawala bora nadhani zilitakiwa ziwe zinapewa ajenda kubwa na hawa jamaa wa kidini lakini sasa najiuliza vipi na wao wamenunuliwa?

Kwa upande wa waislam nadhani kazi ni kubwa kidogo kwa sababu hawana Kiongozi mmoja kama KADHI wa kuikemea serikali na majority ya waislam hawaitambui BAKWATA na hata hiyo Shekhe mkuuu hana nafasi sana kwani wanaona kama kawekwa na serikali na hata gari analotembelea kaewa na serikali sasa lilobaki ni kwa ma SHEKHE na MAIMAMU kuwa active katika kukosoa Serikali na kero zinazowaumiza wanainchi lakini so far naona KIMYAAA hauna na Basaleh wala Gorogosi aliyezungumzia issue ya RICHMOND

Tazama kule Kenya akina Cardinal OTUNGA walivokuwa active

Hivi Krisimasi hotuba zilkuwa nini huko makanisani?Maana najua wengi walienda makanisani lakini wanajua fika Hawana pesa za kulisha familia zao wala hawajui watakula nini wakati watawala wanaendelea kuinshi maisha kamavile wako peponi sasa hata kama serikali ikidai hakuna RUSHWA nani ataamini? the GAP between the haves and Have nots inazidi kupanuka, Kazi hakuna,Zinaa ndio kama dini,Ulevi imekuwa kawaida...sasa jamiii ya namna gani hiyo? No wonder kila kona kuna matangazo ya kuwashawishi watu wanywe ...after all pombe zetu slogan ni URITHI WETU!

Hivi kwa nini viongozi wetu wa kidini hawawi kama wenzao walioko huko LATIN AMERICA au SOUTH EAST ASIA?
Unatoa ushauri..ushauri ukitekelezwa inakuwa tatizo tena. Baada ya kusoma maneno yako yenye ushawishi kama haya, kwakuwa hawana political platform to mobilize mass, the church prepared the document as guideline to the voters. Pengine inayochezwa hapa ni mind game
 
maaskofi wana mbwembwe bwana!

mafisadi waliopelekwa mahakamani karibuni wote wakatoliki...bora wangeanza na waumini wao mafisadi kabla ya kumparamia JK

Mbona walikuwa kimya wakati wa MKAPA ambaye ni mkatoliki mwenzao? ufisadi huuu wa leo haukuanza leo kwani ni endelevu ya ufiadi wa Ben & Co sasa bora hawa maaskofu wakatupumzisha
Shadia, RA na yule bosi wa TICTS nao ni wakatoliki wabobea?
 
Ni ujumbe mzito sana lakini unahitaji watu makini na wenye uelewa mkubwa sana kuhusu masula ya jamii kuweza kuchangia hii maada ndipo tutakapo kuwa tumetimiza malengo ya hii forum na slogan yake ya "The Home of Great Thinkers".

Ili viongozi wa dini waweza kuikosoa serikali kwanza inabidi wao wenyewe watenganisha siasa na dini,wawe ni watu ambao ni model kwenye jamii na siyo vinginevyo.Makanisa na misikiti laziwe zijiendeshe zenyewe na siyo kutegemea misaada kutoka serikalini, sasa kama shehe mkuu anatembelea gari alilopewa na serikali, so what do you expect from him?? lazima hata sisi waumini tuchukue hatua ya kuhakikisha kuwa viongozi wetu wa dini wanapata mahitaji yote muhimu na ikibidi hata kuwanunulia hayo magari ili wawajibike moja kwa moja kwa serikali,Ni viongozi wachache sana wa dini ambao huwa wanapata udhubutu wa kuikemea serikali na huwa waonekana kwa jamii kama ni wanasiasa, lakini hayo yoye yanatokana na jamii kutokuwa na mtazamo positive, wamekuwa ni watu wa kudanganywa, kuambiwa cha kufanya bila hata kufikiria bje hicho kitu kinafanyika au laa!!

Tukitaka hao viongozi wa dini watusaidie ni lazima jamii ikubali kubadilika kimtazamo, la sivyo hakuna chochote kitakachofanyika hata kama watakesha kutuelimisha, nini ambacho hatujui mpaka sasa kuwa viongozi wengi walio madarakani ni wala rushwa,wabinafsi na wenye kujali maslahi yao binafsi, lakini mbona ikifika kipindi cha uchaguzi watu tunapewa kanga, kofia na chumvi na still tunawachagua tena,mimi naamini itakuwa ni upuuzi usiokuwa na kikomo kuwatupia lawama hao viongozi wa dini eti hawakemei serikali kwa maovu na ufisadi unaoendelea hapa nchini, wakisema mtasema tena wamekuwa wanasiasa,

TUKUBALI KUBALIKA KIMTAZAMO KWANZA ILI ELIMU ITAKAYOTOLEWA ITUSAIDIE NDUGU ZANGU.
 
TAFAKARI. Hivi kuna mtu mwenye utu, akili, busara na hekima anayeweza kukataa zuri akakubali baya; au wema akakubali maovu; au la faida akakubali la hasara na la ibada akakubali la ukafiri ?

Haiyumkiniki iwe hivyo ila pale palipo na sababu maalum, iliyofichwa na inayojengewa ajenda ya kuwakatili au kuwadhuru binadamu wengine.

Ni dhahiri kwamba ingawa hatulitarajii hili, ukweli ni kuwa kati yetu binadamu wapo mashetani au tuseme mashetani-watu. Hawa sio wengine ila wale wote wanaolipinga zuri na jema analotaka kulifanya mwenzao au wale wote wanaoshangililia wakati wote mwenzao kukosa, kudhulumiwa, kuonewa, kunyanyaswa, kugandamizwa, kufungwa au hata kuuawa. Je, watu wa namna hii wapo au hawapo ? Jibu aghalabu ni kwamba wapo. Na kama
wapo hao ndio haohao tunaowaita mashetani-watu miongoni mwetu.

Na watu hawa wanakuwa hatari sana pale wanapojikusanya katika kundi moja linalojipa heshima na utukufu wa kujipachika mbele ya wanajamii. Na kauli zao ukizisikia utawajua tu kwamba hawa ni watu wa namna gani. Ni watu wenye uwezo wa kuwa mitume kaitka miaka hii, ni watu wenye uwezo wa kuwafanya binadamu kuwa watakatifu kama Mungu, na ni watu wanaoweza kuwafutia hata binadamu madhambi yao -yawe yale ya kuzaliwa na yale ya kufikia!

Katika miaka hii ya uwezekano wa kuwepo miongoni mwetu kwa 'the Anti-Christs' au wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na mitume yake tunachukulia vipi vitendo na matamshi toka kwa watu walioshikilia nyadhifa za juu katika taasisi mbalimbali za kiuchumi na kijamii, zikiwemo pia zile za imani na kidini.

Ni vizuri ifahamike kwamba hivi leo duniani kuna jambo linaloendelea ambalo ni
hatari sana kwa utu na ubinadamu lakini ni wachache sana wanaojua kinachoendelea.

Na jambo hilo sio kitu kingine bali ule ukweli kuwa WATU WALIOKUWA WAOVU, WENYE ROHO MBAYA, DHULUMATI, WAUAJI, WABAKAJI, WEZI na kila aina ya ubaya unaoweza kuutaja hivi sasa wako katika mbio za kukamata kila ofisi ukubwa ili waweze kuficha meno, kucha na ndimi zao zenye moto unaounguza kila unachogusa ili waweze kufanya madhambi yao bila kujulikana na mtu.

Kwa mfano, mtu ambaye anajua kazaliwa ni mwizi au jambazi anapohaha kusoma na kuingia kwenye tarafu ya uaskari au uanasheria sio kwa sababu ya kuja kutenda mema au kuwa polisi au hakimu muadilifu bali ili aje kuiba, kudai rushwa au hata kuua kwa makusudi anaangukia katika fungu hili.



Aidha mtu anayesoma na kujiendeleza ili aje awe kiongozi wa dini fulani sio kwa
sababu ya kuja kumtumikia Mungu kiwelikweli bali ili aweze kufanya madhambi kama vile Uzinifu, wizi na kuchonganisha dini moja dhidi ya dini nyingine, au jamii moja dhidi ya jamii moja au wananchi na viongozi wao, au dini yao na viongozi na kadhalika pia nao wanaangukia ndani ya kundi hili.


Na ndivyo ilivyo pia kwa wanasiasa. Wapo wengi wenye nia na ajenda zao za siri tofauti na maslahi, mahitaji na matakwa ya wale wanaowaongoza. Viongozi kama hao wengi wao hawakutaka ukubwa au uongozi kwa sababu ya kuwasaidia wananchi waondokane na matatizo mbalimbali yanayowakabili kimaisha, kikazi na kijamii au kuwanufaisha wananchi kwa njia moja au nyingine ila kwa wao kujijenga na kujifaharisha juu ya damu na mifupa ya wananchi wanaosemekana kuwaongoza.

Basi katika miaka hii ya kuja na kuwepo kwa kina ' anti-christs' ni muhimu
kuzichunguza kauli za watu wote wenye dhamana katika jamii yetu.

Inafaa kujiuliza hivi fulani analolizungumza linatokana na AKILI YAKE ? Na je,
tunakumbuka kwamba akili ni nywele na kila mtu ana zake. Na akili hiyo ni
kujinufaisha yeye mwenyewe, jamaa zake na kundi aliloligeuza buzi lake au ni akili zinazotokana na uzima wa roho na kutambua mtu alikotoka na anakokwenda. Tukibaini kwamba wale wanaotambua walikotoka na wanakokwenda wanajua fika wao ni watu wa kupita tu na siyo yale wanayoyataka wao yafanyike ndiyo yanayofanyika bali ni yale
anayotaka Muumba wa Mbingu na Ardhi peke yake ndiyo yanayoweza kuwa au yasiwe kwa
amri yake.

Ni miaka ya kujiuliza kama yanayofanyika au kuamuliwa yanatokana na MOYO na hivyo matamanio ya mtu na sio yale yastahili kufanyika pindi pale watu wanapokubali uongozi na usimamizi wa aliyewaumba? Kuna vingi tunavyovitamani kuvibadili na kuvipata lakini sio vyote tunavyoweza kuvibadili na kuvipata. Tutabadili na kuvipata tu vile tunavyojaliwa kuvibadili na kuvipata.

Lugha ya miili yetu daima imekuwa ni sababu kubwa ya kuhadaa na kuwazaini wengine. Kwa nje tunaonekana ni watu wenye nia njema na utu na ubinadamu kwa wengine lakini ndani ya miili yetu tumejaa husuda, inda, roho mbaya, uzandiki, tadi, roho ya korosho, ufisadi, ufuska, uhayawani na kila asilolipenda aliyetuumba. Tunapenda kuonekana wazuri mbele ya macho ya wafuasi wetu na wale 'tunaowapa riziki' kwa njia moja au nyingine lakini mizani ya matendo yetu sikuzote imelemea uovu, ubaya na uhanaharamu wa kutupwa! Miili yetu imekithiri kwa tamaa ya kula, kunywa, kuvaa,
uzinifu, kujilimbikizia, kujipachika umaarufu na utukufu lakini tungeliweka katika
mizani ya kupimwa kama tunastahili hivyo aghalabu wengi tungejikuta ni wapungufu kiasi cha kutisha!

Kiongozi na uongozi uwe wa nchi, kanisa, msikiti, chuo, shule, kijiji, mtaa na
kadhalika sio biashara ya watu wanaotawaliwa na akili zinazowadanganya kuwa waongo, wezi na watu wasioheshimu haki na usawa; uongozi sio dhamana mustakabala kwa mtu anayetawaliwa na matamanio ya kila aina yakiwemo yale ya yeye kuonekana binadamu bora zaidi kwa mali na vitu alivyo navyo; na aidha uongozi sio mahala pa kuendeleza tamaa za kimwili jambo ambalo ni ngazi ya chini na ya mwisho katika mpangilio wa mambo yaliyo bora kwa mwandamu kuwa nayo.

Hili likieleweka ipo fursa maridhawa ya kuchuja na kuwachagua watu ili watu
mbalimbali watakaongoza jamii ya leo na kesho wawe ni kati ya wale walio bora miongoni mwetu. Na hakuna mtu aliyebora kama Mcha-Mungu kikweli kweli na hakuna aliye mbaya kama mnafiki, mshirikina na hayawani kuwa kiongozi.

RWANDA
Huko Rwanda watu waliojifanya watukufu na watakatifu kupitia kanisa walifikia mahala pa kuamua kwamba kabila moja ni bora kuliko kabila jingine. Na kwa kutumia makanisa hayo hayo wakawaangamiza mamilioni ya waumini wao waliokwenda huko ili kunusurika na mauaji yaliyokuwa yakiendelea. Hapa Tanzania kuna kundi la watu lililozuka ambalo LIMEKAZANA kuonesha kuwa dini moja ni bora kuliko nyhingine; kwamba wanasiasa hawajuia kazi yao ya uanasiasa kama wao wanavyoijua kazi hiyo; kwamba mawaziri
hawajui kutunga sheria kama wao wanavyojua kutunga sheria hizo, na kwamba watumishi wa umma hawajui kazi zao kama wao wanavyozijua kazi hizo na kwamba wao pengine kwa kuchaguliwa na Mungu, kikiwa kikundi cha watu wasiozidi hamsini wana akili nyingi mno kuliko WATANZANIA WOTE MILIONI 40 wakiwekwa upande mwingine. Je, hapa jamani ni
vigumu kutabiri kwamba nchii hii inaburuzwa kuelekea wapi ila kama sisi sote ni
viziwi na vipofu!
​
 
Back
Top Bottom