Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Waraka huu umepatikana tarehe 29 June 2009,ulikuwa ukisemwa kuwa upo zamani na sasa umetiwa mkononi. Hizi ni hila za kanisa kwa Tanzania nzima mafanikio waliyoyapata huko Tanganyika sasa wanayaelekza Zanzibar lakini wameumbuka na hila zao mbaya sana za kujidai kutaka kusaidia na kutoa misaada ,ni aibu ilioje kwa wakiristo kuwa na mipango iliyovishwa ngozi ya kondoo ,yaani imejulikana hata ile mihadhara ya waislamu wao ndio sababu ya kuzuiwa na wakiwatumia wanaowaita watu wao ndani ya serikali ,huu ni ukweli uliokuja juu ,kila Muislamu anatakiwa afahamu na ikiwezekana nakala zipelekwe misikitini ili kuzidi kuuamsha umma wa Uislamu juu ya ubaya wa waliokuwa wakiwaona ni ndugu zao wanaopaswa kuishi pamoja ,kama ilivyokuwa imezoeleka ,kumbe ndugu zao hao wana mikakati ya siri..
___________________________________Endelea.....!



Wapendwa katika Bwana

Ndugu Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa Zanzibar, yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna yoyote. Hapana shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa bado ni ndogo sana na wengi wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio Wazanzibari kama wanavyosema wenyewe.


MAFANIKIO YETU
Kabla kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi sasa. Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa tumsifu Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui zetu. Tunaamini kuwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, Bwana atatupa ushindi na mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu wazidi kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha Zanzibar kidemografia ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho. Mafanikio yetu yameenea katika kila upande - katika uchumi, siasa, huduma za serikali, umiliki wa ardhi, ujenzi, elimu, n.k

1. Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekua ya kuridhisha kupitia nafasi za serikali. Hivi sasa ni rahisi na limekua jambo la kawaida katika kila matangazo ya wito wa masomo kusikia majina ya Wakristo. Kati ya vijana saba hadi kumi, ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka katika makanisa yetu.

2. Sambamba na matangazo ya elimu vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi nyingi za ajira katika Serikali ya Zanzibar. Hali ya kutoelewana kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika zaidi kuliko vijana wa Zanzibar

3. Hali tulioieleza juu imetuwezesha kuwa na Wakirsto wengi katika nafasi za juu serikalini na katika chama tawala.Hali hii ni lazima iendelezwe katika ngazi zote kwani imekuwa ikitusaidia hasa katika kiwango cha masheha na kamati zao kwani huku ndiko kunako mambo mengi ya kila siku.

4. Tumepata fursa ya kutumia Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada zetu hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na inaweza kutupa nafasi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA.

5. Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa mabayo hapo awali hayakuwepo.

6. Idadi ya skuli na vituo vyetu vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli hizi nikuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo Mji Mkongwe (Stone Town Youth Centre) na zinafanya kazi vizuri katika kupandikiza mila za Kikristo.

7. Sera ziliopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji Zanzibar imetusaidia sana katika uingiaji wetu (Wakristo) kutoka Bara na hivyo kusaidia kufuta ile imani ya kuwa Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu na eti Wazanzibari kwa zaidi ya aslimia 99 ni Waislamu.

8. Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka bara umewezesha kuongezeka kwa idadi ya mabaa na klabu za pombe.

9. Kujiingiza kwetu katika Taasisi za dola katika ngazi za mitaa kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara.

10. Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya Mjini ambayo yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa, Mwanakwerekwe, n.k. ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje kwa sasa hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni matupu.

Ndugu wapendwa katika bwana,
Mafanikio hayo yasitufanye tuka lewa na kusahau jukumu la kanisa la kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo. Kosa lolote tutakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa na huenda nafasi hii tulionayo hivi sasa tusiipate kwa karne mpya ijayo. Mambo ya kufanya yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu na kuona yale tuliokwisha yapata hayatutoki na kuyafanyia dira kwa karne ijayo ni haya yafuatayo:

Tusahau tafauti zetu dhidi ya adui

Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana na mila na utamaduni hivyo kila itakapowezekana tusahau tafauti zetu ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vyenginevyo tutarudi kama wakati wa Karume

Tuhakikishe tunapata ardhi
Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika jitihada waliyofanya ni kupata ardhi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu majengo ya hospitali shule zahanati vituo vya chekechea makanisa n.k. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya bwana na Muokozi wetu.

Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa makanisa
Inaonesha Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji kwenye sirikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata viwanja kwa ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu ni kununuwa viwanja vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa itayowashawishi kuviuza na baadae tutaweza kuvijenga au kugeuza nyumba hizo kuwa makanisa.

Tujenga shule na hospitali kwa wingi
Hizi ni taasisi pekee ambazo tunaweza kuzitumia kueneza neno la Bwana kwa Waislamu walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umasikini unaowakabili wengi ya Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri, tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei ndogo kuweka upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali visiweze kuvikaribia vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza mafundisho yetu, zaidi kwa watoto wadogo (Nursery).

Tunadai muda zaidi katika Vyombo vya habari (Tv na Redio)
Kwa muda mrefu sasa uislamu na waislamu wamehodhi vombo hivi vya habari mbali na kuwa siku ya ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi vya kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyengine kadhaa kwa vipindi vya kiislamu na hata kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali kupendelea uislam ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka 25 ya TVZ tulizungumzia suala hili lakini inaonekana halikupata mtu wa kulifanyia kazi. Sasa tuhakikishe kuwa ukristo unapata muda zaidi katika vyombo hivyo au uislam nao upunguziwe nafasi.

Tuongeze mihadhara ya wazi
Wakati Waislam wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Kwa kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone wakristo wa Mjini na Mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria. Vipaza sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la bwana linafika kila pahala. Mihadhara ifanyike karibu na nyumba, misikiti na kwenye viwanja vya wazi.

Tuendelee kutumia shule na sehemu za Umma
Ili kuwafanya waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni lazima kuendelea kutumia mashule na sehemu za Umma zilizo wazi kwa mambo yetu ya ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona tafauti kati yetu na wao.

Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi
Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari waislamu. Hali hii inafanya ongezeko la wakristo kuwa dogo au halipo kabisa ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za kikristo.
Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na Taasisi zetu ni kuongezeka kwa wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo wengi kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa kutumia udugu wetu wa kikabila au asili ya Bara.
Kwa kuwatumia ndugu zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe kuwa suala la uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali
.

Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au vitambulisho
Wakristo tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua kufanya cho chote ili kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa wazanzibari pekee basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu kwa Zanzibar.Jitihada zozote za kuiimarisha Zanzibar kama Zanzibar na nje ya Utanzania ni lazima tuelewe kuwa Uislamu utapata nguvu na kuwa tishio kwa hapa Zanzibar na hata Bara.Iwapo tutawajibika kuunga mkono ni kadi za Uraia na vitambulisho vya Watanzania kwa Ujumla na sio Zanzibar peke yake.

Tujipenyeze Vyamani na kushika nafasi muhimu
Lazima tuelewe kuwa chama cho chote cha siasa kinalenga kukamata serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa ni mazuri kwa chama hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha zaidi kwenye CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika chama tawala na katika jumuia zake.

Tupenyeze wenzetu serikalini
Sambamba na suala tulilolielekeza juu hatuna budi kusomesha vijana wetu na kuhakikisha kuwa tunatumia kila njia na ushawishi ili kuwaingiza serikalini na hasa katika sehemu muhimu. Hii itarahisisha kuungwa mkono mipango yetu na kupunguzwa vikwazo kwa mikakati yetu.

Tuunge mkono sera za utalii
Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanzibar hutokea nchi za Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake

Tujenge mabaa na kuongeza pombe
Waislamu wengi huchukia pombe na huweza kuhama iwapo duka la pombe au baa ipo karibu nao. Waislamu hatari ni wale wanaosoma na kupata muda wa kujishughulisha na dini yao. Pombe ni kitu ambacho humtoa Muislamu katika Uislamu wa vitendo na kumkaribisha na Ukristo.

Tuwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie Ukristo
Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo katika matatizo.. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha kabla hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa kuanzia ili Bwana awateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyo.

Tuwafuate wanawake kwa misaada
Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwamkono duniani kote na hasa zile za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia wanawake kwa jina la kuwasaidia.


Tuongeze vituo vya mafunzo ya kikristo

Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Centre) kimekuwa kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali (bado) halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbali mbali, jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili za kidini.


Tuwaowe wanawake wao kwa kusilimu kimajina

Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo patakuwa na ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake wao.


Tuanzishe NGOS na sisi tuwe viongozi

Kwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia ngos moja kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya zetu ambazo zitawashirikisha waislam lakini uongozi wa juu ni lazima uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na malengo yetu yanatekelezwa kwa kivuli hicho.


Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti waislam

Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbali mbali baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha na matawi ya vyama na kamati za maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima iongezeke ili udhibiti wa shughuli za waislam uwe mzuri zaidi na wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya vyombo vya dola na vyama vya siasa. “Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti waislam”.


Tuwachonganishe mashehe wenye msimamo mkali

Mashehe wenye msimamo mkali wamekuwa ni tatizo kwa ukristo kwani wana wafuwasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo hatuna budi kuwaunga mkono mashehe wote ambo wamekuwa wakitusaidia kwa njia mbali mbali

Tulenge kuifuta tabligh

Pamoja na kuwa tabligh sio hatari moja kwa moja kwa ukristo lakini bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ni aina pekee ya mihadhara ya waislamu inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua baadhi ya waislam ambao ni vyema kubaki bila ya kuzinduliwa.


Tudai turudishiwe taasisi zetu

Serikali ya Zanzibar bado inaonekana kuwa ngumu kurudisha katika milki ya makanisa ardhi na taasisi zetu. Dalili za huko nyuma zilionekana nzuri kwani tulifanikiwa kupata hospitali yetu ya Welezo na eneo la kiungani hata hivyo panakuwepo ugumu wa kurudishiwa shule zetu. Kwa kuwatumia wenzetu waliomo serikalini na baraza la wawakilishi lazima tuzidishe harakati na madai ya taasisi zote zilizobaki.


Tulete waumini kutoka mashamba kujaza makanisa

Hivi sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa utaratibu uliopo hivi sasa chini ya baadhi ya makanisa ni lazima uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi hufikia mashamba hivyo pawekwe na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza makanisa.


NENO LA MWISHO

Wapendwa katika Bwana.

Miongozo hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata hivyo kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu ni haya kufahamika na kila mkiristo apendae kumtumikia Bwana. Pia hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya mapinduzi ambao imefungua milango kwa ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa.

Bwana awe nasi!

------------------------------------------------------------------------

hii ni aibu kwa Wakristo ,hizi ni mbinu ambazo zimeshafanyika huko Tanganyika na zinaendelea kufanyika na sasa na kwa miaka mingi zimekuwa zinaelekezwa Zanzibar na siku hizi imekuwa sio siri tena hata makanisa yanaingilia shughuli za serikali kwa kisingizio cha kuleta huduma nzuri ,kumbe nyuma ya pazia ni mbinu za kuiteka Tanzania ila hamtafanikiwa kwani huku peke yake ni tosha kuwa mumeumbuka na mtazidi kuumbuka hadi mshindwe na mlegee.
 
Asalam Aleikum Ndugu zangu, kwa wenye na wasio na imani kama ya kwangu.

Leo hii mijadala kwenye RADIO, TV na MAGAZETI waandishi na watangazaji wakiwaalika wanasiasa wakongwe, watu wa nyadhifa mbalimbali hamwe na viongozi wa dini ikiwa ni kuwahoji au kutaka mchango wao juu ya nilichoamua kuwaletea leo hii hapa jamvini "Viongozi wa DINI kujihusisha na siasa! nani alaumiwe?. wengi huukimbia ukweli na kubaki kung'ata ulimi. Mbona liko wazi ile mbaaya.

Kutokana na serikali kuchemsha hasa katika utoaji wa maamuzi, ndio maana viongozi wa dini wameamua kujitosa na kuleta miongozo ambayo watu wa madhehebu yao au/na jamii nzima kuufuata.

Kabla ya kulifikiri kwa kina hili, nilikua naogopa sana na kuhisi kwamba Tanzania sasa inaelekea kwenye udini, lakini sasa baada ya ku recall baadhi ya matukio naamini kwamba hawa wakuu wetu wa DINI wako sahihi kabisa.

Hebu tufikiri pamoja
  1. IPTL
  2. Richmond
  3. Mikataba ya madini
  4. Ununuzi wa vitu feki au vilisivyo lingana na thamani iliyotolewa (pesa)
  5. Viongozi waliojisahau na kudhani ni miungu watu (Chenge, Mahita, nk)

Zingatia maamuzi yaliyochukuliwa kutokana na baadhi tu ya matukio hayo hapo.

AHSANTENI JAPO NENO HILI HALINA MAANA TENA SIKU HIZI- Mrisho Mpoto

KAMA DAKTARI KACHOKA HUYO MGONJWA ITAKUAJE?
 
Kuna mtu hajatimiza wajibu wake/katenda kinyume na tulivyomtuma. Huyo mtu ndo abebe lawama zote,viongozi wa dini wanajaribu kuturudisha ktk njia aliyoiacha huyu tuliyemtuma kutufanyia kazi yetu.
 
Ni jambo la kimaendeleo na kwa upande mwingine la kibinafsi. Wanasisa Wanatoa ahadi za kutekeleza matakwa fulani maalum ya kidini kwa mfano ccm, tlp ziliahidi kwenye manifesto zao kushughulikia mahakama ya kadhi jambo ni kinyume cha sheria ya usajili wa vyama vya siasa. Kwa upande wa madhehebu ya dini katoliki limetoa muongozo maalumu kuwaanda washirika wake kuelekea uchaguzi mwaka ttttMmm🙁
 
Ni jambo la kimaendeleo na kwa upande mwingine la kibinafsi. Wanasisa Wanatoa ahadi za kutekeleza matakwa fulani maalum ya kidini kwa mfano ccm, tlp ziliahidi kwenye manifesto zao kushughulikia mahakama ya kadhi jambo ni kinyume cha sheria ya usajili wa vyama vya siasa. Kwa upande wa madhehebu ya dini katoliki limetoa muongozo maalumu kuwaanda washirika wake kuelekea uchaguzi mwaka ttttMmm🙁
Na hilo la wino mwekundu ni kinyume cha nini? eleza kwa zaidi maana kwa upande wa ccm na tlp umeeleza ni kinyume cha sheria za vyama vya siasa.
Lakini lingine umeishia kuonyesha si kosa! Maana kwani kuwaandaa washirika kupiga kura ni kosa?????
 
Na hilo la wino mwekundu ni kinyume cha nini? eleza kwa zaidi maana kwa upande wa ccm na tlp umeeleza ni kinyume cha sheria za vyama vya siasa.
Lakini lingine umeishia kuonyesha si kosa! Maana kwani kuwaandaa washirika kupiga kura ni kosa?????

Usibabaishe maneno, waraka wa kikatoliki ulikuwa unabase na kidini. mimi ninao huo waraka; na unitaka nimchague mtu mwenye "kumcha mungu". maanake anayekwenda kanisani . kwanini waraka haujaniambia nimchague mzalendo mwenye uchungu na inchi hii?
 
Usibabaishe maneno, waraka wa kikatoliki ulikuwa unabase na kidini. mimi ninao huo waraka; na unitaka nimchague mtu mwenye "kumcha mungu". maanake anayekwenda kanisani . kwanini waraka haujaniambia nimchague mzalendo mwenye uchungu na inchi hii?
.



Kiongozi hasiyemcha mungu hatumuhitaji,dini kama za kina kingunge sisi hatuzihitaji.Suala la kumcha mungu si la wakiristu pekee na waislamu pia wanamcha mungu kwa hiyo kama wewe tafsiri yako ya kumcha mungu ni kwa wakristu pekee unasikitisha. Ingawa mtu alazimishwi kuwa na dini fulani ndio awe kiongozi ( kwa maana ya kikristu au kiislamu,Induisim nk.)
 
.
Kiongozi hasiyemcha mungu hatumuhitaji,dini kama za kina kingunge sisi hatuzihitaji.Suala la kumcha mungu si la wakiristu pekee na waislamu pia wanamcha mungu kwa hiyo kama wewe tafsiri yako ya kumcha mungu ni kwa wakristu pekee unasikitisha. Ingawa mtu alazimishwi kuwa na dini fulani ndio awe kiongozi ( kwa maana ya kikristu au kiislamu,Induisim nk.)
Kwa kuongezea tu, si kitu cha kushangaza kusikia kutoka kwa kikundi cha dini kikitaka mtu anaemcha Mungu kuwa kiongozi. Kama ulivyosema, kumcha Mungu si suala la kikristo pekee, maana hata wanaoabudu milima hiyo ndio miungu yao.

Kwa kuwa waraka umetoka kwa viongozi wa dini, ningeshangaa sana kama wangesisitiza kuchaguliwa kiongozi asie na imani na asieabudu Mungu. Labda ndio maana akin Kingunge wameguswa nao sana.
 
.



Kiongozi hasiyemcha mungu hatumuhitaji,dini kama za kina kingunge sisi hatuzihitaji.Suala la kumcha mungu si la wakiristu pekee na waislamu pia wanamcha mungu kwa hiyo kama wewe tafsiri yako ya kumcha mungu ni kwa wakristu pekee unasikitisha. Ingawa mtu alazimishwi kuwa na dini fulani ndio awe kiongozi ( kwa maana ya kikristu au kiislamu,Induisim nk.)

Aisee unataka inchi hii iongozwe na maextrimists na maradical siyo?
 
Kwa kuongezea tu, si kitu cha kushangaza kusikia kutoka kwa kikundi cha dini kikitaka mtu anaemcha Mungu kuwa kiongozi. Kama ulivyosema, kumcha Mungu si suala la kikristo pekee, maana hata wanaoabudu milima hiyo ndio miungu yao.

Kwa kuwa waraka umetoka kwa viongozi wa dini, ningeshangaa sana kama wangesisitiza kuchaguliwa kiongozi asie na imani na asieabudu Mungu. Labda ndio maana akin Kingunge wameguswa nao sana.

mambo ya kuongoza inchi yanataka akili tu na siyo kwenda kanisani.
 
Usibabaishe maneno, waraka wa kikatoliki ulikuwa unabase na kidini. mimi ninao huo waraka; na unitaka nimchague mtu mwenye "kumcha mungu". maanake anayekwenda kanisani . kwanini waraka haujaniambia nimchague mzalendo mwenye uchungu na inchi hii?


Mzee John10 kaka chungulia nje kidogo uangaze nje utaona kwa upana kaka .Kumchunga si lazima uende kanisani na hawajasema kwamba mchamungu ni yule aendaye kanisani.Ukisha muogopa Mungu, ukaacha kutoa hongo ili uchaguliwe , ukisha chaguliwa ukaacha kutetea uozo wa Chama bali ukaitetea katiba, Tanzania na watanzania wote na mwisho wale walio kuoa kura tayari wewe ni mcha Mungu .Twist hizi jamani tuache kabisa ama tuache kusema kama hatuna sababu ya kusema .Ukitete mafisadi kama Kingunge na kundi lake la akina Kakobe hawa hawana Mungu na watamuona Mungu kwa mbali sana .Utakatifu ni matendo hakika na kushinda kanisani kila Jpili .
 
mambo ya kuongoza inchi yanataka akili tu na siyo kwenda kanisani.
really?.................
well sorry to let you know that you are out of phase by 180degrees
 
mambo ya kuongoza inchi yanataka akili tu na siyo kwenda kanisani.

I think in your statement there is a point being made. Let's face it ... a country like ours needs a leader with a sort of "fear for God" and moral values in his/her regime. This excludes religious beliefs - whether a Muslim or Christian

When we argue on good leadership and base our opinions on religious focus - I think it's where we start mixing things up. We need good leadership, that's all!

Hakuna haja ya kubishana sana kuhusu mambo ya response ya wakristu na waislam maana limeshaongelewa sana hapa JF.

The point is, we have reached a point to join our efforts and fight against the many problems we have as one - not as Muslims and Christians. We are both living on the same land, don't you forget it.

Tunachohitaji ni mwongozo mzuri tu wa kuchagua kiongozi bora na jinsi gani ya kuwa makini kwenye uchaguzi - kuwafungua macho wananchi wasiuze haki yao ya kura kwa "Sahani ya wali".

Tukianza kuchagua kiongozi kwa sababu tu watarudisha mahakama ya kadhi, au kwa sababu tu RC wamempendekeza that would be a true sign of selfishness.
 
Usibabaishe maneno, waraka wa kikatoliki ulikuwa unabase na kidini. mimi ninao huo waraka; na unitaka nimchague mtu mwenye "kumcha mungu". maanake anayekwenda kanisani . kwanini waraka haujaniambia nimchague mzalendo mwenye uchungu na inchi hii?
Mzalendo si lazima awe mcha-mungu. Unaweza ukawa mzalendo lakini ukawa nyonga-nyonga kama kina Stalin huko USSR ya zamani, au kina Hitler huko Ujerumani. Kumbe sisi hatutaki mzalendo asiyemjua Mungu, asiyeongozwa na Mungu. Tunataka mcha-mungu, yaani anayemwamini Mungu na kuongozwa na Mungu katika utendaji wake. Na mcha-mungu anapatikana katika dini zote kwani Mungu wetu ni mmoja na amri zake ni zilezile.
 
Ubabaishaji huu.
Mbona hujaeleza kwa nini hawa hawa viongozi wanaapa kuiongoza nchi hii kutumia misahafu yao ya dini?

Big up sana

Na pia dini zipo kwa ajili ya kuongoza pale panapopotoka pakemewe
dini ni kitu kikubwa sana na sauti yake inatakiwa isikike katika jamii zote
 
Kuna kubisha kwa sababu mtu ana hulka ya ubishi tu tangu kuzaliwa kwake, lakini kuna kubisha kwa sababu ya jambo linalobishaniwa kupindishwa kwa makusudi na hivyo mtu kupinga upotoshwaji huo, ambapo wanaomsikiliza humwita mbishi, labda ili kumkatisha tamaa asiendelee kutetea ukweli halisi.

Mwalimu Nyerere alishasema, kiongozi tutakayemchagua ataapa. Kama ni mkristu ataapa kwa Biblia. Kama ni Muislamu ataapa kwa Quran. Kama hana imani hizo tutatafuta utaratibu utakaofaa ili mtu huyo aape. Lazima aape, kuwa atailinda Katiba yetu. Sasa hata kama hakusema wazi, maana yake alitutaka kuelewa kwamba kila mtu ana imani yake na kwa imani hiyo ambayo tutaikubali kuwa inafaa kututhibitishia kwamba mtu huyu hatatuangamiza, maana yake atakuwa na hofu fulani kufanya ndivyo sivyo. Hata imani za kipagani zinatambuliwa kwamba hazimhimizi mtu kuwa mhalifu.

Kwa hiyo basi, ukristo sio pekee njia ya kupata uongozi, wala uislamu. Wapo waendao makanisani lakini pia ni mafisadi japo wameapa. Adhabu ya Mungu weacha tu. Bora upelekwe mahakamani na watu, kuliko wakamwachia Mungu akushughulikie. Hofu ya Mungu ni muhimu sana kwa kiongozi yeyote. Lakini misahafu inatutahadharisha, "Msiziamini kila roho, zijaribuni maana sio roho zote ni za Mungu". Kwa hiyo imani yako itakayotumika kwa wewe kuiapia ni ile iliyo rasmi ambayo hata kanuni zake zinaeleweka kwa watu. Usiape kwa miungu ambayo ina mpango wa kuondoa vichwa vya watu kila siku katika kila kijiji, ukadhani tutaikubali.

Tunaambiwa watiini wakubwa wenu, maana hao wamewekwa na Mungu. Sasa hao watu wakimlilia Mungu wao utaipata kama wewe unashupaza shingo. Kama unabisha kamuulize Nebukadneza au Farao. Unawezasema huko ni mbali sana, basi kamuulize Anania aliyeficha sehemu ya mali - sadaka kwa Mungu. Hofu juu ya Mungu ikipwaya huangamiza taifa lolote. Mataifa yetu hayaangamizwi leo kwa sababu kuna watu wanayaombea sana mataifa hayo Mungu apishilie mbali hasira yake kwao. Usidhani haoni. Ni kama Nuhu alivyomuomba sana Mungu asiiangamize miji ya Sodoma na Gomora ili mradi kuna angalau wacha Mungu wawili watatu katikati ya miji hiyo, lakini ilipofikia kwamba miji yote hakuna hata mmoja mcha Mungu, ilibidi iangamizwe tu na apone Nuhu na wateule wachache.

Waislam wanaposema kiongozi lazima awe mcha Mungu hawamaanishi awe muislamu tu, vivyo hivyo wakristo hawamaanishi awe mwenye kwenda kanisani tu. Wote wana maana kuwa kiongozi awe na hofu juu ya Mungu kwa imani yoyote, maana Mungu ni Mmoja na hakuna photocopy yake ila wanaojidai kuwa, ambao saa yoyote Mungu anaweza kujilipiza kisasi kama wanamharibia jina lake.

Ibra

Hata mizimu huchukia mdanganyifu. Sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi.
 
Back
Top Bottom