Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Just wat our country needs... more religion and politics.. No stem cell research, new 7 deadly sins, no condoms, little boys and the inquisition.. just what we need..
 
Viongozi wa dini za Kiislam pamoja na Kikristo TANZANIA wanatia aibu kwa kukaa kimya bila kukemea jinsi serikali ilivyo wasahau wananchi NA maskendo yanayohusiana na RUSHWA yalivyokithiri

na lawama hizi naziwakilisha moja kwa oja kwa viongozi wa KANISA ambao kwa kiasi kikubwa wanauwezo mkubwa wa kuinfluence mambo serikalini lakini so far kimya

Nasema hiv kwa sababu tunajua jinsi gani walivyokuwa na sauti na wanavyozikosoa serikali zilizopo serikalini na mfano mzuri angalia Bush na Republicans wanavyo wasikiliza hao ma evalengical christians,hapa UK kila kukicha huyo SENTAMU wa Anglikana na MURPHY wa wakatoliki hawaiaichii safasi serikali ya BLAIR

Issue za Rushwa na Utawala bora nadhani zilitakiwa ziwe zinapewa ajenda kubwa na hawa jamaa wa kidini lakini sasa najiuliza vipi na wao wamenunuliwa?

Kwa upande wa waislam nadhani kazi ni kubwa kidogo kwa sababu hawana Kiongozi mmoja kama KADHI wa kuikemea serikali na majority ya waislam hawaitambui BAKWATA na hata hiyo Shekhe mkuuu hana nafasi sana kwani wanaona kama kawekwa na serikali na hata gari analotembelea kaewa na serikali sasa lilobaki ni kwa ma SHEKHE na MAIMAMU kuwa active katika kukosoa Serikali na kero zinazowaumiza wanainchi lakini so far naona KIMYAAA hauna na Basaleh wala Gorogosi aliyezungumzia issue ya RICHMOND

Tazama kule Kenya akina Cardinal OTUNGA walivokuwa active

Hivi Krisimasi hotuba zilkuwa nini huko makanisani?Maana najua wengi walienda makanisani lakini wanajua fika Hawana pesa za kulisha familia zao wala hawajui watakula nini wakati watawala wanaendelea kuinshi maisha kamavile wako peponi sasa hata kama serikali ikidai hakuna RUSHWA nani ataamini? the GAP between the haves and Have nots inazidi kupanuka, Kazi hakuna,Zinaa ndio kama dini,Ulevi imekuwa kawaida...sasa jamiii ya namna gani hiyo? No wonder kila kona kuna matangazo ya kuwashawishi watu wanywe ...after all pombe zetu slogan ni URITHI WETU!

Hivi kwa nini viongozi wetu wa kidini hawawi kama wenzao walioko huko LATIN AMERICA au SOUTH EAST ASIA?

Nimejitahidi kutafuta kijitabu chapisho la "Mpango wa Kiuchungaji Kuhamasisha Jamii Kuelekea Uchaguzi". Nimepata pia Manifesto: Proposal of National Priorities. Nimevisoma kwa makini na nikakuta kilichosemwa si hicho kilichoandikwa kwenye magazeti yaliyotajwa, hasa headline ya gazeti la The Sunday Citizen la wiki ile nyingine.

Machapisho yote ya TEC kuhusu civic education yana nia ya kuwafanya Watanzania kujua chanzo cha matatizo yao, kuyaelezea na njia za kuyatatua. Wamesema nchi yetu imeingia kwenye matatizo makubwa kwa vile sisi wenyewe tumewachagua viongozi tunaojua wana malengo yao binafsi.

Kwa ujumla kinachoongelewa na Kanisa Katoliki as quoted from the MANIFESTO (Proposal of National Priorities) pp. 22-23 ni hiki:

CONCLUSION

Finally, we propose an in-depth reflection on who or what are the "drivers" of our economy and of our national comperative advantage and competence. Encourage a debate led by economists on whether development is pushed by increasing demand or by enabling increased supply.

What drives our economy? Is it investment, or increasing supply of money to create employment and goods and infrastructures? Do we aim at increasing demand and local consumption so that we stimulate local production to fulfill local demand and thereby increase our capacity to produce goods of increased value, instead of only providing raw materials?

Listening to this debate we are convinced that we are not so much in need of money, but in need of ideas and of hardwork. A certain passivity has taken hold of our society and so also has a thirst for easy money without work.

This will not bring us any real development. Indeed, the country has so much intellectual talent, so many unutilised opportunities. And, yet, she has also so many bureaucratic bottlenecks that are exploited for selfish ends.

We need to instutionalise strategic thinking and establish an organ dedicated to the promotion and defence of our common good and the best achievements of our national heritage.

We need a moral revival, a return to basic ethical values and willingness to practise solidarity, care for the common good and giving one another a place, a chance, a responsibility.

CTP - NATIONAL TEAM.
 
DrWho, swali lako ni zito na la msingi lakini ugumu wa jibu lake hauko dhahiri kwa watu wote.

a. Viongozi wa dini wa Tanzania wanapenda heshima. Ni hii heshima ambayo kwa namna fulani inatokana na sababu za Kihistoria inayosababisha viongozi wa dini kutokuwa na ule ujasiri wa kuzungumza mmoja mmoja. Viongozi wa dini hukaribishwa mara nyingi Ikulu, hupata nafasi kadha wa kadha za kuzungumza na viongozi wa serikali hivyo mara nyingi hawaoni ulazima wa kuzungumza hadharani kutokupendezwa kwao. Ni kwa sababu hiyo kitendo cha Askofu Shao wa Zanzibar kuzungumza hatuna budi kukiona kwa mwanga mkubwa.

b. Mara nyingi viongozi wetu wa dini hasa wa makanisa hata wanapozungumza juu ya jambo mara nyingi hawazungumzii jambo moja hususan (specific) mara nyingi wanazungumzia mada fulani rasmi. Ni kwa sababu hiyo utaona kuwa hata wanapozungumza maneno yao yanakuwa ya kijumla na hivyo kukosa ukali wa maana yake. Kitu pekee ambacho kinaweza kutokea sasa ni kwa Askofu mmoja mmoja kujitokeza na kumuunga mkono Askofu Shao. Hata hivyo utaona kuwa hata yeye amechelewa, kwani makali RDC yashapunguzwa isipokuwa kama madai ya kampuni hiyo kuuzwa yatakuwa ya kweli.

c. Tangu zamani Kanisa limelala kitanda kimoja na serikali hivyo ni hadi pale ambapo viongozi wa kanisa watakapotambua kuwa kitanda hicho kimeharibiwa labda wataamua kutoka na kusimama kama viongozi wa dini. Hili hata hivyo ni gumu. Ugumu wake unatokana na ukweli kuwa you don't rock the boat ur sitting in!

d. Kwa upande wa viongozi wa Kiislamu tatizo lao pia ni la kihistoria. Tangu zamani kwao imekuwa vigumu kuikosoa serikali bila kuonekana wanataka kuleta uchokozi au "machafuko ya kidini". Inakuwa vigumu zaidi kwao kukosoa kwani mara nyingi wanakosoa pale ambapo matatizo yanahusu Waislamu zaidi kuliko Watanzania wote. Kwao tatizo ni pale linapokuwa linahusu maslahi ya Waislamu. Ni kwa sababu hiyo utaona kuwa Waislamu hupiga kelele mali za waislamu zinapochukuliwa (kina shehe Khalifa Khamisi na Shura ya Maimamu), utaona wanapiga kelele kuhusu kukandamizwa Waislamu kielimu na kiajira (Dr. Njozi, na Mohammed Saidi), pale Shule za Kiislamu zinapoonekana kutopewa nafasi sawa (Tanzaniamuslims)n.k Hivyo, suala la umeme kwa vile linawahusu watanzania wote haliwaumizi waislamu (msemo wa "msiba wa wengi harusi" unanijia) sana. Ila kama umeme ungekuwa unakatika Tanga, Dar, na Zanzibar zaidi na mikoa kama Kilimanjaro, Mbeya na Kagera ikipata umeme wa uhakika bila ya shaka ungesikia "kilio cha waislamu".

e. Zaidi ya yote, kwa viongozi wa kiislamu inakuwa vigumu kwao kuikosoa serikali yenye viongozi waislamu katika nafasi za juu. Sababu ya hili ni wazi. Kwa maoni ya baadhi ya viongozi wa kiislamu, hakuna kitu chema kama kuwa na viongozi waislamu ambao waliahidi kushughulikia "matatizo" yao. Hivyo, hawataki kuwaudhi na kuonekana kutokuwa na shukurani. Ni hadi pale viongozi wa Kikristu wataweza kukosoa viongozi wakristu na waislamu bila kuwaonea haya, na ni pale viongozi wa Kiislamu wataweza kukosoa viongozi waislamu na wakristu bila haya ndipo tutaona kweli nafasi yao katika jamii ikionesha kujali nchi yetu na maslahi ya watu wake kiujumla.

Pamoja na hayo, viongozi wa dini hawana nguvu kubwa kama ile iliyoko ndani ya chama tawala ambapo vyombo vyote vya dola vimeshehena na kubugizwa "siasa ya chama". Hapa ndipo ugumu ulipo. Chama cha Mapinduzi hakina lengo wala nia ya kusahihisha viongozi wake isipokuwa kwa uwezo wa Mtukufu mwenyekiti wa Chama! Kama Mwenyekiti hataki, hakuna mwenye ubavu wa kufanya jambo kinyume na mwenyekiti

Hapo umesema ukweli mkubwa. Enzi zile Mwalimu alipenda kubalance mambo na kwa kweli pamoja na matatizo yake yote, hakuwa na tatizo la wizi wa mali ya umma au kukosa uzalendo.Kinachonichefua leo ni hizi hotuba za viongozi wakubwa wa kanisa kuwapamba baadhi ya watu ambao wanatiliwa shaka juu ya yale waliyofanya madarakani. Baadhi yao wnadiriki hata kuwaita watuhumiwa wa uisadi kuchangia makanisa.
Unless kanisa likasimama kidete kufanya kazi zake za kiroho na kuacha kutumiwa na wanasiasa na mafisadi, msaada wake kwa ukombozi wa Taifa kifikra bado uko finyu.Siku zote tukumbuke, maadili mabovu ya uongozi hayako tu serikalini..inawezekana pia kuna matatizo ya kiungozi hata kanisani ambayo yanachangia wakuu wa dini kuwa wapole kwenye kukemea uovu. Maana kama viongozi wa kanisa nao ikatokea wakaweka fedha mbele au kulinda maslahi fulani yaliyo kinyume na maadili...duuh, lazima walale kitanda kimoja na serikali tena kwa usingizi mzito mana vinginevyo wataumbuliwa.
Dini nazo zinatakiwa zianze kukemea
 
Ni vema wafanye hivyo ili kutorudia ya 2005 ya kusema mgombea ni chaguo la Mungu na hadi leo ni kichekesho.
 
Cheap Politics!

In short KANISA KATOLIKI ujumbe wao ni mfupi kwa wakatoliki. Ipeni CHADEMA kura kwenye chaguzi zijazo. Hayo mengine ni danganyatoto. Tunafuatilia kwa Karibu nyenendo zao na vyombo ya habari kama IPP media vilivyo nyuma ya agenda hiyo. Nchi hii yetu sote!
 
Cheap Politics!

In short KANISA KATOLIKI ujumbe wao ni mfupi kwa wakatoliki. Ipeni CHADEMA kura kwenye chaguzi zijazo. Hayo mengine ni danganyatoto. Tunafuatilia kwa Karibu nyenendo zao na vyombo ya habari kama IPP media vilivyo nyuma ya agenda hiyo. Nchi hii yetu sote!

Kwa kweli kanisa kuwaelimisha watanzania juu ya wajibu wao wa kuhakikisha wanachagua viongozi wanaofaa sio cheap politics. Kama watu wanaojaa makanisani wangekuwa makini walau kidogo, wajitokeze kujiunga na vyama bila ushawishi au mazoea ya chama fulani, wakajitokeza kugombea, wasikose kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaofaa basi tutakuwa tumepiga hatua. Tatizo la msingi katika nchi yetu ni uongozi. Tuna viongozi wabovu na wasio na uwezo. Wananchi hawadhani kwamba ni rahisi kuwabadilisha.

Kama tulifaniiwa kuondoa wakoloni tutashindwa kuondoa watawala wabovu na kujipanga kuleta maendeleo yetu? Ni mda tu na ninavyoona mwelekeo wa mijadala katika nchi yetu, watawala wa miaka ya karibuni itabidi wachague kuhangaike na shida za wananchi na kuacha kutafuta maslahi binafsi au wananchi watachoka na kuachana na wimbo wa amani. Tutauana!
 
Last edited:
Viongozi wa kanisa walisema JK chaguo la Mungu, hivi Mungu anakoseaga?
 
Hivi CCM itachaguliwa tena jamani? Mbona kila kona inatemewa mate? Ila binafsi nasikitishwa sana na watu wanaojiapisha kuwa hawatapiga kura tena.
 
Viongozi wa kanisa walisema JK chaguo la Mungu, hivi Mungu anakoseaga?

Labda kweli alikuwa chaguo la Mungu la kuhakikisha chama cha mafisadi kinaparaganyika na hivo wadanganyika kupata ukombozi wao kwa mara ya pili! (ni upande wa pili wa shilingi tu)
 
Viongozi wa kanisa walisema JK chaguo la Mungu, hivi Mungu anakoseaga?

What yoou've said were personal opinions of individual bishops and not a Church statement! Hata hivyo, hivi ni wote waliosema au akisema mmoja basi wote wamesema? Ninachoona mimi ni kwamba Watanzania tumeahirisha kutumia akili zetu kiasi kwamba hata kama mtu atasema kitu cha kutujenga still tutaona hajasema kitu.

Hii attitude ni mbaya sana. Nadhani ni muhimu mahali tunapoona panastahili kupongeza, tupongeze na pale panapostahili kutoa changamoto, tufanye hivyo. Lakini kama hatuoni kitu chochote kizuri kinachosemwa na wengine isipokuwa sisi tu, then tuna tatizo kubwa sana! Wengi wa wachangiaji hapa ni wale tunaofuata bendera tu na bila kufanya utafiti wowote tunaunga mkono hoja bila kuwa na sababu za msingi.

Na always huwa kitu kinachoshangaza ni hiki: mara maaskofu wanaingilia siasa, mara hawajakemea rushwa/maovu ya jamii kiasi cha kutosha. Sasa tunachotaka wafanye ni nini? Kwa upande mmoja hatutaki wajihusishe na siasa na kwa upande mwingine tunataka - na ndio maana wakikemea maovu tunawalaumu; wakikaa kimya tunawalaumu. What do we really want?

Kwa wale wanaosema 'viongozi wa dini wasijiingize kwenye siasa' hawana point kwani siasa ni ya watu wote ndani ya nchi. Viongozi wa dini wanao wajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inaongozwa vizuri na kwa maslahi ya wote. Hao viongozi wa dini wanashughulika na idadi kubwa sana ya Watanzania (mijini na vijijini) na wasipochangia katika kuendeleza nchi yetu, ina maana hata hao wanosali pamoja nao hawatakuwa na mwamko wa kisiasa na ultimately watu wataendeshwa kama mbuzi.

Kwa hiyo, wanaotoa hoja kama hizo za viongozi wa dini kutotoa changamoto kwa viongozi wa nchi na vyama vya siasa, then wana tatizo la uelewa siasa maana yake ni nini na inawahusu akina nani. Wanaosema viongozi wa dini hawajakemea maovu kiasi cha kutosha nao pia hawana hoja ya msingi kwa vile wako ignorant na yanayofanyika katika makanisa na misikiti.

Mfano, Kanisa Katoliki linawafundisha wakristo wake namna ya kujua vyanzo vya matatizo yao na kutatafutia ufumbuzi (social consciousness). Kuna mafundisho yanayotolewa kwa waumini (au vikundi mbali mbali vya wakristo na sehemu zingine yanahusisha watu wa dini nyingine) na yanaitwa 'training for transformation' au 'linking faith and action' na katika mafundisho hayo kinachosisitizwa ni moyo wa kujitambua, kuwatambua wengine, kuona kwa pamoja matatizo yanayowarudisha wanajamii nyuma na kutafuta njia za kupambana nayo na kuleta maendeleo.

Pia kuna mafundisho yanayolenga kujenga dhamiri sahihi (informed conscience) ili kuweza kuchagua mambo mema na kuacha mabaya (distiction between right and wrong) na pia moyo wa kujali mali ya umma (honesty). Kuna semina, mafungo na mafundisho mengi tu yanayotolewa katika grassroots level. Yote haya yana nia ya kubadilisha maisha ya watu/jamii (wakiwemo viongozi) na kuleta mabadiliko pia katika nafsi zao, mazingira yao na hatimaye katika nchi nzima.

Let's be objective when we criticise something... sweeping statements will not help much. Kwa kifupi, Tanzania (au siasa ya Tanzania) ni ya Watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini. Kwani wao hawapigi kura? Na je, nchi ikipata shida, wao hawatapata shida? Na kama nchi ikipata neema na wao hawatapata hiyo neema? Tuache viongozi wa dini nao wachangie katika kuboresha siasa ya Tanzania na walete hoja mbadala kwa ajili ya maendeleo ya wote. We shouldn't domesticate people!
 
Last edited:
Tangu enzi za mwalimu kanisa katoliki lilikuwa na program za kuweka sera na siasa linalozihitaji kwa Serekali ya Tanzania.Imefikia wakati sasa kuendeleza ushawishi wake na kutuletea maendeleo ya kweli.
 
Dini ni siasa, na siasa ni dini na haviwezi kutenganishwa kwa sababu ni pande mbili za sarafu moja. Angalia structure of the papacy, anagalia Wamarekani walivyojaribu kufanya "separation of church and state" lakini bado kila siku ya uchaguzi mambo ya dini pamoja na lobbies zake vinavyotawala.

Dini ni siasa, na siasa ni dini.
 
Bikra:

Na-admire juhudi zako za kutumia keyboard. Lakini thread zako ni ndefu mno. Na vilevile wewe kama mwanzishaji ni lazima utulie kwenye threads zako na kutoa maoni.

Hakuna mpango wa kuanzisha thread moja baada ya nyingine bila ku-moderate threads zenyewe.
 
...ndefu sana sijaisoma,na sio kila mtu anaamini hizo dini zenu!
 
Mkuu sijakupata, lengo hasa la maada hii ni nini, katika nchi yenye watu wa dini nyingi kama Tanzania? sio wote wanaomuamini Musa na pia wapagani ndio kabisa hawana dini!

Au lengo ni kumpa 'shavu' Kikwete aendelee na juhudi zake za kuwapa watu fulani vyeo vya bure au watu wamuhubiri Kikwete misikitini?

Au lengo ni kuwa unataka RC wamuweke 'rais' wao kama wanavyosema na tunavyosikia?

au unataka wapentecost, waprotestant, wa rc waseme tena ''ili chaguo la Mungu' ??

DINI SI SIASA DINI NI FACTS, SIASA IKO NDANI YA DINI KAMA KIPINGA DINI!, MKISEMA DINI NI SIASA BASI SI KOSA KUWA NA DINI ZA UONGO! LA SIASA INGEKUBALI DINI INASEMA NINI, BASI TUSINGEKUWA NA SIASA! TUSINGEKUWA NA WEZI, WATOA RUSHWA , WATOA AHADI ZA UONGO, WAUAJI, WABABE NA MADIKTETA! MUSA HAKUOMBA KURA, HAKUPIGA KAMPENI. YOHANA ALIKATWA KICHWA KWA KUSEMA UKWELI! (soma bible)

HIVYO BASI MUSA ALIKUWA KIONGOZI NA KILA MMOJA NI KIONGOZI WA FAMILIA NA VITU VINAVYOTUZUNGUKA, UNGESEMA KUWA DINI INAELEZA NA INATOA MIFANO MIZURI YA VIONGOZI BASI NINGEKUPA TANO!

UONGOZI UNAANZIA NYUMBANI! SOMA BIBLE HIYO HIYO IKUAMBIE ASKOFU ANATAKIWA AWEJE, NA KIONGOZI SIO SIASA! WAKURUGENZI WA MASHIRIKA YA UMMA, WALIMU, N.K KILA MMOJA TUNGESEMA WANASIASA BASI!

Yesu kwa nini hakuwa mfalme wa Israel kama walivyotaka waisrael na Yesu katika agano jipya ni mfano wa Mussa!!!!!! au YOHANA KWA NINI ALIKATWA KICHWA?
Au kwa nini Herode alitetemeka kusikia Yesu amezaliwa??
 
Mkuu sijakupata, lengo hasa la maada hii ni nini, katika nchi yenye watu wa dini nyingi kama Tanzania? sio wote wanaomuamini Musa na pia wapagani ndio kabisa hawana dini!

Au lengo ni kumpa 'shavu' Kikwete aendelee na juhudi zake za kuwapa watu fulani vyeo vya bure au watu wamuhubiri Kikwete misikitini?

Au lengo ni kuwa unataka RC wamuweke 'rais' wao kama wanavyosema na tunavyosikia?

au unataka wapentecost, waprotestant, wa rc waseme tena ''ili chaguo la Mungu' ??

DINI SI SIASA DINI NI FACTS, SIASA IKO NDANI YA DINI KAMA KIPINGA DINI!, MKISEMA DINI NI SIASA BASI SI KOSA KUWA NA DINI ZA UONGO! LA SIASA INGEKUBALI DINI INASEMA NINI, BASI TUSINGEKUWA NA SIASA! TUSINGEKUWA NA WEZI, WATOA RUSHWA , WATOA AHADI ZA UONGO, WAUAJI, WABABE NA MADIKTETA! MUSA HAKUOMBA KURA, HAKUPIGA KAMPENI. YOHANA ALIKATWA KICHWA KWA KUSEMA UKWELI! (soma bible)

HIVYO BASI MUSA ALIKUWA KIONGOZI NA KILA MMOJA NI KIONGOZI WA FAMILIA NA VITU VINAVYOTUZUNGUKA, UNGESEMA KUWA DINI INAELEZA NA INATOA MIFANO MIZURI YA VIONGOZI BASI NINGEKUPA TANO!

UONGOZI UNAANZIA NYUMBANI! SOMA BIBLE HIYO HIYO IKUAMBIE ASKOFU ANATAKIWA AWEJE, NA KIONGOZI SIO SIASA! WAKURUGENZI WA MASHIRIKA YA UMMA, WALIMU, N.K KILA MMOJA TUNGESEMA WANASIASA BASI!

Yesu kwa nini hakuwa mfalme wa Israel kama walivyotaka waisrael na Yesu katika agano jipya ni mfano wa Mussa!!!!!! au YOHANA KWA NINI ALIKATWA KICHWA?
Au kwa nini Herode alitetemeka kusikia Yesu amezaliwa??

mkuu,nadhani makala ya jamaa hujaisoma kwa kituo,irudie kwa hali ya taratibu utamwelewa alichomaanisha..!
 
Ni vigumu kutenganisha dini na siasa kwa sababu hao wana siasa wenyewe wana dini. Dini ni mafundisho ambayo mtu huya fuata na kuna watu wengi sana hufanya maamuzi kutokana na imani zao. Sasa basi hata huyo mwanasiasa anapo fanya maamuzi fulani basi utakuta ana tumia utashi wake wa kidini. Ndiyo maana kuna sheria kama kuto kuruhusu ndoa za jinsia moja, hiyo yote ni kutokana na dini. Kuna sheria za kupinga uchangudoa, nayo ni dini. Una weza kukuta mwanasiasa anamuomba Mungu wake kabla ya kufanya maamuzi mazito na muhimu nayo dini imesha ingia. Kuna mifano mingi tu ila kwa ufupi ni kwamba as long as wanao husika na siasa wana dini basi dini na siasa haviwezi kutenganishwa hata kama tusipo kiri mbele za watu.
 
mkuu,nadhani makala ya jamaa hujaisoma kwa kituo,irudie kwa hali ya taratibu utamwelewa alichomaanisha..!

Mkuu mtimti; majibu ya aina kama hii ni ya watu wavivu kuandika na kutoa hoja, hapa swala ni kukubaliana na mtoa maada, kupinga au kuwa neutral. nadhani ndio maana halisi ya forum! Anasema dini na siasa haviwezi kutenganishwa, mimi simply sijakubaliana naye! wewe ndugu unasemaje? kama unakubaliana naye mwaga points tuzikopi? unapotukosoa watu wenye narrow mind kama mimi , unaninyima haki ya kujua upana wako wa kuelewa na kuinyumbulisha hii maada , nieleweshe nisipopaelewa ukirefer post yangu.


Wewe nia aina ya watu wa busara tunaowataka JF

Na maswali yangu hayajibiki kwa sababu sijasoma nakala yako kwa kituo?
 
JK ni MWISLAMU; JK ni RAIS wetu. Anawezaje kuyatenganisha hayo?
 
Back
Top Bottom