Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Nadhani ni muhimu zaidi kutafuta nakala ili tujadili kitu ambacho tumepata taarifa sahihi. Nashauri itafutwe na kuwekwa wazi tuisome.
 
Tunaweza jikuta tnajadili kitu ambacho siyo sahihi kwani wengi wetu bado hatujaona hiyo nyaraka kama inavyojionyesha kwenye mjadala huu. Muhimu kuipata kwanza kuisoma, kufanya analysis na hapo ndipo tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujadili
 
..badala ya kuwashutumu na sote tuamke tuanze process kama yao.

..at the end of the day, kwasababu kila mtu atakuwa makini na amechangamka, basi lazima tutapata kiongozi mwenye uwezo.

NB:

..habari hii ni isije kuwa kama yale malalamiko ya Kanisa Katoliki kuingia makubaliano na serikali kurejeshewa shule na hospitali zao zilizotaifishwa.

..wengine badala na wao kuingia mkataba wa namna hiyo na serikali waishia kulalamika tu for almost 15 years now.

Bravol Jokakuu.

Kila mtu na kila taasisi ichukue muda kuelimisha watu juu ya

kuchagua kiongozi bora.

The way i see, kanisa katoliki wamefungua hiyo njia, lets all follow.

Bila hamasa za namna hiyo, who will vote?

Baadhi ya watu hawajui au kuamini kwamba

kupiga kura ni halali, hadi waelekezwe na viongozi wa makanisa yao!!!!!!!
 
Kuna taarifa ilitolewa na Gazeti la CITIZEN tanzania tar3-5-2009 na ilikuwa leadingStory, Bahati mbaya Mzee wa copy na paste hakuiona au hakuwa na wasaa wa kuisoma na kuipost hapa.

Kama kuna mdau anaweza ipata hio taarifa tunaomba aiweke hapa tupate ijadili.Taarifa inazungumzia Kanisa Katoliki na Rais anaefaa 2010.

....The Catholic Church in Tanzania has launched a comprehensive project whose aim is to influence the 2010 electorate process, and ensure that the country gets a leader of the Church’s choice.

An apparently well articulated strategy that has been published in a booklet being circulated among Catholics countrywide involves the forging of a mechanism to interview prospective candidates, set the election agenda and assess the results after the bailout has been cast……….

The 18 page booklet entitled “ Mpango wa Kichungaji Kuhamasisha Jamii Kuelekea Uchaguzi says the country is experiencing serious leadership problems and calls on all Catholics to fully participate in the process to elect good leaders for 2010-2015 parliamentary term…..

Kwa alie na kitabu hicho tunaomba aturushie....then tunaweza jadili zaidi
Mkulu

Rais siyo lazima awe Mkatoliki wa Roma.

Suala hapa si ukatoliki, bali ni UWEZO wa kanisa la VATICAN kama SUPERPOWER apart from USA.

Huwezi kuwa Rais wa nchi bila kuwa na uhusiano na Vatican.

Umejiuliza kwa nini wao kama kanisa, mbona wana UBALOZI kwenye nchi mbalimbali.

KANISA LA VATICAN NI ZAIDI YA DHEHEBU.
 
I have the impression that what the article reported was rather the writer's interpretation of the Catholic Church's launched comprehensive project on a presidential candidate than the gist of the project itself.

Yesterday, the same Citizen had an article on the same issue but it said the Christian Professionals of Tanzania (CPT) had launched a campaign to help members of the Church vote for a non-corrupt person and one who respects national ineterests. Yesterday's article never mentioned the Catholic Church's choice of the candidate but the general probity and integrity of a leader.

I intend to have the original copy and when I get it I'll say where to get it. I think it is available at the Catholic Church bookshop near St Joseph's Cathedral.
 
Mkulu

Rais siyo lazima awe Mkatoliki wa Roma.

Suala hapa si ukatoliki, bali ni UWEZO wa kanisa la VATICAN kama SUPERPOWER apart from USA.

Huwezi kuwa Rais wa nchi bila kuwa na uhusiano na Vatican.

Umejiuliza kwa nini wao kama kanisa, mbona wana UBALOZI kwenye nchi mbalimbali.

KANISA LA VATICAN NI ZAIDI YA DHEHEBU.

Ni vyema kama ungesema huo ni mtazamo wako, kuliko kutaka kuweka kama ni fact!
 
Viongozi wa dini ni wanafiki tu, si katika siasa tu bali hata mambo ya kijamii. wanajua kwamba usipotumia kondom utapata unkimwi na utakufa, wanasistizia kwenye kujizuia wakati wao wenyewe hawawezi, si inafahamika kwamba mapadre wana vimada na watoto mitaani? si inaeleweka kwamba wana majumba ya kupangisha mitaani? Je kujizuia kwao kuko wapi?Wasituchanganye, waache watu wafanye chaguo lao bila unafiki wao
 
Ni vyema kama ungesema huo ni mtazamo wako, kuliko kutaka kuweka kama ni fact!
Si mtazamo wangu.
Ni HARD FACTS.
Sijui dini yako wala dhehebu na sitaki kujua.
Kwa mtu anayejishughulisha kupata maarifa mbalimbali kwa kujisomea ,hatoshangaa kwa hilo nililosema.
Unless amejifungia kwenye kisanduku chake cha taaluma aliyosomea baada ya kupelekwa shule na mama yake.
 
Siri imevuja!

Fumbo mfumbie mjinga!

Hizi nyaraka za kichungaji tunajua zitakuwa nyingi tu baada ya kusimama 1995-2005.
 
Yaani viongozi hao kuwasihi waumini wao kuchagua viongozi wazuri imekuwa nongwa? Hizi chuki zenu za kidini zitawaua ninyi!
the country is experiencing serious leadership problems and calls on all Catholics to fully participate in the process to elect good leaders

hapana nongwa hapa maneno yapo wazi hapo juu yanajieleza wenyewe.
"fully participation" tena kwa "catholics" inamaanisha nini?
that catholics will leave no stone unturned for all political positions?
tell us .
this sounds treasonous
 
Do you listen to yourself..? lol
 
If everybody had understood things the way you do everything would have been treasonous as you say.
 
Mw/ubongo,
magobe t
haya yote kayataka baba yenu wa taifa, kakusomesheni biblia na azimio la arusha vimekukaeni kichwani
 
the country is experiencing serious leadership problems and calls on all Catholics to fully participate in the process to elect good leaders

hapana nongwa hapa maneno yapo wazi hapo juu yanajieleza wenyewe.
"fully participation" tena kwa "catholics" inamaanisha nini?
that catholics will leave no stone unturned for all political positions?
tell us .
this sounds treasonous

I'm not Cathoric but more than willing to team-up, Tanzania really needs radical change. This we all know though some argue the truth
 
I'm not Cathoric but more than willing to team-up, Tanzania really needs radical change. This we all know though some argue the truth
THEN these hunger stricken priests should stay away from politics!
 
THEN these hunger stricken priests should stay away from politics!

There's no Tanzanian who's not a politician including priests. So, they have to contribute to the debate on who's the best candidate (qualitywise) because if they stay away from politics and a bad leader is chosen, it is not only politicians who will suffer, the priests will suffer also because of that bad leader. So, politics is for everyone (every citizen and every Tanzanian).
 
Hofu! viongozi wa dini wamekuwa ni mawakala wa serikali

Hofu yao kubwa ni juu fadhila itolewayo na watawala kwa makanisa na misikiti

Mosi hawa jamaa wa dini wanamsamaha wa kodi, hii inawafanya wafunge midomo yao, kwani wakipiga sana kelele wanaweza kuanza kutozwa kodi.

Pili, wachangiaji wakubwa wa mwakanisa ni wana siasa, mara nyingi kuwenye harambee ya ujenzi wa makanisa wanasiasa huwa wanawavuta wafanya biashara wengi waje kuchangia chochote kitu, wakipiga kelele wanasiasa hawatawaunga mkono kwenye michango.

Tatu, viongozi wengi wa serikali ndio watoaji wakubwa wa sadaka makanisani na misikitini, hawa jamaa wana nguvu sana ya maamuzi, kwani viongozi wengi wa makanisa na misikiti wana hali duni ya maisha, kabla ya kutolewa tamko lolote hawa wazee wanawaziba mdomo mapema.

nne, hizi dini haziko huru, ni taasisi zilizosajiliwa na serikali, wakipiga kelele kuna sheria ambazo zinawabana
Ninashindwa kuelewa, kwanini viongozi wa makanisa wamekuwa wasaliti, serikali inasema dini isichanganywe na siasa, pale viongozi wa dini wanapoisifia serilika serikali inashangilia, dini ikikaripia serikali hapo kelele zinapigwa kuwa dini na siasa ni vitu viwili tofauti, na uchochezi unachukua nafasi.

Kuhusu hoja "Mosi" kwamba viongozi wa dini wamesamehewa kozi ndio maana wanaogopa kukemea maovu ya viongozi wa serikali: Jhivi ni nani hasa anafaidika na misamaha hii ya kodi - ni viongozi wa dini kama watu binafsi au ni wananchi wanaotumia huduma zinazotelewa na mashirika ya dini yaliyosahewa kodi? Hivi ni mapato gani ya viongozi wa dini ambayo walitakiwa walipie kodi lakini wamesamehewa? Mishahara yao ambayo wengi wao hata kima cha chini hakifikii? Misaada wanayopata kutoka nje ya nchi ambayo imekusudiwa kwa ajili ya huduma za jamii katika nchi? Hivi serikali inajitoza kodi kwa misaada inayopata kwa ajili ya huduma za jamii kwa ajili ya wananchi wake? Nionavyo mimi ni kuwa mashirika ya dini yanaisaidia serikali kutoa huduma muhimu kwa wananchi na ndio maana nafikiri ni halali kwa mashirika hayo kusamehewa kodi.

Wana JF tunahitaji kuwa na mawazo mapana. Wanaofaidika na misamaha ya kodi sio viongozi wa dini bali wananchi kwa jumla ambao pia ndio walipa kodi. Viongozi wa dini wawakilisha tu wananchi kuiomba serikali itoe misamaha ya kodi, lakini wao wenyewe sio wanufaikaji namba moja, wanaonufaika zaidi na misamaha hiyo ni wananchi walalahoi bila kujali dini zao.

Jaribu kufikiri kama kwa mfano mashirika ya dini yangetozwa kodi ya vifaa vya ujenzi wa hospitali, madawa, na vifaa vingine vya hospitali; vifaa vya kuchimbia na kujengea visima vya maji au vifaa vya kupelekea maji ya bomba kwa wananchi vijijini; na misaada mingine kwa ajili ya huduma za jamii nchini, n.k. hali ingekuwaje? Kwanza ni hela gani ambo mashirika ya dini yangetoa kulipia kodi ya vifaa hivyo? Sadaka ambayo hata huwa haitoshi kulipa mishahara ya watumishi wake? Je, kama mashirika ya dini yasingesamehewa kodi, na hivyo kutokana na kutokuwa na uwezo yakashindwa kulipa kodi hiyo kitu gani kitatokea? Je, atakayeathirika kwa kukosa huduma ambazo zitakosekana kutokana na kushindwa kulipa kodi ni nani? Viongozi wa dini au wananchi?

Kama mnaona viongozi wa dini ndio wanaofaidi matunda ya misamaha ya kodi, ishawishini serikali iyatoze kodi mashirika ya dini halafu muone matokeo yake!

Tusiwe wepesi wa kuwashambulia viongozi wa dini kwa kuwa tu hawakutumia njia tunazotaka sisi wazitumie kukosoa uovu serikalini. Aidha tusidharau mchango mkubwa ambao viongozi wa dini wanatoa katika jamii yetu.
 
Charles Misango – Kiongozi

Kanisa Katoliki nchini limependekeza kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Nchi, ikiwa ni pamoja na kuruhusu kuwepo kwa wagombea binafsi katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge mwakani.

Mbali na kuruhusu wagombea binafsi katika nafazi zote za uongozi wa kisiasa isipokuwa nafasi ya urais, Kanisa Katoliki pia limependekeza kuundwa kwa Baraza la la Mapitio ya Kikatiba ili kupitia upya Katika kulingana na mahitaji halisi ya Watanzania kulingana na wakati uliopo.

Mapendekzo hayo na mengine yamo katika Ilani iliyotolewa na Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hivi karibuni na kusainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Kuu la Tabora, Mhashamu Paulo Ruzoka.

Tume hiyo imesema kuwa kwa vile Katiba ni kitu muhimu katika jamii, na zai ya hati ya kisheria, ni haki kwa wananchi kushirikishwa kuijadili na hata kuifanyia marekebeisho, badala ya kuachia kundi moja kushinikiza au upande ama chama chenye maslahi ya kijamii, kiuchumi ama kidini kuchochea mabadiliko.

“Katiba inamilikiwa na watu na ni ya watu katika anuawi diversity) na katika upokeaji wa watu wenye tofauti mbalimbali (plularity)” imesema sehemu ya Ilani hiyo. Aidha, Kanisa hilo limeongeza kuwa kwa vile taifa ni kitu kinachoishi ni jambo la kiasili na la muhimu hivyo ni sharti kuruhusu mapitio ya vipindi kwa vipindi ili kuwapatia watu fursa ya kutoa maoni yao.

Limesema tangu Tume ya Nyalali itoe ripoti yake mwaka 1991, ombi la marekebi9sho ya Katiba halijapokelewa kwa namna na kiwango cha kuridhisha.

Kanisa limesema hakuna chama cha siasa wala Serikali ya wakati huu wanaoweza kihalali kutumia Katiba kwa faida zao za kisiasa kwa sababu Katiba ni dira ya kimaadili na maelezo ya kifalsafa ya tunu na kanuni watu wanazotaka kuzizingatia katika maisha yao ili kuwahakikishia amani, haki, na vile vile kuheshimiana na kuvumiliana katika kuwa na maoni tofauti.

Limesema kuwa katika mchakato wa kurekebisha Katiba lazima kuwe na tamko dhahiri juu ya tunu za msingi za maadili ya kitaifa ambay yapasa yazingatiwe, ikiwa ni pamoja na kutamka haki za watoto ambao hawajazaliwa.

Kanisa limesema kwamba lazima tunu za kimaadili ziwe ndiyo msingi wa taifa letu, na lazima yahifadhiwe ndani ya Katiba ili kuongoza kanuni na taratibu zote za uendeshaji na utendaji. “Lengo na sababu za mahusiano yote katika jamiini kumpa kila mtu hadhi ya kiutu ambayo ni stahili yake. Maana yake ni kwamba, kila apatiwe mahijai msingi ya kumwezesha kuishi maisha yanayomstahili mwanadamu. Watu wote wamumbwa na Mungu katika usawa, kwa hiyo kila mtu ni sawa na mwingine” imesema sehemu ya ilani hiyo.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhashamu Paulo Ruzoka, amesema wameamua kutoa Ilani hiyo yenye mapendekezo mengi, ikiwa ni sehemu ya haki ya Kanisa na uzalendo walionao kwa taifa.

“Katika uchaguzi, hatupigi kura tu, tunapaswa kueleza makusudio yetu kwa yale tunayofikiri kuwa muhimu sana kwa Taifa.” Amesema Mha. Ruzoka.

Kauli ya Kanisa inalingana na kauli na matamshi mengi yaliyokwisha kutolewa na makundi ya Watanzania, wakwemo wanasiasa, wanasheria, taasisi zisio za kiserikali juu ya kufanyika kwa marekebisho ya Kikatiba ili kuendana na hali halisi ya kisiasa nchini.

Aidha katika suala la kuwa na wagombea binafsi, vyombo vya sheria viliisharuhusu kuwepo kwa wagombea binafsi, hatua ambayo hata imekuwa ikipingwa na serikali kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom