Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Scratch my back, I will scratch yours.Huyo ndiyo Cardinal wetu. Pengine alienda kuungamisha dhambi, halafu baadae akaendeleza sala
 
Sasa hapa mnamlaumu nini Pengo kwenye hiyo sala? Yeye ameombea "kila kilicho chema", kwani hakuna chema katika hiko kitabu kilichoandikwa na muumini wake wa kanisa katoliki mama Regina Lowassa?

Pengo hakuombea ufisadi wa Lowassa, kosa lake tu ni kwenda kwenye hilo tukio bila kujua kwamba wakina Rostam na Lowassa wao kila tukio ni fursa kwao ya kumsafisha Lowassa kupitia Habari Corporation.

Kanisa Katoliki linapaswa kutoa tamko la haraka kuwa tukio hilo sasa linatafsiriwa tofauti.

Ileweke kwamba hata Yesu alikwenda kula nyumbani kwa wadhambi, lakini hakutangaza kuyasafisha madhambi yao. Kwa hiyo Pengo kwenda nyumbani kwa Lowassa sio tatizo kama hakutangaza kumsafisha Lowassa na uchafu wake

SM


Mbona sijasikia PENGO akienda kula Pasaka (kwa mfano) na wafungwa huko segerea au keko?Au wenye dhambi wanaohitaji maombezi na Kardinali na hao tu waliolazimika kujiuzulu uwaziri mkuu?
 
Tutofautishe dini na siasa kwanza wandugu! Pengo hakwenda kwa EL kama mwanasiasa bali kama mchungaji, na kama mchungaji anapaswa kuwatafuta kondoo waliopotea, kuwahubiria habari za wokovu na hatimaye kuwarudisha kundini! So kama tunakubaliana kuwa EL ni mchafu (kibinadamu), basi Pengo na maaskofu wengine walioenda nyumbani kwao ilikuwa ndo mahala pao.....though ilipaswa mdhambi kukiri kwanza makosa yake kabla hajatakaswa na wachungaji wale!

So kwangu mimi wale maaskofu walifanya kitu sahihi kabisa kwenda kumwombea EL (Mwenye dhambi) ali amrudie muumba wake!

When was the last time wamekwenda as such a big team angalau Muhimbili kuombea wagonjwa?Au magerezani kuwaombea wafungwa?

Usijifanye hujui kinachoendelea hapo.Hizo ni mbio kuelekeaa 2010 kaka!
 
Mbona sijasikia PENGO akienda kula Pasaka (kwa mfano) na wafungwa huko segerea au keko?Au wenye dhambi wanaohitaji maombezi na Kardinali na hao tu waliolazimika kujiuzulu uwaziri mkuu?


kanisa katoliki kwenye kila jimbo kuna padre anayeongoza idara inayoratibu masuala ya wagonjwa na matendo ya huruma kwa wahitaji wakiwemo masikini na wafungwa....kila siku wanapita mahospitalini kuwaombea ..na kuangalia wasio na ndugu wanaoweza kuwasaidia au kuwatafutia misaada.pia kuendesha ibada za maombi na mazishi kwa wale ambao wamekufa iwe mahospitalini au gerezani......

hosipitali za rufaa wanakuwa na resident patients father,pale muhimbili mfano ukimuhitaji hata usiku yupo analala na kuamka maeneo ya pale......na pale pia kuna makanisa na msikiti.

kila mwaka kuna siku maalumu ya waumini kuchangia wafungwa na kuwapelekea misaada inayoratibiwa na kitengi hiki..
 
Kiongozi wa dini Getrude Lwakatare ameteuliwa na Rais kuwa Mbunge na anaweza hata kumteua kuwa Waziri.Kadinadi Pengo amekuwa akijihusisha na maswala yanayoshabihiana na siasa.

nijuavyo mimi ni kwamba mama Rwakatare amechaguliwa kuwa mbunge kwa sababu alikuwa runner up katika viti maalumu (wawakilishi wa wanawake mkoa wa Morogoro ambako aligombea na akafuatia kwa mama Nkya ambaye kwa sasa ni naibu). na ni tume inayopendekeza. labda President anaidhinisha tu.
kuhusu Pengo sijakuelewa unavyosema anajihusisha na siasa labda ni kuwa huwa anaishauri serikali yeye kama kiongozi wa wananchi waliowengi. na ni jukumu lake.
 
Hivi sikuza karibuni tulimsikia Pengo kumuonya Jk kutoegemea upande mmoja, kwani yeye pengo ndie mwenye uwezo wa kuwashawishi waumini wake ni nani wampigie kura ,matokeo yake tunashuhudia nini anajaribu kukifanya na ujumbe gani anautuma kwa Jk na waumini wa Dini nyingine.
 
Nadhani masuala mengi ya siasa na dini yanachanganya watu akili pale tunaposhidwa kutofautisha kati ya kanisa na dini na siasa na serikali. Kimsingi, tofauti ipo kati ya kanisa/msikiti na serikali, lakini sio kati ya dini na siasa. Sheria, value, ethics, kwa njia moja ima nyingine zimetungwa kufuatia imani za watunzi. Ndio maana sheria za unyongaji, utoaji mimba, watoto, vita etc, ukiangalia kwa ndani unakuta kuna utu wa binadamu unalindwa kwa kuzingati haki na maadili ya mahusiana ambayo unayapata katika imani mbalimbali.
 
Pengu tunamfahamu tangu siku nyingi kuwa ni mnafiki, anayejificha ndani ya mamlaka ya kanisa katoliki. Anapenda sana ukuu na kutukuzwa. Ni chui ndani ya ngozi ya kondoo. Nadhani wakatoliki hawatakubali kuabudishwa kwa Lowasa, mtu mbinafsi, na mwizi asiye na staha wala karama ya kuwa kiongozi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wakatoliki wasipotoshwe na huyu Pengo kumurudia Lowasa. Amina.
 
Kama Pengo alisema hivyo basi huenda alimaanisha waumini wa jimbo lake la Dar. Huko kwingine kila jimbo lina askofu wake. Kumbuka JK alipata kura nyingi toka kanda ya ziwa ya wasukuma. Siju kuna majombo mangapi huko ya wakatoliki na maaskofu wao. CCM wakipoteza jimbo la Pengo basi wanayo mengine tele.
 
Hivi sikuza karibuni tulimsikia Pengo kumuonya Jk kutoegemea upande mmoja, kwani yeye pengo ndie mwenye uwezo wa kuwashawishi waumini wake ni nani wampigie kura ,matokeo yake tunashuhudia nini anajaribu kukifanya na ujumbe gani anautuma kwa Jk na waumini wa Dini nyingine.

Mbona heading na content haviendani? Hapa umemwelezea tu Pengo issue ya Lowasa je? Umbali wa waislamu kwa JK je?
 
kwa maoni yangu PENGO hawezi kumtakasa LOWASSA kama alivyofanya yule askofu wa kkkt Lowasa alipotoka kwenye uPM, Pengo anajua uchafu wa lowassa. nimgeshangaa sana na ningemdharau moja kwa moja kama nilivyowadharau maaskofu wa kkkt kushabikia UFISADI kwa sababu ya hela nyingi zinazotolewa kusaidia kanisa. yaani they do not care where the money comes from, and who brought that to assist church
 
Aku! Kumbe wakristo hupiga kura kwa mujibu wa akili ya za viongozi wao? Sio akili zao wenyewe!
 
When was the last time wamekwenda as such a big team angalau Muhimbili kuombea wagonjwa?Au magerezani kuwaombea wafungwa?

Usijifanye hujui kinachoendelea hapo.Hizo ni mbio kuelekeaa 2010 kaka!

Naona hujanielewa bado hapa! Ukitaka kuielewa hii, fikiria kiimani zaidi...kama unafikira za kidunia hutanielewa kabisa!
 
Ndugu yangu, mwanzoni mwa post yangunilisema ''tusichanganye dini na siasa'' hapa, we unasema EL hakukiri na hana mpango wa kukiri dhambi zake, nani ka kwambia hayo? wewe ni padre?

Kwa kukusaidia tu, RC kuna kitu kinaitwa Kitubio (Confession) ambapo mwenye dhambi huungama kwa padre madhambi yake wakiwa faragha, na padre hatakiwi kudisclose hiyo fact indefinately! Sasa how do you know EL hakufanya hivyo?

Usinielewe vibaya, sisemi EL hana makosa hapa TZ, ninachotaka kueleza hapa ni tofauti ya taratibu za kiroho (hasa RC) na za kisiasa!
Lowassa sio RC!
 
Kuna taarifa ilitolewa na Gazeti la CITIZEN tanzania tar3-5-2009 na ilikuwa leadingStory, Bahati mbaya Mzee wa copy na paste hakuiona au hakuwa na wasaa wa kuisoma na kuipost hapa.

Kama kuna mdau anaweza ipata hio taarifa tunaomba aiweke hapa tupate ijadili.Taarifa inazungumzia Kanisa Katoliki na Rais anaefaa 2010.

....The Catholic Church in Tanzania has launched a comprehensive project whose aim is to influence the 2010 electorate process, and ensure that the country gets a leader of the Church’s choice.

An apparently well articulated strategy that has been published in a booklet being circulated among Catholics countrywide involves the forging of a mechanism to interview prospective candidates, set the election agenda and assess the results after the bailout has been cast……….

The 18 page booklet entitled “ Mpango wa Kichungaji Kuhamasisha Jamii Kuelekea Uchaguzi says the country is experiencing serious leadership problems and calls on all Catholics to fully participate in the process to elect good leaders for 2010-2015 parliamentary term…..


Kwa alie na kitabu hicho tunaomba aturushie....then tunaweza jadili zaidi
 
Back
Top Bottom