Kwani raisi mzuri ni lazima awe RC?
Kuna ukweli wa hizi habari?
wangerudishiwa nini kama hawakuwa na cha kuitaifishwa...badala ya kuwashutumu na sote tuamke tuanze process kama yao.
..at the end of the day, kwasababu kila mtu atakuwa makini na amechangamka, basi lazima tutapata kiongozi mwenye uwezo.
NB:
..habari hii ni isije kuwa kama yale malalamiko ya Kanisa Katoliki kuingia makubaliano na serikali kurejeshewa shule na hospitali zao zilizotaifishwa.
..wengine badala na wao kuingia mkataba wa namna hiyo na serikali waishia kulalamika tu for almost 15 years now.
Nimesoma ile article, wanasema uongozi wake ni mbovu na umeshindwaSi Pengo alisema Jk ni chaguo la Mungu na walimpigia debe na kumbeba juu juu. Je Hawamtaki tena au ni huyu huyu wanaemfagilia?? .
Hapa tatizo ni shule, wao hujenga shule sasa wanavyuo vikuu, sekondari, chekechea, na vyuo vya ufundi ni vyema na wengine wakaiga na kutoa mazao mazuri. Ila sijali sana kama dini yeyote itasaidia kumtoa sultan na kusaidia wananchi wa kada zote. Wakatoliki wana shule nyingi na hospitali na zinahudumia wote na ubora wake.Ila inajulikana kuwa rc wana task force yao kwa nchi zote duaniani ya kutaka na kupata wanachotaka toka serikali tawala.....hata hapa wakitaka kuongoza wakatoliki wachague rais kwa favor yao wanaweza.....watapambana na mitandao sasa....waangalie isije ikazuka fujo...tena ya kidini au kiimani zaidi.
Je ni kweli kwamba tuna leadership crisis in TZ?? Hili ndiyo swali la kulijadili hapa badala ya kupiga siasa. Kama RC washaona na kutamaka hadharani ni vyema tukawaunga mkono. Na kama si kweli kuwa TZ hatuna leadership crisis kwa sasa basi tuwapinge waziwazi.
Ukifungua JF thread nyingi na watu wengi wanaonyesha kukubaliana na hili lakini kwa vile ni RC basi swala la dini lishachukua mkondo wake. JF watu ni vigeugeu tupu!!!
Mfumwa said:ni haki yao kama raia wa Tanzania, lakini lazima ku-take care kwa matamshi yao. Manake na Waislam wakianza isije ikawa nongwa baadae. Kanisa Katoliki limekuwa likitoa sana matamko, nakumbuka wakati wa Mwinyi mara kibao walitoa. Sasa isije ikatupeleka tukafika yale ya Lebanon tukagawana vyeo.
Mfumwa,
..kila upande utumie haki yake ya kikatiba.
..utaratibu wa upande mmoja kukurupuka baada ya kuona wenzao wanatumia haki yao ya kikatiba ndiyo unaoleta matatizo wakati mwengine.
..hulka ya "bora sote tukose" nadhani ndiyo mzizi wa migogoro mingi ya kiimani Tanzania.
Si Pengo alisema Jk ni chaguo la Mungu na walimpigia debe na kumbeba juu juu. Je Hawamtaki tena au ni huyu huyu wanaemfagilia?? I am sick with this.
Viongozi wa dini ni wanafiki wakubwa wanashindwa kupambana na matatizo tuliyonayo kwa uhalisia wake na kuhuburi haki na sheria mbele ya katiba na Mungu sasa wanataka kuhaha.
Wamwiige Des mond Tutu, Martin luther King, Mother Theresa nk hawa walipigania kila aina ya haki bila kujali vitisho vya serikali zao.