Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Sitegemei mabadiliko ya katiba wakati Rais aliyeko madarakani akiwa bado anataka ugali mwingine kwa miaka mitano ijayo.

Hata hivyo... JK atabadilisha katiba wakati wa muhula wa pili. na mengi atatusikiliza kwa sababu atakuwa hawanii yeye tena urais.

Kwa maana nyingine sitashangaa kusikia CCM ya 2015 inaweka kwenye ilani yake kwamba itafumua Katiba ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania.
 
Viongozi wetu wa dini nao ni opportunists tu. Wanaganga njaa zao. Sijaona mahala wakaonyesha msimamo thabiti wa kuwatetea walalahoi wa nchi hii.

They are part of the elite group in this land. Wanapenda heshima na kutukuzwa kusikostahili.

Nchi ambazo viongozi wa dini wako upande wa walalahoi, tumeona mifano ya viongozi hao kukwaruzana na viongozi wa serikali inayotetea ufisadi. Hali ni tofauti hapa kwetu.
 
Kuna Maaskofu wengine wanaelekea kushirikiana na mafisadi waziwazi, hasa kwenye shughuli za Lowassa.

Ni kweli na hasa kwa waluteri, Mimi ni mluteri na nimekwisha poteza imani na mtazamo wa viongozi wangu kwenye suala la mtazamo wa kanisa kisiasa. Kwa waumini wanaoabudu Azania Front watakubaliana nami, kuwa pesa/mamlaka yamenunua kanisa......fyi Anna Mkapa ni mzee wa kanisa....for what she has done???? God knows.
 
Religious establishments have primarily 2 objectives...
1. Increase the number of adherents
2. Increase influence on the lives of the 'believers'

notwithstanding non-expansionist faiths such as Judaism and Buddhism.. they dont wish to increase the number of adherents (at least not aggressively )...lol but they DO want more control... In Tanzania, Nyerere saw this and put them all on a leash.. Sasa sijui saivi itakuaje...
 
Mzawa, usiwalaumu Walutheri, wafanyaje! ni kujipendekeza, either kwa watwala au kwa mafisadi, mradi wa win sympathy, illa viongozi wadini hawana vision, ubinafsi tu na si utaifa, even if you have to do bad for you good!
 
Mkuu nafikiri waliosema hivyo ni maaskofu wa kanisa la Lutheran [ nipo tayari kurekebishwa ], hawa wa sasa ni RC.
Hata hivyo at least wameongea jambo la maana, na itakuwa na maana zaidi kama watausambaza waraka huu katika parokia zote na vigango vyake.

Nami nauliza nipate kujua, hivi askofu Kilaini ni Mluteli? Yeye ndiye aliyetamka maneno hayo na kumpigia debe sana Jakaya!! Hata alipozulu Kagera , muungwana made a point ya kukutana na baba mzazi wa Kilaini! upo hapo?
 
Sasa nimeamini ni vigumu kujua nini Watanzania wanataka. Kumbe ndio maana!
 
Mkuu nafikiri waliosema hivyo ni maaskofu wa kanisa la Lutheran [ nipo tayari kurekebishwa ], hawa wa sasa ni RC.
Hata hivyo at least wameongea jambo la maana, na itakuwa na maana zaidi kama watausambaza waraka huu katika parokia zote na vigango vyake.

- Sasa Lutheran wakisema one thing ambacho ni contradictory na mafundisho ya Mungu, RC wanatakiwa kufanya nini kunyamaza kimyaa?

FMES!
 
Angalia maneno yako FMES, wewe mwenyewe ulishawahi kusema Lau si Fisadi na siku chache zilizopita ukasema Lau ni Fisadi.

Kama unaamini ulihoandika hapo juu basi ingekuwa ni Busara kuanza kujiita wewe mwenyewe kuwa ni Mnafiki.

Asante

- Wewe una matatizo yako binafsi na mimi ambayo siwezi kukusaidia, sijawahi kusema Lau ni Nabii chaguo la Mungu, hawa wachungaji walsiema Kikwete ni chaguo la Mungu na ni nabii hebu tizama tofauti,

- Na besides nilisema Lau sio fisadi wka sababu sijaona ushahidi, ukajaribu sana kuharibu elimu yake na kazi zake kabla ya kwua waziri, nikakukatalia na facts, sasa naona since then unahangaika sana na kubadilika rangi lakini unapoteza muda bure,

- Leo ninamuita Lau fisadi kwa sababu tu anatakiwa kugombea urais na mafisadi, lakini sio kama ulivyolia sana hapa kwamba ni fisadi maana mpaka leo hujaweza kuweka ushahidi on that zaidi tu ya chuki za binafsi ambazo unazo against kila kiongozi wa Tanzania isipokuwa General Mboma tu!


- Acha unafiki kama wa hawa wachungaji, eti mgombea binafsi ndiye atatusaidia wa-Tanzania? Kama wanaamini hivyo kwa nini hawajaenda kwenye sheria kama Mtikila?

FMEs!
 
Aliyesema Kikwete ni chaguo la Mungu ni Kilaini pekee askofu msaidizi wa Dar es salaam sio mwadhama pengo wala Baraza zima la Maaskofu. Kumbukeni kati ya hawa maaskofu kuna wengine walimpinga Kikwete wazi wazi kama yule Mtega wa Songea aliyempinga Kikwete na Nchimbi mpaka wakamshtaki kuwa anachanganya dini na siasa.

Hata kama wangekuwa kuwa kweli wote walimuunga mkono Kikwete lakini haiwazuii wao kujirudi na kumpinga baada ya kuona ameboronga.

Na hata kama ingekuwa hawajajirudi bado haiwazuii wao kudai mabadiliko ya katiba na suala la mgombea binafsi maana ni mambo tofauti kabisa.

Jambo la muhimu ni kuwa hapa wamekuwa wawazi, wamekosoa CCM na Serikali yake kwa kukataa mambo ambayo ni sauti ya umma na wameunga mkono wazi ajenda ya umma. Ambayo wangeweza kabisa kuinyamazia wasionekane kuwa wanaunga mkono jambo ambalo limesemwa pia na upinzani.

Tuwapongeze na kuwaunga mkono badala ya kulalamika tu

serayamajimbo
 
Aliyesema Kikwete ni chaguo la Mungu ni Kilaini pekee askofu msaidizi wa Dar es salaam sio mwadhama pengo wala Baraza zima la Maaskofu. Kumbukeni kati ya hawa maaskofu kuna wengine walimpinga Kikwete wazi wazi kama yule Mtega wa Songea aliyempinga Kikwete na Nchimbi mpaka wakamshtaki kuwa anachanganya dini na siasa.

Hata kama wangekuwa kuwa kweli wote walimuunga mkono Kikwete lakini haiwazuii wao kujirudi na kumpinga baada ya kuona ameboronga.

Na hata kama ingekuwa hawajajirudi bado haiwazuii wao kudai mabadiliko ya katiba na suala la mgombea binafsi maana ni mambo tofauti kabisa.

Jambo la muhimu ni kuwa hapa wamekuwa wawazi, wamekosoa CCM na Serikali yake kwa kukataa mambo ambayo ni sauti ya umma na wameunga mkono wazi ajenda ya umma. Ambayo wangeweza kabisa kuinyamazia wasionekane kuwa wanaunga mkono jambo ambalo limesemwa pia na upinzani.

Tuwapongeze na kuwaunga mkono badala ya kulalamika tu

serayamajimbo

- Hakuna anayelalamika ila tunatoa maoni yetu kama na wao walivyotoa maoni yao, kama Mchungaji mmkoja anatoa pumba dhidi ya mafudnsiho ya Mungu ni wajibu wa wachungaji wengine kumrekebisha wakinyamaza maana yake ni moja wanam-support, mgonea binafsi sio hoja ya wananchi wote kama ulivyosema jaribu kujizungumzia wewe na maoni yako,

- Binafsi siamini kwamba mgomeba binafsi ndio jawabu la matatizo ya uongoZi mbovu tuliyonayo nchi hii, kwa sababu wale wenye hela ndio wanaoweza kushinda kwa kugombea binafsi, na sio siri kwamba sasa hivi wotew ako kwenye siasa tayari je wamefanya nini cha maana?

Mgombea binafsi na this kind of katiba tuliyo nayo sasa ni waste of time!

FMES!
 
lakini unajua kila mtu amepigwa na butwaa jinsi JK alivyoshindwa ku-perform kinyume cha matarajio

Alikuwa mnafiki tu wakati wa kampeni zake 2005 na Watanzania tukamuamini. Hakuna hata moja alilotimiza katika ahadi zake za kampeni. Watanzania tutanya makosa mkubwa kumrudisha tena kama Rais wa nchi 2010. Huyu hafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kumi.
 
Mkuu nafikiri waliosema hivyo ni maaskofu wa kanisa la Lutheran [ nipo tayari kurekebishwa ], hawa wa sasa ni RC.
Hata hivyo at least wameongea jambo la maana, na itakuwa na maana zaidi kama watausambaza waraka huu katika parokia zote na vigango vyake.

Kwame asante kwa kunikumbusha kuwa Pengo na Kilaini ni maaskofu wa Lutherani! Maana hawa ndio walikuwa wa kwanza kutamka kuwa Muungwa ni chaguo la Mungu.
 
mimi sijali nani wamesema na walisema nini mwanzo cha maana ni hicho wanachosema sasa hivi, je kitaleta mabadiliko gani?
je mgombea binafsi ataongeza ushindani?
je ushindani utakuwa na faida kwa wa tz au hasara?
na hivi ndio vitu tunavyotakiwa kuvijadili na hivyo vikishaisha ndio mnaweza kuongelea wale walisema nini juu ya JK

Mgombea kutoka kwenye cham chenye maandiko safi lakini kina viongozi na wanachama wenye mawazo na msimamo duni kama CCM anakusaidia nini??Mgombea kutoka katika chama ambaye uzalendo na nia yake ya kujenga nchi vinaleta maswali mengi kuliko majibu anakusaidianini?Hofu yako ni kuona mtu katika ubinafsi wake akisimama kugombea au mtu akisimama kugombea baada ya kuteuliwa na kamati za kinyang'au??Ushindani tayari upo, tatizo kubwa ni moja walio wengi kati ya washindanao ni Mafisadi. Watu walio tayari kushindani kwa faida ya wananchi wengi wako nje ya mashindano.Kikubwa zaidi ni Hukumu, hukumu hii imetolewa kwa kufuata katikba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuto tekeleza hukumu hii ni kwenda kinyume cha katiba, kitu ambacho pekee yake bila nyongeza yeyote ni Uvunjaji wa sheria , ni Jinai
 
Last edited:
hawawezi kufanya hivyo hata siku moja, wakijaribu tu, Mengi atachukua form siku hiyohiyo. kila mwaka wananchi wamekuwa wakinong'ona kuwa mengi ajiingize kwenye siasa. ccm inajua kuwa, siku wakiruhusu mgombea binafsi, ndo mwisho wao. hakika utakuwa mwisho wao kwasababu, kuna watz wengi sana waaminifu na wale ambao wanaweza wakakubalika na jamii watakao jitosa na watashinda. hicho kitu hapa tz tukisahau, tutapiga kelele wee lakini wao wanajua madhara yake.
 
Kanisa katoliki Tanzania limejipanga kuleta mabadiliko makubwa nchini, MwanaHALISI limebaini.

Tayari mpango wa kanisa umeanza na taarifa zinasema hatua ya utekelezaji iliyofikiwa hadi sasa ni ya kuridhisha.

Mchakato wa kanisa ulioanza Januari mwaka huu unalenga mafanikio ya kwanza yapatikane katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika mwaka huu au mwaka kesho.

Mpango wa kanisa umelenga kuwaamsha waumini na wananchi wote kwa ujumla ili washiriki kuleta mabadiliko makubwa ya uongozi wa nchi, kuanzia vitongoji, mitaa, vijiji hadi ngazi ya taifa.

Mpango huo shirikishi wa aina yake unaolenga kutoa elimu ya juu ya uongozi bora, viongozi bora na jinsi ya kuwapata wawakilishi sahihi wa wananchi.

Mchakato wa kanisa ambao tayari umechapishwa katika vitabu mbalimbali, unalenga upatikanaji viongozi bora mwaka kesho, lakini unafanya maandalizi ya uchaguzi wa 2015 kwa vile tathmini ya hatua ya kwanza inakamilika mwaka 2011.

Mwana HALISI imepata vitabu hivyo mahsusi kwa mpango huo ambavyo vimetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), vyenye ratiba ya utekelezaji hadi 2011.

Ratiba ya mpango huo iliyobeba kichwa "Mpango wa Kichungaji Kuhamasisha Jamii Kuelekea" inaeleza kuwa "Mungu alimpa mwanadamu wajibu wa pekee, siyo tu mlinzi nz mdhamini wa dunia...bali pia kuwa mshiriki katika kuumba na kutunza".

Kanisa limesema katika miaka ya hivi karibuni limegundua matatizo mengi ya uongozi ambayo yanahitaji kujadiiwa na kupatiwa tiba.

"Uongozi unahitaji watu wenye sifa ya huduma, wanaojali, walio wazi, wanaowajibika, wanyenyekevu, wenye hekima na upendo...Lakini uongozi kila mara unashawishika kutenda kinyume na hayo na kuwa na uchoyo na kutumia madaraka vibaya," linaeleza kanisa.

Katika kukubaliana na hali hiyo kanisa limesema "Ni muhimu kuandaa viongozi, kushirikiana nao na kushikamana nao na kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuwa jasiri walio waaminifu katika kazi zao"

Kanisa linasema watu wanapaswa namna wagombea wanavyoteuliwa na vyama vyao, na pia kutafuta njia na vyanzo vya vya fedha za vyama vya siasa na namna wanavyozitumia.

Lakini pia kanisa linawataka waumini kujadili mfumo wa uwakilishi wa uwiano na kuona kama unaweza kuwa bora kuliko ule wa sasa wa mgombea mwenye kura nyingi ndiye atangazwe mshindi.

"Kuna haja kubwa pia ya kuwasaidia watu kuijua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni lazima katika mambo ya kijamii tuwahimize watu kueleza matatizo wanayokumbana nayo..na kuyatolea taarifa katika ngazi ya Parokiahadi jimbo au wilaya"

"Tuwasaidie kushiriki katika utawala tangu ngazi ya serikali za vijiji au mitaa hadi ngazi ya halmashauri ya wilaya na kutafuta taarifa, kisha kufuatilia nini watumishi wa umma wanafanya katika kuhudumia watu," inasema taarifa ya kanisa.

Kanisa limepanga kuunda timu toka Chama cha Wanataaluma Wakristo (CPT) na wajumbe wa Halmashauri, kutengeneza maswali maalum yanayoendana na mazingira husika ili watu wajadili na kutoa maoni.

"Hapa tusiwape nafasi wale ambao ni wagombea wa kisiasa kutawala mjadala," kanisa limeonya.

Katika kijitabu kingine CPT wametoa "mada za kuongoza maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2010," ambazo ni Uongozi Mintarafu Ufunguo wa Mabadiliko nchini Tanzania, na vipaumbela kwa Misingi ya Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.

Mada nyingine ni mfumo wa Kisheria Tanzania: Mapengo na Changamoto zake, Haki za Binadamu katika sera za Biashara na Fedha, Hifadhi ya Jamii, na mtazamo wa Kimaadili katika Mfumo wa Siasa na Uchumi.

Katika mada ya Uongozi Mintarafu, Kanisa linasema viongozi ni lazima waaminike na wawajali watu, kwa kuwatendea haki na siyo kufukuzia mali na utajiri na kwamba fikra na taratib moya zinahitajika kuwezesha umma kushiriki katika kufanya maamuzi.

"Hatujajipanga kujiongoza, ila kwa ushawishi wa watu kukubali yale wataalam na viongozi wa kisiasa wanayoamini ni mazuri kwa ajili yao," kanisa linaeleza.

Kama ratiba hiyo ya Kanisa Katoliki itatekelezwa kama ilivyopangwa, na wananchi wengi wakafikiwa na kupewa elimu hiyo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010, basi kunaweza kutokea mabadiliko makubwa ya safu ya uongozi wa nchi mwaka ujao.

Mpango huu unadhihirisha kuwa kuna mambo ambayo yatakuwa yamewashtua maaskofu wa Kanisa Katoliki na viongozi wengine wa dini.

Mchakato huu unaweza kuleta mabadiliko ambayo pengine historia ya nchi haijawahi kushuhudia tangu uhuru, kama ratiba ya kanisa itafuatwa na kutekelezwa kikamilifu.

Ratiba inaonyesha ilianza kutekelezwa Januari mwaka huu kwa Baraza la Maaskofu (TEC) kufanya mkutano wa Taifa wa kutengeneza program na wahusika walikwa wakurugenzi wa kichungaji na wajumbe wa Tume ya Haki na Amani.

Kazi ya kukamilisha programu katika mfumo wa vijitabu ilifanyika Februari na mpango wa kutuma mpango huo kwenye majimbo ulitekelezwa Machi, walengwa wakiwa maaskofu, wakurugenzi wa uchungaji, majimbo na viongozi wa Tume ya Haki na Amani wa majimbo.

Aprili mwaka huu kulikuwa na mikutano ya kila jimbo ya kuzindua programu, walengwa wakiwa mapadre, watawa, halamashauri na vyama vya kitume na taasisi. Walioanza ni mapadri na watawa, wakifuatiwa na walei.

Semina kwa ajili ya walei na vyama vya kitume katika ngazi ya parokia zilianza mwezi huu na zitaendelea hadi Juini. Walengwa ni halmashauri zinazojumuisha viongozi wa jumuiya ndogondogo, vyama na kamati katika ngazi hiyo.

Programu itafikishwa katika jumuiya ndogondogo kati ya Julai na Septemba na walengwa watakuwa waumini na wakazi. Wasimamizi wa kazi hiyo ni paroko na halmashauri ya parokia.

Oktoba hadi Desemba 2009 kutakuwa na mijadala na utekelezaji katika ngazi ya jumuiya ndogondogo na vyama vya kitume. Wasimamizi watakuwa paroko, kamati ya utendaji na viongozi wa jumuiya hizo.

Mkutano wa taifa wa tathmini ya kwanza ya uelimishaji wananchi utafanyika January 2010, miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu kwa kushirikisha wakurugenzi wa kichungaji na wajumbe wa Haki na Amani.

Februari hadi Septemba 2010 kutakuwa na mwendelezo wa mijadala na utekelezaji, vinavyolenga waumini na wakazi katika majimbo, parokia, jumuiya ndogondogo na wananchi kwa ujumla.

Hatua hiyo ndiyo itaongoza hadi uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba 2010.

Mkuyano wa kitaifa wa tathmini ya pili ya mpango huu utafanyika Januari 2011, ili kubaini ajenda baada ya uchaguzi.


Chanzo: Gazeti la MwanaHALISI la leo
 
Kubenea akiishiwa habari huwa ana recycle au ku copy kwa wenzie hayo yalishaandikwa na The citizen tokea lini sijui huko....
 
Kubenea akiishiwa habari huwa ana recycle au ku copy kwa wenzie hayo yalishaandikwa na The citizen tokea lini sijui huko....

Well Masatu,

Ni kweli yaliandikwa na The Citizen, Lakini mimi nionavyo ni kwamba hoja yako ingekuwa, Je hapa JF issue hii imeshajadiliwa na wadau au vp, maana Magazeti yanachokoza tu, lakini wataalamu wanaoheshimika kama wewe, ndo wanaochambua hoja za magazeti na vyanzo vingine!

Sasa, kimsingi , thread ya jinsi hii ilishajadiliwa, na wadau kibao wakatundika maoni yao, wengi wakisupport Taasisi za KIDINI kuingilia au kuweka hadharani taratibu ambazo wao wanaona zitaleta uwazi zaidi katika kuboresha mchakato mzima wa uchaguzi.

Nawasilisha...!
 
Kubenea akiishiwa habari huwa ana recycle au ku copy kwa wenzie hayo yalishaandikwa na The citizen tokea lini sijui huko....

Na hiyo The Citizen haikifaulu kutufikia sisi wote.
 
Back
Top Bottom