Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Wakati huo huo BAKWATA wako kimyaaaaaaaaaa, lakini we should expect much from them kwani BAKWATA inaongozwa na mtu ambaye hajui kiingereza...na elimu yake ni ndogo sana

big up to maaaskofu kuhusu hili

Anyway,English is just the language but not the knowledge. BAKWATA can give us its views even by using our national language.Si unajua wenye lugha ya kiingereza wanaitwa makafiri!!!!!
 
Viti Maalumu kwanzi ni Kitu gani? Naomba mwenye maelezo ya kunitosheleza anieleze. kwa nini wawe maalum. Kwani Mama Malechela ni Maalum? na tangu wameingia huko bungeni wametusaidia nini hasa, au wanapata tuu posho wananyamaza. Ujinga kabisa. Kama unajiamini wewe ni mwanasiasa ingia kwenye kinyang'anyiro sio kukaa nyuma ya mkubwa unasubiri waje wakuchague na wewe eti uwe mbunge. Mimi naamini kama uliomba kura kwa wananchi wakakupa una jeuri ya kutembea kifua mbele kwa kuwa una support ya watu wako, lakini kama ulivu...... tuu huyo aliyekupa hiyo dhamana siku moja atakuambia kama hutaki ku... hutapata tena.
Kuna siku nimekuwa nikisikiliza hoja ni kwa nini wapewe viti maalum eti wanawake hawana hela za kufanya kampeni @#$%^&*( mbona wana hela za kuhonga vijana wadogo huku mjini? Halafu naomba mtu aniambie ni Mbunge yupi wa viti maalumu kweli ni mkulima anayewakilisha wakulima wenzake wa kule Tabora, au Kyela. Wooote hao wanakaa mijini na Mafisadi ndio wanateuliwa kwenye viti maalum.

Wanawake amkeni kama Mama malechela, kama Hilary Clinton, Kama rais wa Liberia acheni ku...... kupata ubunge. NASEMA SIPENDI WALA SITAKI KUSIKIA VITI MAALUM. ACHENI HIZOOOOOO
 
Wakati huo huo BAKWATA wako kimyaaaaaaaaaa, lakini we should expect much from them kwani BAKWATA inaongozwa na mtu ambaye hajui kiingereza...na elimu yake ni ndogo sana

big up to maaaskofu kuhusu hili

Am not moslem but I can be the front line to condem them.....

Walichosema Maaskofu ni KUNTU ila tatizo siku hizi ktk madhabahu kuna uroho wa madaraka thus many churches are emerge and vyeo wanajipa kana kwamba hakuna TBS ya IMANI.

Serikali ya ki-zecomedy haitishwi na lolote na ufisadi udumu
 
ujumbe mkubwa walioutoa maaskofu, lakini wauchafua kwa kuomba viti vya ubunge.
 
Hawa maaskofu sijui wamnasomavitabu gani kwani kama ni Biblia wafungue tu sehemu inayozungumzia kuhusu kutmikia mabwana wawili. Naamini kama ni wafuasi kweli wa Kristo basi wajue wazi kuwa wao wamechagua kumtumikia Mungu na si Kaizari. Kuingiza dini kataoika vyombo vya serikali yataturudisha kwenye matatizo makubwa ya kiimani kama ilivyotokea wakati Mfalme Konstanino alipotoa sharti la kukubali kubatizwa kuwa Mkristo ni pamoja na kubadilisha siku ya kuabudu kutoka Jumamosi (sabato) na kuwa jumapili (dominika).
kitu gani ambacho wameshindwa kutekeleza katika kuwahudumia kondoo wao mpaka wawe na nguvu za kidola. Iwapo kweli wamekaa na kufikiria hayo wajirudi. Ni vigumu kuitoa chawa walo nguoni mwako, je wtatpata wapi moral authority ya kuikosoa serikali wakati wao pia ni sehemu ya maamuzi hayo?
 
Maaskofu waionya serikali, Bunge
na Prisca Nsemwa
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAKATI mkutano wa Bunge la Bajeti unatarajiwa kuanza kesho mjini Dodoma, Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), limeionya serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini wakati wanapojadili bajeti ya mwaka 2008/2009, kwa kuwaangalia wananchi kutokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha siku hadi siku ili kuwanusuru.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za jubilei ya miaka 50 ya baraza hilo zilizofanyika katika Kituo cha Msimbazi, Dar es Salaam jana, Rais wa baraza hilo, Askofu Yuda Ruwaichi, alionya kuwa bajeti inatakiwa kumuangalia zaidi Mtanzania wa kawaida, kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Alisema wabunge wanapojadili bajeti hiyo wanapaswa kuangalia kwa makini, ili isiwakandamize na kuwaumiza Watanzania, ambao hadi sasa maisha ya wengi ni magumu.

“Bunge na serikali wawe makini wanapokwenda kujadili suala la bajeti huko bungeni, hasa kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili Watanzania walio wengi, hivyo bajeti hii iwanusuru na isiwakandamize na kuwaumiza zaidi Watanzania,” alisema Ruwaichi.

Pia alisema serikali inatakiwa iangalie suala la maadili na uwajibikaji kwa vijana na watoto, ili kujenga taifa lenye nguvu kazi na maadili ambayo yanakubalika kwa binadamu na Mwenyezi Mungu.

Alisema baraza hilo kwa muda wa miaka 50 limefanikiwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchungaji na kuleta faida katika jamii.

Baadhi ya faida hizo alizitaja kuwa ni pamoja na kuendelea kufungua shule na vyuo, ili kuwawezesha watoto kupata elimu, kuanzisha vituo vya afya na kuimarisha miradi mbalimbali nchini.

Hata hivyo, alieleza kuwa mafanikio hayo yamepatikana kutokana na amani na ushirikiano uliopo na hivyo kurahisisha shughuli mbalimbali kuendeshwa katika hali ya amani na utulivu, ili kuweza kuleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kwa taifa zima.

Askofu huyo alisema mafanikio hayo ni kwa msaada wa Mungu, hivyo katika maadhimisho hayo ni nafasi pia kwao kumuomba Mungu toba kwa yale ambayo hawakuyafanya kutokana na sababu mbalimbali na hivyo kuweza kujipanga upya katika miaka mingine.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo akimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, alisema madhehebu ya kidini nchini yana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi, kwa kuchangia katika sekta mbalimbali, zikiwemo elimu, afya na shughuli nyingine za kijamii.

Alisema baraza hilo linachangia asilimia 20 kwa taifa katika suala la afya, jambo ambalo linatia moyo na kuonyesha ushirikiano mkubwa uliopo kati ya serikali na madhehebu ya kidini, hivyo kuweza kuendeleza amani na utulivu uliopo.

“Madhehebu ya dini yana mchango mkubwa katika taifa letu na kwa kulitambua hilo serikali inashirikiana bega kwa bega na madhehebu hayo ili kuweza kuleta maendeleo na kudumisha amani na utulivu ndani ya taifa letu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Pinda alieleza kuwa tatizo ambalo sasa limelikumba taifa ni imani za kishirikina, ambapo baadhi ya watu wanafanya mauaji ya kutisha kwa imani ya kutaka utajiri.

Kutokana na hali hiyo, alitoa wito kwa viongozi wa dini kukemea vitendo hivyo, kwani ni kinyume cha matendo ya kibinadamu.

Alisema watu wanaofanya hivyo ni wauaji na wanastahili adhabu kali, kwani wengi wanaofanya vitendo vya kuwaua maalbino kwa imani za kishirikina ni watu ambao wanaishi katika maeneo yetu.

“Viongozi wa dini, mimi naamini mkiendelea kukemea vitendo hivi vitakwisha, kwa kuwa hawa wauaji tunaishi nao na tunasali nao, namaanisha na makanisani wanakuja, hivyo kama tukiwa na nia moja, tunaweza kutokomeza vitendo hivi,” alisema Pinda.

Pia alisema kuwa hali ya nchi imebadilika kutokana na maadili ya viongozi kuporomoka, hivyo mkakati mkubwa ambao unatakiwa ni kupiga vita rushwa, ambayo imekuwa ikiathiri shughuli nyingi za maendeleo.

Alisema kuwa viongozi wa dini wana jukumu kubwa la kuwaambia waumini wa madhebu yao kuacha kutoa na kupokea rushwa, kwani rushwa inapunguza imani ya wananchi kwa serikali yao na hivyo kushindwa kufikia malengo.

Wakati huo huo, Mobini Sarya anaripoti kuwa; Chama cha NCCR- Mageuzi, kimeiponda bajeti ijayo, kwa kuielezea kuwa isiyo na tija wala manufaa kwa wananchi wa kawaida, kwani imeanza kuonyesha haitakuwa na unafuu kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho, Faustin Sungura, aliwataka wananchi kutoifuatilia bajeti hiyo, kwani haitawasaidia chochote, zaidi ya kulenga kuwafurahisha wafadhili wa nje.

“Bajeti hii haitakuwa na jambo jipya la kumsaidia mwananchi…. ni wabunge wangapi wamefika kwa wananchi na kuwasikiliza kero zao kutokana na maisha kupanda, ili wakifika bungeni wapitishe kitu kinachowasaidia?” alihoji Sungura.

Alisema bajeti hiyo imeandaliwa kuwafurahisha wageni na mabalozi na wafadhili mbalimbali, ili waweze kuendelea kutoa misaada.

Kwa maoni ya chama hicho, serikali inapaswa kuzingatia mahitaji muhimu ya wananchi na kuwapunguzia kodi, badala ya kuongeza, na kutoa mfano wa mafuta ya petroli ambayo alisema yakifika Bandari ya Dar es Salaam yanakuwa sh 950, lakini kutokana na kodi kuwa kubwa, sasa yanauzwa bei ghali sokoni.

Sungura, alikuwa akitoa tamko la chama hicho kuhusu tathmini ya miaka miwili na nusu ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani.

Akitoa tathmini ya chama hicho, alisema wakati Rais Kikwete akiingia madarakani alijinadi kuwa maisha ya wananchi yalikuwa duni, hivyo katika utawala wake angeyaboresha, lakini ameshindwa kufanya hivyo.

“Wakati huo kilo moja ya sukari ilikuwa inauzwa sh 600, kipande cha sabuni sh 100, kopo la mkaa sh 250 na kilo moja ya unga sh 300, lakini leo hii miaka michache tu sukari sasa inauzwa sh 1,200, sabuni kipande sh 300, mkaa sh 800 na unga kilo sh 700.

“Bei za vyakula, huduma za afya, elimu, umeme na usafiri zimepanda kwa asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka 2005…....visingizio vya kupanda kwa gharama za maisha ni kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia, si kweli, kwani hata bei ya tanzanite, dhahabu na almasi imepanda, hivyo inaweza kufidia bei ya mafuta,” alisema.

Alisema sababu inayofanya gharama ya mafuta kupanda ni kodi kubwa inayotozwa bila huruma wala mpangilio mzuri wa kibiashara katika mafuta baada ya serikali kushindwa kusimamia sekta hiyo.

“Kwa sababu hizi pamoja na nyingine, chama chetu kinaona kuwa serikali ya CCM imeshindwa kusimamia ustawi wa nchi yetu. Hali ya maisha ya Watanzania inazidi kuwa ngumu kila kukicha, huku maisha ya viongozi wa serikali yakizidi kuneemeka, hivyo CCM inatakiwa kuwaeleza Watanzania maisha bora yatakuwa lini,” alisema Sungura.

Aidha, chama hicho kimesema kuwa si vizuri kwa watuhumiwa wa ufisadi kuingia bungeni na kuendelea kuitwa waheshimiwa.

Alisema hata kama watuhumiwa hao hawajathibitishwa kuwa ni mafisadi, ni bora wakajiuzulu ubunge kuliko kuendelea kulidhalilisha Bunge.

“Si jambo zuri kuendelea kumwita fisadi mheshimiwa hata kama hajathibitika, ni bora watuhumiwa wote wajiuzulu,” alisema Sungura.
 
"Si jambo zuri kuendelea kumwita fisadi mheshimiwa hata kama hajathibitika, ni bora watuhumiwa wote wajiuzulu," alisema Sungura.

Mheshimiwa Fisadi, Vijisenti vyako bado viko nje au umevirudisha nyumbani?

Ni upumbavu wa hali ya juu na kuwadharau wananchi pale mafisadi wanaruhusiwa kuingia bungeni. Wabunge wote ambao walikuwa mawaziri au wabunge wa kawaida na wakajiuzulu kufuatia tuhuma za ufisadi wafukuzwe bungeni.
 
on other hand BAKWATA naona hii itawaudhi mana wao na CCM dam dam
 
Wakati ishara ya kupitisha bajeti ni ishara mbaya sana kwa haki ya Mtanzania..Wapinzani wali abstain...Hawajasema kwanini walifanya hivyo...Na hata wale wa CCM walioipigia kura hawajasema nikwanini walifanya hivyo.

Wananchi wengi walilaani kauli za Viongozi walioonyeshwa na MUNGU kuwa KIKWETE NI CHAGUO LA MUNGU.

Ni wazi kuwa ni kweli kwani kama si yeye tusingeweza kujua haya yote ya CCM.

Tunajua SERIKALI ILIPINGA KWA NGUVU ZAKE ZOTE KUHUSU MGOMBEA BINAFSI!

TUNAWAOMBA MUINGIE KWENYE MAOMBI ILI MUTUELEZE NI WAPI MUNGU ATATUPELEKA WAKATI HUU ILI HAKI YAKE ITENDEKE!

KAMA MUNAONA MGOMBEA BINAFSI ANAFAA MUSEME..NA KWA KUSHIRIKIANA NA WAZALENDO WENGINE...FUATILIENI HAYA KWA KARIBU NA MUTUELEZE YUPI NI YUPI.

AHSANTENI

Jmushi.
 
Wakati ishara ya kupitisha bajeti ni ishara mbaya sana kwa haki ya Mtanzania..Wapinzani wali abstain...Hawajasema kwanini walifanya hivyo...Na hata wale wa CCM walioipigia kura hawajasema nikwanini walifanya hivyo.
Wananchi wengi walilaani kauli za Viongozi walioonyeshwa na MUNGU kuwa KIKWETE NI CHAGUO LA MUNGU.
Ni wazi kuwa ni kweli kwani kama si yeye tusingeweza kujua haya yote ya CCM.
Tunajua SERIKALI ILIPINGA KWA NGUVU ZAKE ZOTE KUHUSU MGOMBEA BINAFSI!
TUNAWAOMBA MUINGIE KWENYE MAOMBI ILI MUTUELEZE NI WAPI MUNGU ATATUPELEKA WAKATI HUU ILI HAKI YAKE ITENDEKE!
KAMA MUNAONA MGOMBEA BINAFSI ANAFAA MUSEME..NA KWA KUSHIRIKIANA NA WAZALENDO WENGINE...FUATILIENI HAYA KWA KARIBU NA MUTUELEZE YUPI NI YUPI.
AHSANTENI
Jmushi.

Naona unampa Kikwete sifa kuliko anazostahili. Kikwete amesaidia nini wewe na wengine kujua yote ya ccm?
 
Naona unampaka Kikwete sifa kuliko anazostahili. Kikwete amesaidia nini wewe na wengine kujua yote ya ccm?

Kama si utawala wake huu MAFISADI TUNGEWAJUA?
MUNGU HUWEKA WATU WABAYA KWA WAZURI!
Viongozi wa dini waliposema wameonyeshwa hayo na Mungu...Si lazima awe mtenda mema..Ila hata kama ni mabaya...Basi ni ya kutukomboa!
Umesahahu mambo ya Mungu kuwatumia watu wabaya ili kumkomboa mtu wake?
Soma vitabu vitakatifu utayajua hayo.
 
Kama si utawala wake huu MAFISADI TUNGEWAJUA?
MUNGU HUWEKA WATU WABAYA KWA WAZURI!
Viongozi wa dini waliposema wameonyeshwa hayo na Mungu...Si lazima awe mtenda mema..Ila hata kama ni mabaya...Basi ni ya kutukomboa!
Umesahahu mambo ya Mungu kuwatumia watu wabaya ili kumkomboa mtu wake?
Soma vitabu vitakatifu utayajua hayo.

bado hujajibu swali langu, Kikwete amesaidia vipi wewe kujua unachojua leo kuhusu ccm?
 
Ni muhimu sana kwa watanzania kuwaendea viongozi wao wa dini kuomba msaada wa kiroho na kisaikolojia na kimawazo kama ambavyo wamekuwa wakiwaendea na kuwaeleza matatizo yao ambayo kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na MAFISADI... na maombi yaanzishwe TAIFA ZIMA BILA KUJALI DINI!

HUU NI WAKATI WA MUNGU ALIOULETA KWETU.

Sina maana ya viongozi wa dini waingilie uongozi..La hasha.

Nawakumbishia majukumu yao ambayo mitume wote kuanzia Yesu Kristo pamoja na Muhammad walisimamia...HAKI KWA MNYONGE!

Yesu aliwapinga mafisadi kwa nguvu zote...Kuanzia mafarisayo na watoza kodi mafisadi!

We unafikiri waumini hawalalamiki kuhusu ugumu wa maisha na ufisadi huko misikitini na makanisani?

CCM BYE BYE..Wapinzani bado hawajaonyesha nia ya kweli...Sasa hapa ni MUNGU TU KWA KUPITIA WATU WAKE!

WATANZANIA MUWASIKILIZE VIONGOZI WENU WA KIROHO...HAO MUNGU ATAWATUMIA KAMA WAKIJA PAMOJA BILA KUJALI UISLAM,UHINDU,UKRISTO NK.
 
Ni muhimu sana kwa watanzania kuwaendea viongozi wao wa dini kuomba msaada wa kiroho na kisaikolojia na kimawazo kama ambavyo wamekuwa wakiwaendea na kuwaeleza matatizo yao ambayo kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na MAFISADI... na maombi yaanzishwe TAIFA ZIMA BILA KUJALI DINI!

HUU NI WAKATI WA MUNGU ALIOULETA KWETU.

Sina maana ya viongozi wa dini waingilie uongozi..La hasha.

Nawakumbishia majukumu yao ambayo mitume wote kuanzia Yesu Kristo pamoja na Muhammad walisimamia...HAKI KWA MNYONGE!

Yesu aliwapinga mafisadi kwa nguvu zote...Kuanzia mafarisayo na watoza kodi mafisadi!

We unafikiri waumini hawalalamiki kuhusu ugumu wa maisha na ufisadi huko misikitini na makanisani?

CCM BYE BYE..Wapinzani bado hawajaonyesha nia ya kweli...Sasa hapa ni MUNGU TU KWA KUPITIA WATU WAKE!

WATANZANIA MUWASIKILIZE VIONGOZI WENU WA KIROHO...HAO MUNGU ATAWATUMIA KAMA WAKIJA PAMOJA BILA KUJALI UISLAM,UHINDU,UKRISTO NK.

Watanzania waende kwa MUNGU moja kwa moja na yeye atawasikia na si lazima kupitia kwa viongozi wa dini ambao wengi wao ni vigeugeu tu na wafuata mikumbo.
 
Watanzania waende kwa MUNGU moja kwa moja na yeye atawasikia na si lazima kupitia kwa viongozi wa dini ambao wengi wao ni vigeugeu tu na wafuata mikumbo.

Viongozi wa dini wanapata malalamiko kila siku kutoka kwa waumini wao ambao UFISADI UNAWAFANYA WAWE WATUMWA KWENYE ARDHI YAO WENYEWE ILIYOPIGANIWA NA BABU ZAO KWA DAMU!

RICHMOND NI MSALABA AMBAO MACHUNGU YAKE WANAYAJUA WANANCHI NA VIONGOZI WA DINI KAZI YAO NI KUWAFARIJI NA KUWAPA MIONGOZO YA NANI NI NANI NA KWANINI WAMEHUSIKA KUWAPATIA SHIDA NA MATESO!

Wana haki ya kusimamia haki kwa wanyonge kama mitume wao walivyokuwa wakifanya!
Kumbuka viongozi hao ndio wasimamiaji wa matendo ya mitume wao!
Jesus Christ mwenyewe aliwachukia mafisadi...So as Muhammad kwa wenzetu waislam.
Nia hapa ni kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi kwani muda ni mfupi wa kufanya lolote!
WATUMISHI WA MUNGU NI VIONGOZI WA MAMILIONI YA ROHO ZA WATANZANIA AMBAO WAKO NAO KARIBU MAYBE KULIKO HATA VIONGOZI WAO WANAOWATUMIKIA AMBAO WAMEAMUA KUJIKITA KWENYE UFISADI,UCHAWI NA MENGINEYO UASIYOMPENEDEZA MUNGU WALA MWANADAMU!
 
Back
Top Bottom