Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Naona unampa Kikwete sifa kuliko anazostahili. Kikwete amesaidia nini wewe na wengine kujua yote ya ccm?

Mungu alimtumia AYUBU MAJARIBU MAKUBWA NA HATA KUIANGAMIZA FAMILIA YAKE YOTE!
AYUBU HAKUMWACHA MUNGU!
Mungu alituletea KIKWETE na ni wazi kuwa UDHAIFU WAKE WA KIUONGOZI NA KI MAAMUZI UMEPELEKEA SISI KUJUA MENGI LICHA YA MACHUNGU TULIYONAYO!
Hivyo basi ni mpango wa Mungu kwa watanzania licha ya kwamba tuko wapweke na wenye masikitiko makubwa...BADO TUSIMSAHAHU MUNGU NA TUWASIKILIZE WATUMISHI WA MUNGU MARA MOJA BILA WOGA.
 
Viongozi wa Dini Tanzania kwa kiasi kikubwa wote ni CCM ukiacha wachache walio nje ya taasisi rasmi za kidini.

Huna haja ya kwenda mbali kulithibitisha hili wewe angalia sherehe zote za kidini "waalikwa" ndio hao hao akina JK, PM, Kandoro et al. Je unatarajia nini kutoka kwa watu kama hao?

Hizo taasisi za ndugu zetu waislam mfano Bakwata kujiendeshea mambo yao wenyewe hawawezi seuze mambo muhimu ya kitaifa kila siku timua timua tu.
 
Viongozi wa Dini Tanzania kwa kiasi kikubwa wote ni CCM ukiacha wachache walio nje ya taasisi rasmi za kidini.

Huna haja ya kwenda mbali kulithibitisha hili wewe angalia sherehe zote za kidini "waalikwa" ndio hao hao akina JK, PM, Kandoro et al. Je unatarajia nini kutoka kwa watu kama hao?

Hizo taasisi za ndugu zetu waislam mfano Bakwata kujiendeshea mambo yao wenyewe hawawezi seuze mambo muhimu ya kitaifa kila siku timua timua tu.

Sasa ngoma iweje mkuu?
Maana taarifa nilizonazo hazionyeshi kuwa wanaitaka ccm tena!
Naelewa kuna wale wenye maslahi..Wao wanajulikana..Lakini kuna kina KILAINI na wengineo ambao wana msimamo wa mafisadi kukamatwa!
 
Sasa ngoma iweje mkuu?
Maana taarifa nilizonazo hazionyeshi kuwa wanaitaka ccm tena!
Naelewa kuna wale wenye maslahi..Wao wanajulikana..Lakini kuna kina KILAINI na wengineo ambao wana msimamo wa mafisadi kukamatwa!

Hao kina Kilaini et al they have to stand up and be counted sio kusemea kwenye vibuyu tu...
 
Hao kina Kilaini et al they have to stand up and be counted sio kusemea kwenye vibuyu tu...

Kweli kabisa Masatu...Kila mtu ama watu wote mashuhuri kwenye jamii yetu watoe matamko yao kwani sasa tunajua utofauti wa kauli za kisiasa na zile za kizalendo!
Waseme tu tutamjua yupi ni yupi...Wakichelewa chelewa watakuja kuta mwana si wao!
Hata wale kina BUTIKU WALIOKUWA WAKIDAI WAKAMATWE MBONA KIMYA!
WAZALENDO SEMENI JAMANI...Kimya kikuu kinamshindo na nchi iko njia panda!
 
Sasa ngoma iweje mkuu?
Maana taarifa nilizonazo hazionyeshi kuwa wanaitaka ccm tena!
Naelewa kuna wale wenye maslahi..Wao wanajulikana..Lakini kuna kina KILAINI na wengineo ambao wana msimamo wa mafisadi kukamatwa!

Jmushi.
Hizo taarifa ulizo nazo ni za lini?
Jaribu kufanya utafiti tena maana hivi vyombo vikubwa vinavyounganisha jamii za kidini(TEC,BAKWATA,CCT n.k) serikali ina vipandikizi vyake humo.Hawawezi kuikosoa serikali.Hawa ndio waliompokea Lowasa Arusha,wakasema nyota yake bado inang'ara katika siasa.
Umeshawaona ukumbi wa habari maelezo wakisema chochote?Wanaogopa kweli kwa kuwa nao bado wako ktk mfumo wa chama kimoja.Ni sawa na wale maakofu wa Kenya waliohongwa na Kibaki washawishi watu wampigie kura
 
Haki ya kuwapo kwa wagombea binafsi ipo wazi kabisa na tusubiri Mahakama itoe hukumu yake.Ni haki ya kimsingi ya kidemokrasia kwa raia wa Tanzania.Na Mwenyezi Mungu yuko upande wa wale wenye haki.Hawa wakubwa wa dini ambao J.Mushi anawaomba waingilie suala hili ni wapambe wa ccm.Anapo appeal kwao ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.Experience inaonesha kuwa siku zote wapo na ccm.
 
Jmushi.
Hizo taarifa ulizo nazo ni za lini?
Jaribu kufanya utafiti tena maana hivi vyombo vikubwa vinavyounganisha jamii za kidini(TEC,BAKWATA,CCT n.k) serikali ina vipandikizi vyake humo.Hawawezi kuikosoa serikali.Hawa ndio waliompokea Lowasa Arusha,wakasema nyota yake bado inang'ara katika siasa.
Umeshawaona ukumbi wa habari maelezo wakisema chochote?Wanaogopa kweli kwa kuwa nao bado wako ktk mfumo wa chama kimoja.Ni sawa na wale maakofu wa Kenya waliohongwa na Kibaki washawishi watu wampigie kura

Taarifa nilzokuwa nazo ni kuwa viongozi hao wa dini wamegundua kuwa wananchi wote wana mahitaji sawa na tofauti ni DINI tu..Either mkristo ama msilamu!
Kwani ni wote wanaokwenda kulalamika kuhusu UMEME,BEI YA VYAKULA NK..sasa wananchi itabidi waandamane kudai haki..Inategemea na shinikizo la wazalendo...Hata hivyo viongozi hao wanajua kuwa hakuna mwingine yeyote wa kuiponya nchi hii zaidi ya MUNGU MWENYEWE...Hakuna litakalowezekana bila kuwa na maslahi ya wanyonge ambao according to the History...Ni sisi wenyewe WENYE kujua kuwa other than cokming back to GOD...Its a demising of the Nation NAD THE PEOPLE OF GOD! tutalikomboa Taifa kwa msaada wa MUNGU!
 
Taarifa nilzokuwa nazo ni kuwa viongozi hao wa dini wamegundua kuwa wananchi wote wana mahitaji sawa na tofauti ni DINI tu..Either mkristo ama msilamu!
Kwani ni wote wanaokwenda kulalamika kuhusu UMEME,BEI YA VYAKULA NK..sasa wananchi itabidi waandamane kudai haki..Inategemea na shinikizo la wazalendo...Hata hivyo viongozi hao wanajua kuwa hakuna mwingine yeyote wa kuiponya nchi hii zaidi ya MUNGU MWENYEWE...Hakuna litakalowezekana bila kuwa na maslahi ya wanyonge ambao according to the History...Ni sisi wenyewe WENYE kujua kuwa other than cokming back to GOD...Its a demising of the Nation NAD THE PEOPLE OF GOD! tutalikomboa Taifa kwa msaada wa MUNGU!

Mungu Mwenyewe hawezi kushuka kuiponya nchi.Ni msemo tata
Atawatumia watu(mimi,wewe na wengine) kutimiza hilo kusudi.Kila mtu kama siafu au sisimizi au mchwa abebe jukumu lake,ndipo nchi hii itapona na malalamiko ya umeme,kupanda kwa bei za vyakula vitapungua.
 
Ni wazi kuwa Viongozi wa dini wanaelekea kuitikia mwito wetu wana JF...
Wananchi ni muhimu mukaitikia wito bila kujali dini zetu...NI WAKATI MUAFAKA WA KUMRUDIA MUNGU...

Kanisa Katoliki kuliombea taifa
na Amana Nyembo

KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limezindua maombi ya siku 24 kwa ajili ya kuliombea taifa liondokane na ufisadi, mmomonyoko wa maadili na ubinafsi unaowatawala baadhi ya viongozi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Ukumbi wa Halmashauri ya Walei jijini Dar es Salaam, Balozi Nicholas Kuhanga alisema maombi hayo yaliyozinduliwa jana, yatakuwa yakifanyika katika Viwanja wa Jangwani.

Alisema maombi hayo yamekuja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutoa wito kwa mashirika ya dini kuliombea taifa, ili liondokane na maadili mabaya.

“Tunaliombea taifa kwa sababu kuna mmomonyoko wa maadili, kama mambo ya ufisadi yanayotea nchini kama EPA na Richmond…nchi inakwenda sehemu isiyotakiwa. Viongozi wanafanya fedha za serikali ni zao, lakini pia kuna ushirikina ambao unasemekana kuingia bungeni, kwani wabunge wanatishika na unga uliomwagwa, hii yote ni mmomonyoko wa maadili,” alisema Kuhanga.

Alisema madhehebu mengine yanaruhusiwa kuhudhuria maombi hayo ambayo yatashirikisha wahubiri mbalimbali duniani.



h.sep3.gif
 
Mungu Mwenyewe hawezi kushuka kuiponya nchi.Ni msemo tata
Atawatumia watu(mimi,wewe na wengine) kutimiza hilo kusudi.Kila mtu kama siafu au sisimizi au mchwa abebe jukumu lake,ndipo nchi hii itapona na malalamiko ya umeme,kupanda kwa bei za vyakula vitapungua.

Mungu huwatumia watumishi wake...Tuna uwezo wa kuwajua manabii wa kweli na wale feki wenye maslahi binafsi.
 
When I was a boy I was told that anybody could become President; I'm beginning to believe it !?
 
When I was a boy I was told that anybody could become President; I'm beginning to believe it !?

Mi nakwambia hawa viongozi wa dini wana nafasi yao kama na wao wana msimamo wa mafisadi kukamatwa...Jambo ambalo ccm hawataki..Then hata waumini wao watagawanyika...Wakati wanaendelea na maombi yao hapo Dar...Ni muhimu pia watueleze hayo maombi yao yamesaidia vipi na Mungu anatupa mwelekeo gani.
Maana wao wanajua kuwa upande wa MUNGU NI UPANDE WA MNYONGE!
Kuwakumbatia mafisadi ni kuhatarisha imani ya wana imani hao!
Imani ambayo hata Jesus Christ himself alisema kuwa ni rahisi kwa ngamia.....
Msikubali kutekwa na mafisadi!
 
Viongozi wa dini wakiongozwa na KILAINI.."MUNGU AKUBARIKI EWE MTUMISHI WAKE".....WALIWAEKA WAZI KUWA HAKI SI KURUDISHWA KWA PESA...BALI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WATUHUMIWA WOTE WA UFISADI...

Na Dunstan Bahai

``...Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni, na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri. Tumekuwa yatima waliofiwa na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.

Tunakunywa maji yetu kwa fedha, kuni zetu twauziwa.

Watufuatao wako juu ya shingo zetu, tumechoka tusipate raha yoyote Baba zetu walitenda dhambi hata hawako, na sisi tumeyachukuwa maovu yao. Watumwa wanatutawala, hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.

``Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu, kwa sababu ya upanga wa nyikani. Ngozi zetu ni nyeusi kama tanuu, kwa sababu ya hali ya njaa ituteketezayo Wakuu hutungikwa kwa mikono yao, nyuso za wazee hazipewi heshima.

``... Wazee wameacha kwenda langoni, na vijana kwenda ngomani. Furaha ya mioyo yetu imekoma, michezo yetu imegeuka maombolezo.

``Mbona watusahau siku zote, na kutuacha muda huu mwingi. We Bwana, utugeuze kwako nasi tutageuka, zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. Isipokuwa wewe umetukataa kabisa, nawe una hasira nyingi sana juu yetu,`` hayo ni baadhi maneno ya Bibilia yanayopatikana kwenye kitabu cha Maombolezo sura ya 5:1-22.

Nimelazimika kunukuu sehemu hiyo ya Biblia kama kitabu kitakatifu, kuonyesha maonyo yaliyotolewa wakati wa zamani na dhuluma iliyopo sasa duniani, hasa katika nchi maskini na zile zinazoendelea, dhuluma zinazofanywa na baadhi ya watawala wake.

Katika kipindi cha takribani miaka miwili na miezi minne hivi, Watanzania na Walimwengu kwa ujumla, wameshuhudia viongozi wa juu wa serikali ya awamu ya nne wanavyoachia nyadhifa zao.

Hatua hiyo ya viongozi kuachia nyadhifa zao haimaanishi wamehusika na tuhuma zinazoenezwa juu yao, bali ni ishara ya heshima na uwajibikaji.

Hatuwezi kuwahukumu viongozi hao kuwa `walivaa ngozi ya kondoo`, huku wakijijua ni `mbwa mwitu` bali walionyesha mfano mzuri wa kuwajibika ingawa wapo wengi wa aina hiyo wanaotakiwa kufuata nyayo zao.

Kuwajibika si dhambi, wala kuwajibika si aibu bali kama kiongozi, anazidi kujijengea heshima.

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, anatanabaisha kwamba baada ya Tanzania kupata Uhuru, uongozi wa wakati huo ulikuwa ukitegemea Rais zaidi.

Hata hivyo, alikiri kuwa viongozi wa wakati huo walikuwa na maadili makubwa ikilinganishwa na wa sasa.

Alisema mtu mbadhirifu au aliyepatikana na rushwa, alikuwa hana nafasi wala sifa ya kuendelea kuwa kiongozi, kwani Rais, wakati huo hayati Mwalimu Julius Nyerere, hakusita kumchukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kumfukuza kazi moja kwa moja.

``Wakati huo ilikuwa amri moja tu kwa kiongozi asiye na maadili. Zamani kiongozi akiitwa Ikulu anatetemeka, anajua akirudi hana kazi, ni kiama kwake, lakini sasa hivi mambo tofauti.`` alisema.

Alisema kipindi cha awamu ya kwanza, kulikuwa na matukio mengi ya viongozi kujiuzulu, kufukuzwa na kustaafishwa kazi.

Miongoni mwa tukio la kujiuzulu kwa kuwajibika ni la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kutokana na makosa yaliyotokea katika wizara yake.

Katika serikali ya sasa viongozi wengine walioachia ngazi zao kwa uwajibikaji mapema mwaka huu ni aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na hivi karibuni aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge.

Hata hivyo, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Daud Balali, alifukuzwa kazi ingawa ni baada ya kumuandikia Rais kuwa ameamua kujiuzulu.

Uwajibikaji ni sehemu ya uadilifu, nidhamu na kujijengea heshima ndani ya familia ya anayewajibika, lakini zaidi nje ya familia yake na nje ya mipaka ya nchi, kwani kiongozi anaonyesha kujutia kilichotokea akiwa kiongozi katika eneo lake, lakini kujiuzulu kwa shinikizo la umma, hilo halimletei heshima kiongozi.

Kwa mujibu wa Profesa Baregu, kumekuwa na matukio mengi ya ubadhirifu, hali ambayo imewaudhi wananchi hadi kufikia umma huo kuchukia kudanganywa huku mali zao wakishuhudia zikiporwa.

Profesa Baregu alisema shinikizo la nguvu ya umma limechangia kuibuka kwa mambo mengi maovu.

Pia alivipongeza vyama vya upinzani hasa ushirika wa vyama vinne vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi.

Alisema vyama hivyo kwa kushirikiana na umma wa Watanzania, waliweza kufanikiwa kuufikisha ujumbe, kilio chao cha kuporwa mali zao, na matokeo yalijidhihirisha na kwa upande mwingine serikali imeonyesha nia ya kushughulikia malalamiko hayo.

Hatua iliyofikiwa na serikali ya kuanika uozo uliojitokeza, ni hatua muhimu sana na ya kuungwa mkono na wananchi wengi, hicho ndicho kilichokuwa kikisubiriwa na umma wa Watanzania.

Aidha, hatua hiyo itairejesha heshima na imani ya Watanzania kwa uongozi wa Taifa na mihimili yote ya nchi.
Naye Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katholiki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methedius Kilaini, ameonyesha kukerwa na watu wanaohusika na ufisadi.

``Mimi simjui fisadi, lakini ninachukia sana hali hiyo. lakini nimeridhika jinsi suala hili lilivyoibuliwa, kwani haya mambo yalikuwepo tangu enzi za mababu, lakini, nani awe wa kwanza kumfunga paka kengele,`` alisema.

Aliwashauri Wabunge, kutokana na ujasiri wao kuliibua suala hili na kulizungumzia kwa kina, waendeleze jitihada hizo hadi mafisadi watakapojulikana na kufikishwa mahakamani, kwani huko wananchi watakapowajua na kupata haki yao.

Askofu Kilaini alikuwa akimaanisha, huwezi kumnyooshea mtu kidole kuwa ni fisadi, kwani wengi wanaamini viongozi wote waliojiuzulu ni mafisadi, la hasha, hao walifanya hivyo kama sehemu ya uwajibikaji, kwani tuhuma hizo zimeibuka wakati wao wakiwa ni viongozi wa maeneo yanayotuhumiwa.

Kwa maana hiyo, uchunguzi unaofanywa na serikali katika maeneo hayo wananchi wanaamini utawaibua mafisadi, pengine ni wale waliojiuzulu kwa heshima au wengine.

Inawezekana kabisa, Rais Kikwete ana dhamira ya kweli ya kuwaondolea umaskini na kero zote zinazowakabili wananchi, lakini wapo wanaokwenda kinyume na dhamira hiyo.

Hata hivyo kuna dalili yawezekana Rais Kikwete ameonyesha kukerwa na ufisadi pamoja na rushwa, ndiyo maana alishindwa kulitolea maamuzi suala hilo na badala yake ameviachia vyombo vya dola kulishughulikia, na Watanzania wanasubiri kwa hamu sana matokeo ya uchunguzi huo.

Kumekuwa na maoni mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi na viongozi wa dini, juu ya nini kifanyike kwa wale wote watakaobainika kuhusika na kupora mali za Watanzania.

Pia yapo maoni yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kuchunguza tuhuma za Richmond.

Baadhi ya maoni ya wananchi na viongozi wa dini ni serikali kuwachukulia hatua haraka wale wote wanaodhani ni mafisadi ikiwa ni pamoja na kufilisi mali zao.

Maoni hayo ni ya haraka sana, tunaamini hakuna mtu anayemfahamu fisadi, cha msingi ni wananchi kuwa na subira, kusubiri uchunguzi unaoendelea wa vyombo vya dola.

Cha msingi ni vyombo hivyo kufanyakazi yake kwa umakini na ukweli na uwazi ili Watanzania waendelee kujenga heshima kwa serikali yao ya awamu ya nne na hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ili suala hili lisiendelee kuwa mjadala, tena mjadala wa kutoaminiani, dhamana ya ukweli wa mambo yenyewe iko mikononi mwa vyombo vilivyoteuliwa na serikali katika kuchunguza masuala hayo.

Vyombo hivyo visipofanyakazi yake kwa makini na ukweli, viongozi waliojiuzulu nyadhifa zao hawatakwepa hasira za wananchi, na maisha yao yatakuwa juu ya mikono ya Watanzania.

Watanzania kama kawaida yao ni wapole, hivyo upole wao usichukuliwe kama ni mazuzu.

Tanzania ni yetu, hakuna mgeni atakayetutengenezea amani na utulivu, kwani suala hili likichukuliwa kwa jazba, urithi wa amani yetu utabakia kama historia, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
__________________
 
Wakati ishara ya kupitisha bajeti ni ishara mbaya sana kwa haki ya Mtanzania..Wapinzani wali abstain...Hawajasema kwanini walifanya hivyo...Na hata wale wa CCM walioipigia kura hawajasema nikwanini walifanya hivyo.
Wananchi wengi walilaani kauli za Viongozi walioonyeshwa na MUNGU kuwa KIKWETE NI CHAGUO LA MUNGU.
Ni wazi kuwa ni kweli kwani kama si yeye tusingeweza kujua haya yote ya CCM.
Tunajua SERIKALI ILIPINGA KWA NGUVU ZAKE ZOTE KUHUSU MGOMBEA BINAFSI!
TUNAWAOMBA MUINGIE KWENYE MAOMBI ILI MUTUELEZE NI WAPI MUNGU ATATUPELEKA WAKATI HUU ILI HAKI YAKE ITENDEKE!
KAMA MUNAONA MGOMBEA BINAFSI ANAFAA MUSEME..NA KWA KUSHIRIKIANA NA WAZALENDO WENGINE...FUATILIENI HAYA KWA KARIBU NA MUTUELEZE YUPI NI YUPI.
AHSANTENI
Jmushi.

Ile COALITION YA WAPINZANI, WANASHERIA, VIONGOZI WA DINI NA ASASI MBALI MBALI wakishirikiana na wale ccm wasio wana mtandao.
Yote tulisahwahi kuyasema.

Wakati huu CHEDEMA wakipigana kwa issue za kikabila zilizokuwa zikichochewa na CHENGE NA MKAPA...Basi yametimia yale niliyokuwa nikiyaona kitambo kuwa...

KAMA HOJA YA MGOMBEA BINAFSI ISIPOPITISHWA...Basi COALITION HIYO ITUAMBIE NI KIVIPI ITALISAIDIA TAIFA.

Either itakisadia chama flani cha kisiasa ama kama coalition hiyo itamnadi mgombea binafsi...Tunaomba waweke wazi ili tuwaachie wanaojADILI YA ccm na CHDEMA waendelee kufanya hivyo!
 
Kauli ya Makamba juu ya EPA yamchefua Mtikila

2008-07-01 11:28:02
Na Raymond Kaminyoge

Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amewataka wapinzani kumpuuza Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuph Makamba kwa kauli yake ya kutaka wapinzani wasiendelee kujadili ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kwani hajui atendalo.

Badala yake, amewataka kuendelea kuwazungumzia mafisadi hadi hapo nchi itakapobadilika na kuwa viongozi wanaofuata maadili mema.

Mchungaji Mtikila aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, kufuatia kauli ya Bw. Makamba, aliyoitoa mkoani Tanga kwamba wapinzani wanaozungumzia suala la EPA na Richmond kila kukicha hawana hoja.

``Mpuuzeni Makamba jamani hajui analofanya, hivi anataka tusizungumzie ufisadi wa EPA na Richmond, ina maana yeye hana uchungu na ufisadi uliotokea kwa sababu yuko CCM, `` alisema.

Alisema wapinzani wataendelea kuzungumzia ufisadi huo hadi hapo wanaotuhumiwa kuhusika watakapofikishwa mahakamani.

``Vinginevyo wapinzani wataendelea kuishinikiza serikali ichukue hatua za haraka dhidi ya mafisadi kwani kuwepo kwao huru kunaweza kuendeleza ufisadi kwa kutumia mbinu mbalimbali,`` alisema.

Mchungaji Mtikila alisema kauli ya Bw. Makamba inaonyesha namna alivyokosa uzalendo kwa nchi yake ingawa yeye ni kiongozi wa chama kinachotawala nchi.

Alisema bila wapinzani `kulipua mabomu` mafisadi hao Richmond wasingefichuliwa na ndiyo maana wanaendelea kupiga kelele ili wengine wa EPA wafichuliwe na kuchukuliwa hatua.

``Tunaomba Makamba aendelee kuimarisha chama chake na masuala ya EPA na Richmond awaachie wenzie wenye uzalendo na nchi yao waendelee kujadili ili hatimaye waweze kufichuliwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola,`` alisema.

Bw. Makamba alikaririwa na vyombo vya habari akisema wapinzani wameishiwa nyimbo kwani hivi sasa wana wimbo mmoja tu wanaoimba wa EPA na Richmond.
  • SOURCE: Nipashe
 
Aren't we a secular state? Kwanini tuwatupie mzigo wa kisiasa vionggozi wa dini? why are we trying to avoid our civic duty? Sisi wenyewe tunatakiwa kuikomalia hii kwa kila tunaloweza.
I might agree kuwa Kikwete kwa namna moja au nyingine amesaidia kufichua mafisadi. Pamoja na kuwa sio yeye aliyewataja, inawezekana kuwa na yeye ana mkono wake, lakini lazima tumshukuru kuruhusu media kufunua uozo uliopo na kuruhusu kuwepo kwa honest discussion kuhusu uozo uliopo.
Katiba yetu ni ya kidikitea inampa rais madaraka ya kukataza hata watu kuongea au hata kuwakamata watu kama kina Slaa na wengine waliowaumbua wezi. Lakini JK hajafanya hivyo. Angekuwa Ben nina hakika mtu kama Slaa asingeachwa hivi hivi. Kwa hiyo hapo unaweza kusema ni haki JK akipewa some credit.....
 
Naizungumzia ile COALITION YA KUFUNGUA KESI YA EPA KAMA SERIKALI IKILETA KUJUWA!
COALITION HIYO NI MORE SECULAR KULIKO HATA SERIKALI YETU.
Kinachosubiriwa sasa ni hao viongozi wa ccm wanaotakiwa kujiunga ama kutangaza majina yao hadharani tegemea na mambo yatakavyokwenda huko bungeni.
 
Hii imetoka gazeti la majira la leo 19/08/08

Kilaini: Siko tayari kusaidia chama chochote kujisafisha

Na Said Mwishehe

ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, amesema msimamo wa Kanisa lake ni kutojihusisha na siasa na kwamba wanaheshimu wanasiasa wote.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni na Majira, Askofu Kilaini alisema kazi kubwa ya Kanisa hilo ni kuendeleza shughuli za dini na halipo kwa ajili ya kushughulikia mambo ya wanasiasa kutoka vyama mbalimbali.

"Tunaomba ifahamike wazi, kwamba Kanisa letu lilishatoa msimamo wake kuhusina na mambo ya siasa, tunaomba tueleweke kuwa Kanisa Katoliki halipo kwa ajili ya kusaidia wanasiasa wala kuwasafishia mambo yao, kwa aina yoyote ile tutabaki kuhudumia mambo ya kiroho tu," alisema Askofu Kilaini.

Alisema wao watakuwa wakishirikiana na viongozi wa siasa katika shughuli zote ambazo zinaonekana kulenga kuleta maendeleo ya Watanzania wote bila kujali itikadi zao za kidini, lakini kwa mambo ya siasa, hawawezi kujihusisha nao.

Askofu Kilaini alilazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na taarifa za siri kutoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutaka kulitumia Kanisa hilo kujisafisha baada ya kuchafuliwa na kifo cha Makamu Mwenyekiti wake, Bw. Chacha Wangwe.

kutokana na jina la chama hicho pamoja na viongozi wake wa ngazi za juu kuchafuka baada ya kutokea kifo cha Mbunge wa marehemu Chacha Wangwe aliyefariki kwa ajali ya gari Julai 28 mwaka huu.


Katika kikao hicho cha viongozi wa CHADEMA moja ya mambo waliyokuwa wameazimia katika kikao chao ni kuweka mikakati ya kutumia viongozi wa kanisa hilo akiwamo Askofu Kilaini, katika maeneo mbalimbali nchini, kukisafisha chama hicho kwa waumini wa dini hiyo.

Askafu Kilaini alisema hajapata taarifa zozote kutoka CHADEMA kuhusiana na jambo hilo, lakini kama mpango huo upo, msimamo wao utabaki palepale kuwa Kanisa Katoliki lisihusishwe na mambo ya siasa na badala yake liachwe liendelee na shughuli za kidini.

"Hatuna taarifa zozote kutoka CHADEMA kuhusiana na suala lolote lile likiwamo hilo ambalo mnatueleza, lakini hata wakija kwetu, wasitarajie kuwa tutafanya kazi wanayoitaka na si CHADEMA tu, bali hata chama kingine cha siasa ila tutaendelea kuwaheshimu kama viongozi wa siasa," alisema Askofu Kilaini.

Kwa kuonesha kuwa Kanisa Katoliki liko mbali na mambo ya siasa, alisema kwa upande wao, hakuna Padri wala Mtawa ambaye anaweza kuwa na kadi ya chama cha siasa na kama yupo anaomba apelekewe taarifa.

"Padri au Mtawa wa Kanisa Katoliki hawaruhusiwi kuwa na kadi ya chama chochote cha siasa na Askofu ndio kabisa usiseme. Kama ukisikia kuna kiongozi kati yao niliokutajia, atakuwa na kadi ya chama cha siasa naomba nifahamishe," alisisitiza Askofu Kilaini.

Alisema hiyo yote ni katika kuhakikisha viongozi wa dini wanabaki katika shughuli za kidini pamoja na kwamba watawahimiza wanaumini wao kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Aliongeza kuwa viongozi wa dini kama waumini wengine ni haki yao kufanya ibada katika Kanisa lolote lile ambalo imani yao imeelekea na hawezi kuwa na kipingamizi katika hilo.

Agosti 7 mwaka huu, viongozi wanne wa CHADEMA walifanya mkutano nyumbani kwa Mwenyekiti Bw. Freeman Mbowe, Dar es Salaam, ili kupanga mikakati ya kukisafisha chama, ambapo walikubaliana kuzunguka nchi nzima.

Katika makubaliano hayo waliafikiana kumwomba Askofu Kilaini apewe jukumu la kuzungumza na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kuhusu suala hilo na pia liandaliwe kongamano la vyuo vikuu nchini kuwaelewesha hali hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Hawa makuadi wa ufisadi na waandishi uchwara wanatupeleka wapi, wamemuua Wangwe ili kuivuruga Chadema sasa wanaendelea kuchochea utambi wanataka nini? I dont understand this non sense where comes from. Who is this mwinshehe Mwandishi uchwara na kuwadi wa ufisadi asiyejali maslahi ya nchi yake
 
Back
Top Bottom