Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Kikwete anasema kuwa maadili ya viongozi ITAKUWA KAMA IFUATAVYO;

HAWATANYANG'NYWA MALI ZAO NA WALA WASIDANGANYE KWA KUWEKA MAJINA YA WATOTO WAO, BALI WATATAKIWA TU KUKABIDHI KATIKA BODI YA WADHANI KWA KIPINDI WATAKACHOKUWA VIONGOZI WA WANACHI.

MIMI NINASEMA BAADA YA HAPO KUNATAKIWA KUFANYIKE UCHUNGUZI ILI KUJUA HZIO MALI WALIZIPATAJE NA KAMA WALIZIPTA KWA KUTUWEKA KWENYE MIKTABA MIBOVU ITABIDI WANYANG'ANYWE HIZO MALI NA HAKIKA HATUTAKUBALI KUONA MTU KAMA MALEGESI, MRAMBA , YONA AND THE LIKE ETI WAKIACHWA WAENDELEE KUTUMBUA HUKU WATU WAIFA KUTOKANA NA MIKATABA MIBOVU, IT IS POSSIBLE FOR FEW YEARS TO KEEP SILENT LAKINI TUTAIBUKA NA KUWAKAMATA NA KUWAFILISI MUDA WETU WA KUTAWALA UKIFIKA NCHI HII SI YA HAO TU WALIOKO MADARAKANI KWA SASA! WANANCHI TUTAWAAMBIA NA TUTAPEWA(WENYE UZALENDO) RIDHAA YA KUIONGOZA MUDA SI MREFU!.

NI AJABU NA ETI MTU ANSEMA HAMTANYANG'ANYWA MALI ZENU ETC! PIA ETI CCM WANA MRADI NA MRADI WENYE HUKO PEMBA NA BARA NI WA KUONGEZA IDADAI YA WANACHAMA WA CCM!! NILIDHANI NI MRADI WA KUINUA HALI NZURI YA WANACHI KWA KUWAPATIA HUDUMA ILI BAADAYE WARIDHIKE NA KUJIUNGA NA CCM,

THINK BEFORE YOU SAYA YOU HAVE BEEN TRUSTED TO BE OUR LEADER.
 
hawajipendi? si walilala kitanda kimoja na ufisadi na kujifunika mablanket ya unafiki! Leo wakurupuke na kusema "kitanda kinachawa"?

M'Kijiji nakumbuka uliwahi kuandika Waraka kwa viongozi wa Dini kuhusiana na Ufisadi, Hivyo hivyo na mimi labda ni kwa njia nyingine ningependa Viongozi wetu hao wa Dini waende kistaarabu tu na kumkumbushia Maafa aliyo leta katika taifa letu na Njia za kuchukua ili kujutia dhambi zake na kuliokoa taifa na Rushwa na kadhia zingine.
Pili utakumbuka wakati wa Uongozi wa Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Kardinali Pengo/TEC waliwahi kutoa waraka kuhusu Himaya ya Warumi ilivyo anguka na kudhalilika kutokana na kutokuwa na utawala bora, hivyo issue ya kusema hawajipendi naona haito kuwepo.Tena Alhaji akiwa Bado Raisi sembuse sasa hivi BWM yupo nje ya Madaraka
Kuhusu kulala na Mafisadi inawezekana na au sivyo, lakini tukichukulia walilala kitanda kimoja na Mafisadi basi ni jukumu lao kumwambia tulicho fanya kimejulikana Sasa tuzime huo moto kwa Kurudisha tulicho chukua Mombasa Style kwa wale walioiiba wakati wa Machafuko kufuatia uchaguzi wa 27/12/07 kwa kuogoba Albadiri.
 
Ningependa Si sote tuliopo hapa Jamvini/Kijiweni kuwaomba Viongozi wetu wa Dini Kuanzia Sheikh Mkuu Kassim Bin Simba , Muhashamu Kardinali Pengo na Msaidizi Wake Method Kilaini, Dr Alex Mtetemela na Bishop Mokiwa, wamfuate Mkapa kiutu uzima kumuomba hizo Mali alizo Iba au kuchukua kwa Njia zisizo faa, Awakabidhi ili wazirudishe Serekali

Hilo litakuwa gumu. Kumbuka fadhila ambazo Mkapa kawafanyia akiwa Madarakani. Kumbuka hawa mafisadi sadaka zao ni ndefu na michango yao ni minene. Na kumbuka katika Dini, kuna kusamehe na kumuachia Mungu.

Nachelea pia kusema kuwa wananchi na au muda ndio watakaofanikisha. Mume wa Bhuto Asif Ali Zardari maarufu kama Mr. 10% mtuhumiwa wa rushwa na mauaji katika serikiali ya Bhuto miaka ya 90 ndio anayeaminiwa kama atawaletea Pakistani unafuu hivi leo!

Tunahitaji Kiongozi kama mwanawasa, ambaye hatomuonea aibu wala huruma Chiluba!
 
UFISADI: Viongozi wa dini wasiishie kukemea tu

Chesi Mpilipili Aprili 2, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

MCHUNGAJI wetu na Mwenyekiti wa chama cha DP, Christopher Mtikila, ametangaza kufanya kile anachokisema kuwa ni maandalizi ya kuwaburuza mahakamani mafisadi wote waliohusika katika kuchota shilingi bilioni 133 kutoka akaunti ya EPA isivyo kihalali.

Katika mkutano wake na waandishi wa Habari, hivi karibuni, Mchungaji Mtikila ametanabaisha kuwa amechelewa kufungua kesi hiyo kwa sababu yeye na wanasheria wake walikuwa wanasoma sheria kwa makini na kuchambua vifungu vya katiba ili kuhakikisha kuwa watakapofungua kesi yao Mkurugenzi wa mashitaka DPP hataweza kuingilia na kuitupa.

Hakufafanua kwa nini amekimbilia kujihami dhidi ya Mkurugenzi wa Mashitaka hata kabla ya kufungua kesi yenyewe. Labda uzoefu wake katika kufungua kesi za kikatiba una siri yake katika hili.

Inawezekana kuwa maamuzi ya Mchungaji Mtikila ya kufungua kesi hii yanatokana na utaratibu aliojiwekea mwenyewe wa kuwaweka roho juu watawala wa nchi kwa kufungua kesi za kikatiba kila pale inapotokea nafasi ya kufanya hivyo.

Na kwa hakika, kama katiba viraka ya nchi inayotumika sasa ni kigezo, basi Mchungaji Mtikila bado ana nafasi nyingi tu za kuendelea kuwakosesha amani watawala kwa kipindi kirefu tu kijacho.

Anaweza pia akawa ameamua kufungua kesi hiyo baada ya kusoma makala ya mwandishi wa gazeti hili, Johnson Mbwambo aliyoiandika kwenye safu yake ya 'tafakuri jadidi' katika gazeti hili toleo namba 19 la Machi 5.

Katika makala hiyo, Mbwambo amefafanua juu ya umuhimu wa Watanzania katika umoja wao, kwa vikundi vya kijamii ama mtu mmoja mmoja kutumia njia ya mahakama kudai haki zetu badala ya hii iliyozoeleka zaidi ya kutumia vyombo vya habari kuanika maovu ya watawala wetu.

Johnson Mbwambo amekwenda mbali zaidi na kusema kwa kuwa watu wanamuona Mchungaji Mtikila ni kama kichaa kutokana na kasi yake ya kufungua kesi hii na ile dhidi ya adha hii ama kero ile, basi, ifike mahali Watanzania wote tuwe vichaa kama yeye na tuanze kufungua mashitaka dhidi ya yanayotukerehesha.

Ni wazo zuri mno. Laiti tungeweza kujihakikishia bila shaka yoyote kwamba linaweza likatekelezwa na Watanzania hawa ambao ni wanung'unikaji wazuri sana dhidi ya matendo wanayofanyiwa na watawala wao lakini linapokuja suala la kuyafanyia kazi, ghafla, miguu yao huota matende!

Kwa hakika, haishangazi basi kuwa katika watu karibuni milioni arobaini wa nchi hii na kelele zote wanazopiga kupinga ufisadi, ni raia mmoja tu ambaye amepata ushujaa wa angalau kuonyesha tu nia ya kuwafikisha mahakamani wale wanaochezea hela zetu kama vile ni za kwao!

Nchi hii imesheheni asasi za kiraia na vyama vya wanasheria, wanafunzi, waandishi wa habari, walimu, madakitari, wafanyakazi na kadhalika ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimewahi kutoa matamko makali kupinga ufisadi unaendelea nchini iwe Richmond, EPA, IPTL ama Kiwira.

Na kumbuka kwamba unapotaja kundi kama la waandishi wa habari mathalani unazungumzia vyama vidogo vidogo lukuki kama chama cha waandishi wa habari za michezo au chama cha waandishi wa habari wanawake na kadhalika, kama ilivyo kwa utitiri wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini angalia, pamoja na matamshi hayo mengine yakiwa makali makali kabisa, hakuna hata kimoja kati ya vyama ama asasi hizo ambacho kimechukua hatua madhubuti ya kushughulikia ufisadi husika kama aliyochukua Mchungaji Mtikila.

Tuchukulie kwa mfano 'mzaha' unoaendelea sasa kuhusu fedha za EPA ambapo wakubwa wanatuambia kuwa sio vyema kutaja majina ya wanaorejesha fedha hizo kwa vile kufanya hivyo ni kuharibu uchunguzi.

Hiki ni kichekesho cha karne na kinachotia hasira kwa sababu iwapo serikali itaamua kutumia nguvu zake watu hawa wanaweza kukamatwa, wakatajwa majina na bado wakasema hayo yanayosemekana kuwa wakikamatwa wataharibu uchunguzi!

Hivi, tuulizane hapa, uchunguzi unaweza ukaharibika vipi zaidi kati ya njia mbili hizi; kuwataja, kuwakamata, kuwatia ndani na kuwapa kibano wahusika wataje zilipo pesa zetu ama kuwaacha wakitanua barabarani huru huku wakiwa na uwezo wa kuingilia na kuvuruga uchunguzi huo?

Na kadri wakubwa wanavyojitahidi kutoa maelezo ndivyo wanavyozidi kujikanganya kama pale kwenye kikao walichoitisha na waandishi wa habari wakati mmoja wa wajumbe wa tume alipotuambia kuwa hawawezi kuwataja wanaorudisha pesa kwa vile kufanya hivyo kutaharibu uchunguzi.

Lakini hapo hapo mjumbe huyo akaishia kutoa mfano kuwa mtu akiiba gari na akamuuzia mtu mwingine na huyu mwingine akamuuzia mwingine yule wa mwisho atakayekutwa na gari hilo ndiye atakayematwa ili kusaidia kuwakamata wengine. Neno kubwa hapa ni 'atakayekamatwa'!

Ni ajabu basi kwamba hawa wanaorudisha hela zetu ambao ni kama ndio wa mwisho tuliowakamata na 'gari' letu (pesa) hawakamatwi na kupewa kibano ili wataje wenzao na badala yake wanaachwa waendelee kutanua na kutukejeli!

Tulitegemea asasi za kiraia na vyama lukuki vya wanasheria vichimbue na kuchambua vitabu vya sheria kutafuta ni kifungu gani ambacho vinaweza vikakitumia kuwalazimisha wahusika kuwataja waliochukua fedha zetu na kisha bado wanaendelea kulelewa badala ya kuwa saa hizi wanajisaidia kwenye debe.

Lipo suala la aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daud Balali ambaye anatajwa kama mtu muhimu katika suala zima la EPA. Tumeambiwa kuwa mtu huyu anatibiwa kwenye hospitali ambayo hakuna ajuaye ilipo.

Kama ilivyo kawaida ya Watanzania, kadri siku zinavyokwenda habari kuhusu mtu huyu aliye kiungo muhimu katika sakata la EPA zinazidi kusahaulika.

Mtu ambaye jina lake lilikuwa ukurasa wa mbele wa kila chombo chetu cha habari kila kukicha 'siku mbili' tu zilizopita sasa hapati nafasi hata kwenye kurasa za matangazo madogo madogo ya biashara!

Tunataka vyama vyetu vya wasomi na wanasheria wachimbue na kuchambua vitabu vya sheria kutafuta kifungu ambacho kinaweza kutumika kumrejesha nchini mhusika huyu muhimu kwenye ufisadi wa EPA ambaye ni dhahiri sasa kuwa kuna watu wanataka atokomee huko huko aliko na asirudi tena nchini.

Juzi hapa tumesherehekea siku kuu ya Pasaka. Tumesikia kauli na matamshi makali makali kutoka kwa viongozi wa dini zikiitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya ufisadi na mafisadi.

Wamekemea ufisadi wa EPA kama walivyokemea ufisadi uliokuwa kwenye chati wakati wa Pasaka ya mwaka jana na kama watakavyokemea ufisadi utakaokuwa kwenye chati wakati wa Idd El Fitr na Krisimasi ijayo. Wanakemea vizuri sana.

Tatizo ni kuwa wanaishia hapo hapo pa kukemea. Husikii hata siku moja viongozi wetu wa dini wakiwataka Watanzania kuchukua hatua madhubuti dhidi ya ufisadi kwa kuamua kugeuka vichaa na kwenda mahakamani ili kutafuta haki yao huko.

Tulidhani kuwa baada ya kuona makemeo yao hayafui dafu dhidi ya ufisadi wa wanasiasa unaotingisha nchi, viongozi wetu wa dini wangebadilisha mbinu za vita na sasa kuwashauri waumini wao kutafuta haki kwa kufanya kile anachofanya Mchungaji Mtikila.

Tatizo kubwa la Watanzania kama inavyosemwa kila mara ni nidhamu ya woga na ubinafsi uliokithiri. Unapotaja, kwa mfano, neno kugoma ama kuandamana ama kwenda mahakamani, kila mtu kwanza anafikiria kazi yake, familia yake na jinsi maandamano ama mgomo huo utakavyomuathiri yeye binafsi.

Tumekuwa wagumu mno kuangalia miaka mia mbele na kufahamu kuwa maandamano ama kesi tunayofungua leo faida zake ni kwa ajili ya vijikuu na vitukuu wetu, hata kama sisi wenyewe tutaingia kwenye matatizo kutokana na migomo ama kesi hizo wakati huu.

Ugonjwa huu wa kutoangalia ya mbele upo hata kwa wakwapuaji wetu wanaoididimiza nchi. Wanapokwapua mabilioni ya fedha zetu hawaangalii madhara yake kwa jamii miaka mia moja ijayo.

Wanachoangalia ni kuwa wao na vizazi vyao vinavyofuata wataishi kwa raha mustarehe, basi, angalau katika miaka 50 ya utu uzima wao. Ya miaka 100 ijayo watayajua wa miaka mia moja ijayo wenyewe!

Ndio maana tumeishia kuwaachia akina Mtikila peke yao kufungua kesi za kutafuta haki zetu wenyewe huku wasomi wetu na wanasheria wetu wakiishia kupenda kuonekana kwenye vipindi vya mahojiano vya televisheni tu wakitema cheche, lakini linapokuja suala la kwenda mahakamani miguu yao huota matendo!

Johnson Mbwambo amesema, ifike mahali Watanzania wote tuwe vichaa wa kufungua kesi iwapo kwa kufanya hivyo tutapata haki zetu za msingi. Mchungaji Mtikila ameishafungua njia, tujiulize, mimi je? Wewe je?


Chesimpilipili.blogspot.com
 
Mara nyingi sana tunapokutana nao katika nyumba za ibada au sehemu za matembezi, huonekana ni watu tofauti kabisa na wengine. Tembea yao, ongea yao na hata muonekano wao ni tofauti kabisa na wanasiasa ama watu wa kada nyingine.

Suala kubwa hapa nalopenda kujadili katika forum hii ya kipekee ni suala zima la UFISADI miongoni mwa viongozi wa madhehebu ya dini, hasa dini ambazo asili yake si hapa kwetu Afrika, namaanisha dini za kigeni Ukristo na Uislamu kwa pamoja.

Mara nyingi sana tumekuwa tukisoma na kushuhudia misaada mbalimbali inayotolewa na watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika taasisi hizi ambazo moja ya jukumu lake kubwa kabisa ni kutangaza neno la Mungu.

Kwangu mimi nimejaribu kufuatilia misaada hii ya wafadhiri na kugundua kuwa baada ya udhadhili kupokelewa waumini wanaambulia kidogo sana na wanaofaidika ni viongozi na jamaa zao.

Nimeshuhudia kabisa dhehebu moja huko kanda ya ziwa ambako taasisi moja ya kimarekani ilitoa nafasi za masomo kwa waumini lakini kilichotokea, nafasi karibu zote zilijazwa na watoto wa kiongozi wa dhehebu hilo bila kuzingatia maombi mbalimbali ambayo yalitumwa na vijana wengi tu.

Tumeshuhudia pia pesa nyingi zianzotolewa na 'wanaotupenda' kwa ajili ya kujengea makanisa na misikiti, shule na vyuo vinavyoongozwa na taasisi za dini, pesa hizi mara nyingi huishia matumboni mwa viongozi hawa.

Wakati tunapopiga kelele za mapambano ya kukomesha ufisadi miongoni mwa viongozi wa serikali ni vizuri tutambue kuwa mafisadi hawa wanabarikiwa na viongozi wa dini zao na hivyo kwa kutokanywa makanisanai na misikitini hali inaendelea kama jana.

najua kuna wenye uelewa mkubwa sana kuhusu mambo haya na watachangia vizuri na mimi kama mdau wa forum hii 'ya maana na yenye hoja za mashiko' niemona niongelee na wengine watambue mtizamo huu


MKANYE MJINGA AKUCHUKIE
 
Waraka mzito wa maaskofu kwa JK

na Kulwa Karedia
Tanzania Daima~Sauti ya Watu


MAASKOFU wa makanisa kadhaa kupitia kile wanachokiita Ushirika wa Maaskofu Tanzania, wameandika waraka maalumu wenye ujumbe mkali na mzito kwa serikali, wakitaka kuchukuliwa kwa hatua kubwa ili kulinusuru taifa dhidi ya misukosuko linayokabiliana nayo.

Waraka huo wa maaskofu wanaofanya kazi chini ya uenyekiti wa mtu anayetajwa kuwa ni Askofu John Mwela, unaelezwa kuwa ni matokeo ya kikao cha pili cha kamati ya maaskofu hao kilichokutana Dodoma kwa siku nne kuanzia Mei 13 hadi 16 mwaka huu.

Kwa mujibu wa waraka huo wa maaskofu ambao Tanzania Daima imeusoma, pia kuchapwa katika baadhi ya magazeti jana, maaskofu hao wanaeleza kuguswa na matukio kadhaa wanayoyaelezea kuwa yaliyochangia kuliyumbisha taifa.

Miongoni mwa mambo yanayotajwa katika waraka huo wa kwanza wa aina yake, ni pamoja na ufisadi, mpasuko wa kisiasa Zanzibar, uwakilishi wa viti maalumu bungeni, migomo vyuoni na katika mashirika na tatizo la usafiri kwa wanafunzi wa mijini.

Wakirejea matukio ya siku za hivi karibuni, maaskofu hao wanasema kuwa yana sura nne, zikihusisha ubadhirifu wa fedha za Watanzania kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu (EPA), Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond, na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wengine kadhaa.

Mawaziri waliojiuzulu wanaotajwa katika waraka huo ni pamoja na Dk. Ibrahim Msabaha, Nazir Karamagi na Andrew Chenge.

Maaskofu hao wanabainisha kuwa mwelekeo wa mambo hapa nchini unaonyesha kuwa serikali inahitaji msaada mkubwa katika kuweka hali sawa.

Wanasema kuwa matukio hayo ya ufisadi yamesababisha Watanzania wagawanyike katika makundi manne, ambayo hata hivyo hawataji chanzo chao cha utafiti kilichowawezesha kufikia katika mpangilio wao huo.

Kwa mtazamo wao, kundi linaloongoza ni lile linalojumuisha watu wanaofikia asilimia 60, wanaochukizwa na kuumizwa na viongozi na watu wachache waliojilimbikizia mali.

Kundi la pili wanalolitaja ni la watu wanaofikia asilimia 25, ambao wao ni wale wanaolia na kutoa hukumu yao kwa kulalamika wakiiona serikali kuwa iliyoshindwa kuwajibika.

Aidha, walilitaja kundi la tatu (asilimia 14.75) kuwa ni lile la watu wasioona shida yoyote, kwa maana wao wana kila kitu, huku kundi la nne na la mwisho likijumuisha watu wachache (asilimia 0.25) wanaomlilia Mungu aliponye taifa la Tanzania.

Kutokana na mambo hayo, maaskofu hao wanatamka kujifunga kuisaidia serikali na hususan Rais Kikwete, katika maeneo kadhaa, kwa kutoa ushauri katika masuala ya ufisadi, mabadiliko yanayohitajika katika kuandaa uchumi wenye nguvu, pamoja na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Aidha, ushauri wao huo unahusisha pia jinsi ya kufikia muafaka kati ya CCM na CUF huko Zanzibar, na kugusia njia ya kushughulikia migomo katika vyuo vikuu, mashirika ya umma na makampuni binafsi, pamoja na serikalini kwenyewe.

Kwa upande mwingine, wakati serikali imekuwa ikifikiria kuongeza idadi ya viti vya wabunge maalumu hadi kufikia asilimia 50 mwaka 2010, kwa lengo la kukuza ushiriki wa wanawake katika hatua za maamuzi, maaskofu hao wamelitaka Bunge kufuta mara moja sera ya uwakilishi bungeni kupitia utaratibu wa viti maalumu.

Kamati hiyo imesema iwapo Bunge halitachukua hatua hiyo, basi kanisa nalo litaomba viti saba vya uwakilishi, wakivigawa vitatu kwenda kwa makanisa ya kiprotestanti yaliyo chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), viwili Kanisa Katoliki chini ya TEC, na makanisa ya kipentekoste yapate kimoja na kimoja kingine kiende kwa makanisa yanayojitegemea.

Tamko la kamati hiyo, lililosainiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu Mwela na Katibu wake, Godfred Lema, linasema hatua yao hiyo imelenga kuboresha uwiano wa uwakilishi bungeni, tofauti na hali ilivyo sasa.

Katika hayo yote, maaskofu hao wamesema kuwa wapo tayari kusimama kidete kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kutafuta suluhisho dhidi viongozi mafisadi ndani ya serikali.

Maaskofu hao wanasema wamejitoa kupambana na ufisadi kwa sababu hali hiyo imefika katika hatua mbaya, ambayo rais anapaswa kusaidiwa haraka, ili kupunguza hatari ya mgawanyiko ndani ya jamii.

“Tumekubaliana kusimama na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na serikali zao kutafuta suluhisho la matukio haya, kwa sababu tunajua nchi ni ya Watanzania wa dini na rangi zote, hivyo sote tunawajibika mbele za Mungu kuitunza,” inasomeka sehemu ya waraka huo.

Wanasema kuwa wakati umefika kwa makanisa kujiingiza katika vita dhidi ya ufisadi, kwa sababu baadhi ya watu wanaoendeleza vitendo hivyo wamo ndani ya makanisa hayo.

“Wengi wa watu hawa wanaoitwa mafisadi wako katika makanisa yetu, hivyo tutatumia nguvu kutoka kwa Mungu ili kuwaumbua na kuwaongoza, kuwa mabadiliko haya yanahitajika katika kuandaa uchumi wenye nguvu,” inasomeka taarifa hiyo.

Sambamba na vita dhidi ya ufisadi, waraka huo unasema maaskofu hao wamekubaliana pia kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Katika hili wanatoa ahadi ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kushauriana kwa pamoja, mambo yanayohusu umoja wa kitaifa na masilahi yake.

“Tutawaelekeza na kuwafundisha wale wanaowaongoza, umuhimu wa kutuunga mkono katika azima yetu. Tunaamini kwa kufanya hivi na kwa maelekezo haya sahihi ya Mungu, tutakuwa na umoja wa kitaifa, taifa lisilo na magonjwa kama vile malaria, ukimwi na vifo katika umri mdogo pamoja na kuondokana na umaskini na maisha duni,” inasomeka sehemu ya waraka huo.

Katika sehemu moja ya waraka huo, maaskofu hao wanaandika kuwa wanasubiri kuundwa kwa kamati ya kudumu ya maaskofu, baada ya kufanyika kwa vikao vya makanisa yaliyo chini ya CCT, TEC na PCT.
 
Kamati hiyo imesema iwapo Bunge halitachukua hatua hiyo, basi kanisa nalo litaomba viti saba vya uwakilishi, wakivigawa vitatu kwenda kwa makanisa ya kiprotestanti yaliyo chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), viwili Kanisa Katoliki chini ya TEC, na makanisa ya kipentekoste yapate kimoja na kimoja kingine kiende kwa makanisa yanayojitegemea.

Tamko la kamati hiyo, lililosainiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu Mwela na Katibu wake, Godfred Lema, linasema hatua yao hiyo imelenga kuboresha uwiano wa uwakilishi bungeni, tofauti na hali ilivyo sasa.


Sasa kumekucha na makucha yake,hao watu wa dini nao wameona maombezi tu hayatoshi hadi wametoa tamko.Isiishie hapo,waseme kweli daima hata kwenye misiba ya viongozi na pia Waalikwapo wakati rais anaapishwa kwa kuwa hivo vitabu vitakatifu siku hizi haviogopwi watu wanashika bila uoga,bali matendo yanakuwa tofauti.
 
Wakati huo huo BAKWATA wako kimyaaaaaaaaaa, lakini we should expect much from them kwani BAKWATA inaongozwa na mtu ambaye hajui kiingereza...na elimu yake ni ndogo sana

big up to maaaskofu kuhusu hili
 
Kamati hiyo imesema iwapo Bunge halitachukua hatua hiyo, [B]basi kanisa nalo litaomba viti saba vya uwakilishi, wakivigawa vitatu kwenda kwa makanisa ya kiprotestanti yaliyo chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), viwili Kanisa Katoliki chini ya TEC, na makanisa ya kipentekoste yapate kimoja na kimoja kingine kiende kwa makanisa yanayojitegemea[/B].

Tamko la kamati hiyo, lililosainiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu Mwela na Katibu wake, Godfred Lema, linasema hatua yao hiyo imelenga kuboresha uwiano wa uwakilishi bungeni, tofauti na hali ilivyo sasa.


Sasa kumekucha na makucha yake,hao watu wa dini nao wameona maombezi tu hayatoshi hadi wametoa tamko.Isiishie hapo,waseme kweli daima hata kwenye misiba ya viongozi na pia Waalikwapo wakati rais anaapishwa kwa kuwa hivo vitabu vitakatifu siku hizi haviogopwi watu wanashika bila uoga,bali matendo yanakuwa tofauti.

haya na dini nyingine zikiomba viti bungenii, budha, hindus, wapagani vya kwao, sunni, ismailia, bohora, ithnasheri, ansari sunna, na hatimaye viti kutoka kila kabila! kaazi kweli kweli
 
Wakati huo huo BAKWATA wako kimyaaaaaaaaaa, lakini we should expect much from them kwani BAKWATA inaongozwa na mtu ambaye hajui kiingereza...na elimu yake ni ndogo sana

big up to maaaskofu kuhusu hili
Taratibu babu eh!

Kha.......!
 
Swala la viti maalum ni kupoteza maana ya Bunge. Bunge linapaswa kuwakilisha watanzania propotionally kutoka kila sehemu ya nchi na kwa ridhaa ya wananchi.

Hii ndio demokrasia, tunapoanza kurundika viti maalum mpaka kufikia asilimia 50 tunataka kubadilisha bunge liwe kama shirika tu la serikali.

Hii inapaswa kupingwa kwa nguvu zote.
 
Wakati huo huo BAKWATA wako kimyaaaaaaaaaa, lakini we should expect much from them kwani BAKWATA inaongozwa na mtu ambaye hajui kiingereza...na elimu yake ni ndogo sana

big up to maaaskofu kuhusu hili


Kuna uwezekano mwenzetu wewe maana ya elimu imekupiga chenga.
 
Wanasema kuwa wakati umefika kwa makanisa kujiingiza katika vita dhidi ya ufisadi, kwa sababu baadhi ya watu wanaoendeleza vitendo hivyo wamo ndani ya makanisa hayo.
Mungu awatangulie na hili lifanikiwe!

“Wengi wa watu hawa wanaoitwa mafisadi wako katika makanisa yetu, hivyo tutatumia nguvu kutoka kwa Mungu ili kuwaumbua na kuwaongoza, kuwa mabadiliko haya yanahitajika katika kuandaa uchumi wenye nguvu,” inasomeka taarifa hiyo.
Wow...! Ujumbe mzuri sana kwa fisadizzzz wazoefu! Zitawabana sana mwaka huu.

Sambamba na vita dhidi ya ufisadi, waraka huo unasema maaskofu hao wamekubaliana pia kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
He he he he he.... Mtarejea na "CHAGUO JIPYA LA MUNGU"?
 
haya na dini nyingine zikiomba viti bungenii, budha, hindus, wapagani vya kwao, sunni, ismailia, bohora, ithnasheri, ansari sunna, na hatimaye viti kutoka kila kabila! kaazi kweli kweli

Tena dini zingine hizo za asili ya Asia na Bara Hindi wakiomba pia ni vema kwa kuwa itachochea hata katiba kuandikwa upya ili kuweza kuwaweka au kutowaweka wawakilishi wa dini.Viongozi wadini walikuwa wamenyuti kweli hadi inatia huruma
 
sheikh mkuu wa BAKWATA hajui kiingereza kwani uwongo?

na kiarabu hajui vile vile

LAKINI la muhimu zaidi he is not even a graduate. No wonder serikali inamkeep close
 
sheikh mkuu wa BAKWATA hajui kiingereza kwani uwongo?

na kiarabu hajui vile vile

LAKINI la muhimu zaidi he is not even a graduate. No wonder serikali inamkeep close

Ukipata nafasi na iwapo bado hujafanya hivyo basi pitia kitabu cha Malcolm X, itakuwezesha kutambua kuwa elimu sio mpaka ukae kwenye dawati halafu upewe cheti.
 
Naona kuna halufu mbaya uchaguzi ujao, kama tutafika na watawala tulionao. Hata maaskofu wanaamua kuingia kwenye siasa? Haya yote asiraumiwe mtu ni dhambi iliyofanyika katika kutafuta madaraka 2005
 
sheikh mkuu wa BAKWATA hajui kiingereza kwani uwongo?

na kiarabu hajui vile vile

LAKINI la muhimu zaidi he is not even a graduate. No wonder serikali inamkeep close

Sasa kwani kiingereza ndo kitu gani!. nitajie nabii mmoja aliyekuwa anajua Kiingereza. masiha mwenyewe aliishi wakati wa dola kuu la kirumi lakini alikuwa haongei kirumi,

kuhusu kiarabu, nani kakuambia kuwa nguzo kuu mojawapo ya kuelimika katika uislamu ni kujua kiarabu!!?.

GT inaelekea unahusudu sana vyeti, let me tell you this vyeti ni makaratasi, yakiungua haimaanishi huna elimu, na hivyo hiyo unaweza usiwe na haya makaratasi lakini ukawa na elimu,shule ina maana pana sana ndugu yangu kuliko unavyofikiri. vyeti ni formalities tu, ka utaratibu tulikojiwekea wanadamu, kama unakataa hebu niambie katika maisha yako ya darasani umepata kusoma mambo mangapi na kwa hivi sasa unakumbuka mangapi?, hapo ulipo ukipewa mtihani uleule uliofanya form six utaweza kufaulu kwa kiwango kile kile?,kama sivyo kwa nini basi kuelimika kwako au kwa mtu mwingine kusipimwe kwa factor nyinginezo zaidi ya static education ambayo kilele chake ni vyeti?.
 
sheikh mkuu wa BAKWATA hajui kiingereza kwani uwongo?

na kiarabu hajui vile vile

LAKINI la muhimu zaidi he is not even a graduate. No wonder serikali inamkeep close

Ukipata nafasi na iwapo bado hujafanya hivyo basi pitia kitabu cha Malcolm X, itakuwezesha kutambua kuwa elimu sio mpaka ukae kwenye dawati halafu upewe cheti.

Wabunge wetu wote ni magraduate?Na wote wanajua Kiingereza?Na Kiarabu ni lugha rasmi bungeni?

Na je kujua Kiingereza ni kuelimika?
 
Ukipata nafasi na iwapo bado hujafanya hivyo basi pitia kitabu cha Malcolm X, itakuwezesha kutambua kuwa elimu sio mpaka ukae kwenye dawati halafu upewe cheti.

Yaani unataka kumlinganisha Malcolm na Shee mkuu?

give me a break
 
Back
Top Bottom