GE2025 Viongozi Serikalini Wanataka Wananchi Mkinukishe Kwanza ili Wawaunge Mkono

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Ukifanya upembuzi yakinifu utagundua viongozi wengi serikalini sio kwamba hawaoni yanayotendeka.

Shida inakuja ni kuwa wenye uwezo wa kusema hapana ni wananchi wenyewe. Hivyo viongozi wengi wanasubiri kuona nguvu ya umma ikifanya maamuzi.

Fuatilia kwa umakini tu huko maofisini utagundua wengi hawaridhishwi na utendaji kazi wa serikali ya sasa. Wanangoja tu wananchi wakinukishe hili nao watoe sapoti.

Hawa viongozi wana mengi ya kusema ila hawawezi, kuhofia maisha yao. Pia wengine wanasema watanzania ni ngumu kuwapigania kwa sababu hawajali, na wanasahau shida ndani ya siku chache. Mfano polepole katekwa, baada ya wiki chache wananchi watasahau na itakuwa kama hakuna kilichotokea. Hii inafanya viongozi wengi wafyate mkia, kwa sababu wananchi wanasahau haraka.

Ni hatari sana kwa mtu mmoja kutoka mbele ya umma na kuikemea serikali, ila ni rahisi sana na salama kama umma wote wa wananchi watakuwa na kauli moja.

Ogopa sana wananchi wakichoka na wakajitoa kupambana na ukiritimba
 
Kila mtu anamsubiria mwenzie 😂😂😂😂
Ngoja tuone mwisho wake.
 
Usijidanganywe, ukajidanganya, na kutudanganya. Wengi wao ni machawa na woga kama walivyo wengi humu jf. Tanzania itakombolewa na ajali au Mungu mwenyewe. Sisemi haya kwa kukata tamaa. Ni kwa sababu, fursa nyingi zimetokea, lakini hakuna aliyekinukisha zaidi ya kila mmoja kujitoa akitaka wengine wafanye hiyo kazi ili yeye akafaidi bila kutoa jasho.
 
Back
Top Bottom