Viongozi 20, Balozi 83 kushuhudia kuapishwa Rais Mteule Dkt. Magufuli

Vipi na mabeberu na wao watakuwepo?
Beberu kashatoa karipio kali kupitia EU, the Commonwealth, USA, Sweden, etc. etc. kwamba uchaguzi ulikuwa mchafu.

Wenzetu wana misimamo, hawawezi kukandya uchaguzi halafu wakaja kupiga piga makofi na kuuza sura kwenye uapisho.

Watakuja waliopongeza uchaguzi, the Ugandas and Zimbabwes of the world....
 
Zimbabwe, Uganda na Comoro!! Halafu dhehebu jipya la CCM wanasema huyu ni Rais wa Afrika na anakubalika duniani kote.
 
Kenya, Rwanda, South Sudan maana ni EAC? Pia nilitegemea marais wote EAC wahudhurie was wenyewe!!!!@@.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi amesema maandalizi ya hafla ya kuapishwa kwa Rais Mteule John Pombe Magufuli yamekamilika na yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali takribani 20 wakiwemo marais watatu wa Uganda, Comoro na Zimbabwe.

Wengine ni; Makamu wa Rais wa Nchi Kadhaa na Mawaziri Wakuu wa Nchi kadhaa wakiwemo pia viongozi wengine mashuhuri kama Rais Mstaafu wa Nigeria, Olussegun Obasanjo, Nabii T. B Joshua na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar.

Aidha, amesema mabalozi 83 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini watahudhuria.

Chanzo: HabariLeo
Hao Mabalozi ni wakazi wa Dodoma walipewa viwanja bure watakuwa wamehamia siku nyingi, kwa hiyo kama Wagogo wote hawawezi kupitwa na usanii huo wa kihistoria. Wageni mashughuri labda ni kina Museveni aliyepewa Tausi wetu anataka kikubwa zaidi na Mnangagwa kutubu kwa Wazimbabwe kumtukana Rais wetu mpendwa. Makamu wa Marais na Mawaziri Wakuu wa nchi zisizojulikana waje tu wasipitwe na tukio hilo adhimu. Toka Uhuru tumezoea Marais wetu wamekuwa wanaapishwa Ikulu!
 
Kagame haji!! Katutenga au?
Ujio wa Nabii T B Joshua katika sherehe za kumuapisha Rais Magufuli jijini Dodoma ni jambo la baraka kubwa kwa taifa la Tanzania.

Kwa hakika baraka hizi siyo za kukosa nami nikiwa na mchungaji Erasto na mzee Mgaya tuko njiani kuelekea Dodoma na kwa sasa tupo hapa Kibaigwa tunapata msosi.

Karibuni uwanja wa Jamhuri mpate baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Alishatoka porini alipoenda kuombea corona akisema atorudi Hadi dawa ipatikane?
 
Swahiba wetu hayupo kwenye list mbona au baada ya kula hela ya student ya mihogo urafiki ukafa Kati ya Mwalimu na mwanafunzi wake
 
Back
Top Bottom