Viongozi 20, Balozi 83 kushuhudia kuapishwa Rais Mteule Dkt. Magufuli

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema maandalizi ya hafla ya kuapishwa kwa Rais Mteule John Pombe Magufuli yamekamilika na yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali takribani 20 wakiwemo marais watatu wa Uganda, Comoro na Zimbabwe.

Wengine ni; Makamu wa Rais wa Nchi Kadhaa na Mawaziri Wakuu wa Nchi kadhaa wakiwemo pia viongozi wengine mashuhuri kama Rais Mstaafu wa Nigeria, Olussegun Obasanjo, Nabii T. B Joshua na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar.

Aidha, amesema mabalozi 83 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini watahudhuria.

Chanzo: HabariLeo
 
Rafiki wa kweli wa siku zote wa rais wa Tanzania kupitia chama cha CCM awasili akitokea Burundi kuja kushuhudia uapishwaji wake
AIRPORT: WAZIRI MKUU WA BURUNDI ALIVYOTUA NCHINI KUHUDHURIA UAPISHO WA MAGUFULI.




VIONGOZI mbalimbali wa kimataifa wameeanza kuwasili nchini leo Novemba 04, kwa ajili ya kuhudhuria kwenye hafla ya uapisho wa Rais mteule wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, itakayofanyika kesho Novemba 05, jijini Dodoma.
 
Utakuwa mwaliko wa kuwalazimisha tu na pengine wameahidiwa tenda mbalimbali pindi mara baada ya kuapishwa.
 
Hakuna Rais anayeheshimu demokrasia anayeweza kuja kushuhudia kuapishwa kwa kiongozi aliyepatikana kwa njia najisi. Na hao hao Marais wa ajabu ajabu ndio wataonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Marais wa Uganda, Comorro, na Zimbabwe"

Watu wanaojiheshimu hawawezi kujivunjia heshima zao waje kwenye hilo igizo.
Hao ni marais waonevu watu wanakuja kushuhudia uonevu mwingine.
 
CCM Mpya watasingizia corona imesababisha wafalme, wana-wa-Mfalme, marais na mawaziri wakuu toka maBara ya Marekani ya Kaskazini na Kusini, Ulaya , Mashariki ya Kati, Asia na Afrika kushindwa kufika wakati viongozi hao wangependa kuja Tanzania kuonesha mshikamano na CCM Mpya.
 
Viongozi wanaojielewa hawawezi kuja kuzifedhehesha nchi zao katika kushangilia dhulma iliyotendeka katika sanduka la kura kwa kisingizio cha kuwa mabalozi wanaoziwalilisha nchi zao hapa Tanzania, hata hivyo Msemaji wa serikali anajua kupika habari kama NEC ilivyopika uchaguzi na kumpakulia mgombea wa Chama cha Mapinduzi ushindi.
 
Back
Top Bottom