Mtanzania,
Sio lazima tuwe tunafahamiana kama unavyofahamiana na rafiki yangu Sikonge(ingawa naye sifahamiani naye) ndio tuheshimiane. Heshima ni jambo la kawaida na busara kwa binadamu mwenzako na heshima hiyo inaongezeka kadri unavyomuona mtu anakuwa na mawazo yenye kuongeza tija, kwahiyo sihitaji kufahamiana sana na wewe ili nikuheshimu, kwani naamini hata kwa kukutana jf tumeshafahamiana kiasi cha kutosha kuheshimniana, na kama hutaki heshima yangu hakuna tatizo kwani siwezi kukulazimisha.
Kiukweli kabisa mkuu wakati mwingine mnapokaa huko majuu huwa mnasahau mambo mengi ya huku nyumbani, sio kila tukio la kifo linahusiana na mkono wa mtu lakini ni ukweli kwamba yapo matukio ya watu kufariki kutokana na mikono ya watu, na kwa mazingira ya kitanzania watu kufa kutokana na mkono wa mtu ama watu fulani limekuwa si ujambo geni, kukana kuwepo vifo vya mkono wa mtu ni kuukana ukweli ulio dhahiri.
Kutokana na aina ya siasa zetu za kiafrika, haya ni mambo ambayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara, hata hivyo ninauhakika kwamba unafahamu hata ulaya haya mambo ya kuzimisha yapo, utakumbuka kilichompata yule kachero wa kirusi ambalo ni tukio la hivi karibuni kabisa.
Mkuu kama mkapa aliendesha kampeni za ccm igunga bila kuwakashfu wapinzani nao hawkumgusa, nini kilimtuma kumshambulia Vincent? alidhani akimshambulia Vincent atakaa kimya? Mkuu uelewe tu kwamba hizi siasa za kushambuliana hazina tija sana kwa wananchi lakini inapofikia kiongozi wa kitaifa mstaafu kama mkapa anaamua kufanya siasa za majitaka, majibu yanayomstahili ni yale yenye ujazo ule ule, kama wanavyosema mjini mkapa alimwaga mboga Vincent Kamwaga ugali, sasa kazi kwetu wananchi kupembua.
Kwakuwa alichofanya Vincent ni kumjibu mkapa bila shaka mtamshauri siku nyengine awe mstaarabu kwani akiigusa chadema tu anakula za uso, hapa ni jino kwa jino!! Kabla hujamshangaa mbunge kuingia kwenye siasa za namna hii,naomba uanze kumshangaa raisi mstaafu kuanzisha siasa za majitaka!!