Mkuu Mwita,
Wala huna haja ya kuniheshimu mimi kwasababu hata hunifahamu. Una uhuru wa kuheshimu au kupuza mawazo yangu utakavyo.
Sitaingia personal, kwasababu haisaidii mjadala huu. Ni kweli Kyela hawakunipa kura za kutosha. Nililikubali hali na kuwatakia heri walioshinda. Nilifikiri hiyo ndio demokrasi ambayo tunaiongelea hapa siku zote? Kumbe kwasababu watanzania walimnyima Dr. Slaa urais mwaka 2010 basi hafai hata kusikiliza mawazo yake? Kumbe kwasababu watanzania walimnyima JK mwaka 1995 basi hakufaa kuchaguliwa 2005? Kumbe wote walioshindwa 2010 hapa basi mawazo yao ni ya kupuuzwa? Well, yapuuze ukitaka maana ni uhuru wako.
Narudia tena Vincent kusema kifo cha Nyerere ni mkono wa mtu ni ujinga mkubwa sana. No wonder taifa zima linashinda kwa babu wa Loliondo badala ya kushughulikia matatizo ya magonjwa yetu hospitalini.
Hakuna sehemu yeyote niliposema mimi najua ugonjwa wa mwalimu, nilikuambia nilikuwepo hapa London wakati mwalimu anafariki na pia kwa kukaa kwangu hapa ninazifahamu sheria za hospitali inapokuja mgonjwa ambaye ugonjwa wake una utata. Hiyo ndio ilikuwa maana yangu.
Ila tu mkuu acha personal attacks, hazikusaidii wewe, hazilisaidii taifa la Tanzania. Mimi sio mpenzi wa rais Mkapa na maandiko yangu mengi huko nyuma yanaonyesha hivyo. Lakini pia sio mpenzi wa hizi gutter politics na ndio maana naona kumtanguliza mbele Mkapa kwenye politics za CCM ni makosa. Siasa za maji taka hata siku moja hazijengi nchi bila kujali zinafanywa na Mkapa au Vincent.
LAKINI ni mpinzani mkubwa wa haya mambo ya kuweka mkono wa mtu hata kwenye vitu ambavyo viko obvious. haya mambo yako mpaka kwenye familia, nako tunakemea hivyo hivyo. Kule kwetu mpaka watu wanauana kwa kusingiziana kurogana wakati ukweli ni magonjwa tu.
Sasa inapofikia mbunge mzima anaingia kwenye politics za namna hii unataka tukae kimya? No, tutaandika mawazo yetu tena kwa uhuru mtupu hata kama watu wengine mtayageuza.
hivi kuishi jirani na mahakama ndiko kujua sheria????????????????
ni wa east africa wangapi walikuwepo london na tena hawakuwa na taarifa za uwepo wa Mwalimu london???
wewe kuwemo london sio kigezo cha kujua kilichomsibu Nyerere
Ni watanzania wangapi wapo INDIA na hawajui/wanajua kinachomsibu Mwakyembe???????