Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

I think Mkapa hakutegemea hii issue ku backfire hivi aliona Igunga walimwacha akawaona wajinga. CHADEMA wanafanya kazi nzuri sana kama Mwanakijiji alivyoshauri si vizuri kuacha kusema mabaya ya hawa watu hata kama wengine wanadai hatuna sera zaidi ya ufisadi/Uuaji ni vizuri kuwaelimisha wananchi kuwa matokeo ya matatizo yetu ni sababu kadha wa kadha.
NI WAKATI WA KUUWASHA MOTO UPYA
 
Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!


Well, Vicent naye katumia haki yake ya msingi kabisa ya kujitetea. Unapojitetea kwa mtu anayetaka kukunyonga unatumia silaha yoyote iliyopo jirani na ambayo unadhani itamfanya adui yako akae pembeni kujipanga upya na uharamia wake. Nyie mnasema MR CLEAN, usafi na uuaji ni wapi na wapi? Vicent katusaidia wengi kujua kitu ambacho isingewezekana kukijua kama Mkapa angetulia kule lushoto anakotumbua 80% ya mabepari aliowauzia nchi.
 
TWO WRONGS CAN NEVER MAKE IT RIGHT. Watanzania tumezoea sana kufumbia macho makosa. Tena mbaya Zaidi hata kwa Capital Offences. Matokeo yake tunazalisha chuki za mioyoni. Alichokisema Vicent ni kitu ambacho kimemkaa moyoni kwa muda mrefu, na hatimaye kaamua kuropoka siri hiyo. Hii hata Makongoro anayo moyoni, ni kutokana na system ndio maana wananyamaza. Lakini hawawezi kuvumilia siku zote, Iko siku tu utaingia kwenye anga zao lazima walipe tu. Cha pili watu wa Mara sio wanafiki, hawawezi kuita nyeusi kuwa ni nyeupe. Ni kweli kabisa baba wa Taifa alikwenda London akiwa anatembea mwenyewe, tena aliaga pale Airport akiwa na kicheko chake cha kawaida na vijiutani vyake. It was so amazing kufika hospital for check up akawa hajitambui mpaka umauti. Si yeye tu, mbona kuna vifo vyenye utata utata kama Kibona (aliyewahi kuwa waziri wa fedha), K. A. Malima, H. Kolimba, Balali na wengineo. Uchunguzi wa vifo vyao ni wa mashaka tupu na matokeo ya uchunguzi yalipokewa kwa shingo upande. Wauaji wanapeta, masikini wanahukumiwa. CCM IS MAFIOSO
 
Nimeshusha pumzi nzito baada ya kufika ukurasa huu wa 17. Dah, kweli haya mashati tunayoyavaa wanaume yanaficha mambo mengi nje na ndani ya vifua vyetu!
RIP Mwalimu. Many loved you but some didn't and wanted you to go...
 
wakati upo london uliwahi kwenda kumuon mwl hosp?

unajua kiini cha maradhi yale yalianzia wapi?

uwepo wako london ni proof tosha kuwa mwl alikufa kifo cha kawaida?

mtikila alisema mwl kapandikiziwa sumu(arsenic) kwenye damu na hivyo kuibua hiyo kansa?

hapo ulipo unamwamini mkapa?

unajua ni kwa nini prof mwakyusa alizuiwa kumgusa mwl?

unawajua madaktari waliokuwa wanamtibu mwl huko london baada ya prof mwakyusa kuzuiliwa?

Mkuu,

Mimi nilienda kumwona Mwalimu na pia wawakilishi mbalimbali wa Watanzania walikuwa wanaenda kumwona kila siku.

Unachoandika hapa ni majungu na inatakiwa uone hata aibu kuingiza majungu kwa ajili tu ya siasa za maji taka.

Hata madaktari waliokuwa wanamtibu mwalimu walisamehe malipo yao kama heshima zao kwa mwalimu na watanzania.

kwa taarifa yako kwa UK ni sheria, mgonjwa yeyote akikutwa na kitu chochote ambacho kinaonekana huenda kuna mkono wa mtu, huita polisi hapo hapo. Hiyo ni sheria na hakuna daktari anayeweza kupuuza.

Kama kulikuwa na mkono wa mtu kwenye ugonjwa wa Nyerere na madaktari wake walijua, HAIWEZEKANI, narudia HAIWEZEKANI wanyamaze kimya.

Hizi story mtawadanganya watu ambao hawajui jinsi sheria za UK zinavyofanya kazi.
 
Vincent Nyerere ni mtoto wa nje wa mdogo wake Nyerere, Familia ya Nyerere hawamtambui kabisa mdogo wake Nyerere alizaa na mwanamke mmoja pale Makoko.
Acha porojo, awe au asiwe mtoto wa Nyerere ukweli unabaki palepale, Ben kamuua Julius Kambarage.
 
Ungesoma thread toka mwanzo ungeelewa kuwa Vincent hajazungumzia Mwakyusa kupewa uwaziri hayo ni maoni ya wana JF.

Mkuu Feedback,

Nimesoma yote toka juu na hata magazeti mengi tu ya leo yameandika. Alitamka kwamba Mkapa alimnyamazisha prof. mwakyusa kwa kumpa uwaziri.

It's a big shame wanamwingiza hata prof. Mwakyusa, a very gentleman, kwenye siasa za maji taka.
 
Mkuu,


kwa taarifa yako kwa UK ni sheria, mgonjwa yeyote akikutwa na kitu chochote ambacho kinaonekana huenda kuna mkono wa mtu, huita polisi hapo hapo. Hiyo ni sheria na hakuna daktari anayeweza kupuuza.

Kama kulikuwa na mkono wa mtu kwenye ugonjwa wa Nyerere na madaktari wake walijua, HAIWEZEKANI, narudia HAIWEZEKANI wanyamaze kimya.

Hizi story mtawadanganya watu ambao hawajui jinsi sheria za UK zinavyofanya kazi.
YAELEKEA NDUGU UMESAHAU NGUVU YA FEDHA na Umakini wa operesheni za Mafia!
Umesahau kuwa mtuhumiwa alipata kukabidhiwa tofali la dhababu huko Geita/Bulyanhulu?
 
Itabidi tukumbushane ili tuwekane sawa.


what i remember,is nilikuwa south africa wakati mwalimu anakufa, na is truth, nilishuhudia pat ya watu kujipongeza mahala kwa kugongeana glas mbaya, nilishangaa sana baadaye ndiyo nikajagutuka ohooooooooo,mmojawapa ni yule jamaa anayesimamia shughuli za uchimbaji wa tanzanite ya wasouthafrika kule arusha


Hapo Unamzungumzia Ami Mpungwe, Fisadi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchi SA kwa sasa anaendeleza Ufisadi wake na kusaidiana na Makaburu kuiba Tanzanite na yeye anaishi Johannesburg na familia yake yote ameihamishia huko.
 
-
-Naungana na Mkuu Mtanzania kuwa vicent amepotoka na alitakiwa kujibu alichokisema Mkapa..


-Kaibua hoja ambayo haiwezi na Hana mamlaka ya kuzungumzia kifo cha JKN!

Kwa hiyo Mkapa yeye alikuwa na hoja na mamlaka wa kuzungumzikia UKOO wa Nyerere? (READ UKOO).
Hivi kwanini WACHINA hawaleti pia MASHINE za KUINUA BONGO za Watanzania, maana masaburi mengine yanatia kinyaa!

Jana nilisema Mkapa is a walking deadman, sasa hivi anacheza muziki wa Kikwete tu, maana akabisha anafahamu he will be brought to Justice.

VN Nyerere amesma mengi kwenye kampeini kama Ufisadi wa EPA, Kununua rada na ndege ya Rais, Kujimilikisha mgodi wa Kiwira, Kuuza mashirika kama NBC, kuanzisha Bank yake ANBEN etc. Lakini mbona mmeshikilia hili la kifo cha JK? Kisu kimefika kwenye mfupa nini?

Mkapa akizidi na siasa zake za maji taka ataumbuliwa jinsi anavyolea watoto wa Basil Mramba. Amesahau alivyokumbushwa Makamba Snr kuhusu chanzo chake cha kufukuzwa Ualimu?! Tangia siku hiyo Makamba Snr aliacha siasa za maji taka dhidi ya Dr. Slaa. Mkapa hapa amefikia mwisho nafikiri sasa hivi BP iko juu na anajuta kuanzisha UGOMVI huu.
 
Malipo yapo hapa hapa duniani, na huu ni mwanzo wa siri nzito zilizofichika na wahusika wataumbuka na kuhukumiwa hapa hapa duniani.
 
Mkuu,

Mimi nilienda kumwona Mwalimu na pia wawakilishi mbalimbali wa Watanzania walikuwa wanaenda kumwona kila siku.

Unachoandika hapa ni majungu na inatakiwa uone hata aibu kuingiza majungu kwa ajili tu ya siasa za maji taka.

Hata madaktari waliokuwa wanamtibu mwalimu walisamehe malipo yao kama heshima zao kwa mwalimu na watanzania.

kwa taarifa yako kwa UK ni sheria, mgonjwa yeyote akikutwa na kitu chochote ambacho kinaonekana huenda kuna mkono wa mtu, huita polisi hapo hapo. Hiyo ni sheria na hakuna daktari anayeweza kupuuza.

Kama kulikuwa na mkono wa mtu kwenye ugonjwa wa Nyerere na madaktari wake walijua, HAIWEZEKANI, narudia HAIWEZEKANI wanyamaze kimya.

Hizi story mtawadanganya watu ambao hawajui jinsi sheria za UK zinavyofanya kazi.

hujanijibu maswali yangu yote...naomba uyajibu


hujui kwa undani kifo cha mwalimu Nyerere...narudia hujui.

aina ya ubishi wako tunaita ''INVINCIBLE IGNORANCE''.....
 
Back
Top Bottom