Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Unajua dhana ya kumwua mgonjwa ni pamoja kumpa ushauri feki. Swali ninalojiuliza kwa nini hawakujaribu kuicontain hii cancer kwa njia kama bone marrow transfussion na chemotherapy miaka miwili baada ya kugundua ni mgonjwa?

mkuu inaitwa bone marrow transplantation hii kitu huwa haina suluhisho la kudumu kwani kansa hu metastas tena na kuvamia ile marrow iliyoplantiwa mkuu.
 
Sasa hapa ninani mwenye uthibitisho kuwa ni kweli mwalimu alikuwa na leukaemia au ilikuwa ni changa tu.
 
Mtanzania,

Sio lazima tuwe tunafahamiana kama unavyofahamiana na rafiki yangu Sikonge(ingawa naye sifahamiani naye) ndio tuheshimiane. Heshima ni jambo la kawaida na busara kwa binadamu mwenzako na heshima hiyo inaongezeka kadri unavyomuona mtu anakuwa na mawazo yenye kuongeza tija, kwahiyo sihitaji kufahamiana sana na wewe ili nikuheshimu, kwani naamini hata kwa kukutana jf tumeshafahamiana kiasi cha kutosha kuheshimniana, na kama hutaki heshima yangu hakuna tatizo kwani siwezi kukulazimisha.

Kiukweli kabisa mkuu wakati mwingine mnapokaa huko majuu huwa mnasahau mambo mengi ya huku nyumbani, sio kila tukio la kifo linahusiana na mkono wa mtu lakini ni ukweli kwamba yapo matukio ya watu kufariki kutokana na mikono ya watu, na kwa mazingira ya kitanzania watu kufa kutokana na mkono wa mtu ama watu fulani limekuwa si ujambo geni, kukana kuwepo vifo vya mkono wa mtu ni kuukana ukweli ulio dhahiri.

Kutokana na aina ya siasa zetu za kiafrika, haya ni mambo ambayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara, hata hivyo ninauhakika kwamba unafahamu hata ulaya haya mambo ya kuzimisha yapo, utakumbuka kilichompata yule kachero wa kirusi ambalo ni tukio la hivi karibuni kabisa.

Mkuu kama mkapa aliendesha kampeni za ccm igunga bila kuwakashfu wapinzani nao hawkumgusa, nini kilimtuma kumshambulia Vincent? alidhani akimshambulia Vincent atakaa kimya? Mkuu uelewe tu kwamba hizi siasa za kushambuliana hazina tija sana kwa wananchi lakini inapofikia kiongozi wa kitaifa mstaafu kama mkapa anaamua kufanya siasa za majitaka, majibu yanayomstahili ni yale yenye ujazo ule ule, kama wanavyosema mjini mkapa alimwaga mboga Vincent Kamwaga ugali, sasa kazi kwetu wananchi kupembua.

Kwakuwa alichofanya Vincent ni kumjibu mkapa bila shaka mtamshauri siku nyengine awe mstaarabu kwani akiigusa chadema tu anakula za uso, hapa ni jino kwa jino!! Kabla hujamshangaa mbunge kuingia kwenye siasa za namna hii,naomba uanze kumshangaa raisi mstaafu kuanzisha siasa za majitaka!!

Nafikiri hilo jamaa umelipa ukweli wake wa kutosha. Kwani wakikaa London na utamaduni wao nao unafutika? Mswahili hakuvumbua msamiati wa Uchawi. Naye ameukuta. " Wachawi wa farao nao wakageuza fimbo zao kuwa nyoka" lakini kwa sababu Mungu yuko juu ya Uchawi, Nyoka aliyetokana na fimbo ya Moses akameza wale Nyoka wengine. Unajua, uchawi ni matunda ya yule joka kuu aitwaye Ibirisi. UPO na unakuwa practised na jamii kubwa hapa duniani. Ikiwa ni pamoja na hao wanaukana hapa duniani. Unakuta mtu anasema majukwaani kwamba uchawi haupo lakini amevaa mkanda wa hirizi. Anajikinga na nini?

Kwenda kumsalimia Mwl. wakati amelazwa hakutudhibitishii kwamba hakuna mkono wa mtu kwenye kifo cha Mwl. Kutokana na experience ya Dr. mwakyembe, sumu ziko za aina nyingi, siyo lazima uinywe, unaweza hata ukainawa kwenye sabuni, au hata ukapigwa mionzi ya Gamma kama yule kachero wa urusi aliyefia uingereza. Leukemia Nyerere aliirithi kwa nani? au amemurithisha nani? SN ameanzisha mjadala ambao unahitaji majibu kutoka kwa wahusika.
 
Sikonge ndugu yangu,
Wengine tumenyamaza na hizi habari kifuani mwetu kwa miaka mingi tu. Nilijua kuna siku itamwagika hadharani. Sikutegemea kwamba itamwagika nikiwa bado hai.

Mkuu, la kuvunda halina ubani. Ulevi wa madaraka mwisho wake ni kuumbuka.
 
na mimi nalia machozi kama wewe mkuu.

Kwahiyo Mkapa ndo aliniulia shujaa wangu siyo?

Yaani jemedari wangu ameuliwa na Mkapa siyo?
Yaani huyuhuyu aliyepigiwa debe na Nyerere wangu awe rais kamgeuka kamuua shujaa wangu siyo?
Huyu huyu ambaye huwa anatuwekea foleni akienda kanisani na kukaa kiti cha mbele!

Kama ni kweli: I hate Mkapa!
Kama si kweli Mungu ambariki.

Mimi jamani mimi napata uchungu sana nikimkumbuka shujaa wangu.
Angekuwa hai hivi sasa kuna baadhi ya upumbavu ungekuwa umekoma....:iamwithstupid:
 
Mh..hii dhambi itawatafuna CCM na Mkapa wao mpaka itameguka tena ndani ya kipindi cha JK....VICENT NYERERE ni mbunge wa MSOMA mjini na ni mwanafamilia wa NYERERE km ameyasema haya basi tutegemee makubwa zaidi kwani sio siri tena kua MKAPA alihusika na kifo cha kipenzi wa waTanzania ili tu auze migodi na kijibinafsisha baadhi ya migodi....hili sijambo dogo ni lazima JK alazimishwe aunde tume ili kuchunguza ili swala kwani sio dogo km akishindwa basi waTanzania lazima tuingie barabarani ili haki itendeke.....Mr Clean hizo ndo faida za kutumiwa na ukatumika kwanini usiwaachie vijana wakapiga kampeni? Bravo V nyerere long live CDM
 
Kwahiyo Mkapa ndo aliniulia shujaa wangu siyo?

Yaani jemedari wangu ameuliwa na Mkapa siyo?
Yaani huyuhuyu aliyepigiwa debe na Nyerere wangu awe rais kamgeuka kamuua shujaa wangu siyo?
Huyu huyu ambaye huwa anatuwekea foleni akienda kanisani na kukaa kiti cha mbele!

Kama ni kweli: I hate Mkapa!
Kama si kweli Mungu ambariki.

Mimi jamani mimi napata uchungu sana nikimkumbuka shujaa wangu.
Angekuwa hai hivi sasa kuna baadhi ya upumbavu ungekuwa umekoma....:iamwithstupid:

Speechless!!!!!!!!!!
 
Mkuu Mwita,
Ungeandika ujumbe wako mara ya kwanza bila personal attacks kama ulivyofanya hapa ungeeleweka vizuri zaidi. Bahati mbaya tumehalalisha siasa za jino kwa jino kiasi kwamba inafika mahali wote tunakuwa losers. Na pia kama unamheshimu mtu basi uwe tayari pia kutofautiana naye kimawazo maana hata ndugu wanakuwa na mawazo tofauti. Huwezi ukaacha kumheshimu mtu kwasababu mara moja ameandika ambacho wewe hukubaliani nacho. Hapo ina maana ulikuwa humheshimu toka mwanzo na labda ulikuwa tu unafurahishwa tu na mawazo yake.

Kama nilivyosema mwanzoni, hizi imani za kwamba kila ugonjwa kuna mkono wa mtu zinatumaliza bure nyumbani. Hii ya wanasiasa nao kuingia kuimba mambo hayo hayo bila kuangalia effects zake ni mbaya sana. Ningetegemea mbunge ajenge hoja zake kwa kuangalia facts zilizopo. Unaposema kumnyamazisha prof. Mwakyusa alipewa uwaziri wakati mtu anajua profesa hajawahi kupewa uwaziri na Mkapa sijui inakuwa na maana gani?

Kuna watu hata tulikosana na familia kwenye mambo ya kwenda kwa babu. Watu wanasema hata viongozi wa juu wameenda na wamethibitisha kwa babu unapona. Maneno ya wanasiasa yanaaminiwa na wananchi wengi, wawe makini wanaposema hasa pale ambapo facts ni tofauti.

Nilifikiri kifo cha Nyerere kingewafundisha Watanzania umuhimu wa ku screen cancer mara kwa mara. Nyerere alikuwa na afya nzuri sana muda wote na matokeo yake ni kama kwenda kufanya check-ups kwake ilikuwa sio muhimu kabisa. Kwa nafasi ya Nyerere laiti ugonjwa wake ungejulikana mapema angeweza kupona. Bahati mbaya ulikuja kujulikana ikiwa too late. Pia ugonjwa wa Nyerere ungekuwa fundisho kwa wanasiasa wetu kuelewa kwamba hospitali zetu zinahitaji kuwa na vifaa vya maana. Hata kama una uwezo wa kutibiwa nje lakini inaweza kuwa too late. Ni muhimu kujenga uwezo wa hospitali zetu kuwezo kuzuia magonjwa mbalimbali yasifike hatua ambayo ni mbaya zaidi. lakini kama ni mkono wa mtu, hapo ni kwenda kwa Sangoma tu kujikinga.

Binafsi sio mumwini wa haya mambo ya mkono wa mtu. wakati tukiwa vijana tuliambiwa Sokoine aliuawa na Kawawa, hatukuamini wakati huo kama ambavyo siamini sasa kusema Nyerere aliuawa na Mkapa. Hata kwenye familia inapotokea migogoro hiyo unawakalisha chini na kuwaambia kila mtu aweke facts zake. Baada ya dakika chache unagundua mtu alikuwa na HIV na alikuwa anatibiwa muda wote, leo amekufa, wanasema karogwa.

Huyo Litvinenko wa Russia ni kwamba kabla hata wananchi wengine kujua, tayari polisi walishajulishwa na walikuwa wanachunguza. Ni sheria kwa UK kama kuna wasiwasi wowote lazima uwajulishe polisi. Nyerere alikuwa anatibiwa kwenye hospitali ya serikali, hapo sheria hazipindishwi kirahisi maana hata daktari mmoja akipindisha wengine wanatoa siri. Ukweli ni huo Nyerere alikufa kwa cancer na kosa kubwa ni kuchelewa kuanza kupata matibabu.

nimekwambia kuwa hujui undani wa kifo cha baba wa taifa.....hao waingereza unaowaamini huwajui licha ya kwamba unaishi hapo....mbinu ya costra nostra inapotumika kufanya kazi hughubikwa na siri nzito na kwa mtu wa kawaida kama wewe huwezi kujua....nakushauri unyamaze uwe msomaji tu....
 
Hii dhambi itawatafuna

mlimuua mpendwa wetu
hakika hamko salama
siiiiriii imefichukaaa x5
utaficha wapi uso wako.

kumbe mh ben na david
 
"....Na wale wote wanaodhani na kuota ndoto kuwa kufa kwa Mwalimu kutalisambaratisha Taifa, Ndoto zao hizo zitageuka kuwa Jinamizi na mipango yao haitafanikiwa"
......Na Ben William Mkapa(Siku ya Mazishi ya Kitaifa ya Mwalimu, Uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam)
 
Mkuu Mwita,
Ungeandika ujumbe wako mara ya kwanza bila personal attacks kama ulivyofanya hapa ungeeleweka vizuri zaidi. Bahati mbaya tumehalalisha siasa za jino kwa jino kiasi kwamba inafika mahali wote tunakuwa losers. Na pia kama unamheshimu mtu basi uwe tayari pia kutofautiana naye kimawazo maana hata ndugu wanakuwa na mawazo tofauti. Huwezi ukaacha kumheshimu mtu kwasababu mara moja ameandika ambacho wewe hukubaliani nacho. Hapo ina maana ulikuwa humheshimu toka mwanzo na labda ulikuwa tu unafurahishwa tu na mawazo yake.

Kama nilivyosema mwanzoni, hizi imani za kwamba kila ugonjwa kuna mkono wa mtu zinatumaliza bure nyumbani. Hii ya wanasiasa nao kuingia kuimba mambo hayo hayo bila kuangalia effects zake ni mbaya sana. Ningetegemea mbunge ajenge hoja zake kwa kuangalia facts zilizopo. Unaposema kumnyamazisha prof. Mwakyusa alipewa uwaziri wakati mtu anajua profesa hajawahi kupewa uwaziri na Mkapa sijui inakuwa na maana gani?

Kuna watu hata tulikosana na familia kwenye mambo ya kwenda kwa babu. Watu wanasema hata viongozi wa juu wameenda na wamethibitisha kwa babu unapona. Maneno ya wanasiasa yanaaminiwa na wananchi wengi, wawe makini wanaposema hasa pale ambapo facts ni tofauti.

Nilifikiri kifo cha Nyerere kingewafundisha Watanzania umuhimu wa ku screen cancer mara kwa mara. Nyerere alikuwa na afya nzuri sana muda wote na matokeo yake ni kama kwenda kufanya check-ups kwake ilikuwa sio muhimu kabisa. Kwa nafasi ya Nyerere laiti ugonjwa wake ungejulikana mapema angeweza kupona. Bahati mbaya ulikuja kujulikana ikiwa too late. Pia ugonjwa wa Nyerere ungekuwa fundisho kwa wanasiasa wetu kuelewa kwamba hospitali zetu zinahitaji kuwa na vifaa vya maana. Hata kama una uwezo wa kutibiwa nje lakini inaweza kuwa too late. Ni muhimu kujenga uwezo wa hospitali zetu kuwezo kuzuia magonjwa mbalimbali yasifike hatua ambayo ni mbaya zaidi. lakini kama ni mkono wa mtu, hapo ni kwenda kwa Sangoma tu kujikinga.

Binafsi sio mumwini wa haya mambo ya mkono wa mtu. wakati tukiwa vijana tuliambiwa Sokoine aliuawa na Kawawa, hatukuamini wakati huo kama ambavyo siamini sasa kusema Nyerere aliuawa na Mkapa. Hata kwenye familia inapotokea migogoro hiyo unawakalisha chini na kuwaambia kila mtu aweke facts zake. Baada ya dakika chache unagundua mtu alikuwa na HIV na alikuwa anatibiwa muda wote, leo amekufa, wanasema karogwa.

Huyo Litvinenko wa Russia ni kwamba kabla hata wananchi wengine kujua, tayari polisi walishajulishwa na walikuwa wanachunguza. Ni sheria kwa UK kama kuna wasiwasi wowote lazima uwajulishe polisi. Nyerere alikuwa anatibiwa kwenye hospitali ya serikali, hapo sheria hazipindishwi kirahisi maana hata daktari mmoja akipindisha wengine wanatoa siri. Ukweli ni huo Nyerere alikufa kwa cancer na kosa kubwa ni kuchelewa kuanza kupata matibabu.

Mtanzania,

Mimi nadhani tuanze kwanza na mbunge wetu wa Kyela, yeye anasema amepewa sumu, jee ni kweli au?
 
nasikia BWM anatarajia kuongea mchana huu juu ya tuhuma .. ameshaongea ?
 
Kuanzia chaguzi kuu hadi hizi ndogo wanachofanya CCM ni kama kumtupia mbwa mfupa anabaki anahangaika nao kuula wakati mwizi anapita getini. hilo ni moja tu mengine yanakuja, matokeo yake kampeni za CDM zinakuwa za kujibu mapigo badala ya sera

mkubwa umeongea
 
nasikia BWM anatarajia kuongea mchana huu juu ya tuhuma .. ameshaongea ?
Useme ni uwoga wa Waandishi wetu wa habari, lakini kama atathubutu kufanya hivyo ilikuwa ndiyo siku nzuri sana ya kumuuliza maswali yote yenye utata juu ya tuhuma zake kwa Taifa hili alipokuwa kwenye Ofisi kuu ya nchi!
 
Maneno ya mwalimu wakati anakwenda kutibiwa alisema anakwenda kufanyiwa uchunguzi tu wa afya yangu kwa maana hiyo hakuwa anaumwa kivile tukashangaa inarudi maiti yake baba huyu Mkapa naroho yake ya kishetani hakutangaza kifo cha mwalimu mapema iliafanye maandalizi alikuwa anajua anachokifanya leo yako wapi Benny.

Hili nimekuwa nikijiuliza siku nyingi bila kupata jibu. Hiyo Leukemia yenye kusababisha severe brain stroke kwa muda mfupi hivyo inaonekana kama planned justification. Binadamu ni muovu sana...
 
nasikia BWM anatarajia kuongea mchana huu juu ya tuhuma .. ameshaongea ?

Kweli VN kagonga Ikulu,huyu Mzee Mkapa hizi siasa haziwezi,atashindana vipi na vijana tena kwa kurusha makombora ya kuchafuana,kweli alibeep na wamempigia.
 
Back
Top Bottom