Video: Tundu Lissu atoa ufafanuzi wa hoja aliyoitoa Babati Aprili 26, 2024 kumjibu Fatma Karume kuhusu 'Ubaguzi na Muungano wetu'

Mimi naona tofauti kidogo. Kilichopo sasa ni kutaka kuitawala Zanzibar na inapokuwa ngumu tunaanza kulialia. Inatafutwa gia ya kuenda kwenye serilkali moja, jambo ambalo WAZANZIBARI wengi hawalikubali.
Hapana.
Wakitaka kuitawala Zanzibar ni kazi rahisi kabisa. Ni kumpata mtu kichaa kama Magufuli katika swala hilo. Hutasikia tena fyokofyoko unazosikia sasa hivi. Kwa taarifa yako, ni kikundi kidogo sana kilichoko Zanzibar ambacho hupiga kelele zaidi ya wingi wao, hasa toka Pemba. Hawa wana maslahi na kwingineko, na hawautaki Muungano toka mwanzo. Kukidhibiti hiki kikundi siyo kazi kubwa. Ni kikundi hiki sasa ndicho kimeiingilia CCM Zanzibar, na ndicho huibua mara kwa mara habari za "kero" ambazo ndizo zimelegeza Muungano sasa hivi.

Hayo niliyo yandika hapo yatafakari kidogo, utaona ukweli ndani yake.
 
Dodoma ninayoizungumzia ni ile aliyoizungumzia Lissu katika Video. Kama hujaisikiliza hiyo video (ipo kwenye uzi huu), tafadhali isikilze kwanza ndio twende pamoja. Katoa mfano wa idadi wapiga kura wa Dodoma na wabunge wake akilinganisha na wale wapga kura wa Zanzibar na wabunge wake. Kazi kwako, ndio urudi tujadiliane.
Sifa za majimbo ya uchaguzi muulize Lissu, kwa maana mimi nikiziorodhesha hutridhika. Ngoja huyo mchungaji Lissu aseme hadharani. Ndio utajua kuwa una mchungaji BAGUZI, na hana tofauti na wale makaburu wa A. kusini ktk miaka ya 1960. Aende Ubelgiji akaishi huko.
Kidogo nashindwa kuelewa wewe na mimi tunapishana wapi katika hili.

Mimi nilielewa, na siku zote najuwa kwamba mbunge anayechaguliwa kwenye jimbo la Zanzibar, anachaguliwa na watu wachache sana, sana; ukilinganisha na mbunge anayechaguliwa katika jimbo la uwakilishi Tanganyika.
Na kwa maana hiyo, mbunge wa Zanzibar huwakilisha watu wachache sana ukilinganisha na Mbunge wa Tanganyika.

Hebu nieleze, hili lipo sawa, au bado ni tofauti na wewe unavyo elewa?

Nakuomba jibu lihusu swali hilo tu pekee kabla ya kwenda mbele zaidi na maelezo mengine.
 
Na ukishayaelewa na kulewa hayo maneno ya Lissu, kinachofuata ni vita vya vyenyewe kwa wenyewe. Huko ndio Lissu anakotupeleka.

Sikia nikwambia, idiolojia za Lissu hazina afya kabisa katika nchi yeyote ile ya Afrika. Jirani yako ndio mtu utayefanya naye biashara kwa ustawi wa Afrika na nchi moja moja. Huwezi kujua Ethiopia waliingiaje kwenye vita za wenyewe kwa wenyewe. Ni kama hizi siasa za Lissu ndio mbolea nzuri sana ya kukupeleka katika nchi ya ahadi ya Lissu.

Baada ya maelezo yake, tuchukulie kesho mmetengana, na yeye ndio Rais, hivi atakwendaje kwa jirani kuomba ujirani mwema?
Unaumia ukiwa mchambawima, mchafukoge, makunduchi, kibandamaiti au wapi?
 
Kidogo nashindwa kuelewa wewe na mimi tunapishana wapi katika hili
Mimi kumwuita Lissu "MBAGUZI" ndio tofauti zetu. Uchaguzi wa Lugha na hisia za mwanasiasa ndio mwelekeo wa ubatizo wa jina lake.
Mimi nilielewa, na siku zote najuwa kwamba mbunge anayechaguliwa kwenye jimbo la Zanzibar, anachaguliwa na watu wachache sana, sana; ukilinganisha na mbunge anayechaguliwa katika jimbo la uwakilishi Tanganyika.
Na kwa maana hiyo, mbunge wa Zanzibar huwakilisha watu wachache sana ukilinganisha na Mbunge wa Tanganyika
Upo sahihi kabisa. Ni ukweli usiopingika. (Usisahau kuwa Zzibar ni nchi iliyokuwa na utaratibu wake na utamaduni wake hata kabla ya kuungana).
Kwa kuongezea tu, hata Tanganyika mbunge wa Mafia anawapiga kura wachache sana ukilinganisha na mbunge wa Kawe au Kinondoni. Hali hii utaipata mahali pengi hata huku Tanganyika.
 
Hapana.
Wakitaka kuitawala Zanzibar ni kazi rahisi kabisa. Ni kumpata mtu kichaa kama Magufuli katika swala hilo. Hutasikia tena fyokofyoko unazosikia sasa hivi. Kwa taarifa yako, ni kikundi kidogo sana kilichoko Zanzibar ambacho hupiga kelele zaidi ya wingi wao, hasa toka Pemba. Hawa wana maslahi na kwingineko, na hawautaki Muungano toka mwanzo. Kukidhibiti hiki kikundi siyo kazi kubwa. Ni kikundi hiki sasa ndicho kimeiingilia CCM Zanzibar, na ndicho huibua mara kwa mara habari za "kero" ambazo ndizo zimelegeza Muungano sasa hivi.

Hayo niliyo yandika hapo yatafakari kidogo, utaona ukweli ndani yake.
Wewe huna ujualo kuhusu hayo mambo halafu unajifanya mjuaji wakati wewe ni mbumbumbu
 
Jibu hoja.kupigana kunasababishwa na mambo mengine sio hoja za lissu.Mbona hatuoni tukipigana na kenya?.Mbona congo tumepakana nao na wanapigana wenyewe je sababu ni hizo alizozisema lissu.Hoja za lissu ziko wazi ili kama kuna changamoto zifanyiwe kazi.usifikiri vizazi vyote vitakavyokuja vitaendelea kurubuniwa na hii tabia yakufichaficha mambo kwa propaganda mfu wakakubali.
Lissu atatuelewa tu. Msikilize alivyowahutubia waandamanaji Morogoro tar 30/4. Katoa hotuba nzuri isiyo na mihemko na hisia za kibaguzi ukilinganisha na ile aliyoitoa babati. Haya ni matokeo ya kumpigia kelele! Tutaendea kumpigia kelele kila anapotereza, lugha za kibaguzi hazina afya kwa Taifa. Ajirekebishe!

Shukurani kwa wote waliosimama kidete na kumrekebisha, kumuonya na kumsahihisha Lissu katika hotuba yake ile ya KIBAGUZI.

Iko hivi: Naweza nikapingana na maamuzi ya kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma. Hapa chini natoa hotuba mbili, moja ya kibaguzi na nyingine ya kihoja:
1) Mzananki mmoja, kutoka Butiama anaamua kuwahamisha nyie wagogo na ardhi yenu yote ichukuliwe na Serikali. Ngombe zenu mtafugia wapi? hakuna! Kwanini huyu Mzanaki kutoka huko Kaskazini Mara asinyanganye ardhi ya wakulya huko kwao nakujenga makao makuu huko.....Imejaa hisia za KIBAGUZI.
2) Rais na serikali ya Tanzania imeamua kuhamishia makao makuu Dodoma. Kitendo hiki kinamadhara makubwa kwa wakazi wa Dodoma, ikiwa pamoja na kuhamiswa toka katika ardhi yao ambayo itachukuliwa na serikali...... Unajenga hoja.
 
Nyie wapemba maandazi kweli,yani mtu kudai taifa lake la.asili Tanganyika ndio kuketa vita vya wenyewe kwa wenyewe? nyie ndo mnajiona mna haki sana ya kuisemea nchi yenu zanzibar ila sisi watanganyika tukisema tunakua wahatarisha amani shwaini kabisa!!
Akimalizana na Zanzibar atahamia katika siasa za Majimbo. Kwa mihemko hii ya Lissu ndio utajua kuwa Singida sio Arusha au Moshi. Kila jimbo litakuwa na sheria zake na Polisi wake. Isome katiba ya CHADEMA na Ilani zao za uchaguzi 2010, 2015, 2020. Utanielewa tu.
 
Ukweli halsi ni kinyume na hivi unavyodhani wewe. Huenda huijui Zanzibar.
Kwenye swala la maslahi ya Zanzibar, Wazanzibari hawatofautiani.
Wanatofautiana sana inapokuja kwenye maslahi ndani ya CCM au nje; ACT Wazalendo.
Matatizo ya Muungano wetu yapo kwenye makundi hayo mawil, huko visiwani. Kati ya wanaolinda "Mapinduzi Tukufu" yasizolewe na wale wasio yatambua mapinduzi hayo.
Kuwemo kwenye muungano ndiyo kete wanayoitumia kundi la Mapinduzi Tukufu, kuwatumia waTanganyika kuhakikisha usalama wao.
 
Mimi kumwuita Lissu "MBAGUZI" ndio tofauti zetu. Uchaguzi wa Lugha na hisia za mwanasiasa ndio mwelekeo wa ubatizo wa jina lake.
LOoo. Kumbe?
Hii itakuwa ni mada nyingine tunayoweza kuitumia kujadili tofauti zetu katika uelewa huo.
Yeye kaueleza anaoona ni ubaguzi wa waZanzibari dhidi ya waTanganyika; wewe ukaona ni mbaguzi; ila wewe unabaki ukiwa siyo mbaguzi!
 
Upo sahihi kabisa. Ni ukweli usiopingika. (Usisahau kuwa Zzibar ni nchi iliyokuwa na utaratibu wake na utamaduni wake hata kabla ya kuungana).
Kwa kuongezea tu, hata Tanganyika mbunge wa Mafia anawapiga kura wachache sana ukilinganisha na mbunge wa Kawe au Kinondoni. Hali hii utaipata mahali pengi hata huku Tanganyika.
Hapana, mfano wa Mafia siyo sahihi hata kidogo katika kuelezea uwakilishi wa wabunge toka Zanzibar. Mkuu, kama ni maswala ya utamaduni, hata huko Tanganyika kulikuwepo tamaduni nyingi tu kila sehemu. Mnapoingia kwenye muungano ni muhimu muwe na mambo mengi yanayowaunganisha na kuyakubali kwa kuweka baadhi ya tamaduni zenu binafsi pembeni kwa manufaa ya muungano wenu. Huwezi kuingia kwenye Muungano ili ukadumishe tamaduni zako huko bila kujali wengine ulioungana nao huko.
 
Wanatofautiana sana inapokuja kwenye maslahi ndani ya CCM au nje; ACT Wazalendo.
Uko sahihi unapozungumzia vyama vya siasa, ila linapokuja swala la maslahi ya nchi hakuna tofauti wote huwa na msimamo mmoja.
Kuwemo kwenye muungano ndiyo kete wanayoitumia kundi la Mapinduzi Tukufu, kuwatumia waTanganyika kuhakikisha usalama wao.
Ni kweli ukizungumzia Watanganyika kuhakikisha usalama, ila bado linapokuja swala la maslahi ya Zanzibar wanakuwa na msimamo mmoja usioyumba.
 
Uko sahihi unapozungumzia vyama vya siasa, ila linapokuja swala la maslahi ya nchi hakuna tofauti wote huwa na msimamo mmoja.
Ni kweli ukizungumzia Watanganyika kuhakikisha usalama, ila bado linapokuja swala la maslahi ya Zanzibar wanakuwa na msimamo mmoja usioyumba.
Mi nadhani wewe na mimi tunakubaliana kwa kiasi kikubwa. Sioni sababu ya kutafuta visababu vinavyotutenganisha hapa.
 
Kama anazungumzia idadi ya watu na uwiano wa wabunge, ni vizuri tuanze na Dar na Dodoma. Dar inawapiga kura wangapi (kwa takwimu za 2020) na Dodoma ina wapiga kura wangapi na Wabunge wangapi.
Mliosoma mahesabu tupeni uwiano ndipo tutajua kuwa Lissu ni mbaguzi namba 1.

Mbaya zaidi yeye mwenyewe aqmekuwa bungeni na anajua wazi kuwa majimbo ya uchaguzi wa wabunge hautegemei wingi wa watu/wapiga kura. Atupe vigezo ili twende pamoja.
Huyu ni mbaguzi namba moja, kwani akimalizana wa Uzanzibari na utanganyika atakuja kwenye Usingida na Uchagani au Umasaini au UDar. Nyie subirini pale nchi yetu itageuzwa kuwa kama Ethiopia na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Huna hoja yeye kafafanua katiba kaelezo ubovu wakatiba hajasema kwamba wazazibari ni wabayal Wala hajawatukana
 
Na ukishayaelewa na kulewa hayo maneno ya Lissu, kinachofuata ni vita vya vyenyewe kwa wenyewe. Huko ndio Lissu anakotupeleka.

Sikia nikwambia, idiolojia za Lissu hazina afya kabisa katika nchi yeyote ile ya Afrika. Jirani yako ndio mtu utayefanya naye biashara kwa ustawi wa Afrika na nchi moja moja. Huwezi kujua Ethiopia waliingiaje kwenye vita za wenyewe kwa wenyewe. Ni kama hizi siasa za Lissu ndio mbolea nzuri sana ya kukupeleka katika nchi ya ahadi ya Lissu.

Baada ya maelezo yake, tuchukulie kesho mmetengana, na yeye ndio Rais, hivi atakwendaje kwa jirani kuomba ujirani mwema?
Huja mwelewa lisu au unajizima Data, hajasema tuwachukie MAJIRANI anfafanua katiba ambayo kwayo ndio inaleta ubaguzi
 
Hapana, mfano wa Mafia siyo sahihi hata kidogo katika kuelezea uwakilishi wa wabunge toka Zanzibar. Mkuu, kama ni maswala ya utamaduni, hata huko Tanganyika kulikuwepo tamaduni nyingi tu kila sehemu. Mnapoingia kwenye muungano ni muhimu muwe na mambo mengi yanayowaunganisha na kuyakubali kwa kuweka baadhi ya tamaduni zenu binafsi pembeni kwa manufaa ya muungano wenu. Huwezi kuingia kwenye Muungano ili ukadumishe tamaduni zako huko bila kujali wengine ulioungana nao huko.
Naona kuna shida ya kuelewa point kuu ninayotaka kuzungumzia. Nilipoandika mfano wa Mafia, lengo kuu lilikuwa kwa ujumla, si Zzibar tu bali hata bara ubunge kati ya jimbo na jimbo haulinganishwi kwa idadi ya watu.
Nilichotaka kusema, Lissu kama anataka kuwa muwazi basi vile vile alaumu kwanini Mafia ina mbunge mwenye hadhi sawa na mbunge wa Kawe, kama idadi ya watu ndio vigezo?

Suala la Muungano. Kwanza tukubaliane kuwa ni nchi 2 ndio zilizoungana, sio mikoa 2. Kumbuka Zanzibar ilkuwa na kiti umoja wa mataifa kilichokuwa na uzito sawa na Tanganyika. Tunaposema Tanzania imepiga kura umoja wa mataifa kupitisha suala fulani, kura hiyo ina uzito sawa na kura ya Burundi na Rwanda zenye watu chini ya 6 mil kila moja. Hivyo suala la nchi huheshimiwa kama nchi bila kujali kuna watu wangapi. Twende pamoja!

Mwaka 1964 Tanganyika ilikuwa na watu 12 milioni na Zanzibar takriban laki 3.5. Ni nchi mbili zenye uzito sawa kimataifa. Hivyo kulihitajika majadiliano yenye uzito sawa kwa kila upande. Katika kulinda hadhi ya watu wa Zanzibar ambao walikuwa 3.5 milioni, na Tanganyika Mengi yalifikiwa. Unaweza kukubaliana na baadhi ya mambo au hapana. Kwa maneno mengine Kila nchi ilitakiwa kuwa na kura ya Veto kwa kila nchi.
 
Back
Top Bottom