Hapana.Mimi naona tofauti kidogo. Kilichopo sasa ni kutaka kuitawala Zanzibar na inapokuwa ngumu tunaanza kulialia. Inatafutwa gia ya kuenda kwenye serilkali moja, jambo ambalo WAZANZIBARI wengi hawalikubali.
Wakitaka kuitawala Zanzibar ni kazi rahisi kabisa. Ni kumpata mtu kichaa kama Magufuli katika swala hilo. Hutasikia tena fyokofyoko unazosikia sasa hivi. Kwa taarifa yako, ni kikundi kidogo sana kilichoko Zanzibar ambacho hupiga kelele zaidi ya wingi wao, hasa toka Pemba. Hawa wana maslahi na kwingineko, na hawautaki Muungano toka mwanzo. Kukidhibiti hiki kikundi siyo kazi kubwa. Ni kikundi hiki sasa ndicho kimeiingilia CCM Zanzibar, na ndicho huibua mara kwa mara habari za "kero" ambazo ndizo zimelegeza Muungano sasa hivi.
Hayo niliyo yandika hapo yatafakari kidogo, utaona ukweli ndani yake.