Vicky Kamata asema marehemu mume wake "Alikuwa na vinyumba vya kawaida na msururu wa watoto!"

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Vicky.JPG

Nakuomba msamaha mume wangu kwa kuwa mimi ni Mkatoliki na Imani yangu inaniambia unaona na unajua kila kitu kinachoendelea kati yangu na wanao.

Najua muda utaongea lakini kwa kuwa nami ni binadamu naomba niseme yafuatayo! Ni kweli mimi ni kiumbe dhaifu na mwenye dhambi nyingi tu kama wengine.

Lakini wanangu kwanini mnapindisha ukweli? Nimedhulumu mali gani? Nimemfukuza nani? Nyumba ipi? Wanangu hata kama ni chuki iwe na kiasi basii.

Sitaki kumuaibisha mume wangu lakini mnanichochea na kunisukuma wanangu! Niambie Dunia ukweli wa maisha yangu na Baba yenu? Alikuwa na pesa kunizidi yes! Lakini alikuwa na asset gani ya maana kunizidi mimi?

Baba yenu alikuwa na vinyumba vya kawaida na msululu wa watoto! Kwanini alipokuwa na Mama zenu hakufanya maendeleo? Leo mnanichafua na kunipaka matope kwa jasho langu? Mungu mnamjua nyie watoto?

Nimetoka familia masikini sana, na nimefika hapa kwa jasho la damu. Naomba sana mshangilie ushindi wenu kwa heshima! Sijafukuza mtu! Sijadhulumu na sintakuja kudhulumu maishani kwangu.

Nafanya kazi usiku na mchana kwa kuwa najua sina wa kunipa cha bure. Baba yenu hata swimming pool ameikuta kwangu. Na baadae nikachimba kwa pesa zangu ili nifurahie uzee wangu mimi na yeye. Bahati Mbaya Mungu kamuita mapema ange enjoy na alikuwa anaenjoy. Najua mnamuumiza sana. Tulieni sihitaji hata kijiko ambacho siyo cha jasho langu. Jasho la mama zenu mtalifaidi na mimi jasho langu hayupo wa kunidhulumu.

Maisha ni hadhithi tu. 🙏🙏🙏🙏

Pia, soma=> Kesi ya Mirathi ya Dkt. Likwelile: Vicky Kamata ashindwa, mahakama yasema ndoa yao haikuwa halali
 
Hawa wanaccm ifike mahali wawe wanapeana semina wao wa wao huku namna ya kuishi na watu, wanatia aibu sana na kutia aibu chama chao, manake wengi hasa hao wanawake wanaonekana kama ni wadangaji tu na gold diggers. waacheni watoto washangilie ushindi wa nyumba za baba yao.
 
Back
Top Bottom