Ubinafsi na Utapeli wa Sisi wanaume ndani ya Familia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
UBINAFSI NA UTAPELI WA SISI WANAUME NDANI YA FAMILIA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Niliwahi kuandika hapa, unaweza kupitia👇Wanaume tuache Ubinafsi

ukitaka familia yako ianguke basi moja Kati yenu awe mbinafsi. Aidha Mke au Mume. Chanzo kikubwa cha umaskini wa familia nyingi hapa Tanzania na Duniani ni ubinafsi. Sio tuu familia Bali hata taifa. Nchi ili isiendelee basi Watu wake wawe wabinafsi.

Jambo la Kwanza Wakati unaunda Familia au taifa basi ni kuwaweka Watu pamoja, wawe wamoja, washirikiane pasipo kuwa wamimi, wabinafsi.
Yaani unapochumbia Mwanamke au kuchumbiwa na Mwanaume, Baada ya kujua NIA ya mwenzako hatua inayofuata ni kujua Ubinafsi wa mtu huyo.

Ogopa mwanaume mbinafsi kwenye Maisha yako. Kaa naye mbali. Usikubali kumbebea mimba asijekukuzalia vitoto vibinafsi.

Mwanaume mbinafsi yupoje? Anafananaje? Anafanyaje mambo yake? Yaani utamjuaje?
Hizi ni Sifa za Wanaume wabinafsi;

1. Anajali hisia zake kuliko zako.
Anajiona yeye ndiye anaumia wewe huumii. Anajali tamaa zake za mwili na kujipa Haki ya kuwa yeye anastahili kutamani Ila wewe haustahili.
Anaweza kutaka kukuongezea Mwanamke mwingine bila kujali hisia zako lakini yeye hataki wewe uongeze mwanaume mwingine.
Huo ni ubinafsi. Kujijali wewe zaidi kuliko kumjali Mwenza wako huo ni ubinafsi.
Sisi watibeli tunaongozwa na Kanuni isemayo; Kile usichotaka kufanyiwa basi usimfanyie mwingine. Na kile unachotaka kufanyiwa basi wafanyie wengine. Huo ndio upendo.

Mwanaume unataka kurudi Usiku na umechelewa kisa ulienda kwenye Mpira, mkeo au Watoto wanapenda uwe karibu nao wewe hujali. Huo ni ubinafsi. Alafu muda huohuo wewe hautaki wao wafanye hivyo. Huko ni kujijali mwenyewe.
Labda uwe Kazini hapo Sawa lakini kama ishu ni kujifurahisha, elewa kuwa hata Mkeo naye anatamani kujifurahisha na marafiki zake.
Kama umeshindwa kumfanya Mkeo Rafiki yako mpaka unaenda kufurahia na marafiki zako Huko Bar basi muachie na Mkeo naye akafurahie na marafiki zake. Vinginevyo nendeni wote Huko Bar.

Kujijali mwenyewe ni pamoja na kuvutia kwako vitu vizuri ikiwemo kutaka kupewa kipaombele kwenye chakula kizuri kama Mapaja ya kuku, wewe kama Baba na Mwanaume elewa kuwa kama unapenda Kula vitu vizuri kama Baba ikiwa ni pamoja na Mapaja ya kuku, elewa hata Mkeo anapenda Kula vitu vizuri kama Mama wa hiyo familia.

Kitendo cha kusema wewe ndiye mtafutaji basi unahitaji kupewa zaidi huo ni Ubinafsi mkubwa. Na Sisi Watibeli Jambo Hilo halivumiliwi. Kama ni paja ni moja au mawili gawaneni na Mkeo, au wekeaneni zamu ya Kula. Mkiwahusisha na watoto. Kwa sababu ninyi ni kitu kimoja/Familia.
Sio kuleta utengano na ubinafsi.

Sijui Yale mambo ya wale kina Baba alafu kitakachobali ndipo wale Wanawake huo ni Mtazamo wa libinafsi. Ni ubinafsi tuu hakuna Lugha nyingine ya kuelezea Jambo Hilo. Ni ubaya bila kujali unafanywa na Nani.

2. Kauli za kibinafsi.
Jitu binafsi utalijua kwenye Lugha anayoitumia. Kila kitu anapenda Kutumia kauli ya umimi badala ya umoja.
"Nyumba yangu" Gari langu" shamba langu"
"Nitawafukuza kwenye nyumba yangu"
"Sitaki MTU achezee Pesa yangu"
Yaani kila kitu anatumia umimi.

Mwanaume kama huyo hafai kuwa Mumeo. Huyo ni mbinafsi.
Hao ndio wale hata siku mkiachana au akifa Ndugu zake watakusumbua kwenye mgawanyo wa Mali. Ni wabinafsi ambao wanakuchukulia wewe kama ziada tuu. Kinyamkera, hakuthamini.

Unajua Sisi Watibeli Watu wa hivyo hatuwezi hata kukaa nao karibu. Ni Watu wa hovyohovyo! Hamuwezi kuunda familia na Mwanaume mwenye Lugha ya ubinafsi.

Ogopa mwanaume ambaye hataki mchangie Pesa pamoja. Ogopa mwanaume ambaye anataka awe anakipa tuu Pesa nawe kama mjinga unakuwa ombaomba Kwa MTU unayejinasibu kuwa ni Mumeo. Hakunaga Mume WA hivyo.

Binti za Tibeli, ukiolewa na kijana, wewe na yeye ni mwili mmoja. Chochote chake ni chako. Na chochote chako NI chake. Huwezi omba kitu chako. Na kama unafanya hivyo basi unajidanganya. Na Watibeli hatujidanganyagi.

Wekeni Bajeti na ratiba Kwa pamoja, Pesa za matumizi ya muhimu ziwe bayana na zijulikane zinakaa wapi, Pesa za urembo na utanashati zijulikane kila MTU kulingana na kiwango cha urembo na utanashati wake. Pesa za Wazazi, Ndugu na marafiki Kwa wote Wawili zijulikane, Pesa za mke na Mume binafsi zijulikane.
Mfano inatolewa laki mbili Kwa kila mmoja kama Pesa binafsi. Na matumizi ya Pesa binafsi hayaingiliwi na mwingine, ilimradi yasilenge kufanyika uhalifu au uovu au Jambo lolote litakalozorotesha Familia.
Kwa mfano Kuhonga michepuko na hii ni Pande mbili, yaani MKE hairuhusiwi Kuhonga na Mume vivyohivyo.

Sio mambo ya Pesa yangu, Sisi Watibeli ukishaleta mambo ya Pesa yangu, sijui nyumba yangu, tunakuacha hapo na mambo yako.

Tumia kauli za umoja na upendo. Kama,
Nyumba yetu, Gari letu, biashara yetu, Kampuni yetu, Mali zetu, Watoto wetu.
Hata kama Baba ndiye umefanya Jambo Hilo Kwa jasho Lako, lakini uwepo wa Mkeo na watoto lazima uutambue na useme tumefanya kazi tukazalisha kiasi hiki, hata kama Mkeo hafanyi kazi.
Halikadhalika na MKE hata kama kitu umenunua wewe, kamwe usitumie kauli ya umimi.
Kauli ya umimi Kwa Sisi Watibeli Moja Kwa moja inaelezea Nafsi yako jinsi ilivyokosa upendo. Na inaeleza nafasi ya wengine kuwa Hawana nafasi yoyote kwako. Na hakika ni Hawana.

Hata Biblia au Quran, Mungu akiwa anaumba Dunia alikuwa anatumia kauli ya Wingi kana kwamba wapo wengi licha ya kuwa alikuwa pekeake. Natuumbe MTU Kwa mfano wetu, tufanye hivi au vile, hiyo ni kauli ya Wenye upendo, kujali nafasi za wengine hata kama mchango wao ni mdogo. Kauli za upendo.

3. Kumpiga Mkeo na kumfokea Fokea Kwa Lugha chafu.
Huo ni ubinafsi.
Kwa nini umpige Mkeo, wewe ukikosea nawe utapigwa? Hakuna cha kusema wewe ni Mwanaume au sijui ni Baba. Ukiwa Baba au Mwanaume Isiwe sababu ya kufanya uhalifu, ukatili, unyanyasaji. Huo ni ubinafsi na kukosa upendo.
Vinginevyo na wewe ukikosea Mkeo naye akupige au akutolee maneno Makalu yenye kukuumiza.

Hakuna kosa hata Moja ambalo litamfanya mtu mwenye Upendo amtolee maneno Makali Mkewe. MTU akikosea hasa Mkeo au Mtoto. Kuna Njia mbili za kufanya moja ni kunyamaza mpaka hasira zipungue, kisha baadaye mjadili Jambo Hilo. Pili, kama imeshindikana amekuwa mkaidi yaani ni Tabia yake kufanya Jambo lilelile, mnaweza kutengana.

Ni Watu wadhaifu, wakatili, wanyanyasaji na matapeli wanaopiga Wake zao. Mkeo ni MTU mzima mwenzako. Ni mwili mmoja wako. Kwa nini umpige? Au kisa yeye ni dhaifu, unanguvu kumshinda ndio maana unampiga? Lakini wewe ukikosea haupigwi?

Visingizio vya kipumbavu vinavyotolewa na watu wapumbavu wasio na upendo ndio husema Mimi ni Mwanaume au Baba ndio maana ninahaki ya kumpiga. Ni upumbavu.

Ni sawasawa na wale Wanawake wapumbavu ambao hutoa visingizio vya kipumbavu kuwa Mimi ni Mwanamke ninatakiwa kuhudumiwa lakini Mimi sitakiwi kumhudumia Mume wangu Wakati NI MTU mzima. Huo ni ubinafsi, unyonyaji, Utapeli na kukosa Upendo.
Na Watibeli Hilo hatutalivumilia hata tungeshikiwa bunduki.

4. UBINAFSI katika mahusiano.
Mwanaume anakataza Mkewe asiwasiliane na Ndugu zake au kwenda kusalimia kwao. Lakini yeye(mwanaume) anawasiliana na Ndugu zake na kwenda kwao kila atakapoamua. Huo ni ubinafsi.
Ukimuuliza atakujibu Mimi ni Mwanaume, sijui nilitoa Mahari. Ukiuliza hiyo Mahari yenyewe atakuambia ni milioni tano sijui ngapi. Ndio maana Sisi Watibeli hatutoi Mahari wala Binti zetu hawatolewi Mahari Kwa sababu Binti zetu ni Binti Huru.

Au Mume anamkataza Mkewe kuleta Ndugu zake alafu Wakati huohuo Ndugu zake(Mume) wanakuja kila mara. Huo ni ubinafsi.
Kama hamtaki Ndugu na marafiki basi iwe Kwa wote na kuwe na sababu reasonable.
Na Kwa Sisi Watibeli Kabla hatujaamua kuwa MKE na Mume hayo mambo yanazungumzwa mapema na sheria za mahusiano ya Watu kama wazazi na Ndugu zinawekwa kwamba ikitokea mambo moja mbili tatu iwe Kwa wazazi au Ndugu au marafiki wa upande wowote mimi(Mume) na wewe(MKE) wakafanya mambo haya 1,2.3 n.k hatutawaruhusu kukanyaga hapa nyumbani. Mfano, ikiwa Ndugu au mzazi au Rafiki au yeyote ambaye itabainika pasi na Shaka akiwa hapa nyumbani kwetu akawa anatumia Ulozi, Uchawi na ushirikina au Aina yoyote ya uganga na Uchawi basi MTU huyo bila kujali nafasi yake na mchango wake katika familia yetu tutamfukuza na hatakanyaga tena nyumbani kwetu.
Au ikitokea mtu yeyote Kutoka upande wowote wa Mume au MKE, ikabainika analengo la kuharibu Maisha yetu au moja ya Watoto wetu Kwa namna ya kutuangusha kiuchumi, au kutaka kudhuru Maisha(uhai) wetu au kuvunja mahusiano yetu iwe Kwa fitna, ulaghai, Uongo au aina yoyote ya hila, basi MTU huyo atafukuzwa na hatakanyaga tena nyumbani kwetu nafasi hatutaenda nyumbani kwake. Na hivyo ndivyo itakavyokuwa.

Sheria hizo ziwe bayana na wazazi, Ndugu, jamaa na marafiki wazijue. Ndio maana unatakiwa Watu wakujue falsafa na mitazamo yako ili mtu akijichanganya awe amefanya Makusudi.

Sio tuu MTU mwanaume unaroho Mbaya unasema sitaki Ndugu au wazazi wako. Umelogwa nini. Huwataki wamekufanyaje? Kama uchumi ni mdogo hiyo inaeleweka, basi hawatakuja au labda wanakuja siku Mbili tatu wanaondoka. Huo ndio undugu. Pumbavu!

Acha nipumzike sasa!

Ni Yule Shahidi, Kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Na ndio maana mara Kwa mara ninawaandama.
Ila pia wapo wanaume ukihadithiwa mambo wanayoyafanya utabaki kushangaa.

Hivi mwanaume unakunywa bia na kununuliwa Bia Watu Huko Bar lakini Mkeo na watoto unazaidi ya miezi na miezi hujawanunulia hata soda, Kweli!!
Kwaiyo tusinywe bia kisa wake zetu hawajanywa soda mwezi mzima
 
Lengo la bia nadhani Kwa wengi ni kujifurahisha, achilia mbali wale wanaopoteza mawazo.
Ikiwa unaenda kufurahi, basi hakikisha kiwango kilekile utakachofurahi umfanyie na Mwenza wako. Hiyo ndio Familia.
 
Katika 100% wanawake wabinasfi ni 99%.
 
Attachments

  • IMG-20170803-WA0071.jpg
    IMG-20170803-WA0071.jpg
    84.5 KB · Views: 9
Well-said!

Ninyi mnaotaka Pesa mkidhani ndio ukarimu. Ndio mnajiingiza katika hatari ya kufanywa kama Bidhaa na wanaume.
Mwanaume anakuambia ninakulisha, ninakuvalisha, unapata kila kitu lakini hapohapo anakuletea Wanawake wengine, kutwa kucha vipigo, au kukusemea maneno machafu, au maneno ya kibinafsi, Hii nyumba hukuwepo nikijenga, hapa sio kwenu, nitakufukuza uende kwenu, sitaki MTU acheze na Pesa zangu. Umenisikia wewe Mwanamke.

Unajaza tuu Choo humu ndani.

Hayo ndio mnayoyapata Kwa sababu ya kutoelewa nini maana ya mapenzi na upendo.

Shenzi kabisa,
 
Weweeee hao washenzy washenzy wa hivyo Mimi siwezi olewa nao,ndio maana kitu Cha kwanza nakutest na vitu vidogo vidogo kama nauli,ukishindwa vidogo vikubwa utaniweza?
 
Back
Top Bottom