Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Kwa hili Samia yuko sahihi,yaani Dar mji mkubwa uko hovyo , holela mbaya kila mahali vibanda, kariakoo mara boda boda , mara bajaji ukigeuka huku vibanda inakuwa ni uchafu, unaweza fikiri uko masasi kumbo uko Dar , chamsingi wawatafutie mahali pakufanyia biashara zao ndogo ndogo na hao boda boda sehemu nyingine ndani ya jengo ili biashara zao zitambulike.
 
Yote yamesababishwa na kufa kwa uchumi wa nchi.Mfano korosho, mbaazi, ufuta,mifugo bei ikiwa nzuri kilimo kikilipa nani awe machinga hali wanunuzi ukufuata shamba.
Kabla ya mwendazake Wakenya walijaa hadi vijijini wakichumbia mazao yaani unapewa advance mazao yakikomaa unamaliziwa cash yako wanavuna mazao yao we unabakia na pesa.Walijaa Mbeya,njombe,iringa, kilimanjaro kwenye ndizi,viazi mviringo,walijaa dodoma iringa rukwa ruvuma kwenye mahindi walijaa pwani tanga kwenye matikitiki,nyanya,mboga nk.Huku wacongo,wazambia wakijaa kanda ya ziwa hadi visiwani wakinunua dagaa, samaki,mabondo,Wasudani Wakenya wakinunua vitunguu,nk Wacomoro, zimbabwe, zambia wakijaa kariakoo kuleta pesa hii ilisaidia Sana watu kubakia sehemu moja kuzalisha.Baada ya sera chakavu za kuwafanya matajiri wawe masikini,na kufunga mipaka,bifu zisizo kichwa majirani zetu wote walipotea hali ikawa ngumu vijijini ikapelekea wimbi la machinga mijini.Pesa zilijaa toka KILA nchi jirani ikapelekea kushamiri kwa bureau de change mijini,thus uliona nyumba za nyasi zikipotea kwa kasi ya 5G nchi nzima Bati zikienea kwa kasi vijijini sababu ya mzunguko mzuri wa pesa kabla ya sera chakavu.
Tukivutia Wawekezaji ajira zitakuwepo,tukifungua mipaka wakulima na wafugaji watauza nje uzalishaji utarejea na idadi ya machinga itapungua mijini.
Huu ndiyo ukweli mtupu

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Ila watu wanashindwa kuelewa ,tatizo la wamachinga wanaweka biashara kwenye barabara kabisa na ndio chanzo cha foleni huko DAR.

Hata wasipokaa barabarani wakapelekwa sehemu husika lazima mtu aende kufuata mahitaji,kwahiyo hata wakiondolewa wakapelekwa sehemu mahususi kwa kufanyia biashara watu wataenda kununua bidhaa zao.

Kwasasa wamachinga ni kero tupu kwenye barabara na road reserve.
 
Yote yamesababishwa na kufa kwa uchumi wa nchi.Mfano korosho, mbaazi, ufuta,mifugo bei ikiwa nzuri kilimo kikilipa nani awe machinga hali wanunuzi ukufuata shamba.
Kabla ya mwendazake Wakenya walijaa hadi vijijini wakichumbia mazao yaani unapewa advance mazao yakikomaa unamaliziwa cash yako wanavuna mazao yao we unabakia na pesa.Walijaa Mbeya,njombe,iringa, kilimanjaro kwenye ndizi,viazi mviringo,walijaa dodoma iringa rukwa ruvuma kwenye mahindi walijaa pwani tanga kwenye matikitiki,nyanya,mboga nk.Huku wacongo,wazambia wakijaa kanda ya ziwa hadi visiwani wakinunua dagaa, samaki,mabondo,Wasudani Wakenya wakinunua vitunguu,nk Wacomoro, zimbabwe, zambia wakijaa kariakoo kuleta pesa hii ilisaidia Sana watu kubakia sehemu moja kuzalisha.Baada ya sera chakavu za kuwafanya matajiri wawe masikini,na kufunga mipaka,bifu zisizo kichwa majirani zetu wote walipotea hali ikawa ngumu vijijini ikapelekea wimbi la machinga mijini.Pesa zilijaa toka KILA nchi jirani ikapelekea kushamiri kwa bureau de change mijini,thus uliona nyumba za nyasi zikipotea kwa kasi ya 5G nchi nzima Bati zikienea kwa kasi vijijini sababu ya mzunguko mzuri wa pesa kabla ya sera chakavu.
Tukivutia Wawekezaji ajira zitakuwepo,tukifungua mipaka wakulima na wafugaji watauza nje uzalishaji utarejea na idadi ya machinga itapungua mijini.

Waziri wa kilimo na wadau wajaribu kutoa stimulus packages na mikopo kwa vijana wajikite kwenye kilimo na waachane na uchuuzi mitaani.
 
Mzee kuchukuwa mkopo ukaweka kibanda barabarani nisawa kweli! Mimi nashauri hata leo viondolewe,kwanza nikelo kubwa kwa watembea kwa mguu na vilevile ikija kutokea hajari ya gari kuacha njia ndo unaweza kuelewa.Viondolewe safi kabisa
Hivi unaweza ukachukua mkopo VICOBA bila kuwa na physical address na collateral ikawa kibanda kilichopo kwenye road reserve?

Back
Top Bottom