Jumanne Sagini: Serikali inafuatilia kwa ukaribu matukio ya utekaji yanayoendelea Jijini Dar es Salaam

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mbunge wa Nyang’hwale, Hussein Amar ameihoji Serikali ina mpango gani wa haraka kuzuia utekaji unaoendelea katika Jiji la Dar es Salaam.

Miongoni mwa matukio matano ya watu kutekwa na kutoweka katika mazingira ya kutatanisha yalitokea mwaka 2023, limo la kutekwa mfanyabiashara Mussa Mziba (37), aliyekuwa akimiliki Kampuni ya Mziba Empire Investment Ltd ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Tukio lingine ni la kutekwa kwa aliyekuwa mfanyabiashara na fundi wa simu katika eneo la Kariakoo Dar es Salaam, Innocent Elias Liveti (34) maarufu Macheni.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumatano Februari 7, 2024, Amir amehoji Serikali ina mpango gani wa haraka kuzuia utekaji unaoendelea ndani ya jiji la Dar es Salaam na kupoteza maisha ya watu. Amesema amehoji hilo kwa sababu utekaji huo unaendelea kila kukicha.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema wanafuatilia kwa karibu matukio yanayoendelea kutokea katika Jiji la Dar es Salaam kwa madhumuni ya kudhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wanaohusika na hicho kinachoitwa utekaji.
 
bunge la ccm kwa faida ya ccm na sio Nchi!
maaumuzi ya ki-ccm kwa faida ya ccm na sio Nchi!
kwa manufa ya ccm na sio kwa Nchi
 
Tuko na habari za Lisu, hizo za bunge kibogoyo la majizi ya kura hatuna mpango nalo. Wao waendelee kupitisha miswaada ya Sheria za Hila lakini wao ni useless.
 
Back
Top Bottom