Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,407
2,000
Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.

Ni sahihi kabisa wakafanye hivyo na pale stand ya JPM Mbezi ni kero.....yaani ukitaka kupanda gari za Moro hasa Abood mlango wa gari ulipo hapohapo kuna machinga kapanga bidhaa zake ni kero tupu, pia vituo vingi vya daladala vimegeuka masoko
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,612
2,000
Kuna maamuzi wakati mwingine magumu lakini katika hili naunga mkono 100% na sio Dar tu iwe miji mingine yote mikubwa ni lazima tuanze sehemu na tuwe serious katika hili kuwe na muendelezo.
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
29,446
2,000
jath.gif

Waondolewe! Waondolewe! Mama safisha Jiji.
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,612
2,000
Wenye nguvu ya fedha washafanya Yao tena,

Ndiyo tunajua, kila kitu lazima kiende Kwa utaratibu, Labda niulize Kwa Mleta uzi, Je Hilo gari linalotangaza halisemi mbadala wa hao wenye vibanda wanapaswa wapelekwe wapi?

Kama ndivyo, tayari hili ni kosa lingine kubwa baada ya lile la Kwanza la makampuni ya kigeni yanayokuja kuwekeza nchini hayatakiwi kuwekewa limiti ya wafanyakazi wanaotakiwa kuja nao kutoka makwao ili kufanya kazi kwenye kampuni hizo za kigeni!!

Hilo ndilo kosa kubwa kuliko mengine yote ambayo yameendelea kuwepo Wakati huu,

Watanzania mtegemee kukosa ajira kwenye makampuni yote ya kigeni na hata ysliyowekeza tayari mtaanza kutimuliwa mdogomdogo na wageni kuletwa kufanya kazi hizo

Yetu macho
Kwa taarifa yako JPM kabla hajafariki ziara yake ya mwisho Dar alishaongelea hili kuwa kuna uganganyifu wenye maduka wanafunga ila bidhaa wanawapa watu kuuza nje na serikali wanapoteza pesa nyingi katika kodi za maduka. Hoja yako ya pile kuwe eti wawekezaji hawana limit sio kweli Mama kasema ziko taratibu za kuajiri lakini kuna key positions mwekezaji anahaki ya kuweka watu anaowaamini yeye na nafasi zingine ziende kwa mujibu wa taratibu. Na katika hili kusema hakuna ajira wakija wawekezaji sasa wasipokuja ajira zitatoka wapi? Majiji yote hawaruhusu vibanda hovyo mtaani waende soko lao la wamachinga mtu unashindwa hata kutembea barabarani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom