Waziri Bashungwa simamia na kukamilisha miradi ya barabara za Dar au ujiuzulu na kumpisha anayeweza

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Niaje waungwana

Huyu Mhe. Innocent Bashungwa, alikuwa ni miongoni mwa mawaziri wachache sana niliowaheshimu sana katika baraza hili la mawaziri wa raisi Samia.

Kila alipopelekwa alionesha kupamudu vizuri kiutendaji, na kiusimamiaji lakini sasa huku alipoletwa sasa hivi (wizara ya ujenzi) kunaonekana wazi kumshinda, na hii ni baada ya waziri huyo kutembelea maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam na kujionea ubovu wa barabara zetu, kisha kuahidi ahadi hewa na baadae kutoweka bila kutekeleza ahadi zake alizoahidi.

Kila mtu anakumbuka jinsi alivyoahidi kuishughulikia haraka iwezekanavyo barabara ya Mbezi - kuelekea Msumi lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika na hajarudi tena kuwaambiwa wananchi wa maeneo hayo kwamba nini kinafanyika ili mradi huo wa ujenzi uanze, na sio barabara hiyo tu, ni nyingi mno amekuwa akiahidi bila utekelezaji.

Sasa kwa maana hiyo, huyu waziri ashaanza kuonekana kuwa hafai kuendelea na wizara hiyo, ni bora tu ajiuzulu, ahamishwe au apambane tena kuikamilisha. Hawezi kuendelea kutupiga changa la macho watu wazima na akili zetu kama vile mzee awadanganyae wajukuu zake. No.. no.. no again.
 
Yaani mkuu wewe umeyaona matatizo kwenye barabara tu? Kila sekta ni shida tu.

1. Umeme shida.
2. Afya NHIF inasumbua.
3. Utumishi ajira na kikokotoo tabu.
4. Biashara Kodi na tozo havibebeki.
5. Mambo ya ndani, huko Zanzibar wananchi wanachapwa viboko na magaidi wa kidini hovyo hovyo kwa kula mchana.
n.k
.
Nadhani mtu sahihi wa kumuwajibisha ni Samia na serikali yake yote
 
Waziri Bashungwa amekuwa akitumia kodi zetu kuzunguka na magari nchi nzima kupiga picha na kutoa mikwara kwa watendaji fulani, ila hakuna barabara hata 1 ambayo ishajengwa kutokana na mzunguko wake huo.
 
Waambie tarura sio waziri wenye budget sio waziri ni tanroad na tarura hawa ndio tatizo nchi hii

Bashungwa mtamuonea bure kila siku tanroad na tarura wanaruhusu makapuni ya ujenzi wanamwaga vifusi ovyo tu

Na barabara wanaowapa tenda wanajenga muda mrefu ili kuiba pesa

Tatizo kubwa ni wao na wanaowapa tenda ni ndugu zao na washikaji wao ndio maana barabara hazijengwi kabisa.
 
Huyu waziri amepwaya mno Kwa mfano hii barabara ya kutoka chanika,kitonga, msongola Hadi mmbande ni mbovu na imeachwa kama ilivyo baada ya mkandarasi kuingia mitini..

Barabara ya kitunda, kivule Hadi fremukumi imeachwa kama ilivyo
Waziri Bashungwa akiona watu wanalalamika sana, anafika katika eneo la walalamikaji kutoa ahadi kem kem hewa. Akishamaliza hapo inakuwa imetoka hiyo. Namaanisha hamtamuona tena eneo hilo.
 
Waambie tarura sio waziri wenye budget sio waziri ni tanroad na tarura hawa ndio tatizo nchi hii

Bashungwa mtamuonea bure kila siku tanroad na tarura wanaruhusu makapuni ya ujenzi wanamwaga vifusi ovyo tu

Na barabara wanaowapa tenda wanajenga muda mrefu ili kuiba pesa

Tatizo kubwa ni wao na wanaowapa tenda ni ndugu zao na washikaji wao ndio maana barabara hazijengwi kabisa.
Kazi ya waziri wa ujenzi ni nini?
Je yeye kama waziri anapoona hayo yanatokea anachukua hatua gani kama waziri husika ili kuhakikisha hayo unayosema yanafanywa na tarura au tanroad hayatokei tena?
 
Yaani mkuu wewe umeyaona matatizo kwenye barabara tu? Kila sekta ni shida tu.

1. Umeme shida.
2. Afya NHIF inasumbua.
3. Utumishi ajira na kikokotoo tabu.
4. Biashara Kodi na tozo havibebeki.
5. Mambo ya ndani, huko Zanzibar wananchi wanachapwa viboko na magaidi wa kidini hovyo hovyo kwa kula mchana.
n.k
.
Nadhani mtu sahihi wa kumuwajibisha ni Samia na serikali yake yote
Hama nchi wewe
 
Ulichoandika naona kinakaribiana na ukweli halisi.
Mkuu watu wanapiga hela bila huruma
Nchi ingekuwa mbali kama watu wangekuwa wanafungwa maisha kwa wizi wa mali ya Umma
Ila kwa kuwa wanajuana tena wengine mpaka miaka zaidi ya 50 basi usitegemee wa kuwajibishwa

Nashangaa mnaletewa report za mkaguzi wa mahesabu ila hazina faida yoyote kwetu bali machungu tu

Hapo ni kama anatuambia oyaa nyie mafala angalieni wenzenu wanavyopiga
Inauma lakini
 
Inasikitisha sana aisee.
 
Waziri Bashungwa amekuwa akitumia kodi zetu kuzunguka na magari nchi nzima kupiga picha na kutoa mikwara kwa watendaji fulani, ila hakuna barabara hata 1 ambayo ishajengwa kutokana na mzunguko wake huo.
Jamaa akiwa mbele ya kamera anatema mkwara mwingi, nje ya kamera hana lolote la maana analofanya kuhakikisha barabara zinatengenezwa.
 
Huyu waziri amepwaya mno Kwa mfano hii barabara ya kutoka chanika,kitonga, msongola Hadi mmbande ni mbovu na imeachwa kama ilivyo baada ya mkandarasi kuingia mitini..

Barabara ya kitunda, kivule Hadi fremukumi imeachwa kama ilivyo
Hizo barabara za Tarura siyo TANROADS, Tofautisha
 
Hizo barabara za Tarura siyo TANROADS, Tofautisha
Nilikuwa ninaitafuta hii comment.

Barabara anazozitaja mtoa mada zipo chini ya TARURA ambayo kimsingi wazara husika ni TAMISEMI ambayo Waziri wake ni Mchengerwa.

NB: Hata kama Bashungwa alitoa ahadi akiwa waziri wa TAMISEMI, bado hastaihili kulaumiwa.
 
Back
Top Bottom