Mpango Mji wa Dar es Salaam unavyopotea kwa Kasi, Ujenzi bila Mpangalio

ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,788
1,302
Wadau, nimepita mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam katika hali ya kawaida mpango mji haueleweki tena au haufuatwi. Watu wanajenga hovyo sijui kama wanavibali au ni mamlaka zimelala.

Baadhi ya vitu vinashangaza, kwa sasa asilimia kubwa ya nyumba zilizopakana na barabara wanaweka frame za maduka, najiuliza hivi wanavibali vya ujenzi vinavyoainisha matumizi husika kwa maana ya biashara na makazi au ndio kila mtu anaamua anavyotaka matumizi ya eneo lake.

Wingi wa mabaa na kumbi za starehe katika maeneo na makazi ya watu imekuwa shida sana, hapa vibali vinatolewa na vinaendana na maeneo husika au kila mtu anajiamulia kuweka pub, duka, bar, genge etc

Nilipita Coco beach last week, kumekuwa na vibanda na wingi mkubwa sana wa watu. Vibanda kila sehemu wala huwezi kupata tena sehemu tulivu ya kukaa kama zamani.

Leo nimepita Sinza Africa Sana, Kuna jamaa anajenga nyumba ame extend barabarani mpaka nguzo za nyumba amechimba kwenye lami ya barabara na watu wanapita wala hawachukui hatua. Hii ipo jirani na pale petrol station Africa Sana Sinza too much, ni vyema kuzuia mapema kuliko kusubiri amalize alafu umbomolee

Kwa kweli Jiji la Dar wahusika wasipokuwa makini tunatengeneza mji wa hovyo sana in the future, jiji lenye vibanda na viduka kile sehemu, Masaki na Oysterbay kwa sasa ujenzi wa maduka na vibanda nao unakuwa bila mpangilio.

Mamlaka husikua hebu fanyeni operation maalumu ya kuondoa hii kitu mapema kabla ya kuja kujuta.
 
Jiji la Dar es Salaam ni eneo lote la Wilaya ya Ilala.

Huko Masaki na Coco Beach ni eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Hiyo iko kwenye makaratasi tu, ila nilimaanisha Dar es Salaam na wilaya zake 5, Kinondoni, Ubungo, Ilala, Kigamboni na Temeke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom