Kitu gani kinakwamisha mradi wa DMDP katika jiji la Dar es Salaam?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Utekelezaji wa mradi DMDP katika awamu ya 4 na 5 ulibadilisha kwa kiasi kikubwa taswira mbaya ya miundombinu ya barabara kwa jiji la Dar es salaam.

Kuna maeneo ambayo yalionekana kama ni ya walalahoi kama Mwanayamala, Mbagala, Tandale nk barabara zake za mitaa zilijengwa kwa kasi kwa kiwango cha lami.

Kwa sasa mradi umesimama na kila kukicha wanasiasa hasa wabunge wanawaambia wananchi barabara zinajengwa mradi wa DMDP ukianza.

Je, unaanza lini maana hali ya miundombinu katika mitaa ya Jiji ni mibovu sana ambayo sidhani kama Tarura wanaweza kutekeleza chochote. Ni wapi tumekosea tukapoteza huu mradi bora wa kulibadilisha jiji la Dar es salaam
 
Back
Top Bottom