Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Mlima simba

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
3,707
6,628
Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.

--- UPDATE MAY 11, 2021--

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amewataka wafanyabiashara waliojenga vibanda katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuviondoa kabla ya Mei 18, 2021.

Wakati Shauri akieleza hayo, gari lenye spika za matangazo linapita katikati la mitaa ya Jiji hilo likitangaza kuhusu mchakato huo kwamba vibanda havitakiwi kuonekana kando ya barabara.

Akizungumza na Mwananchi Digitial leo Jumanne Mei 11, 2021 Shauri amesema hawajazuia wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao, wanachotakiwa kufanya ni kutojenga vibanda na kuwataka wauze bidhaa zao kwenye meza ili wakimaliza iwe rahisi kuziondoa na kuacha maeneo wazi.

Amebainisha kuwa sheria ya mipango miji hairuhusu kujenga vibanda, kuwataka wafanyabiashara hao kutii agizo hilo.

“Mwisho Mei 18 kama ambavyo gari la matangazo linavyotangaza waviondoe vibanda vyao kwa sababu vingine vinajengwa hadi kwenye njia za watembea kwa miguu na barabarani na kuleta adha kwa watumiaji. Wanatakiwa watii sheria bila shuruti waviondoe wenyewe,” amesema Shauri.

MWANANCHI

machinga.jpg
 
Swala la machinga waondoke tu mjini wanaua biashara watengewe maeneo yao Magufuli alibugi sana.

Kwanza hawalipi kodi na wanaponunua bidhaa hawaombi risiti kwenye maduka makubwa so serikali inapata hasara ya kodi.

Vile vile wengi mjini ni wafanya biashara wakubwa wanafanya kutoa pesa kwenye mfuko wa suluali na kuweka kwenye mfuko wa shati.

Ndio maana ukwepaji kodi unaongezeka kwa sababu watu wenye address za kulipa kodi biashara zao wanachukua machinga.

Halafu machinga wenyewe wanauza sana halafu hawana leseni za biashara za kufanyia kazi wengine unakuta ndio wale waliofunga maduka kipindi cha Magufuli unakuta machinga ameweka bidhaa za milio 10 nje hii sio haki hata kidogo.

Watafutiwe maeneo maalumu kama Tandika tegeta, Ubungo mbagala wawe na shopping mail zao na walipe kodi ili tuone kama watauza tens bidhaa ovyo na kuhatarisha hata maisha ya wanunuzi.

Unakuta mtu anauza nyanya kariakoo katikati ya barabara seriously sehemu ambayo mnasema ni soko la kimataifa.?
 
Back
Top Bottom