Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Katika zurura zurura nilipita kijiji kimoja kinaitwa kalando kama sijakosea kijiji hiki kipo sumbawanga kama unaenda mpanda unaingia kushoto , kipo pembeni ya ziwa Tanganyika . Huku kuna fursa lukuki ikiwemo mchele samaki na mbao , mizigo ni mingi sana ya kuja mjini ila magari ni yakusua sua . njia ni vumbi japo inapitika . mbali na usafiri huku kuna fursa saaaana kwa biashara tajwa hapo juu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Kirando Mkuu!! Mwambao wa ziwa Tanganyika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio ifakara ila ni mji mdogo katika wilaya ya kilombero huku kwanza mashamba ni Bei nafu unapata 200000 kwa hekali tena vijiji vyake vina umeme vile vile ardhi inakubali kila aina ya mazao mpunga gunia unapata kwa 50000 vilevile Kuna kilimo cha ufuta afu Kuna mazao ya mboga mboga nyanyachungu wanauza debe 5000 na Kuna wakulima wengi wa ndizi ndizi tunazonunuaga dar 250 mojahuku mkungu unapata kwa1500 Kijiji Cha mbingu afu Kwenye mavazi wanauziwa Bei kubwa lakini wananunua afu ukiwa na mashine ya kupukuchua mahindi unapiga sana pesa Kuna jamaa anayo anawakusanya sana
Msimu wa mavuno huko ni mwezi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naomba msaada wa connection au kujua bei za vitu vifuatavyo. (Nimetumwa kuuliza)

1. Mashine ya kupukuchua mahindi inayotumia mafuta.
2. Mashine ya kupiga mpunga inayotumia mafuta.
3. Mashine ya kupiga mtama,uwele,ulezi na alizeti inayotumia mafuta.
4. Bei ya ng'ombe wa Boran saizi zote (dume kubwa, jike na ndama)
5. Bei ya kukodi Fuso Tandam au scania ya tani26 toka Songea au Rukwa kuja Dar.
6. Bei ya mashine ya kukoboa mpunga ili uwe mchele za aina zote pia za kugrade mchele.
 
Back
Top Bottom