Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

AFRICAN BOYI

Member
Dec 9, 2019
49
150
1617694764022.png
Kama kichwa cha habari kinavyo someka ningependa uzi huu uwe maalum kwa kupeana connection mbalimbali za biashara. Biashara bila connection unaweza fanya bila mafanikio, hivyo basi ni vizuri tupeane connection mbalimbali za biashara.

Uzi huu utumike kuwakutanisha watu mbalimbali katika biashara tofauti tofauti na mwisho wa siku kupeana connection za biashara kutokana na ombi la muhusika. Wapo watu mbalimbali katika dunia hii, wana mitaji mizuri tu lakini kutokana na kutokuwa na connection wametulia na mitaji yao. Hivyo basi uzi huu uwe msaada kwao.

Elezea unahitaji connection ipi katika biashara kisha subiri kupewa connection na wahusika katika biashara hiyo. Lengo ni kusaidiana na si vinginevyo. Tuweke roho mbaya pembeni kisha tuungane pamoja katika gurudumu la maendeleo.

Wadau karibuni katika uzi huu tupeane connection za biashara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom